Madaktari wenzake wakajitolea kufa na kupona, wakahakikisha inapigwa harambee fasta, akapelekwa sauzi tena chini ya ulinzi mkali, yote kwa ajli ya maisha yake, hiyo yote igeuke kuwa bure jamani! hapana haifai hata kidogo, kama unavyosema bila support hiyo saa hizi angekuwa historia, tena ndio kesi ingeisha kiulaini kabisa. post namba 30 hapo juu
mohamedi tantawi anasema tumwache apiganie uzima wake, huo uzima angeupata wapi bila support ya hao anaotaka kuwasaliti sasa (kama ni kweli). Halafu kumbuka mohamedi, hili siyo suala la kisiasa tena ni suala la ubakaji wa haki za binadamu,
Pia lazima muelewe kwamba siri haiwezi kufichwa daima, huwa inamkereketa mtu kuisema, kwa hiyo ataitoa kwa mtu wake wa karibu na kumwambia usimwambie mtu, na huyo naye atampata mshikaji wake atamwambia na kumpa masharti kama hayo ya kutomwambia mtu... yani ni kama mtandao wa 'tuko wangapi' unavyokuwa. sasa kwa kuhofia hilo sidhani kama....
Huyu dokta asitake kutuzingua hapa aseme kilichomkuta atakuwa salama zaidi kwa sababu watesi wake hawatakuwa na haja naye tena baada ya ukweli kuwa umewekwa wazi labda kama ni kwa ajili ya kulipa kisasi tu baada ya kuumbuliwa, na sijuji huko alikokuwa anakutana nao kama hawajamwambukiza kitu.