Madama gashimba
JF-Expert Member
- Aug 13, 2012
- 321
- 118
Poorest Tanzanian ktk uwezo wa kufikiri, hivi huyu mtoa maada anajua kuwa kuna suala la kujiandikisha kwny daftari za kudumu akapost kitu kinacholenga kuchafua cv ya mtu bila vidhibitisho?
Waziri mkuu pinda aliliambia bunge analipwa 3,000,000+ alafu katibu wa chama awe analipwa 9,000,000 !!!???
mkuu tuliambiwa hapa zamani kwamba kabla ya kuchukua nafasi ya Ukatibu Mkuu, Dr. Slaa alitoa sharti la kulipwa stahili zote ambazo alikuwa anapata akiwa Mbunge. Lakini leo unasema hajawahi kutoa sharti lolote. Kuna ukweli hapo?Habari hii, kama zilivyo nyingi za wapinzani wa CHADEMA (CCM and its cronies) hazina ukweli wowote zaidi ya kuendeleza mradi wa kufanya diversion na kuwa-keep busy watu makini kulazimika kuangalia na kujadili propaganda muda wote huku masuala muhimu yanayohusu wananchi yakionekana kuwa side issues...
Kwa sababu upuuzi kama huu unakuwa unaendekezwa katikati ya mijadala muhimu, kuna wakati tunalazimika kutopuuza kama tunavyopuuza upuuzi wao mwingi kama huu.
Katibu Mkuu Dk. Slaa hajatoa sharti wala dai lolote katika kutumikia nafasi hiyo ambayo kila Mtanzania makini na maisha yake (anayefuatilia siasa) anajua amekuwa akiitumikia kwa uwezo, weledi, utayari na uadilifu wa hali ya juu.
Tangu ameanza kutumikia nafasi hiyo hajawahi katika wakati wowote ule wa utumishi wake kutoa sharti au dai kwa ajili ya kutoa utumishi wake kwa Watanzania kupitia CHADEM A
Mshahara wa Katibu Mkuu wa CHADEMA unajulikana. Summa umewahi kuelezwa kwa kinagaubaga hapo nyuma wakati mjadala wa upotoshaji kama huu ulipoibuka.
Kama watu wale wale kwa malengo yaleyale wamerudisha tena upotoshaji wao wakati huu, kisha wakaruhusiwa kuweka uongo huo hapa, kisha ukaendelea kuwepo basi tuko tayari kurudia ufafanuzi ule ili Watanzania wasiendelee kulazimika kujadili taarifa potofu wakati kuna masuala ya msingi sana kwa sasa.
Dada yangu,
Nakupongeza sana kwa hiyo hoja ya ku-burgain mshahara!
Kuna kitu nadhani una-miss kwenye hii mijadala inayohusu maslahi ya viongozi. Sijui ni kutokana na ugeni wako kwenye mitandao ya kijamii au kuna sababu zingine.
Miaka ya nyuma kidogo katika hii mijadala, Dr Slaa alikuwa akilaumu sana viongozi waandamizi wa serikali wanavyolipwa mishahara mikubwa huku wakiifanya siri!
Hapa alimjumuisha Rais, Makamu wa rais, Waziri mkuu, Spika na jaji mkuu.
Sasa mtu wa aina hiyo ambae kabla hajapata nafasi ya ukatibu mkuu alikuwa akisema kuwa mishahara ya viongozi inanyonya hazina, je iweje leo mtu huyo huyo ambae ameipata nafasi ya ukiongozi ndani ya chama atumie fursa hiyo kujipandishia mshahara tena mpaka ifike Tshs. 13 milioni!?
Huu ni undumi la kuwili na mtu wa aina hiyo usitarajie afanye mabadiliko yoyote yale hata akipewa nchi.
mwongo mkubwa.unafikiri watu wote wajinga kama wewe?
mkuu Tetty Dr. Slaa ni public figure, Dr. Slaa anapigiwa chapuo kuwa Rais wa nchi. Kwa mantiki hiyo sioni ubaya kujadili suala hili. Shida yangu ni ukweli wa hizi habari. Kama habari ni za ukweli basi hatuna budi kujadili hakuna cha privacy kwenye suala linalomhusu kiongozi ambaye tunasema anafaa kuwa Rais wa nchi na huenda akapitshwa na UKAWA kuwa mgombea.Ninauelewa vyema ninachokiongea,si kwamba si kielewi au kwa sababu ni mgeni wa mitandao ya kijamii la hasha.Mitandao ya kijamii inatakiwa iongelee masuala nyeti ya nchi yetu na si kuongelea watu.Kama Dr.Slaa amebargain mshahara wake na iwe kwake si kwetu.Waje walalamike waajiri wake na si watu wengine.Kama aliwalaumu viongozi wengine basi aende akaulizwe yeye Dr.Slaa kuwa wakati fulani au tarehe fulani uliwalaumu viongozi kwa suala hili na hili,vinginevyo kupamba infomation za watu binafsi kwenye mitandao si vyema.
Kama umeshindwa kwenda kumuona USO kwa USO basi usimseme nyuma ya mgongo wake.Nenda kamuulize majibizano yenu yaleteni kwenye mitandao lakini usimshtumu mtu ukiwa hata proper information huna.
Je anazo documents zinazoonyesha alienda kudai?Kama hana tumfanyeje huyu?Na kama anazo amezipata kwa njia halali?Tusiwe wepesi kukimbilia mitandaoni ndiyo maana tumetungiwa sheria isiyokuwa na miguu wala kichwa.Ujinga wetu ndiyo umetufanya tutungiwe sheria hizi zilizopita juzi.
Muulize mleta mada alienda akamuuliza kwanini anadai au anabargain mshahara mkubwa?Akikujibu Mkataba wake wa ajira uanmruhusu kulipwa anavyolipwa utasemaje?Utamlaumu Dr.Slaa au Muajiri wake?
Hivi mleta mada ameshaenda kudadisi CDM kujua kwanini analipwa navyolipwa?Mbona tunaona kila siku wabunge wasioenda shule wengine wameishia darasa la saba wanalipwa mamilioni na dakatari analipwa tulaki fulani hivi,kuna mtu amelipigia kelele hili?Kuna aliyeenda mbali akaliweka kwenye mitandao?Hebu tuseme ukweli ni mara ngapi wabunge wanajiongezea mishahara na marupurupu kibao lakini ni nani anaweka taarifa hizi kwenye mitandao?
Lakini inapokuja viongozi waupinzani wanalipwa kiasi kinacholingana na viongozi wa CCM basi mnapiga mayowe mengi?
Inachosha................
Mtoa mada hivi wajua kulingana na sheria ya mitandao ukitoa information za uwongo kuhusu mtu akikushtaki unaenda jela?
Hivi kweli inaingia akilini mwamtu kuutangazia umma mshahara wa mfanyakazi?Hivi siri ya Dr.Slaa na CDM ilipitia kwako?
Hivi unapoweka kwenye maandishi Dr.Slaa anatumia kwa siku lita 33.33 huyu mtu inaelekea anapuyanga sana na hilo gari.Kweli kabisa kumaliza lita 33 kwa siku?
Hebu tufike mahali tuache propoganda zisizokuwa na maana,tuache uzushi na pia tuache kuingilia maisha binafsi ya mtu.Si kwa Dr.Slaa hata kwa watu wengine pia.Inatia kinyaa kila siku Dr.Slaa.Haaaaaaatumewachoka sasa ,tuleteeni mada za kuijenga nchi yetu.
Tuna uchaguzi na Katiba isiyoeleweka hayo ndiyo mambo ya kujadili siyo issue za mishahara ya watu ambayo ahatuna hata sababu ya kuijua.
mkuu Tetty Dr. Slaa ni public figure, Dr. Slaa anapigiwa chapuo kuwa Rais wa nchi. Kwa mantiki hiyo sioni ubaya kujadili suala hili. Shida yangu ni ukweli wa hizi habari. Kama habari ni za ukweli basi hatuna budi kujadili hakuna cha privacy kwenye suala linalomhusu kiongozi ambaye tunasema anafaa kuwa Rais wa nchi na huenda akapitshwa na UKAWA kuwa mgombea.
Suala lingine ni kwamba CHADEMA inajipambanua kuwa mbadala wa CCM, hivyo basi si vyema mbadala kutaka kufanya yale ambayo tunaona ni mabaya ya CCM kama hizo posho ama kuwalipa madktari kiduchu. CHADEMA inatakiwa ijitofautishe na CCM kwa maneno na vitendo. Kama CCM wanafanya dhambi ya kuficha mapato ya viongozi wake, CHADEMA itoke huko ili kuwa tofauti.
Naona hatuna tofauti kubwa. Nimesema shida yangu ni ukweli wa habari yenyewe.Unapojadili kitu chochote ukiwa huna proper evidence au facts haumtendei haki muhusika.Na suala kama hili kwanza lilitakiwa liulizwe mwenyewe kwanza ili tumtendee haki.
Wajua twaweza kuepusha mengi kama tukiwatendea haki hawa tunaowaita Public Figures ,wengi wao wameishia kutukanwa kwenye mitandao mpaka matusi ambayo yanaudhi sababu tu hakuna upande wa pili wa muhusika kujitetea.
Kama Dr.Slaa halipi kodi hili si kosa lake ni kosa la mwajiri wake kutomkata kodi husika kwani PAYE inapelekwa TRA na muajiri.Je kaka unauhakika aliyeleta mada anazodocuments zinazoonyesha Dr.Slaa kudai madai mengine ya mshahara?Je gari ni la ofisi yaani la CDM ni kiasi gani analitumia kwa safari binafsi?
Je Ofisi inaweza kuziainisha safari binafsi na za kikazi?Tusije tukawa tunalumbana kumbe safafri binafsi ni asilimia 10 tu ya safari zote.
Ni vizuri kuzijadili issue za viongozi wetu lakini tuwe na mipaka na evidence vinginevyo sidhani kama tunawatendea haki kwa kuweka tu information zao hata kama ni za uwongo.Wakati tunawalazimisha wanasiasa wawe wa kweli tuanze na sisi kuwa wakweli.
Hivi mswaada wa cybercrime utasainiwa lini?
Hilo jiko unakopikia hizi habari halijaisha kuni?
Japo simuungi mkono Slaa, ningefurahi na ungelitendea haki jukwaa hili kwa kutoa vielelezo vinavyothibitisha tuhuma hizo.Unashangaa mafuta Lita 30 kuisha kwa siku moja? Au unadhani Dr Slaa anatumia Vitz? By the way, nadhani hujui shughuli za kichama zinaendeshwaje hivyo nisingependa kukulaumu.
Pia umegusia suala la maisha binafsi, hemu wewe Tetty jaribu kutembea na chup.i mtaani uone kama nitaleta uzi hapa wa kukuhusu wewe kutembea na chup.i. Kamwe siwezi, because you're no body. Huyu Dr Slaa nimeweka habari yake hapa kwa kuwa huo mshahara na matumizi yake mengine yanakuwa covered na pesa za chama ambazo kimsingi ni ruzuku zinazo tokana na kodi zetu wananchi.
Sasa kama kichwani mwako unachowaza ni katiba mpya tu na huoni kama kuna ishu zingine, basi wewe baki na umbumbumbu wako.
Naona hatuna tofauti kubwa. Nimesema shida yangu ni ukweli wa habari yenyewe.
Tehteh kweli mkuki kwa nguruwe ila kwa binadamu mchungu. Ni kweli taarifa haina source ya kutosha lakini mdau umesahau kuwa chadema ilishawahi kutangaza hadharani mshahara wa waziri mkuu pinda? ??? Kama unabisha nenda YouTube tafuta ziara ya chama sumbawanga kupitia akina zitto. Ukweli unauma likini vumilia