Elections 2010 Dr. Slaa mgombea urais 2010 kupitia CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Hatujachelewa. Lipumba aende Sikonge au jimbo lolote analoona atashinda ili tuunganishe nguvu!
Halafu Lipumba wampe PM au waziri wa fedha, waangalie wenzao wa kenya wanavyo unga unga mpaka upinzani umefanikiwa.
Na sasa ziara ya Spain tutaikatisha sasa hivi.
 
Mkubwa
Sio wewe peke yako. Hata mimi nilikuwa nategemea waseme kitu fulani. Sio TBC tu, hata ITV kimya. Wanaogopa reaction ya boss wao?

Wananchi ndio wenye nchi; na watashinda tu. Zilikuwepo dola za kirumi na zikaanguka; sembuse hii CCM ya waswahili wa pwani, ya mipasho?
Hata Michuzi kimyaaaa!!
Utawatambua kwa matendo yao...
 
Pia mnatakiwa mjue kuna ubunge wa kuteuliwa, hivyo akiukosa wa karatu, bado anaweza ingia mjengoni. na lazima kwenye Uraisi tutie timu huko.
 
Hali ilikuwa hivi:

14jxds6.jpg

ayn2j7.jpg
 
Mkuu Invisible asante sana kwa hizo picha. Ninamtakia Kila la Heri Mzee Slaa na ninamuunga mkono kwa 100%!
 
hii tabia ya kuvaa KHAKI fatigues imetoka wapi,i thought this belonged to a bygone era associated mainly with countries of the eastern bloc.
 
Pia mnatakiwa mjue kuna ubunge wa kuteuliwa, hivyo akiukosa wa karatu, bado anaweza ingia mjengoni. na lazima kwenye Uraisi tutie timu huko.

Nani aliyekwambia mwaka huu kutakuwa na idadi kubwa ya wabunge wa Chadema ku-warrant kuteuliwa wengi? Wabunge wa kuteuliwa hawaiingii tu bungeni kwa miguu au kwa ku-drive. Kuna mchakato wake. Let us be realistic kwa level ya JF.
 
huu ni ujinga wa hali ya juu kutokana na system mbovu ya uchaguzi.kama uchaguzi ungekuwa wa haki hapo ningesifia maamuzi haya.

tumepoteza kichwa cha maana sana msimu wa bunge unao kuja,mijadala mizito yote sijui nani ataileta bungeni.
 
Kumbu kumbu zangu zinaniambia ni kama sijawahi kutoa comment/kuchangia mada zinazohusiana na mambo ya kiasiasa hapa JF, lakini kwa furaha niliyonayo leo inabidi niseme kitu.

Kwa hali ya kawaida (watu walivyolewa na CCM na kuwepo kwa tume ya uchaguzi ambayo imani ya baadhi yetu kwao ni ndogo), inawezekana kabisa mtu akasema Dr Slaa kushinda nafasi ya urais siyo kitu rahisi.

Hata hivyo kama kila mmoja akianza sasa kushawishi familia yake, ukoo wake, rafiki zake, majirani zake, tunaoabudu pamoja, wafanyakazi wenzetu miezi mitatu iliyobaki inaweza kabisa kuleta MABADIRIKO katika nchi hii ambayo CCM hawataamini kama kweli yametokea. Mimi binafsi na mke wangu tayari tunafahamu jinsi alivyo jasiri na mwenye moyo wa kupenda nchi hii Rais mtarajiwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr. Wilbroad Slaa.

Mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa lakini ni mpiga kura aliyejiandikisha, Mungu akitupa uzima kura yangu ameshaipata.
 
Yaelekea habari hii imekuchoma kumtima. Pole we!

Mkuu, wala! Yaani hata chembe ya hisia sina. Naangalia hali halisi ya TZ. Mabomu ya huyu jamaa aliyorusha na umaarufu wake alionao sasa hivi,,, ni mimi na wewe ndo twayajua. 90% hawako kabisa. Ndiyo maana yangu. Nipo hapa hapa JF kuelekea kwenye final whistle. Tutaongea...
 
Pia mnatakiwa mjue kuna ubunge wa kuteuliwa, hivyo akiukosa wa karatu, bado anaweza ingia mjengoni. na lazima kwenye Uraisi tutie timu huko.

Wanaume wanaweza kupata Ubunge wa kuteuliwa na Rais tu. JK akishinda uchaguzi hawezi kumteua Dr. Slaa kuingia mjengoni maana atakuwa anajipalia makaa ya moto. Viti vya kuteuliwa kwa upande wa Upinzani ni vya Wanawake tu, labda kama ikitokea yale makubaliano ya CUF na CCM kama jinsi Juma Duni Haji alivyoukwaa.

Pamoja na hayo, CHADEMA wanapokuwa na mgombea strong kama Dr. Slaa inawapa pia opportunity ya kupata support kubwa kwenye ngazi za Ubunge.

CCM hawakutarajia kama Dr. Slaa angekubali kugombea maana siku zote amekuwa akikanusha kwamba hana nia ya kugombea. Lakini nadhani pressure ya watu kumuomba agombee imemzidi na hivyo kuona haja ya kutaka kuwatumikia wananchi. Let us wait CCM's next move maana najua kwa sasa matumbo yanawachemka.
 
Chadema wana mpango gani au wamejiandaa vipi kusimamia wizi wa kura? manake wajue wamepoteza kichwa kikubwa sana bungeni na bila kufanya mpango makini wa kusimamia wizi wa kura kitachotokea ni kama miaka ya nyuma ni kulalamika tumeibiwa kura na hakuna hatua zozote zinafanyika.

nilikuwa nafuraha sana na chadema kuweka nguvu kwenye nafasi za ubunge sasa leo wanaenda kutoa kichwa chao kikubwa bungeni.
safari ndefu sana kwa wapinzani.

Naona sasa macho yote yatakuwa kwenye hio nafasi ya uraisi kuliko kwenye wabunge.
 
Kitendo cha vyombo vya habari kutotangaza hili japo kwa kuparaza na kwa wakati itawatokea puani. Hakuna uhuru kamili wa habari
 
Wanaume wanaweza kupata Ubunge wa kuteuliwa na Rais tu. JK akishinda uchaguzi hawezi kumteua Dr. Slaa kuingia mjengoni maana atakuwa anajipalia makaa ya moto. Viti vya kuteuliwa kwa upande wa Upinzani ni vya Wanawake tu, labda kama ikitokea yale makubaliano ya CUF na CCM kama jinsi Juma Duni Haji alivyoukwaa.

Pamoja na hayo, CHADEMA wanapokuwa na mgombea strong kama Dr. Slaa inawapa pia opportunity ya kupata support kubwa kwenye ngazi za Ubunge.

CCM hawakutarajia kama Dr. Slaa angekubali kugombea maana siku zote amekuwa akikanusha kwamba hana nia ya kugombea. Lakini nadhani pressure ya watu kumuomba agombee imemzidi na hivyo kuona haja ya kutaka kuwatumikia wananchi. Let us wait CCM's next move maana najua kwa sasa matumbo yanawachemka.

Kabla hatujasema mengi humu, labda tungefanya tathmini kutoka vijijini namna gani watu wamepokea habari hii, maana huko ndiko mtaji wa CCM uliko, sina tatizo na mjini. baada ya hapo angalau tunaweza kupata picha ya nini kitatokea.
Baada ya hii habari nilimpigia mmoja wa wana CCM, yeye anasema Slaa sio tishio kwa sababu Chadema haina network vijijini, tujadili hili pia
 
Bwa ha ha ha ha

Umepiga simu vijiji gani hivyo?

Hizi propaganda za sisiemu bana ..... zinawezekana mtaani sio JF
 
Angalau uchaguzi huu utakuwa na upinzani wa nguvu na tofauti..All the best Dr.Slaa!..Nafikiri tu nani atachukua karatu, eneo tata kisiasa!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom