Dr. Slaa, Mbowe waweka historia Kilombero!

Hongereni wana-Kilombero kwa kuwapa habari wakoloni weusi....Viva CHADEMA, Viva wana-Kilombero.
 
Hao walikuwa wamepata entertainment kabla ya futari, ulitaka wasiende?
 
Safi sana, halafi si mnaona wenyewe hakuna fujo hapo, wastaraabu watupu hadi raha... duh.
 
wanasaccos mpo au internet cafe zimeshafungwa? Nawasubiri niwape darasa inaoneokana upeo wenu bado finyu sana

Chama
Gongo la mboto DSM
 
DK.slaa anatetea gazeti la mwanahalisi kwa sababu yeye ndie aliekuwa mhariri mkuu wa gazeti hilo kwa kutumia jina la saed kubenea wakati akijua kwamba kubenea ni standard seven!
Pole mzee kwa kukufungia gazeti naomba umuombe Anton komu aliyekuwa mmiliki wa gazeti hilo aanzishe gazeti lingine.pole sana babuuuuuuu!utapata urais tu hata wa kigamboni tutakupa tu.
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA kimeacha historia ambayo ni vigumu kufutika katika uzinduzi wa operesheni Sangara kanda ya kati uliofanyika Ifakara-Kilombero jana.

Katika mkutano huo ulikusanyika umati mkubwa kuwahi kushuhudiwa katika wilaya hiyo kwa miaka ya karibuni.

Akihutubia maelfu kwa maelfu ya wananchi katika mkutano huo jana, ikiwa ni sehemu ya Operesheni Sangara awamu ya pili, Kiongozi mkuu wa upinzani nchini ambaye pia ni Katibu mkuu wa CHADEMA Dk.Wilbroad Slaa aliyeambatana na viongozi wakuu wa chama hicho, akiwemo Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Mbowe, alisema kuwa Serikali ya CCM imekuwa na kiburi cha kuwatisha wanaotaka kutetea maslahi ya wananchi huku ikifungia hata vyombo vya habari kama Mwanahalisi.

"Serikali ina nguvu ya kuvifungia vyombo vya habari kwa sheria dhalimu ya magazeti ya mwaka 1977, lakini kamwe haitaweza kuzuia kina Dr Slaa kupiga kelele'' alisema kiongozi huyo. Dk. Slaa ambaye alikuwa akishangiliwa kwa nguvu na halaiki hiyo huku anga likihanikizwa kwa kelele za RAIS....RAIS...RAIS...., aliongeza kuwa, kuanzia sasa CHADEMA itaanzisha mapambano kwa ajili ya haki ya Watanzania.

Akizungumza katika mkutano huo, Mbowe alisema umati uliokusanyika unaonesha namna wakazi wa Kilombero walivyomthamini aliyekuwa mbunge wa viti maalumu, marehemu Regia Mtema.

Mbowe aliomba jina la uwanja wa Ifakara libadilishwe na kuitwa Uwanja wa Ukombozi, na kwamba hali hiyo iwe chimbuko la ukombozi kwa Mkoa wa Morogoro.
Aliwataka wakazi wa Kilombero kuacha kulalamika na badala yake wachukue hatua kwa kuachana na CCM na kujinga na CHADEMA.

Katika mkutano huo maelfu ya wananchi walijiunga na CHADEMA wengi wao wakiwa ni kutoka CCM.Mara baada ya mkutano huo baadhi ya watu walionekana wakifuta machozi huku wakisema wanaamini bado siku chache tu CHADEMA kuingia madarakani na kukomboa watanzania kiuchumi.

Mbali na Dk. Slaa na Mbowe, viongozi wengine waliokuwa katika msafara huo ni Joshua Nassar (Arumeru Mashariki), Tundu Lissu (Singida Mashariki), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini), Hamad Yusuph (Naibu Katibu Mkuu Zanzibar), Suzan Kiwanga (Viti Maalumu), Joyce Mukya (Viti Maalumu) na wengine wa makao makuu.

Source: Majira/Tanzania Daima/Nipashe
Mkuu hiki cheo alipewa lini na nani? kama wewe ndio umempa rekebisha kauli yako na usiseme ...kiongozi mkuu wa upinzani nchini.!
 
Picha hizi zinadhihirisha ni kiasi molemo na kundi lake walivyokuwa wachovu hivi niwaulize kwa mnaokaa Kilombero baada ya saa kazi ngumu za kujenga Taifa kuna social activities gani? Hii mikutano watu na wanatumia kama ni sehemu ya outing tu hata wiki mh. Mrema akienda kuhutubia watajitokeza tu hawana cha kufanya baada ya saa za kazi, si Lema alijaribu Dare salaam, alishindwa hata nyie wapambe mnaoipiga kelele mlikuwa mnashindwa kuhudhuria kwa sababu Dar baada ya saa za kazi ni kujirusha. Na kama sio propaganda na uwongo ni kitu gani huo idadi hiyo kwa molemo imekuwa ni historia kweli watu nyie mna vituko hebu niambieni idadi ya watu wa Kilombero .
Chama
Gongo la mboto DSM
Chama umesoma vibaya vibaya hali ya kisiasa inayoleta mikusanyiko ya watu wa sehemu Kama kilombero. Itakua hatari iwapo wapanga mikakati wa CCM nao wanafikiria Kama wewe. Katika siasa hakuna kazi iliyongumu na kubwa Kama kukusanya WATU ili wakusikilize.(Nape anajua anajua kiasi cha pesa na matumizi ya shuruti na sababu za kutega mikutano kwenye masoko katikati ya miji). Kwa hali ilivyo CCM inahitaji badiliko la haraka la kimkakati kukabiliana na uwezekano wa kushindwa vibaya kwanye uchaguzi ujao. Kwa ushauri CHAMA CHA MAPINDUZI kinatakiwa kirudishwe kwa "wenyewe" ambao ni vijana wengi wao walipitia chipukizi na JKT ambao walijifunza katiba ya CCM Kama sehemu ya mitaala Yao shuleni na Wazalendo wa kweli. Hawa wakina Nape, Mwigulu n.k nawaona Kama wadandiaji wa "gari la baba" wasio na misingi wala upeo wa kukabiliana na wimbi la wanasiasa Kama Mnyika, Lissu n.k
 
DK.slaa anatetea gazeti la mwanahalisi kwa sababu yeye ndie aliekuwa mhariri mkuu wa gazeti hilo kwa kutumia jina la saed kubenea wakati akijua kwamba kubenea ni standard seven!
Pole mzee kwa kukufungia gazeti naomba umuombe Anton komu aliyekuwa mmiliki wa gazeti hilo aanzishe gazeti lingine.pole sana babuuuuuuu!utapata urais tu hata wa kigamboni tutakupa tu.

So mmelifungia ili kumkomoa Dr. slaa?:wacko: Tume yenu itatoa lini Majibu?au ndiyo vijana wako jikoni?mkimaliza tutaomba na behind the scene.....:israel:
 
Picha hizi zinadhihirisha ni kiasi molemo na kundi lake walivyokuwa wachovu hivi niwaulize kwa mnaokaa Kilombero baada ya saa kazi ngumu za kujenga Taifa kuna social activities gani? Hii mikutano watu na wanatumia kama ni sehemu ya outing tu hata wiki mh. Mrema akienda kuhutubia watajitokeza tu hawana cha kufanya baada ya saa za kazi, si Lema alijaribu Dare salaam, alishindwa hata nyie wapambe mnaoipiga kelele mlikuwa mnashindwa kuhudhuria kwa sababu Dar baada ya saa za kazi ni kujirusha. Na kama sio propaganda na uwongo ni kitu gani huo idadi hiyo kwa molemo imekuwa ni historia kweli watu nyie mna vituko hebu niambieni idadi ya watu wa Kilombero .

Chama
Gongo la mboto DSM
Dhana ya 'kujirusha" ndo maana mwendo ni TOT,kanga na pilao.
 
Mungu amesikia kilio cha watanzania na sasa ameleta hamasa ya ajabu kwa watanzania walalahoi kuhakikisha kwamba 2015 ccm inajifia
 
Dhana ya 'kujirusha" ndo maana mwendo ni TOT,kanga na pilao.

jmushi1
Unaishi dunia gani? acha unafiki kujirusha ni sehemu ya maisha kila siku si lazima uende baa unaweza kwenda kucheza bao na shughuli nyingine za kustarehesha; huyo Dr. Slaa angekuwa hajui kujirusha hadi leo hii angekuwa padri. Au leo umesahau mh. Mbowe shuguli zake?

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Chama umesoma vibaya vibaya hali ya kisiasa inayoleta mikusanyiko ya watu wa sehemu Kama kilombero. Itakua hatari iwapo wapanga mikakati wa CCM nao wanafikiria Kama wewe. Katika siasa hakuna kazi iliyongumu na kubwa Kama kukusanya WATU ili wakusikilize.(Nape anajua anajua kiasi cha pesa na matumizi ya shuruti na sababu za kutega mikutano kwenye masoko katikati ya miji). Kwa hali ilivyo CCM inahitaji badiliko la haraka la kimkakati kukabiliana na uwezekano wa kushindwa vibaya kwanye uchaguzi ujao. Kwa ushauri CHAMA CHA MAPINDUZI kinatakiwa kirudishwe kwa "wenyewe" ambao ni vijana wengi wao walipitia chipukizi na JKT ambao walijifunza katiba ya CCM Kama sehemu ya mitaala Yao shuleni na Wazalendo wa kweli. Hawa wakina Nape, Mwigulu n.k nawaona Kama wadandiaji wa "gari la baba" wasio na misingi wala upeo wa kukabiliana na wimbi la wanasiasa Kama Mnyika, Lissu n.k

Chama kinarudi kwa wenyewe hilio halina tatizo na hakuna kushindwa kwenye uchaguzi

Chama
Gongo la mboto DSM
 
jmushi1
Unaishi dunia gani? acha unafiki kujirusha ni sehemu ya maisha kila siku si lazima uende baa unaweza kwenda kucheza bao na shughuli nyingine za kustarehesha; huyo Dr. Slaa angekuwa hajui kujirusha hadi leo hii angekuwa padri. Au leo umesahau mh. Mbowe shuguli zake?

Chama
Gongo la mboto DSM
hapana unakuwa mgumu kuelewa,unachanganya madawa hapa,sasa hilo la kujirusha linawasaidia kuwapata wananchi wengi kwenye mikutano yenu ya kujirusha?Una uhakika wananchi hawaufuati na kuupata ujumbe kwenye mikutano ya chadema?
 
Ndugu yangu unachokifanya wewe ni kupiga konzi mkuki, hapa JF jukwaa la siasa anayeongoza kwa ujinga ni huyo Chama, wenzake kina Ritz wamebadilika na wanachangia kiuweledi kiasi, lakini huyo hamna kitu ndio wale wale saa 7 usiku.
 
Nadhani wewe ndio umekuwa mgumu wa kuelewa usichanganye maneno rudia kuisoma posti yangu usitie kauli yako kwenye kinywa changu, hata mikutano ya Chadema wanapiga nyimbo za kuwaburudisha wasikilizaji kabla ya mkutano haujaanza rasmi.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Ndugu yangu unachokifanya wewe ni kupiga konzi mkuki, hapa JF jukwaa la siasa anayeongoza kwa ujinga ni huyo Chama, wenzake kina Ritz wamebadilika na wanachangia kiuweledi kiasi, lakini huyo hamna kitu ndio wale wale saa 7 usiku.

matola huna nyimbo vipi umerudi Malawi? Hapa ni watanzania tunajadili siasa za Tanzania

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Molemo akili yako finyu sana hivi Kilombero ina wakazi wangapi mpaka iweke historia ambayo haiwezi kufutika katika Taifa ambalo linawakazi takribani mil. 40? historia ambayo haiwezi kufutika ni Dr. Slaa na wenzake kuigeuza Chadema saccos mkumbushe deni alilikopa saccos linatkiwa lilipwe.

Chama
Gongo la mboto DSM
Namwombea msamaha aliyetukanwa (hapo kwenye red), lakini pia Mkuu, uwe unatusamehe tunapotoa maoni yetu, tusitukanwe hivyo!!!! Najua unaipenda nyinyiemu, lakini pia, mwenzako ameweka hata picha kukuonesha kuwa chama anacho kipenda, kinakubalika na wengi. Matusi ya nini???? Soma alama za nyakati, ikikubidi jiunge na wengi. "Wengi wape." Hata wewe hukuzaliwa na nyinyiemu, wenzako wamekwisha liachia, unang'ang'ania la nini????? Achia lisikufie.
"Huu ndiyo ushauri wangu kwako"
 
Back
Top Bottom