Dr. Ulimboka azimwa

Mwacheni anyamaze manake hata akisema hakuna tutakachokifanya zaidi sana ni kujificha nyuma ya keyboard ,,,mwacheni baba wa watu aishi kwa amani na familia yake. Watanzania kwa uoga wetu tutaendelea kunyamazishwa mpaka siku tutakapoacha woga.......Ulimboka amegundua hata akisema wala hakuna kitakachofanyika ...........alipelekwa msitu wa pande yeye, alipigwa na kuteswa yeye.....je ni nani aliyekiendeleza kile alichoanzisha Ulimboka? Wote mikia imerudi nyuma.....hata ningekuwa mimi ndie Ulimboka ningeuchuna kabisa! Tunashukuru Mungu vile amemwezesha kupona na kuungana tena na familia yake!
 
Tutasikia mengi sana kabla dr.ulimboka hajafunguka......funguka dr funguka!!!!!!
 
Dr. Ulimboka akumbuke kuwa ni sisi watanzania wazalendo ndio tuliookoa maisha yake kwa kumchangia na kumpeleka kwenye matibabu nje ya nchi...na sasa ni watanzania haohao ndio tunaitaji kuwajua hao wahuaji ili tuwaangamize kabisa tusijepata garama tena ya kumpeleka mwingine nje ya nchi kwa matibabu....Asanteni

kweli mkuu ulichangia au?
 
Pole Dr Ulimboka, hata kama ukikaa kimya lazima waliokufanya vile wahakikishe kuwa uwezekanao wa walio yafanya kusemwa ni hakuna. Watakufanya nini mimi sijui lakini kuwa watafanya ni uhakika, tena kabla ya awamu hii kwisha. Hesabu yako itaisha kabla ya uchaguzi mkuu ujao.

Tena ni nafuu useme kuliko kukaa kimya kwasababu ukisema utakuwa umewafanyia madhara makubwa na itakuwa kama kinga yako. Ni kwamba wewe uwa wahi au wao wakuwahi. Delaying tactics wanazokufanyia wanataka kukuwahi.

Kimbia, siyo dalili ya woga, mataifa yote yatakupokea kama mkimbizi, urudi hali ikiwa nzuri. Naukifika huko mwaga ugali na mboga pamoja.

Pole hapa Tanzania hupo salama, nafuu hata ya albino
 
angeyasemea pale airport alipotoka huko alikokuwa
lakini kwa sasa hata mimi naona kana kwamba dr. hawezi kuwa na ushujaa wa kusema kitu.
japo hata asiposema akikaa vibaya watahakikisha wanammaliza kabisa,
na hakika ataondoka na siri yake.
 
Tumeshasema habari za Dr. Ulimboka zimetuchosha hapa JF pelekeni Issa Michuzi Blog hizo habari

Wewe unataka watanzania tushi kwa matukio, kila linalokuja leo tulishabikie tusahau lililotokea jana. Hatukubali-tunakomaa na linalogusa wananchi wengi! Tunataka huduma za afya ziboreshwe!
 
Ulimboka, ni dhambi kubwa kuudanganya uma wa watu wote waliolia kwaajiri yako na kukuona kama mpigania haki,then leo unanunuliwa.fanya maamuzi mazuri la sivyo hautokaa kwa amani rohono mwako.hata mungu hapendi.
Shauri yako.

siku anaondoka alisema endelezeni mapambano,badala yake mkamuangusha.unategemea nini?angekufa hasara ingebaki kwa family yake.huku nyinyi mkiendelea na kazi kama kawaida.
 
Ulimboka, ni dhambi kubwa kuudanganya uma wa watu wote waliolia kwaajiri yako na kukuona kama mpigania haki,then leo unanunuliwa.fanya maamuzi mazuri la sivyo hautokaa kwa amani rohono mwako.hata mungu hapendi.
Shauri yako.

mi nadhani ni kuwa na amani ni kulinda usalama wako na ustawi wa familia yako.
Utamu wa ngoma ingia ndani ucheze, asidanganywe na wanaojifanya kum suport wkt hawaathiriki moja kwa moja na kilicho mkuta au kitakacho mkuta.
Dr ni mtu mzima, msomi mwenye akili zake timamu.
Atachagua lili lililobora zaidi kwa maslahi yake na familia yake kwa ujumla.
 
Dr.is walking on a "THIN LINE BETWEEN LIFE AND DEATH" sasa ni juu yake kuamua juu ya maisha yake.Sisi wengine ni washauri na watazamaji tu!
 
daah tuliguswa sana juu ya unyama alio fanyiwa ndugu yetu.ukweli kama hatataja watu husika wa kisa hiki basi usaliti huu juu ya watu wote utamtafuna.
 
This is very clear! Huu mgomo ni wa madaktari wote,mshikamano wao wote ndio muhimu.sometimes namuelewa Ulimboka,hakuna jemedari anaweza kusimama imara bila uhakika wa jeshi analoliongoza.

Ulimboka kupigwa tu Madaktari wakasambaratika hadi leo alafu wanataka yeye alianzishe tena!

nafikiri mwenendo wa madaktari umemkatisha tamaa Ulimboka na alitarajia wenzake wangekomaa zaidi baada ya kuumizwa vibaya lakini ikawa kinyume! kumbe hata kama wangemuua kabisa mgomo ungeisha hivi hivi kiuoga!

naelewa nafasi ya Dr Ulimboka!


Madaktari hawakumsaliti Dr. Ulimboka. Waliacha mgomo kutii amri ya mahakama ya kuwataka warudi kazini. Ni madaktari, wanaharakati na watu wengine wenye mapenzi mema ndio waliomsadia dr. ulimboka kwenda kupata matibabu Afrika ya kusini. Sikutegemea kama angenyamaza kiasi hiki baada ya kurejea. Inawezekana naye ametii amri ya mahakama kwa kuwa kesi ya aliyemtesa ipo mahakamani
 
Someone or some people have a target of spreading wrong information for their own benefit, this is one of the information. By the way I know Dr Ulimboka cannot be bought or lured by anything... Wanachofanya ni kuchokonoa ili jamaa aongee na Tetesi ni kuwa jamaa anajipanga... People should learn that amongst the smartest people in tz today Ulimboka is one of them, suala ni kuwa Hawaii tu jamaa atatokaje. TAARIFA HIYO HAPO JUU INAPOTOSHA NA MWANDISHI ALIYEIANDIKA HAJAPATIKANA HATA SASA NA HAIELEWEKI KWA NINI ANAFICHWA....chanzo Mimi mwenyewe!!!
 
Dr.Ulimboka alitakiwa kuongea na press huko huko africa ya kusini. Alitakiwa kumwaga ukweli wote kwa vyombo vya habari kama BBC, CNN, SKY news etc. Ona sasa!
 
yeye na Mungu wake ndio anajua nini kilimpata tumuacheni ni mtu mzima ana akili timamu akipenda lolote na afanye sawa tu maadamu yuko hai
 
Godwinnko
Ilishasemwa humu JF kuwa Ulimboka ni mtaalamu na siyo mwanasiasa, hawezi kupelekwa pelekwa na wanasiasa na wanaharkati kwa maslahi yao binafsi. Haya sasa mmeanza kuja na "azimwa" Chanzo chenyewe cha taarifa Tdaima, ndo wale wle Kubenea type. Mwacheni Dr. wa watu apumzike ili aiendeleze taaluma yake, kama waliokuwa wakimtumia hawajaridhikana wabuni mbinu nyingine ya kujipatia umaarufu.
Hicho unachokisema sio sahihi Dr. Uli anatakiwa kwanza amtendee hati Bw. Mgaza halafu na si watanzania wote kwani wakati wa tukio hili watu walifanya maombi ikiwa ni pamoja na kutoa michango yao kwa ajili ya matibabu yake. hivyo anabidi atutendee haki kwa kutoa maelezo na ikiwezekana kuwataja waliohusika ili tukio kama hili lisiweze kutokea kwa mwingine na asipofanya hivyo atakuwa amefanya usaliti kwa Bw. Mgaza, madaktari, Bi Kijo, na watanzania wote tuliokuwa pamoja nae wakati wa maumivu yake.
 
Mwacheni ajidanganye kwamba sasa eti hao vigogo wanampenda. Atajuta tu!
Sasa hivi watamtuliza kwa pesa baada ya kuchoka kumtunza kwa pesa, wakiona kisha dhalaulika. Mwisho wake mutauona. Ngonja azubae tu!

Kama walimpenda kiasi hicho kwa nini hawakumpa hizo pesa kabla ya kumung'oa meno? Sasa kama anadhani anaelewana nao, mpeni mwaka mmoja wa kudhalaulika na wananchi halafu tuone kama ataishi tena.

Kinga yake kubwa ilikuwa ni kuwataja basi! Apewe pesa na safari za nje vyote havimpi usalama. Hiyo nina hakika kabisa!
 
Amekaa ametafakari kwa kina na amejua mchezo wote mwanzo hadi mwisho amesikitika sana ndio maana amesema anamuachia Mungu. ninasikitika kusema "mission failed"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom