Dr. Ulimboka azimwa

dr ulimboka kumbuka na naamini nia na dhamira ya Mungu kukuweka hai ni kuiumbua serikali iliyoko madarakani kwa unyama unaoufanya dhidi ya wananchi,usiposema ukweli tena adhalani hakika Mungu akupige kofi mara tatu ya hongo utakayokuwa umepewa.Jitokeze bila woga eleza ukweli bila kumuonea mtu wala kumficha mtu hiyo ndio lengo la Mungu kukuacha hai mpaka leo.kumbuka neema ya Mungu iliyokunusuru na kifo itakulinda milele
 
Kwa hili ninakubaliana nawe JJB, bora anyamaze yaishe. Sisi tunaotaka aseme sio kwa sababu yoyote zaidi ya kutaka kusoma umbea tu. Watanzania sote tumemsaliti Dr.Ulimboka na wanaharakati wote waliowahi kuthubutu kulenga jiwe la kwanza lakini sisi tukaficha mikono yetu. Moja ya maneno na rai aliyoitoa Dr. baada ya kudhulumiwa afya na uhuru wake yalikuwa kuwataka Madaktari wenzake (na Watanzania kwa jumla) kuwa yeye yamemfika yaliyomfika, lakini waliobaki wanendelee na mapambano; matokeo yake, Madaktari walifanya nini na Watanzania tumefanya nini?
Baada ya Mwanahalisi kulezea kile ilichokijua na kuwataja watu na ubini wao na nambari zao za simu, Watanzania tumefanya nini? Tuseme Dr. Ulimboka aje na habari zile zile za Mwanahalisi, Watanzania tutafanya nini? Kama tuwatendaji kweli na sio wambea tu, tuchukue hatua juu ya yale ambayo tayari tunayajua kabla ya kutaka mengine mapya.
Tumwache Dr. apumue na sisi tuendelee na woga na blah blah blah zetu. Uchune Dokta, uchune!

Bado Madr; Watanzania, na wanaharakati tupo pamoja.

Kweli tumesikia mengi kuhusiana na hili; tumeshuhudia Viongozi wetu wa juu wakikanusha (Kikwete, Pinda na Afande Sele)

Gazeti Mwanahalisi limesema mengi na kwa uwazi.

Lakini yote kwa yote D. Ulimboka ndiye anayejua siri ya tkio zima na pia anawajua waliohusika. Kwa namna ya pekee Watanzania wanasubiri kauli yake, kisha ndip tutajua mbichi na mbivu (LIWALO NA LIWE)

Wanaharakati bado wanapenda kujua Sababu na matokeo ya tukio lile la kinyama. Tusiongee kisiasa bali turudi katika hali ya kibinadamu.

Huwezi kukurupuka na kuingia mitaani kulaani kitu ambacho huna point ya kukulinda kuhusu ukweli wake. Lazima ujue ukweli kwanza ndipo uamue.

IPO SIKU KITAELEWEKA tu!!!!


CCM Mahututi.jpg


MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
du kweli magamba ni noma na unyama wote alio mfanyiwa wamemtulza!..............
 
Tumeshasema habari za Dr. Ulimboka zimetuchosha hapa JF pelekeni Issa Michuzi Blog hizo habari
Tena hazina tija hata chembe, lakini kwa vile ndizo wanazotumia wahariri uchwara kuuzia gazeti zitaendela kutawala sana!
 
  • Thanks
Reactions: PPM
Kwa habari nilizo nazo, Dr. Ulimboka anapaswa kuwa mwangalifu na hao wakubwa wa serikali. Damage aliyoisababishia hii serikali na idara nzima ya TISS ni kubwa mno, na kwa uhakika, kuna watu wameapa "Hawatamsamehe".

Hakuna shirika lolote la kijasusi ulimwenguni linaloweza kuvumilia mtu aliye na siri zake bila control ya namna fulani. Yeye kuahidi kukaa kimya haiwahakikishii majasusi wetu kuamini kuwa daima atakaa kimya. Dawa ya hili katika mashirika yote, huwa ni kumalizana ili kuwa na uhakika kuwa ushahidi umekufa. Ndiyo maana, wakati wa Coup de'tat, rais anayeingia huwa anawamaliza waliomsaidia mmoja baada ya mwingine kwa sababu hawezi kuwa salama kwa kuwa na subordinates wanaofahamu udhaifu wake.

Ni suala la muda tu, Dr. Ulimboka ama atapoteza uwezo wa kusema wala kuandika; au atalazimika kuandika taarifa ya uwongo na kisha apotezwe kisha taarifa hiyo itumiwe kuisafisha serikali; au tu - atapotea na huo utakuwa mwisho wa hadithi hii. Worst scenario ni pale atakapojengewa mazingira ya kuchukiwa na wenzake, kisha amalizwe na ndipo wenzake watakaposingiziwa kuwa ndiyo wamemmaliza ili kulipiza kisasi cha kusalitiwa. Kukaa karibu na Dr. Ulimboka ni risk sana kwa sasa.

Mimi si nabii wala mtoto wa nabii!
 
Mnataka aseme ili tuje humu kwa majina feki kumgongea "like" huku akiishi kwa mashaka bila msaada? Tunataka kujua nini zaidi ya kilichomtokea?

Tuliambiwa ripoti itatoka haraka kurudisha imani kwa wananchi mpaka leo kuna wanaharakati au wanahabari wanaohoji mbona ripoti imechelewa na hiyo kamati haijamhoji hata mtuhumiwa mmoja! Madaktari ndio wasaliti namba moja wa Dr Ulimboka!

Ulimboka aseme nini zaidi ya aliyokwisha sema tena alitaja mpaka majina!
 
du kweli magamba ni noma na unyama wote alio mfanyiwa wamemtulza!..............
 
Godwinnko
Ilishasemwa humu JF kuwa Ulimboka ni mtaalamu na siyo mwanasiasa, hawezi kupelekwa pelekwa na wanasiasa na wanaharkati kwa maslahi yao binafsi. Haya sasa mmeanza kuja na "azimwa" Chanzo chenyewe cha taarifa Tdaima, ndo wale wle Kubenea type. Mwacheni Dr. wa watu apumzike ili aiendeleze taaluma yake, kama waliokuwa wakimtumia hawajaridhikana wabuni mbinu nyingine ya kujipatia umaarufu.

Leo mwacheni apumzike, angekufa je? Hope ulifurahishwa na kitendo cha kutekwa and kuteswa Uli
 
akitusaliti watanzania ilikuwafurahisha chama cha mabwepande asifikili ameshinda maana wanajua iko siku anatema ukweli tu hivyo kabla hajasema ukweli watammaliza..
 
Umasikini unaweza kuwa chanzo cha kufungwa mdomo pia.......ila hii inampotezea utu wake na heshima pia aliyopewa na Ma dr wenzake.
 
hakuna siri idumuyo milele
lazima atatoaa siri kwa mkewe na mkewe atasimulia kwa mwingine
tutajua ukweli soon.nlishajua mapema hatasema chochote kuna dr mmoja
akanipinga hii serikali ni zaidi ya tuijuavo
 
Bado Madr; 1.Watanzania, na wanaharakati tupo pamoja.

Kweli tumesikia mengi kuhusiana na hili; tumeshuhudia Viongozi wetu wa juu wakikanusha (Kikwete, Pinda na Afande Sele)

Gazeti Mwanahalisi limesema mengi na kwa uwazi.

Lakini yote kwa yote 2a).D. Ulimboka ndiye anayejua siri ya tukio zima na pia anawajua waliohusika. Kwa namna ya pekee Watanzania wanasubiri kauli yake, kisha ndip tutajua mbichi na mbivu (LIWALO NA LIWE)

Wanaharakati bado wanapenda kujua Sababu na matokeo ya tukio lile la kinyama. 3.Tusiongee kisiasa bali turudi katika hali ya kibinadamu.

Huwezi kukurupuka na kuingia mitaani kulaani kitu ambacho huna point ya kukulinda kuhusu ukweli wake. 2b.Lazima ujue ukweli kwanza ndipo uamue.

4.IPO SIKU KITAELEWEKA tu!!!!


View attachment 62579


MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
Ninajaribu kueleza kwa points kama nilivyoainisha kwenye nyekundu hapo juu:
1. Nimefurahi kusikia kuwa bado Wanaharakati mpo.

2a&2b. Mimi na wewe tunajua kuwa UKWELI katika nchi hii unamilikiwa na dola, na ndio maana dola hiyo kama mtuhumiwa nambari moja wa tukio hili iling'ang'ania kuunda tume ya uchunguzi ili kujichunguza wenyewe na kutoa ukweli kama wanavyotaka wao, ikiwa siku moja watautoa. Ikiwa ukweli wa Dk. Ulimboka utakuwa kinyume na ukweli wa dola, usishangae kuwa Dk. atashitakiwa kwa kupotosha ukweli wa dola.

3. Kama Mtanzania muathirika na matendo ya serikali yetu, ninalizungumzia hili kibinadamu na hisia zangu na sio kisiasa.
4. Ninasubiri kwa hamu kuona kile kitakchachotokea baadaye. Tupo pamoja.
 
Kama Ulimboka anafahamu jinsi watu walivofanya juhudi kuokoa maisha yake yeye akiwa hajitambui? Ajue sasa anakitu cha kuwalipa wale wote walishiriki kwa njia moja ama nyingine kuhakikisha anaendelea kupumua kwa UWEZO WA MUNGU.
Mungu hamfichi mtu mnafiki...
 
Ni hao hao waliomteka kumtesa na kumwacha nusu kaputi hawana chembe ya huruma wanachofanya sasa ni kumrubuni anyamaze mwisho wa siku watamwondoa taratibu so long ameamua kunyamaza sasa wanamlia timing kumnyamazisha moja kwa moja.
Usalama wake ni kuweka mambo hadharani vinginevyo wabaya wake watahakikisha wanamuondoa hili kuficha kuhusika kwao.
 
This is very clear! Huu mgomo ni wa madaktari wote,mshikamano wao wote ndio muhimu.sometimes namuelewa Ulimboka,hakuna jemedari anaweza kusimama imara bila uhakika wa jeshi analoliongoza.

Ulimboka kupigwa tu Madaktari wakasambaratika hadi leo alafu wanataka yeye alianzishe tena!

nafikiri mwenendo wa madaktari umemkatisha tamaa Ulimboka na alitarajia wenzake wangekomaa zaidi baada ya kuumizwa vibaya lakini ikawa kinyume! kumbe hata kama wangemuua kabisa mgomo ungeisha hivi hivi kiuoga!

naelewa nafasi ya Dr Ulimboka!
Nakubaliana na wewe kwa asilimia 100. hata kurudi nchini na kuona hakuna kilichoendelewa tayari ni stress sana kwake. hii nikama mtu laikua napigania haki za watu akauawa then akafufuka akapewa story jinsi watu walivyomsaliti, nafikiri atatamani afe hapohapo na asikumbuke kitu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom