Kwa habari nilizo nazo, Dr. Ulimboka anapaswa kuwa mwangalifu na hao wakubwa wa serikali. Damage aliyoisababishia hii serikali na idara nzima ya TISS ni kubwa mno, na kwa uhakika, kuna watu wameapa "Hawatamsamehe".
Hakuna shirika lolote la kijasusi ulimwenguni linaloweza kuvumilia mtu aliye na siri zake bila control ya namna fulani. Yeye kuahidi kukaa kimya haiwahakikishii majasusi wetu kuamini kuwa daima atakaa kimya. Dawa ya hili katika mashirika yote, huwa ni kumalizana ili kuwa na uhakika kuwa ushahidi umekufa. Ndiyo maana, wakati wa Coup de'tat, rais anayeingia huwa anawamaliza waliomsaidia mmoja baada ya mwingine kwa sababu hawezi kuwa salama kwa kuwa na subordinates wanaofahamu udhaifu wake.
Ni suala la muda tu, Dr. Ulimboka ama atapoteza uwezo wa kusema wala kuandika; au atalazimika kuandika taarifa ya uwongo na kisha apotezwe kisha taarifa hiyo itumiwe kuisafisha serikali; au tu - atapotea na huo utakuwa mwisho wa hadithi hii. Worst scenario ni pale atakapojengewa mazingira ya kuchukiwa na wenzake, kisha amalizwe na ndipo wenzake watakaposingiziwa kuwa ndiyo wamemmaliza ili kulipiza kisasi cha kusalitiwa. Kukaa karibu na Dr. Ulimboka ni risk sana kwa sasa.
Mimi si nabii wala mtoto wa nabii!
Bila ubishi wewe ni NABII tena aliyetumwa na MUNGU. Naprint huu uzi kwa ajili ya kumbukumbu binafsi server ya JF ik collapse.