Wana Ukumbi,
Katibu mkuu wa CHADEMA, Dr Slaa, ametoa madai mapya ya kuongezewa mshahara na stahiki zake kufuatia mafanikio aliyoyapata ya kuongezewa mshahara katika madai yake yaliyopita ambayo yalikuwa ni ongezeko la asilimia 40 tu ya kile kiwango alichokitaka!
Mchanganuo sahihi wa mshahara wa katibu mkuu wa CHADEMA na stahiki zake:
Mshahara anaolipwa Dr Slaa kwa sasa ni Tshs. 9,300,000 kwa mwezi wakati kabla ya madai yake ya mara ya mwisho alikuwa akilipwa Tshs. 6,600,000. Ambalo ni ongezeko la 40%.
Stahiki za Dr Slaa kama Katibu Mkuu:
Dr Slaa anawekewa kiasi cha lita 1000 za mafuta ya Petrol kila mwezi ambayo kwa wastani ni Tshs milioni 2,000,000 katika gari lake alilokabidhiwa na chama ambalo pia ulitumia kwa shughuli zake binafsi na za chama. Ifahamike, hii ni nje ya mshahara!
Haijaishia hapo, Dr Slaa pia anapewa pesa kiasi cha Tshs 2,500,000 kama fedha ya matumizi ya ofisi ya katibu mkuu wa chama kila mwezi. Hii pia ipo nje ya mshahara wake na matumizi yake hayaeleweki.
Kama hiyo haitoshi, Dr Slaa kila afanyapo vikao vya chama vya ngazi mbalimbali uinuka na wastani wa Tshs. 1,500,000 kwa kikao kimoja.
Madai Mapya:
Mshahara: Dr Slaa kwa sasa ameitaarifu CHADEMA kuwa wakati wa kukamilisha asilimia 60 zilizobaki za madai yake ya awali ya mshahara wake umewadia. "Hii ni kutokana na ongezeko la gharama za maisha na pia kuongezwa mkataba wa kutumikia chama kwa nafasi ya ukatibu mkuu" alieleza Dr Slaa.
Hivyo basi, kama CHADEMA itaridhia madai hayo mapya na kumuongeza Dr Slaa kiasi cha asilimia 60 kilichobaki, Dr Slaa ndiye atakuwa katibu mkuu wa chama cha siasa anayelipwa pesa nyingi kuliko wote katika nchi za ukanda wa Afrika mashariki! Kiasi hicho kitafikia Tshs. 13,200,000 kwa mwezi huku kikienda sambamba na kuongezeka kwa posho na stahiki zingine.
Hebu soma hapo chini labda itakudaidia zaidi
Kwa nyakati tofauti, Mukama na Nape wamekaririwa wakiwashutumua viongozi wakuu wa CHADEMA, Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dk. Willibrod Slaa, kwa maelezo kuwa wameshnikiza mshahara mkubwa wa Sh milioni 7.5 kwa Dk Slaa, na uuzaji wa magari matatu ya Mbowe kwa pesa nyingi mno.
Komu jana alisema kwanza Mukama na Nape wanapotosha umma kuhusu ukweli wanaoujadili, na akasema hata hiyo sehemu ya ukweli wanaougeuza tuhuma imeshapitwa na wakati, kwa kuwa CHADEMA hakifanyi mambo kwa kificho, na kilishafafanua hoja hizo.
Alisema Dk. Slaa hajawahi kushinikizwa alipwe Sh.7.5 milioni. "Kwanza, hatumlipi kiasi hicho, lakini pia Dk. Slaa hajawahi kuomba, kushinikiza wala kuchagiza kulipwa kiasi hicho cha fedha kama ambavyo viongozi wa CCM wanavyotaka kuaminisha umma," alisema Komu.Badala yake, alisema, chama ndicho kilipanga jinsi ya kumwezesha Dk Slaa kwa kuwa ndicho kilichomwomba agombee urais, huku kikujua kuwa angegombea ubunge na kushinda kirahisi.
Lengo la chama kufanya vile ni kumwezesha Dk Slaa kutenda vema kazi zake za katibu mkuu kama alivyokuwa akitenda kazi za ubunge; hivyo kwa pamoja wakakubaliana awezeshwe kulingana na masharti ya utumishi katika nafasi ya ubunge.
Huku akikosoa takwimu za Nape, Komu alisema Dk. Slaa analipwa Sh 7,174,000 kama kwa mwezi, na si Sh. 7,500,000.
Alisema vilivyochukuliwa vipengele vichache sana katika marupurupu ya mbunge, hivyo si sahihi kusema kuwa Dk. Slaa alipwa sawa na mbunge.
Mkurugenzi huo yalisema vipengele hivyo ni mshahara wake Sh. 1,725,000, wakati mbunge analipwa Sh. 2,305,000 kabla ya kukatwa kodi. Komu alisema kiongozi huyo analipwa mafuta ya kwenda ofisini na kurudi nyumbani kwake lita 30 kwa siku, sawa na lita 900 kwa mwezi; kwa bei ya kila lita moja Sh. 2000.
Wakati mbunge analipwa lita 1,000 kwa mwezi kwa bei ya kila lita moja Sh. 2,500, bei ambayo haipo, lakini Bunge limeridhia kulipa.
Alisema sekretarieti ya Kamati Kuu ilipeleka pendekezo hilo katika vikao vya Kamati Kuu na Baraza Kuu kupitishwa kwa njia ya uwazi na likaingizwa katika mpango kazi wa chama.
"Wakati wote wa kujadili pendekezo hilo, Dk. Slaa aliachia nafasi yake na kikao kiliendeshwa na katibu wa Wanawake, Dk. Naomi Kaihula, ambaye ni mbunge wa Viti Maalum kutoka Mbeya," ilisema.
Alisema mbunge akikaa katika kikao cha Kamati ya Bunge au akihudhuria mkutano wa Bunge analipwa Sh. 70,000 kama posho ya kikao, Sh. 30,000 posho ya mafuta na Sh. 80,000 posho ya kujikumu akiwa Dodoma.
Na akiwa Dar es Salaam, mbunge analipwa Sh. 50,000 kama posho ya mafuta, Sh. 70,000 posho ya kikao na Sh. 80,000 kama posho ya kujikimu huku fedha hizo zikilipwa bila kujali kama mbunge huyu amekuja na gari lake Dar es Salaam na amekwenda nalo Dodoma.
Akahoji: "Mbona hakuna mtu alishawahi kuuliza wakati hizo zote ni fedha za umma?"
Alihitimisha kwamba Dk. Slaa anastahili kulipwa kiasi hicho kwa kuwa aliombwa na chama kugombea urais, naye kukubali, zaidi kukubaliwa na umma pamoja na wanachama kutokana na ukweli wake katika kazi ya siasa.
"Baada ya kukubaliwa na umma, alionyesha umakini, umahiri na uwezo wa hali ya juu katika kujenga hoja zenye tija kwa taifa, na kwamba Dk. Slaa alithibitisha na bado anaendelea kuthibitisha kuwa yeye ni kiongozi bora na shupavu anayestahili kulipwa mshahara mzuri," alisema Komu.
Alisema matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita, ambapo Dk. Slaa alikuwa mgombea wao wa urais yanathibitisha kuwa hata bila kuzingatia uchakachuaji wa kura, ameanzisha ukurasa mpya wa mwisho wa mwanzo wa zama za mwisho wa CCM.