Ritz,
Utabwabwaja na propaganda mpaka utachoka. Basi angalau ungelikuwa hata na Taarifa
Sahihi.
1. Kwanza hoja ya kukutana na Wajapani nyumbani, pamoja na kuwa Dr Slaa hazuiwi na sheria au utaratibu wowote kukutana na yeyote anayetaka nyumbani kwake au mahali popote, siyo ya kweli. Hakuna siku hata mmoja, siyo mwezi Juni tu, wajapani 20 walipofika na kula nyumbani kwangu. Kama ni hivyo, mbona unawake picha za Mama Slaa alipokuwa Japan basi. Isitoshe picha za safari ya Mama Slaa hazikuwa siri zilikuwa kwenye FB yake. Mtihani wa kwanza umefeli vibaya sana. Fanya mwingine tuone.
2. Ah! Kumbe ujenzi wa Hospitali! Pamoja na kuwa sina mpango huo, labda Kama utakuwepo baadaye tatizo ni nini. Dr. Slaa nimeasisi taasisi ya CCBRT mwaka 1994 na kujenga, pamoja na programs zingine, Hospitali kubwa kuliko zote hasa kwa performance( look at statistics) Afrika South of Sahara inayoshughulikia disagbilities under one roof, ten a katika Ardhi tuliyopewa na Serikali ya JMT. Sasa hivi, tunajenga Hospitali kubwa ya Mama na Mtoto itakayokuwa tayari 2014/15, nayo pia katika nyongeza ya ardhi tuliyopewa na Serikali. hospitali zote ziko exempted. Ukwepaji kodi uko wapi. Kama CCBRT imepata cheti cha TRA, Kama stori yako ungekuwa kweli, si ni utaratibu huo huo ungelifuatwa! Tatizo liko wapi hapo? ritz una akili ya ajabu, ningetaka kufanya biashara ningeshindwa kufanya hivyo kupitia CCBRT. Nadhani mnatafuta pa kushikiza, piga ramble zaidi labda itakusaidia!