Dr. Ulimboka: Hali ya afya (Updates)

Dr. Ulimboka: Hali ya afya (Updates)

Sasa mtu mmoja kula kipigo ndio hakuna amani, amani ipo tena kwa sana na CCM itahakikisha kuwa amani itaendelea kuwepo,usipotoshe umma kijana. Mnakaa kulaumu serikali bila hata kupata ushahidi wowote. CCM itatawala milele, na nyie CDM acheni uhaini,mtafia jela.

Kuna ushahidi gani unaouhitaji ili ujue kuwa Serikali ndo "the bad animal of this scandal"?
Suala hapa ni issue ya Dr. Je, Serikali hii inaongozwa na nani? na kwanini uingize CDM hapa?
Wakati fulani kukaa kimya ni HEKIMA kuliko kujibu UTUMBO hapa!! si lazima kila bandiko ukaja kuchangia...
 
Shiriki maandamano tarehe 04.07 2012 ubungo mataa kuwa shaidi wakudai huduma bora ya afya mwambie na mwenzako
 
Mungu amsaidie apone haraka. Mengineyo haki itatendeka hata ikiwa miaka mbele watajulikana, kina Kombe walifanyiwa mchezo kama huu..tumwombee Mungu apone.

Kwa sala na maombi ya yetu Watanzania wote wenye mapenzi mema na akili timamu, kweli Mwenyezi Mungu atamsaidia apone ili aje kuendeleza mapambano ya kudai haki.


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Kwani wameumbuka kidogo? Mungu ndiye anayetupa na kuchukua uhai kwa sisi tunaoamini. Haya matishio mengine kama wengine hawatakufa hayana tija. Siamini kabisa katika kuteketeza maisha ya mtu au watu wengine....either kwa siasa, ujambazi, wivu au lolote lile!

Halafu mdunge mmoja akadiriki kusema eti kipigo hicho kinamstahili Huyo mbunge alaaniwe
 
Mkuu wangu najua sana kwamba nimeandika mambo mazito sana yanayouma lakini Ndivyo Ilivyo! Na tunaytakiwa kujifunza ktk kila jambo linalotupata hapa duniani maana kinachoendelea nchini haikina huruma kwa watu wengineo. Tazma picha utaona Dr.wetu kawekewa vifaa vya kila aina kuhakikisha anapata huduma ambayo kuna watu 100 hawaipati tena kwa sababu ya mgomo wa Madaktari...


Kwa kuhemu matukio tunayoishi sasa nisingeta kugeuza huu uzi uwe wa malumbano, lakini itoshe nikisema kuwa sijasoma hiyo post yako hapo juu. I just decided not to.
 
Kwa kuhemu matukio tunayoishi sasa nisingeta kugeuza huu uzi uwe wa malumbano, lakini itoshe nikisema kuwa sijasoma hiyo post yako hapo juu. I just decided not to.
Well n good..Haibadilishi kitu!...
 
Hata kama azma ya serikali ya kutoa uhai wa Ulimboka ukatimia, kamwe JK na serikali yake watakuwa paranoid for as long as it exists
 
Get well soon kamanda, we are praying for you!!!
 
Wabongo bana, so ndugu zetu wanaondelea kufa kutokana na mgomo wa akina Ulimboka hawana haki ya kuishi ama, mimi simuonei huruma huyu jamaa honestly, mgomo wao unawaumiza ndugu zetu sana, na simuombei kupona.
 
Na akifa ndiyo utaumia zaidi.

Mtanzania kwa sasa upo kati ya NYUNDO na JIWE.

Sasa kama hutafahamu wapi ukimbilie kujinasua, basi wanakuponda.

Huyu jamaa anaweza hata kufa kwa mfano, ila bado tatizo halitakwisha.

Endelea kulaani na ghafla utasikia nyundo Mbaaang, wakati wenzio wanakwenda kutibiwa nje.
Wabongo bana, so ndugu zetu wanaondelea kufa kutokana na mgomo wa akina Ulimboka hawana haki ya kuishi ama, mimi simuonei huruma huyu jamaa honestly, mgomo wao unawaumiza ndugu zetu sana, na simuombei kupona.
 
sasa itafika wakati hawa polisi tunaoishi nao mitaani tutawageuzia kibao kwa mishale ndipo watakapooacha kutumikia kila jambo ovu wanalotmwa na viongozi wao.WAKUMBUKE TUNAISHI NAO MITAANI,MAANDAMANO WANATUPIGA TENA HUKU URAIANI KWENY KUTAFUTA HAKI ZETU,AU KWA KUWA WAO HAWANA VYAMA VYA WAFANYAKAZI
 
eee mwenye Mungu,ulie nusuru uhai wa Dr ulimboka,toka mikononi mwa wakoloni tunakuomba uwe naye mpambanaji huyu,kwani kazi uliyomtuma hajaimaliza
 
Litania ya Huruma ya Mungu Bwana utuhurumie – Bwana utuhurumie
Kristu utuhurumie – Kristu utuhurumie
Bwana utuhurumie – Bwana utuhurumie
Kristu utusikie – Kristu utusikilize
Baba wa mbinguni Mungu – utuhurumie
Mwana Mkombozi wa dunia Mungu - utuhurumie
Roho Mtakatifu Mungu - utuhurumie
Utatu Mtakatifu Mungu mmoja – utuhurumie.
Huruma ya Mungu iliyo sifa kuu ya Muumba wetu - Tunakutumainia (iwe kiitikio)
Huruma ya Mungu iliyo kilele cha ukamilifu wa Mwokozi wetu
Huruma ya Mungu iliyo upendo usiopimika wa Roho Mtakasa
Huruma ya Mungu fumbo lisilofahamika la Utatu Mtakatifu
Huruma ya Mungu iliyo ishara ya uwezo mkuu wa Mungu Mwenyezi
Huruma ya Mungu iliyofumbuliwa katika kuziumba Roho za Malaika wa mbinguni
Huruma ya Mungu iliyotuumba na kutuamuru tuwepo bila kutokana na chochote
Huruma ya Mungu inayotujalia maisha ya kutokufa
Huruma ya Mungu inayotukinga na adhabu tunazostahili
Huruma ya Mungu inayotuinua tutoke katika taabu, unyonge na maumivu ya dhambi zetu
Huruma ya Mungu inayotufanya wenye haki katika Neno aliyejifanya Mtu
Huruma ya Mungu inayofurika kutoka katika majeraha ya Kristu
Huruma ya Mungu inayobubujika kutoka ndani ya Moyo Mtakatifu wa Yesu
Huruma ya Mungu iliyotupatia Bikira Maria Mtukufu awe kwetu Mama wa Huruma
Huruma ya Mungu iliyoonyeshwa katika kuanzishwa Kanisa Katoliki
Huruma ya Mungu inayopatikana katika mafumbo ya Sakramenti Takatifu
Huruma ya Mungu inayotolewa kwa wanadamu wote kwa njia ya Sakramenti ya Ubatizo na Kitubio
Huruma ya Mungu inayotolewa katika Sakramenti ya Ekaristi na Upadrisho
Huruma ya Mungu inayoonyeshwa kwetu pale inapotuita na kutuingiza katika kuwatakatifuza wenye haki
Huruma ya Mungu inayotimilika katika ukamilifu wa watu watakatifu
Huruma ya Mungu chemchemi ya afya kwa wagonjwa na wote wanaoteseka
Huruma ya Mungu iliyo faraja ya wote wenye uchungu moyoni
Huruma ya Mungu iliyo tumaini la roho zinazosumbuliwa na mkato wa tamaa
Huruma ya Mungu iliyo mwenzi wa daima na popote wa watu wote
Huruma ya Mungu inayowahi kutuletea neema zake
Huruma ya Mungu iliyo amani yao wanaokufa
Huruma ya Mungu iliyo burudisho na faraja yao marehemu wa toharani
Huruma ya Mungu iliyo furaha ya mbinguni kwa watakatifu wote
Huruma ya Mungu iliyo taji la watakatifu wote
Huruma ya Mungu chemchemi ya miujiza isiyokauka
Mwanakondoo wa Mungu uliyetuonyesha huruma yako kuu katika kuikomboa dunia kwa msalaba wako mtakatifu, - utusamehe ee Bwana
Mwanakondoo wa Mungu unayejitolea kwetu kwa mapendo na huruma katika kila adhimisho la Sadaka ya Misa Takatifu,- utusikilize ee Bwana
Mwanakondoo wa Mungu anayeondoa dhambi za dunia kwa njia ya huruma yako isiyo na mwisho,- utuhurumie.
Kiongozi : Bwana utuhurumie –
Wote: Kristu utuhurumie, Bwana utuhurumie.
Kiongozi : Huruma anana za Bwana zi juu ya kazi zake zote –
Wote: Huruma za Bwana nitaziimba milele.
Tuombe: Ee Mungu uliye na huruma isiyo na mwisho, na hazina za wema na upendo wako hazina mipaka. Tunakusihi umtazame Stephen Ulimboka huku duniani na kumuongezea huruma yako tena na tena, ili imsaidie asije akakata tamaa hata mara moja, haidhuru akumbane na majaribu makubwa kiasi gani, bali aweze daima kuzielekea na kuzishika amri zako, kwa matumaini na kutimiza mapenzi yako matakatifu, ambayo ndiyo huruma yenyewe. Tunaomba hayo kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristu Mwanao, Mfalme wa Amani na Huruma, aishiye na kutawala nawe, na Roho Mtakatifu, kwa pamoja mkituonyesha huruma, daima na milele. Amina.
 
mungu wetu aliye kila kona atamponya dr. kama alivyomnusuru katika kifo, hii ni laana hakika, serikali ya mabavu inataka kuharibu amani katika nchi yetu..mungu isaidie tanzania..mungu mponye dr. ulimboka...amen
 
Mbegu lazima ife, ili izae zaidi. Tunakuombea upone, ingawa hata kama Mungu akipenda vinginevyo, mbegu utakayotuachia haitakufa, bali itazaa zaidi.
"MUNGU IBARIKI TANGANYIKA, MUNGU IBARIKI ZANZIBARI, RIP TANZANIA"
 
Back
Top Bottom