Dr. Slaa bado anayo kadi ya CCM?


sifa kuu ya mwanachama ni kuwa na kadi .
hayo mengine unauajua wewe.
kabla hujaendekea kutoa povu naomba tushirikiane hiki kibwagizo cha kotide!
slaa anaweza anaweza anawezaaaaa iyo iyooooo anaweza sanaaa kumnadi mwakyembe 2010 na kumuacha eddo mgombea wa chadema anaweeeezaaaa iyo iyooooo anaweza sanaaaaa
 


Mkuu umeniacha hoi

Kumbe kwako kusafiri ndani ya ndege ni kuwa na ticket, hajalishi ni valid au la! ime-expire au hapana wala ya lini nakama

imetumika au hapana kwako sio tatizo! Je unataka tuamini hivyo mkuu kwamba kadi ni kadi tu chamsingi rangi?
 

Huyu mwandishi ni mmojawapo wa wale waandishi uchwara wa magazeti ya Magamba (Uhuru na Mzalendo). Kwanza sio raia wa Tanzania, ni Mrundi ndo maana anajipendekeza kwa magamba ili asifutiwe uraia. Na huyu Katibu aliyesimamishwa ameshanunuliwa na magamba hafai tena kuwa mwanachama wa chama cha ukombozi wa Mtanzania (CDM). Huyu hana tofauti na Shibu
 
Hawa jamaa walitaka Dr aseme kuwa hana hiyo kadi ili wamtuhumu kwa uongo, lakini yeye amekuwa muwazi kabisa na hapo ndipo alipowafunga mdomo sasa wanaanza kutapatapa. Watu kama Dr ndo wanatufaa kwa ukombozi wa kweli kwasababu hawana hila, ni wakweli daima hata katika yale mambo magumu hawayumbi, wana misimamo. Big Up Dr.
 
Akili za watu bwana! Hivi kudai Slaa ana kadi ya CCM ndiyo jibu la umaskini na ufisadi Tanzania? Akili ndogo kuongoza akili kubwa, ama kweli. Tukiendelea kucheka na nyani (chama cha majambazi) tutavuna mabua.
 

Umesema vema, walidhani na kufikiri kwa ukilaza wao, Dr wa ukweli kawapiga bao.
 
Labda niongeze hili: kwamba kila mwanaM4C mwenye umri mkubwa--kama say alikuwa miaka kati ya 18 hadi 25 mwaka 1977 lazima atakuwa na historia ya uanachama wa CCM.

Tulikuwa tunalazimishwa kujiunga na chama hiki ili kupata huduma za jamii, kupata migao ya bidhaa muhimu katika maduka ya umma, kupata elimu ya juu ama ajira katika serikali. Kwa hiyo watakuwapo wengi sana wanazo kadi za CCM bila itikadi ya CCM kuwapo katika mioyo yao.

Dr. Slaa ni huo umri wa sisi tuliokuwa tukilazimishwa kadi za CCM. Mimi ninayo hiyo kadi darini somewhere..... Kajisuvenier ka kiaina. What is wrong with that.....

Labda tuwaombe vijana kuelewa hili: kwamba M4C inachanganya watu wa zamani sana na wao--yaani vijana. Na hakuna mwenye uwezo wa kuchange past. Can anybody change the past? The answer is no....


kinachonitatiza kwenye hili ni kwamba, ALIYETOA SHUTUMA ZA KADI YA DR. SLAA NI NAPE AMBAYE YEYE ALIKUWA ANAANZISHA CHAMA CCJ NA WAKATI YUPO CCM sasa kati ya hao nani mnafiki? Na nadhani kila mtu anajua kwamba Dr. Slaa alikuwa ni mwanachama wa ccm
 

Magamba mnamatatizo kweli kweli yaan mmemlipia jamaa nauli kuja dar kujakuongea huu utumbo?Na aliojiwa na magazeti haha tu uhuru,majira na habari leo Vipi TBC1 walicover tukio? Kajipangeni upta!
 

Amrudishie nani? Kikwete? Aichane tu hadharani nyoyo za wanachama zitulie. Yote ni propaganda za kuchafuana tu. Nina ya kwangu ya CCM kwani kuna sharti la kuirudisha? Tangu nimejiunga CDM mbona hawajanidai kadi yao? Sijailipia miaka 33 iliyopita!
 

Waandishi wa habari wana muda sana, wanaandiika habari hazina mantiki wala maana
 
Sisi tumeridhika jamaa kuwa mamluki na nilitarajia iwe furaha kwenu kwani anafanya kazi bila kushtukiwa na mtu yeyote
SWALI ni ili kama kweli Dr ni kibaraka cha ccm ndani ya CDM y ss nyie(ccm) ndo iwaume?
2.uliona wapi jeshi linamtuma komando akapeleleze maadui thn jeshi iloilo limtangaze hadharani(we binafsi huoni kama ni utoto uo) Binafsi naona kama mwampigia Mbuzi gitaa acheze kwani kwa watu walioenda shule cdhani kama ii mada inaingia akili...kajipange upya kesho uje na nyingine
 
Jiulize wewe katibu mfukuzwa umekifanyia nini au nini mchango wako kwa chadema na Dr. Slaa amekichangia kiasi gani chama kisha utaweza kupambanua mamliki ni nani kati yako na Dr, Slaa.
 
Naona jamvi limeingiliwa na hawa jamaa wa mabwepande!...suala Dkt kuwa na kadi yake ya ccm si muhimu katika jamvi hili, kila mtu anafahamu fika kuwa Dkt aliwahi kuwa mwanachama na baadaye akatoka na kujiunga na CDM, sasa suala lakuwa na kadi yake ya zamani ambayo haitumii zaidi ya kuwa kumbukumbuyake binafsi. Ninahisi kuna watu wametumwa na Nape humu au wanajipendekeza, wanasahau kuwa kuna masuala mengi muhimu kwa mustakabali wa taifa, na hayajapatiwa ufumbuzi. Tuache kujadili watu binafsi na badala yake twende katika issues
 
teh teh...nani kakuambia hapa tunashindana kiingereza?hapa tunahitajia ushahidi na si majungu.Usiwe mpuuzi kiasi hicho.Unakua kama mtu anayekimbiza mwizi halafu anampita na baadaye kudai kwa mbwembwe kuwa kamshinda mwizi kukimbia badala ya kumshika.Sasa ulidhani English proficiency ndio inahitajika thibitisha umbea wako kuhusu Dr. Slaa.?hadi hapa matusi uliyotukana huna hata moral authority ya kumnyooshea kidole mwizi au hata mzinzi.

Nina mashaka sana na Jinsia yako na mchanganyiko wako wa hormone .Km upo comfused siwezi shangaa.Huwezi jisifia kitu kingine wakati issue ni nyingine sana.Lugha, na vitu vidogo vya apperance?Unaoga mara ngapi kwa siku?

If my I IQ is that low and below the average, then you would be somewhere in a the left side of Zero.
 

So much for your chademic IQ.
See no wrong, hear no wrong Dr Slaa rules your airwaves.
Long live your mentor.

To the rest of us you are one person rotting for lack of intellect.
 
Tuache kujadili watu binafsi na badala yake twende katika issues

Dr Slaa alihamia CDM baada ya kuenguliwa kwenye kura za maoni za CCM! Kwa hiyo itakuwa aliondoka kwa hasira tu za kukosa uongozi ila sio kukichukia chama. Tusidharau huenda anataka kumaintain number ya kadi yake ya CCM. Kwani ni wapinzani wangapi walikuwa wapiga debe wa upinzani na kuikomalia CCM mwisho wa siku wakarudi kule kule walikotoka? CDM msidharau, mfuatilieni DR Slaa mumchunguze asije siku moja akavua gwanda akavaa gamba!
 

Leo tena nimeamini bila shaka yoyote, kwamba huyu bwana W.Malecela, Le Mutuz, Le baharia ndiye huyu huyu "Field Marshall ES".
Nimejaribu ku-recall uzi fulani huko nyuma ambao alipata kumshambulia sana Dr. Slaa na Mhe. Mbowe na mara kwa mara alipenda kutumia neno "
mediocre".
Tabia ya mtu huwa haijifichi. Hata kama angejibadiri sura, lakini tabia ataionesha tu hadharani bila kukusudia.
 
If he is working 100% for the interests of Chadema, and 100% against the interests of CCM then who cares!

That is why CCM are making all these noise. And all great thinkers know that he is feared and hated by CCM for that!

Are you proud to have someone with your card who is damaging your party?
 

Mkuu, kwani ni dhambi mtu akirudi alikotoka? Au katiba ya Tz hairuhusu?
Suala siyo kumfuatilia, bali ni namna Dr. anavyojitoa katika kukijenga chama.

CDM siyo baba na mama wa Dr. Slaa. Aliingia kwa mapenzi yake na akitaka kutoka atatoka kwa mapenzi yake, lakini si kwa mashinikizo ya wanasiasa vijana uchwara kama huyo Edo ambaye anaongea hadi povu linamtoka hadi kushindwa kuwatofautisha Dr. W. Slaa na Mzee Peter Slaa. Halafu naye anajiita mwanasiasa mwenye kundi la watu nyuma yake.

Only in Tanzania, one can find such useless young politicians who can't contemplate political issues logically.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…