Msipotoshe mambo. JK aliambatana na kijana wake Kenya kwenye sherehe za kuapishwa rais wa Kenya. Tulipiga kelele sana Ridhwan alipopiga picha akiwa mbele ya viongozi wa serikali kwani tuliona kama protokali haikuzingatiwa. Ujinga tunaolaani unapofanywa na ccm hatuwezi kukaa kimya kwa kuwa tu ujinga huohuo umefanywa na Slaa au na CDM.
Wengi tunamfahamu Dr Slaa kama mtu makini, lakini anapokaa kwenye kikao rasmi na gavana wa jimbo na mawaziri wake huku akiwa na mkewe, huyo mkewe anamwakilisha nani, au ni nani CDM? Tumeyaona Anna aliyomfanyia Mkapa, hatutaki yajirudie kwa Josephine na Slaa, na kwa vyovyote mstibue imani ambayo wananchi wameanza kuijenga kwa CDM.
Mliopo karibu na huyu mzee msaidieni. Inawezekana amezidiwa na nshutama.