Elections 2010 Dr. Slaa mgombea urais 2010 kupitia CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Kama wapinzani watamsimamisha Dr Slaa kwa urais na Hamad Rashid kwa ugombea mwenza. wandugu! CCM haikitaeleweka...hao jamaa ni mabingwa wa kujenga hoja....kama ni hivyo nitaanza kupiga kampeni sasa hivi....juhudi binafsi.....nasikitika nilishakatishwa tamaa na mfumumo wa upiogaji kura nchini....nikaacha kupiga kura....kwa hiyo sijajiandikisha......

Lakini nooooo! nijitoa kwa hali na mali kupiga kampeni. Period!
 
Yawezekana bila ya shaka huu ukawa ni mwanzo mzuri wa kuelekea mabadiliko. Mtu kapatikana sasa ni ujumbe!

Ni kweli MM, Lakini uzoefu wangu wa 2005 unaonyesha kwamba mawakala wa vyama ndiyo chanzo kikuu cha ushindi wa kishindo wa CCM, tukirebisha hili, for sure huu utakuwa mwazo mzuri
 
Mwanzo mpya? Naamini Mungu ataipatia nchi hii mwanzo mpya siku moja...labda ndio sasa...Thank you GOD.
 
Hatujachelewa. Lipumba aende Sikonge au jimbo lolote analoona atashinda ili tuunganishe nguvu!
 
Tatizo la upinzani, pamoja na Dr. Slaa kukubalika kwa sasa bado vyama vingine vitasimamisha wagombea, hili linanipa taabu sana
 
Mungu mkubwa..at last ameanza kusikiliza kilio chetu. Muda wa mabadiliko umewadia. Mwaka wenyewe ni 2010 na siyo zaidi ya hapo kwani waTz tumekwishachoka mbaya.
Go..goo Dr. Slaa. Tutawasapoti wanamageuzi kwa nguvu zote.
 
Mkuu,
Tafadhali bwana. Huyu Kaka Lipumba hatokei Sikonge na wala siyo mwanyeji wa Sikonge kabisa zaidi ya kwamba alisomea hapo Sikonge Mbirani, miaka hiyo ikiitwa MIDDLE SCHOOL. Yeye mwenyeji wa Lolangulu (Ilolangulu) kama unakwenda Urambo. Sijui wako jimbo gani hawa watu ila kwa uhakika siyo Sikonge.

Ila naungana na wewe kusema kuwa Wanyamwezi tufanye kazi ya kumuambia huyu Brother kwa kimila chini ya Mtemi wetu Fundikira kuwa aachie wenye uwezo wagombee kama kweli anataka Wanyamwezi wenzake tubadili maisha. Ona Tabora ilivyochoka na hata mtemi mwenyewe badala ya kuishi Itetemya, kwa sasa anaishi Dar es salaam.

Yes, muda wa mabadiliko ni huu.....

Hatujachelewa. Lipumba aende Sikonge au jimbo lolote analoona atashinda ili tuunganishe nguvu!
 
Duh! Habari hii imenipa furaha, faraja na matumaini. Licha ya kwamba kura yangu anayo, pia nitashiriki kupiga kampeni kwa ajili ya kiongozi huyu jasiri, na mtetezi wa rasilimali za wanyonge, Dr Slaa.

Leo lazima nijipongeze kwa laga. Chama numero uno kaeni chonjo.
 
Kwa mara ya kwanza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaweza kutoka miongoni mwa members wa JF......! Tumuunge mkono..!
 
Mkuu Ndege ya Uchumi,

Naona Mungu kasikia kilio changu. Ni zaidi ya miaka miwili sasa nilikuwa nikimpigia KAMPENI ya waziwazi humu ndani ya JF huyu Dr. Slaa.
Siku wakimtangaza mshindi, bila ya kujali ataniandikia au lahh, ntakuwa mwenye FURAHA zaidi yake. Kuna sababu fulani fulani zinanifanya niwe hivyo. Wakati wa Mwinyi, kutokana na siasa yake ya RUKSA, nilipoteza ndugu wawili muhimu sana kwenye familia na kisa ni Muhimbili kutokuwa na mashine fulani ambayo sidhani hata ina bei kubwa.

Dr. Slaa, nitahakikisha NAKUSANYA NDUGU na JAMAA zangu zaidi ya 100 ili wakupigie kura. Nitawapa somo hadi kieleweke na nina imani hawatavunja ahadi tutakayowekeana kuwa WAKUPE WEWE KURA. Leo peke yake nimeshapata watano.

MODS: Tafadhali ifungulieni ile PETITION ya Dr. Slaa kugombea URAIS na mbadilishe tu kichwa cha habari kuwa WANAOMUUNGA MKONO DR. SLAA wajiandikishe hapo. Ikibidi basi ifungeni hiyo Kura ya Maoni ya Kikwete na muweke ya DR. SLAA.

Nilipoanzisha hii petition, kuna wengi waliona kama upuuzi. Ila ukweli ni kuwa Wasomi wa UDSM wamefanya kitu kama hichohicho na kwenda kumsinikiza Dr. Slaa agombee Urais. Nina uhakika kama tungelifika walau watu 500 humu ndani na kumuandikia barua, basi tungelizidi kuipandisha hadhi JF. Lakini bila ya kujali nini kimetokea, nina imani bado JF tuna kazi kubwa ya kufanya ili tubaki kwenye ramani ya Tanzania kuwa TULIHUSIKA NA MABADILIKO.

_____________________________________________________________________________________________
Wanachama wasomi wajiorodhesha kumtaka Dk. Wilbroad Slaa
Wakati Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikiumiza kichwa juu ya mgombea wake wa urais, wasomi wanachama wa chama hicho kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wamejiorodhesha kuwasilisha hoja yao kwenye chama hicho kutaka Katibu Mkuu wao, Dk. Wilbroad Slaa, awanie nafasi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani ambazo Nipashe imezipata wasomi hao kwa muda wa wiki kadhaa sasa wapo katika harakati za kukusanya majina ya wanachama wao ili kuwasilisha hoja yao kwenye chama.
Tayari orodha yenye majina 412 imewasilishwa kwenye chama ikitaka Dk. Slaa akubali kubeba jukumu hili zito ili kupeperusha bendera ya Chadema kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 31, mwaka huu.
Nipashe jana iliwasiliana na Dk. Slaa kumuuliza kama ana habari za harakati hizo na alisema hajui lolote.
"Kama kuna lolote tafadhali wasiliana na Mwenyekiti. Hayo ni mambo ya ndani ya chama," alisema Dk. Slaa ambaye hakuwa na muda mrefu zaidi wa kuingia kwenye mahojiano ya simu kwa sababu alikuwa akihudhuria vikao vya chama.
Dk. Slaa amekuwa mbunge wa Karatu tangu mwaka 1995 akiwa ni moja ya mihimili imara ya Chadema ndani na nje ya Bunge, lakini akiwa miongoni mwa wanasiasa walijizoelea heshima kutokana na msimamo wake wa kupambana na ufisadi na kutetea maslahi ya umma.
Kama Dk. Slaa atakubaliana na shinikizo la wanachama hao itakuwa ni mara ya pili kwa Chadema kumsimamisha mgombea urais tangu kufanyika kwa uchaguzi wa vyama vingi mwaka 1995.

CHANZO: NIPASHE




Sikonge Roho Kwatu He he he heeeeeeeee
 
Sasa kazi ni moja tu nayo ni kumnadi mgombea huyu makini. Kampeni mbele kwa mbele: mtaa kwa mtaa, nyumba kwa nyumba, chumba kwa chumba, kitanda kwa kitanda - mpaka kieleweke mwaka huu. Hongera Dr. Slaa! Tuko nawe.
 
Hata kama akiukosa urais atafanikiwa kuingiza upinzani bungeni kwa asilimia kubwa. CHADEMA...TANZANIA MPYA, MWANZO MPYA!!
 
Hii kwangu siyo habari ya kujivunia maana nafahamu kabisa umuhimu wa Slaa kuwa Bungeni umepotea. Nadhani lengo lake ni kupumzika ubunge kwa muda.

Ukombozi wetu ungeanzia Bungeni kwa CUF na CHADEMA kuingiza wabunge wengi. Ina maana nguvu yao kubwa ingeelekezwa kwenye Ubunge. Sasa tena turufu yetu inajitoa!
 
Kati ya watu waliopokea kwa furaha uamuzi wa Dr. Slaa ni pamoja na mimi, namjua Dr. Slaa ni mtu wa watu, mtu makini sana katika kazi zake, ana uchungu na nchi yake uchungu unaotoka moyoni si uchungu wa usoni.

Tanzania inahitaji mtu wa design hiyo, lakini yeye kama yeye si rahisi kuyafanya yote tunayotarajia, yeye katimiza haki yake iliyobaki ni sisi watanzania kufanya sehemu yetu kwa kumuunga mkono.

Inshallah Mungu najua atatutangulia, hata Obama wakati akitangaza nia watu wengi hawakuamini, kwanza kama atapitishwa na chama chake na baadaye kushinda uchaguzi lakini haiwi haiwi mwisho ikawa.

Let me tell you, nothing is impossible under the sun let us join our hands tutashinda.
Go Slaa Go.
 
Nilikuwa nimeamua kutopiga kura mwaka huu, lakini kwa mtaji huu, kesho naenda kwa Mtendaji kuhakiki kadi yangu.

./Mwana wa Haki
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom