Duh... Netanyahu kayakanyaga aisee!

Duh... Netanyahu kayakanyaga aisee!

Mzayuni hawezi toboa miezi miwili mtu bee na muajemi. Amshkuru US Kwa kumkingia kifua kila mara Hali ingekua mbaya zaidi, mkubwa Mpishe zayuni kazi yake ni tuvikundi tuu kama Hamas.
Fikiria majeshi ya nchi 2 tofauti yanapambana na jeshi la nchi moja yenye vikwazo, na bado wanahenyeshwa mpaka kuomba vita iishe 🤣🤣🤣
 
Thread ingekuwa nzuri lakini umeiharibu kwa kuandika kiushabiki tena ushabiki wa kijinga.
1. Iron dome na Alloy 3 zime intercept karibia 95% ya makombora ya Irani, kumbuka kuwa hakuna mfumo au mashine ambayo inaufanisi wa 100%.
2. Lengo la Israel ilikuwa kuvuruga program ya nyuklia ya Irani. Wao wameona wamefanikiwa.
3. Wananchi wengi wa Israel wako kwenye Bomb shelters na kufanya kazi za kujenga uchumi zisimame, wanataka vita iishe ili wawndelee na shughuli za kiuchumi.
4. Irani imepata harasa ya vita hii kuliko Israel ambayo imepoteza raia wa kawaida wachache.
 
Anaujua Trump alieomba vita isimamishwe. Kama kusingekuwa na ushindi kwa Iran hii vita Netanyahu na Trump kamwe wasingeisimamisha. Hata wewe mwenyewe unalijua hilo.
Malengo ya Israel na US yalikuwa kuharibu vinu vya nukes baada ya kufeli kwa mazungumzo. Je hayo yamefanyika au hajafanyika?

Au wewe twambie kitu gani Iran wamefanikiwa kuzuia kufanyika pale kwao
 
Niaje waungwana

Nafikiri mashambulizi ya mwaka jana kati ya Iran na Israel, yalimpofusha sana Netanyahu kwa kuamini kwamba Iran ilikuwa na silaha chache, na dhaifu kwa kuweza kufanya maangamizi katika ardhi ya Israel.

Ikumbukwe kwamba katika mashambulizi yale Iran alitumia makombora ya kawaida na ya masafa mafupi, hivyo hata madhara na uharibifu wake huko Israel haukuwa mkubwa kivile, hali iliyomfanya Netanyahu aamini kwamba Iran haina silaha za maana za kupambana nae, lakini pia aliamini kwamba Iron dome na Thaad zikiongezwa na kurekebishwa vizuri, basi muajemi atachapika vizuri bila kurusha au kuingiza chochote katika ardhi ya Israel.

Masikini, jamaa hakujua kwamba Ayatollah alikuwa anampimia upeo wake wa akili ulipoishia. Akaenda Marekani kuonana na Trump kisha wakapanga namna watakavyoivamia Iran, kutawala anga, na kuzuia kombora kurushwa nchini kwao Israel.

Waswahili wanasema usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Neta akaanza uvamizi kwa mashambulizi ya kushtukiza huku wakiwa wameshajipanga na Marekani, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa na washirika wengine kuzuia mashambulizi ya Iran kwenda Israel. Mpaka hapo walikuwa wanajua Iran haina silaha au makombora ya maana ya kupenya ulinzi wao. Kwa bahati mbaya hali ikawa tofauti na walivyotarajia.

Vinu vikaanza kutumwa Israel katika speed na nguvu ya ajabu kiasi ya kwamba Iro dome na Thaad zao zikabaki kama maonesho tu au mavyuma ya kukamatia kumbi kumbi. Iron dome balada ya kuzuia kombora, inazuia nzi na upepo.

Netanyahu akaona maji yamezidi unga, kinachozuiwa hakionekani, akamwambia baba yake Trump aingilie kati. Baba na yeye kuingilia kati kaishia kupiga hewa, huku mzigo ukiwa umeshahamishwa zamani. Baada ya hapo wakafikiri hilo tukio linamfanya muajemi aogope au kusalimu amri, badala yake ikawa kama vile wamempeleka mzaramo mkoleni. Yani ndo amezidisha mashambulizi na kuigeza Tel Aviv kama Mogadishu.

Baada ya plan kushindwa eti wameamua kuomba poo kwa kutaka vita isimame. Muajemi hataki kusikia hilo, bado anaendeleza kipondo tu huko Israel. Japo wao ni mabingwa wa kuficha taarifa, lakini ukiona Trump anakimbilia kutaka mapigano yasitishwe au vita iishe basi ujue ameona madhara makubwa mno yaliofanywa na Iran huko Israel. Maana ni yeye ndio alikuwa anasema eti waachwe waendelee kuchapana. Sasa imekuaje tena kutaka vita isimame. Za kuambiwa changanya na zako.

Vita sio poa. Nina imani Netanyahu anajuta kuanzisha huu mzozo na vita ikisimama naamini hatokuja tena kuigusa Iran kindezi ndezi vile.

Ukiona mtu mzima analia ujue kuna jambo. Fikiria leo hii Trump anapambana ili vita iishe. Ujue kuna jambo kubwa limetokea huko Israel halitaki kusemwa 🤣🤣🤣
Hakuna lolote ni baada ya Iran kukubali kuachana na mpango wake haramu wa kutaka kumiliki silaha za nyuklia.

It's as simple as such. Mengine ni porojo tu za jihadists wanazotoka nazo masjid.
 
Hakuna lolote ni baada ya Iran kukubali kuachana na mpango wake haramu wa kutaka kumiliki silaha za nyuklia.

It's as simple as such. Mengine ni porojo tu za jihadists wanazotoka nazo masjid.
Ni wapi Iran imekubali mpango wa kuachana na nyuklia?

Au umeokota taarifa zako kutoka katika vikao vyenu vya gongo!
 
Thread ingekuwa nzuri lakini umeiharibu kwa kuandika kiushabiki tena ushabiki wa kijinga.
1. Iron dome na Alloy 3 zime intercept karibia 95% ya makombora ya Irani, kumbuka kuwa hakuna mfumo au mashine ambayo inaufanisi wa 100%.
2. Lengo la Israel ilikuwa kuvuruga program ya nyuklia ya Irani. Wao wameona wamefanikiwa.
3. Wananchi wengi wa Israel wako kwenye Bomb shelters na kufanya kazi za kujenga uchumi zisimame, wanataka vita iishe ili wawndelee na shughuli za kiuchumi.
4. Irani imepata harasa ya vita hii kuliko Israel ambayo imepoteza raia wa kawaida wachache.
Israel hata ikipata hasara kubwa, huwa inaficha taarifa kwa kukataa kuonekana dhaifu. Hata hivyo madhara iliyopata Israel ni makubwa ndomaana aliamua kuiita Marekani ije imsaidie kupambana.
 
Najiuliza tu kwa sauti.

Hivi kama Iran angekuwa kachapika kisawasawa kama habari tunavyozipata hili tangazo la cease fire lingesikika kweli?

Yaan adui wa Israel na USA awe dhaifu halafu wampe muda ajipange.?

Labda em ngoja nijipe muda maana mimi ni mtazamaji tu wa hivi vita hapa duniani.

Ila kiukweli na uhalisia niko upande wa Urusi japo ananiudhi namna anavyopeleka OP yake kihuruma.
 
Hatukudai mzee ,jihad halisi imeonekana ...

1000103043.jpg
 
Najiuliza tu kwa sauti.

Hivi kama Iran angekuwa kachapika kisawasawa kama habari tunavyozipata hili tangazo la cease fire lingesikika kweli?

Yaan adui wa Israel na USA awe dhaifu halafu wampe muda ajipange.?

Labda em ngoja nijipe muda maana mimi ni mtazamaji tu wa hivi vita hapa duniani.

Ila kiukweli na uhalisia niko upande wa Urusi japo ananiudhi namna anavyopeleka OP yake kihuruma.
Ukiona Netanyahu na Trump wanajadili usitishaji wa vita, ujue madhara yalikuwa makubwa kwao kulivyo tunavyofiri. Wao wanaojua ni wanajeshi wangapi pamoja na raia wameuwawa.

Wao ndio wanajua ni kambi ngapi na mifumo ya ulinzi vimelipuliwa.

Ila wayahudi wa kazula mimba hawaelewi kinachoendelea, kazi yao ni kubisha na kuivika ushindi usiyostahili Israel.
 
Ni wapi Iran imekubali mpango wa kuachana na nyuklia?

Au umeokota taarifa zako kutoka katika vikao vyenu vya gongo!
Ili kuokoa maisha yake asiuwawe, Ayatollah ameomba poo na kukubali yaishe kwani alikua apelekwe kwa mabikra 72.
 
Sasa wajinga wameongezeka jf vita ishaisha, kama unaweza anzisha tena wapigie wenyewe na sio kuleta matapishi jf,

Vichwa vinataka sometimes new
 
Israel kachapwa mchana kweupe kwasasa wale wenye kuamini Israel ndio Taifa teule kwasasa polee yenu Jehova wenu ndio uyo kapigwa na Ayatollaah..,
Uzuri wa uongo huwa hauishi muda mrefu. Waliotudanganya kuhusu Israel sasa wameumbuka vibaya.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom