Mimi ni mgeni humu jamvini, lakini naomba wanaJF mniruhusu nichangie kidogo huu uzi kama ifuatavyo-
Ndugu Edo Mwamalala, napenda nikuulize swali dogo tu, mtu kumiliki kadi ya ccm ndio indicator ya kupima kuwa ni mamluki wa CCM? Matendo ayafanyayo mtu katika kukiendeleza na kukiimaisha chama ndio kiwe kipimo. Kumbuka kuwa majority ya wanachama wa vyama vya upinzani wametokea chama tawala na hivyo kuna uwezekano mkubwa wengi wao, MIMI nikiwa mmoja wao bado tunazokadi za ccm. Lakini ni wanachama wafu. Huenda hata wewe bado una kadi za chama cha kijani kama vile kadi ya umoja wa vijana nk. Mimi kwa upande wangu hata sikumbuki niliihifadhi wapi hiyo kadi ya kijani na huenda imeshaliwa na panya au mende! Ila kadi yangu ya chama kitukufu cha sasa(CHADEMA) ndio iko kwenye waleti yangu na ndio ninailipia ada za uanachama. Hata huyo mpuuzi Nape anamilki kadi ya CCJ na kadi ya ccm, hivyo apuuzwe. Mamluki wa CCM ndani ya CHADEMA utawagundua kwa matendo yao ya kujipendekeza kwa JK na CCM kama wafanyavyo ZITTO na SHIBUDA. Dr Slaa amefanya mengi katika kuimarisha CHADEMA. Kwa sasa CDM imefungua kata, matawi na mashina mengi sehemu mbalimbali nchini tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma. Maendeleo hayo yanawapata kiwewe magamba ndio sababu kila kukicha hawaishi kumtafutia kashfa Dr. Slaa. Lakini wameshachelewa kwani current more than 55% ya Watanzania wameshatambua kuwa CCM ni pumba na CHADEMA ni mchele. 2015 Kura za Urais, Ubunge, Udiwani ni kwa CHADEMA. Mwisho kabisa naomba WANACHADEMA makini tusiyumbishwe na magamba akiwemo NAPE. Dr. Slaa anawanyima usingizi hawa magamba, usiku kucha hawalali bali nikumuwaza Dr. wetu wa ukweli. Big up sana Dr. Slaa na WANACHADEMA!!!