Sr. Magdalena
JF-Expert Member
- Aug 10, 2011
- 803
- 472
Unalinganisha usiku na mchana. Fisadi dhidi ya Mwadilifu?
dr slaa atachukua kilaini
Heshima mbele sana wakuu,
Najaribu kuichungulia 2015 miezi ya october endapo mchuano utakuwa ni kati ya hawa vinara wawili ni nani atakuwa na nafasi kubwa ya kuukwaa urais wa nchi hii.
Wote ni wanasiasa wa siku nyingi wenye heshima zilizotofautiana kutokana na historia na nyadhifa tofauti walizowahi au wanazozikalia hivi sasa,
Je come 2015 nani ataibuka kidedea endapo team hizi zinakutana kwenye viwanja sawa vya haki na usawa, bila zengwe wala mizengwe.
Hii kitu bado ni ngumu sana mkuu Sr. Magdalena
Kuna uwezekano mkubwa sana kwa vyama vyote hivi kupandisha sura ngeni kabisa kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Unaonaje kama kwa mara ya kwanza CDM wapandishe mtu kutoka znz, Hamad Rashid kwa mfano?
Wasalaam
Unalinganisha usiku na mchana. Fisadi dhidi ya Mwadilifu?
Hii kitu bado ni ngumu sana mkuu Sr. Magdalena
Kuna uwezekano mkubwa sana kwa vyama vyote hivi kupandisha sura ngeni kabisa kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Unaonaje kama kwa mara ya kwanza CDM wapandishe mtu kutoka znz, Hamad Rashid kwa mfano?
Wasalaam
muombe msamaha dr.slaa,.umelinganisha usingizi na kifo
Kama ni kwalinganisha Dr. Slaa na Lowasa basi ni ukweli uliowazi kuwa Dr. Slaa atachukua nchi. Ila tukija katika mizania inayoangalia usawa hiyo comparison sio sahihi hata kidogo. Dr. Slaa ni mzalendo kwelikweli na mpinga ufisadi kwa maneno na vitendo wakati Lowasa ni Fisadi aliyekubuhu. mimi nadhani ungempambanisha Dr. Slaa na mtoto wa mkulima (Pinda) hapo angalau tungekuwa na mizania sawa kwa sababu mtoto wa mkulima hatujasikia kashfa za ufisadi kwake.