Kunyamaza kw Dr. Ulimboka hakumpi uhakika wala kunusuru usalama wake. Wahusika wa mpango wa kumteka wangependa hali iendelee hivi, yaani yakikudhaniadhania tu bila tamko rasmi kutoka kwa muhiska. Nahisi kuna uwezekano wa mpango wa uhakika zaidi ya ule awali maana nao wanapenda kuwa na hakika kuwa hakuna hata sikumoja akatokea mtu wa kuaniaka adharani uwazi wa tukio. Iko siku atanyamazishwa kabisa na hapo utakuwa mwisho wa sinema maana sterling atakuwa kaondoka. Namshauri aseme lililotokea. liwalo na liwe! Akiisha sema atakuwa ametua mzigo aliojitwika na itabaki kwa wasikilizaji kuchambua, wakujikosha wajikoshe, wakijitetea wajitetee, wakuamini waamini, wakupotosha waposhe lakini yeye atakuwa huru. Naamini kuwa watekaji wanamuhutaji zaidi Dr. Uli kabla hajasimulia tukio kuliko watakavyo muhitaji baada ya simulizi maana hawatakuwa na la kuzuia. Asome hii thread atafari na afanye maamuzi magumu.