Duh! Kumbe Brazil imelipwa kuja kucheza Bongo!

Duh! Kumbe Brazil imelipwa kuja kucheza Bongo!

Vipi umerudi tena baada ya ofisi za serikali kufunguliwa nini usitegemee komputa za serikali tafuta yako maana siku za weekend utakuwa unapitwa mengi hii topic ina thread yake imejadiliwa weekend nzima iunganishe huko, pole.
 
Baada ya watz kushindwa kumuona kaka akiwa na real madrid, Jk amefanikiwa kumleta Kaka akiwa na brazili.
Jk mpenda michezo pia na mpenda mendeleo lkn pia kutokana na kukubali kuja kwa brazili kunamfanya Jk anakubalika kitaifa na kimtaifa

leo kweli ndio nimekubaliana na maoni ya wengi humu ndani unamatatizo kichwani sio bure. Yaani ukiamka tu unafikiria kukera watu dah.
 
kwani brazil wamekuja bure au pesa za walipa kodi zimetumika kuwaleta.
 
leo kweli ndio nimekubaliana na maoni ya wengi humu ndani unamatatizo kichwani sio bure. Yaani ukiamka tu unafikiria kukera watu dah.

pole kwa kuchelewa kung'amua hilo, ni majeruhi wa ubongo wake. mbu jike amemtafuna, anateseka.
 
Vipi umerudi tena baada ya ofisi za serikali kufunguliwa nini usitegemee komputa za serikali tafuta yako maana siku za weekend utakuwa unapitwa mengi hii topic ina thread yake imejadiliwa weekend nzima iunganishe huko, pole.

DUH! Yaani huyu mgonjwa sugu anapenda kubabia vya bure tu kama vile watu wa CCM? kweli hawa wanalifilisi taifa! Sugu -- bila shaka sasa unasubiri fulana na capelo za bure kutoka CCM! Kumbuka hawa huwa hawatoi nguo za chini -- hizo tafuta mwenyewe!

Huko nyuyma niliomba Mods wamfute, lakini nimegauza mawazo. Nainjoi jinsi anavyoshambuliwa kwa hoja na kujianika kuwa ni mpumbavu tu -- kama vile wengi tu wanaoiongoza hii nchi! it's a real a fools' show!!
 
Mie kusema kweli nachukia sana thinking ya Kikwete........laiti kama ningeweza ningembadilishia. :angry:
 
DUH! Yaani huyu mgonjwa sugu anapenda kubabia vya bure tu kama vile watu wa CCM? kweli hawa wanalifilisi taifa! Sugu -- bila shaka sasa unasubiri fulana na capelo za bure kutoka CCM! Kumbuka hawa huwa hawatoi nguo za chini -- hizo tafuta mwenyewe!

Huko nyuyma niliomba Mods wamfute, lakini nimegauza mawazo. Nainjoi jinsi anavyoshambuliwa kwa hoja na kujianika kuwa ni mpumbavu tu -- kama vile wengi tu wanaoiongoza hii nchi! it's a real a fools' show!!
Yeye mwenyewe hajagundua kuwa watu wanamuinjoi badala ya kujadili topic zake anazozileta wanamjadili yeye.
 
Ameshatufahamu jinsi tunavyong'aka JK na CCM yake wakisifiwa. Infact, yeye ndiye anatu-enjoy kwa hamaki zetu humu. Tukiacha, ataacha.
 
Tatizo Jk kapata ushauri mbaya kwa mara nyingine tena.Priority iliyofanyika ni mbovu sana,inasikitisha.
 
Priorities mazee.

Hapa mtu angeweka chart ya "Unaweza kutumiaje dola milioni sita za Kimarekani" tungelia.

Kuanzia madawati ya shule, kama unakwenda kwa estimate za dawati la uhakika la shilingi 100, 000 na exchange rate ya dola moja kwa shilingi 1500 for simplicity's sake. Dola milioni sita ni shilingi bilioni tisa, katika shilingi bilioni tisa unapata madawati tisini elfu.

Madawati tisini elfu tungekuwa tumebadili kabisa picha za wanafunzi wanaokaa chini nchi nzima.Sijui hata kama mahitajin yetu yanafikia hapo.

Hii inamaanisha hizi habari za kusema kwamba hatuna pesa, nchi masikini ni uongo.Kama nchi inaweza kutumia $ 6 m kuleta timu ya Brazil, then suala si umasikini, suala ni priorities kama anavyosema mazee mbebabox hapo juu.

Hapo sijaenda kwenye tiba na huduma nyingine za jamii. Watu wenye UKIMWI wanachukua zaidi ya nusu ya vitanda vilivyopo mahospitalini Tanzania. Kama unatumia figures hizo hizo za madawati kwa vitanda vya hospitali Tanzania ingeweza kuongeza vitanda 90,000 vya hospitali kwa pesa hizi. Tungeweza kumaliza tatizo la vitanda hospitalini, au hata kama tusingemaliza tatizo hili, tungelipunguza vizuri sana.

Tuna magonjwa, tuna UKIMWI (imebidi niuweke tofauti na magonjwa mengine kutokana na ulivyo tishio) tuna ujinga (Tanzania inarudi nyuma katika kufuta ujinga) kuna umasikini.

Kuna kuwapatia watu maji, kuna kuwapatia watu umeme, kuna kuwapatia watu pembejeo, kuna kuwapatia watu ajira viwandani, kuna elimu, kuna miundombinu, kuna lishe kuna maswala lukuki.

Less than 29% of the rural Tanzanian population has access to clean water. And these are Ministry of Water figures so you know to take them with a pinch of salt, the real figure is probably less than half of that.

Sisi tunaenda kulewa mvinyo wa mamilionea!

Leo hii tunashabikia kutumia hela zote hizi kwa siku moja tu. Hivi watu wanatumia akili hapa?

Yaani tunafanya mambo utadhani hatuna external debt ya about $ 6 billion ?

Priorities.

Kwa tatizo la maji safi vijijini kwa hela hizo hizo tungeweza kuchimba visima vya maji safi kati ya 3000-4500 kwa wastani wa kisima kimoja tshs 2000000-3000000/= kwa maana kwamba vijiji 3000-4500 vingekuwa vinapata maji safi na salama.

kwa shule za msingi kwa hela hiyo hiyo kwa wastani wa 5000000/= kwa kila nyumba ya mwalimu shule ya msingi tungejenga nyumba 1800 za walimu shule za msingi au tungepata zahanati kama 1000. tukiongelea vitabu mashuleni kwa wastani wa kitabu kimoja 20000/= tungepata vitabu 450000/=
Kila mzazi akienda kujifungungua kuna kitu wanaita delivery kit ambayo wastani wake ni kama 10000/= kwahiyo ungekuwa na delivery kits 900000 kwa maana hiyo ungesaidia kina mama 900000/= wanaoenda kujifungua. Hili la afya naliongelea kwa uchungu baada ya shemeji yangu kupoteza maisha kwa kukosa gari kwenye zahanati ya kata kumkimbiza kituo cha afya cha tarafa kwani alifia njiani baada ya watu kuamua kumpeleka na baisikeli na kutumia zaidi ya saa 3 kwenye umbali wa dakika 45 kwa gari kwa maana hela kama hii tungepata magari 90 ya wastani wa milioni 100 kwa gari na yakagawiwa kwa kata. Na hii ndio sababu itakayonifanya niitumie kura yangu kujaribu kubali upepo wa kisiasa tunahitaji uongozi makini jamani tuhamasishe mabadiliko kwani watu wamekaa madarakani mpaka wamejisahau

kumbuka jamaa alitaka kuwaleta real madrid ikashindikana sasa kageukia huko kwa Brazil.
Naomba kuwasilisha
 
Baada ya watz kushindwa kumuona kaka akiwa na real madrid, Jk amefanikiwa kumleta Kaka akiwa na brazili.
Jk mpenda michezo pia na mpenda mendeleo lkn pia kutokana na kukubali kuja kwa brazili kunamfanya Jk anakubalika kitaifa na kimtaifa

kumbe wameletwa kumfanyia kampeni siyo?
wameletwa kwa fedha nyingi kuonesha kuwa kikwete anakubarika
lakini wananchi ambao ni wafanyakazi wa secta za umma kuongezwa mishahara no!


kwangu mi naona ni aibu
 
Hii mechi haina hata umuhimu kwetu kima cha mshahara 100000/= kodi na pension 10000/= kiingilio 30000/= nitabaki na 60000/= wastani wa 20000/= kwa siku na hayo ndiyo maisha bora kwa kila mtz au Bora maisha kwa kila mtz

na huu ndio bora uongozi na si uongozi bora

Jamani hivi ukimpa kura kama huyu unafikiria nininiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii? au ile kanga na fulani upate shida kama mimi kwa miaka mingine mitano?????????????????

sipati jibu?
 
kumbe wameletwa kumfanyia kampeni siyo?
wameletwa kwa fedha nyingi kuonesha kuwa kikwete anakubarika
lakini wananchi ambao ni wafanyakazi wa secta za umma kuongezwa mishahara no!


kwangu mi naona ni aibu
Ndugu utaweza kwenda uwanjani kwa mshahara ulionao na kiingiliio kilichotajwa? naona bora wasingekuja
 
Ari mpya, Kasi mpya na Nguvu mpya kwa michezo na si kwa maisha ya maskini ambaye hana uhakika na hata mlo moja kwa siku. Hizo bil 3 za kuilipa Brazil zingetosha kuwafikia kwa huduma maskini wangapi ambao hawana maji safi na salama, chakula, malazi, nguo, dawa, shule na nyumba za waalimu/madaktari, n.k. Yaani eti unafanya fund raising ya kuwapa matajiri hela wakati the similar fund raising can serve lives of many who are facing abject pooverty. Ni wakati umefika sasa kwa serikali ku-organise fund raising events to subsidize the well-being of the poorest Tanzanians! Inaniuma sana. Ningekuwa tajiri kama Manjis, Patels, Somaiyas, Rostam Azis, the list is endless, ningejitoa sana kwa jamii. Ninachoweza kusaidia kwa sasa hakifiki kokote, the demand pool is endless! Oh Lord serve the mind of our leaders so that they can commit themselves to serve the life of the needy. I hope with 100% sure our presidaa will grace the event!!
 
Kila sehemu ni mzaha tu! hivi hatuna vipaumbele jamani? Mkuu wa kaya lazima akauze sura na kujichesha na kuiga picha na Dunga

Vipaumbele vya mkwere vipo vingi tu - tayari mpango wa kukopa $250m toka stambic ushaiva. Harambee ya kuwaleta brazil kwa more than 3b umefanikiwa lakini harambee ya kuhakikisha mama zetu wanajifungua salama na kuboresha wodi za wazazi nchi nzima zii.
 
bahati yao (serikali ya JK) kuna uwanja wa kisasa ambao utasaidia kuraise amount of that money...

hivi anayependaa michezo bila miundo mbinu kama viwanja, mpango imara wa kuendelezaa michezo nk na ambaye aliweka miundombinu (ujenzi wa kiwanja cha kisasa barani afrika) tofauti yao ni nn!!!

3bn jamani kwa Tanzania ni hela ambayoo natumai tatizoo la maji dar lingepunguaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom