- Thread starter
- #81
Unapojadili kitu chochote ukiwa huna proper evidence au facts haumtendei haki muhusika.Na suala kama hili kwanza lilitakiwa liulizwe mwenyewe kwanza ili tumtendee haki.
Wajua twaweza kuepusha mengi kama tukiwatendea haki hawa tunaowaita Public Figures ,wengi wao wameishia kutukanwa kwenye mitandao mpaka matusi ambayo yanaudhi sababu tu hakuna upande wa pili wa muhusika kujitetea.
Kama Dr.Slaa halipi kodi hili si kosa lake ni kosa la mwajiri wake kutomkata kodi husika kwani PAYE inapelekwa TRA na muajiri.Je kaka unauhakika aliyeleta mada anazodocuments zinazoonyesha Dr.Slaa kudai madai mengine ya mshahara?Je gari ni la ofisi yaani la CDM ni kiasi gani analitumia kwa safari binafsi?
Je Ofisi inaweza kuziainisha safari binafsi na za kikazi?Tusije tukawa tunalumbana kumbe safafri binafsi ni asilimia 10 tu ya safari zote.
Ni vizuri kuzijadili issue za viongozi wetu lakini tuwe na mipaka na evidence vinginevyo sidhani kama tunawatendea haki kwa kuweka tu information zao hata kama ni za uwongo.Wakati tunawalazimisha wanasiasa wawe wa kweli tuanze na sisi kuwa wakweli.
Dr Slaa ni member active humu JF. Uwa anakuja kukanusha taarifa za uongo zinazomuhusu yeye. Hivyo basi, ukiona kimya kingi ujue msumari umegusa mfupa na Dr Slaa hana la kukana katika hili.