Wana Ukumbi,
Katibu mkuu wa CHADEMA, Dr Slaa, ametoa madai mapya ya kuongezewa mshahara na stahiki zake kufuatia mafanikio aliyoyapata ya kuongezewa mshahara katika madai yake yaliyopita ambayo yalikuwa ni ongezeko la asilimia 40 tu ya kile kiwango alichokitaka!
Mchanganuo sahihi wa mshahara wa katibu mkuu wa CHADEMA na stahiki zake:
Mshahara anaolipwa Dr Slaa kwa sasa ni Tshs. 9,300,000 kwa mwezi wakati kabla ya madai yake ya mara ya mwisho alikuwa akilipwa Tshs. 6,600,000. Ambalo ni ongezeko la 40%.
Stahiki za Dr Slaa kama Katibu Mkuu:
Dr Slaa anawekewa kiasi cha lita 1000 za mafuta ya Petrol kila mwezi ambayo kwa wastani ni Tshs milioni 2,000,000 katika gari lake alilokabidhiwa na chama ambalo pia ulitumia kwa shughuli zake binafsi na za chama. Ifahamike, hii ni nje ya mshahara!
Haijaishia hapo, Dr Slaa pia anapewa pesa kiasi cha Tshs 2,500,000 kama fedha ya matumizi ya ofisi ya katibu mkuu wa chama kila mwezi. Hii pia ipo nje ya mshahara wake na matumizi yake hayaeleweki.
Kama hiyo haitoshi, Dr Slaa kila afanyapo vikao vya chama vya ngazi mbalimbali uinuka na wastani wa Tshs. 1,500,000 kwa kikao kimoja.
Madai Mapya:
Mshahara: Dr Slaa kwa sasa ameitaarifu CHADEMA kuwa wakati wa kukamilisha asilimia 60 zilizobaki za madai yake ya awali ya mshahara wake umewadia. "Hii ni kutokana na ongezeko la gharama za maisha na pia kuongezwa mkataba wa kutumikia chama kwa nafasi ya ukatibu mkuu" alieleza Dr Slaa.
Hivyo basi, kama CHADEMA itaridhia madai hayo mapya na kumuongeza Dr Slaa kiasi cha asilimia 60 kilichobaki, Dr Slaa ndiye atakuwa katibu mkuu wa chama cha siasa anayelipwa pesa nyingi kuliko wote katika nchi za ukanda wa Afrika mashariki! Kiasi hicho kitafikia Tshs. 13,200,000 kwa mwezi huku kikienda sambamba na kuongezeka kwa posho na stahiki zingine.

Habari hii, kama zilivyo nyingi za wapinzani wa CHADEMA (CCM and its cronies) hazina ukweli wowote zaidi ya kuendeleza mradi wa kufanya diversion na kuwa-keep busy watu makini kulazimika kuangalia na kujadili propaganda muda wote huku masuala muhimu yanayohusu wananchi yakionekana kuwa side issues...
Kwa sababu upuuzi kama huu unakuwa unaendekezwa katikati ya mijadala muhimu, kuna wakati tunalazimika kutopuuza kama tunavyopuuza upuuzi wao mwingi kama huu.
Katibu Mkuu Dk. Slaa hajatoa sharti wala dai lolote katika kutumikia nafasi hiyo ambayo kila Mtanzania makini na maisha yake (anayefuatilia siasa) anajua amekuwa akiitumikia kwa uwezo, weledi, utayari na uadilifu wa hali ya juu.
Tangu ameanza kutumikia nafasi hiyo hajawahi katika wakati wowote ule wa utumishi wake kutoa sharti au dai kwa ajili ya kutoa utumishi wake kwa Watanzania kupitia CHADEMA.
Mshahara wa Katibu Mkuu wa CHADEMA unajulikana. Summa umewahi kuelezwa kwa kinagaubaga hapo nyuma wakati mjadala wa upotoshaji kama huu ulipoibuka.
Kama watu wale wale kwa malengo yaleyale wamerudisha tena upotoshaji wao wakati huu, kisha wakaruhusiwa kuweka uongo huo hapa, kisha ukaendelea kuwepo basi tuko tayari kurudia ufafanuzi ule ili Watanzania wasiendelee kulazimika kujadili taarifa potofu wakati kuna masuala ya msingi sana kwa sasa.