- Thread starter
- #61
Songa mbele Jembeeezzzzz!! eti sasa hivi wanaombea uzeeke haraka, ustaafu!
Mkuu Mzizi wa Mbuyu watazeeka wao huku Kamanda Dr Slaa akizidi kutikisa.
Last edited by a moderator:
Songa mbele Jembeeezzzzz!! eti sasa hivi wanaombea uzeeke haraka, ustaafu!
Yule mama yake wa kambo wa LEMUTUZ atakuwa keshatia timu kutengeneza mambo,mama mchawi sana yule
Mkuu Kanundu acha kuvua watu nguo.
Mkuu Communist watu wanaoimba migogoro na makundi ni mawakala wa Magamba wanaotumwa hapa JF kuchochea mambo ambayo hayapo.
Nimeshangaa kuna mtu mmoja anajiita mwanachadema anaitwa Tuko kaanza kuleta mambo ya CCM hapa eti Chadema ina makundi.
Wao wakipika majungu mtandaoni Dr Slaa yuko busy kuimarisha chama vijijini.
C.c Mwita Maranya, SEBM, Shardcole, Crashwise, Mungi, Ben Saanane.
Molemo
Mkuu Kanundu acha kuniharibia siku mkuu wangu.
Mkuu Communist watu wanaoimba migogoro na makundi ni mawakala wa Magamba wanaotumwa hapa JF kuchochea mambo ambayo hayapo.
Nimeshangaa kuna mtu mmoja anajiita mwanachadema anaitwa Tuko kaanza kuleta mambo ya CCM hapa eti Chadema ina makundi.
Wao wakipika majungu mtandaoni Dr Slaa yuko busy kuimarisha chama vijijini.
C.c Mwita Maranya, SEBM, Shardcole, Crashwise, Mungi, Ben Saanane.
wana Same tunamuomba Dr.W.Slaa atembelee eneo la Chome ambako kuna uharibifu mkubwa wa mazingira kutokana na mradi wa uchimbaji wa madini ya bauxite. tunaiomba Chadema iliangalie suala hili kwa umakini zaidi kwasababu mazingira ya msitu wa Shengena ambao ndiyo chanzo cha maji kwa wilaya nzima ya Same yanaathiriwa kwa kiasi kikubwa. athari za uharibifu huo wa mazingira umeanza kuonekana katika mto Saseni.
tunawaomba CHADEMA waliwasilishe tena suala hili BUNGENI, pamoja na kwa wanaharakati wa mazingira ndani na nje ya nchi. suala hili lilifika bungeni ambapo mbunge wa Same Mashariki, Mama Kilango Malecela alidai ana video zinazoonyesha uharibifu wa mazingira msitu wa Chome. WAZIRI MKUU alitoa amri bungeni kwamba uchimbaji wa bauxite usimamishwe, kitu ambacho kilifanyika. Muda mfupi baada ya kikao cha bunge kuisha, mwekezaji amekwenda baraza la mazingira na kupata barua ya kutengua agizo la Waziri Mkuu, na sasa hivi uchimbaji unaendelea kwa kasi ya kutisha.
Wananchi tunataka kujua huyu mwekezaji ametoa wapi kiburi cha kutengua amri na maagizo ya Waziri Mkuu? Je, kwanini Waziri Mkuu, Waziri wa Mazingira, pamoja na wabunge wa Same[Malecela, Mathayo] wote wamekaa kimya huku maisha ya wananchi yakiathirika kiasi hiki? Je, viongozi hao wamenunuliwa?? Serikali iko wapi? CCM iko wapi?
Kwasababu wabunge wa CCM wameshindwa kutusaidia wananchi wa Same sasa tunaomba msaada wa Chadema tuone na nyinyi mtatusaidia vipi.
nakala: Zitto, John Mnyika, Mikael P Aweda, Josephine, Molemo, Mwita Maranya, Edwin Mtei, MTENGETI, Nape Nnauye
Kiongozi Mkuu wa Upinzani Nchini ambaye ni Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Peter Slaa anatarajiwa kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara mjini Hedaru-Same Jumanne tarehe 15 January 2013.
Mbali na kuhutubia mkutano wa hadhara Dr Slaa anatarajiwa pia kupokea wanachama wapya wa Chadema,kufungua ofisi za Chadema kata ya Hedaru na kuzindua matawi ya Chadema maeneo ya Hedaru,Makanya na Same.
Tayari mji wote wa Same na vitongoji vyake kuna gumzo kubwa kuhusu Ujio huo wa Dr Slaa ambaye anaonekana kama kiongozi aliyevuka vizingiti vingi vya mahasimu wake huku nyota yake ikizidi kung'aa kila siku kuelekea mwaka 2015
Kwa sasa Katibu Mkuu huyo amejichimbia mkoani Kilimanjaro akiongoza vikao vizito vya Sekretariati yake ikiwa ni maandalizi ya operesheni kubwa ya kuimarisha chama chake kwa mwaka huu.
Hivi nani anachagua Kiongozi Mkuu wa Upinzani? Hivi vyeo vinatoka wapi? Kama kuna Kiongozi Mkuu wa Upinzani je naweza kuruhusiwa kusema Kiongozi Mkuu wa Utawala ambaye ni Rais wa Jamuhuri anatembelea China?
Kama imekuuma mkuu wangu kanywe mataputapu ulale
View attachment 79190
Hali sio nzuri hospitali ya wilaya, hapo ni maternity ward kina mama wanalala mzungu wa nne kwenye single bed.
Mkuu Molemo!
Kazi iliyoko mbele ya CHADEMA ni kukoboa na kusaga. Hii habari ya hao walio zoea mipasho ya TOT kama Mwenyekiti wao tuachane nao Mkuu. Kwanza kuchangia mada zao ni kuwapa ujiko. Tukizi puuza watakosa la kuzusha na kuandika.
Tafadhali Mkuu, tunaomba utupatie yaliyo makini na ya kujenga chama. Mengine acha "WAFU WAZIKE WAFU WAO".