Dr Slaa Atoa Madai Mapya Ya Kuongezwa Mshahara - CHADEMA

Dr Slaa Atoa Madai Mapya Ya Kuongezwa Mshahara - CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Kwa kazi anayoifanya Bado analipwa Hela ndogo sana wangemuongezea Mara mbili yake.
 
Kwa nyakati tofauti, Mukama na Nape
wamekaririwa wakiwashutumua viongozi wakuu
wa CHADEMA, Mwenyekiti Freeman Mbowe na
Katibu Mkuu Dk. Willibrod Slaa, kwa maelezo
kuwa wameshnikiza mshahara mkubwa wa Sh
milioni 7.5 kwa Dk Slaa, na uuzaji wa magari
matatu ya Mbowe kwa pesa nyingi mno.
Komu jana alisema kwanza Mukama na Nape
wanapotosha umma kuhusu ukweli wanaoujadili,
na akasema hata hiyo sehemu ya ukweli
wanaougeuza tuhuma imeshapitwa na wakati,
kwa kuwa CHADEMA hakifanyi mambo kwa
kificho, na kilishafafanua hoja hizo.
Alisema Dk. Slaa hajawahi kushinikizwa alipwe
Sh.7.5 milioni. "Kwanza, hatumlipi kiasi hicho,
lakini pia Dk. Slaa hajawahi kuomba, kushinikiza
wala kuchagiza kulipwa kiasi hicho cha fedha
kama ambavyo viongozi wa CCM wanavyotaka
kuaminisha umma," alisema Komu.Badala yake,
alisema, chama ndicho kilipanga jinsi ya
kumwezesha Dk Slaa kwa kuwa ndicho
kilichomwomba agombee urais, huku kikujua
kuwa angegombea ubunge na kushinda kirahisi.
Lengo la chama kufanya vile ni kumwezesha Dk
Slaa kutenda vema kazi zake za katibu mkuu
kama alivyokuwa akitenda kazi za ubunge; hivyo
kwa pamoja wakakubaliana awezeshwe kulingana
na masharti ya utumishi katika nafasi ya ubunge.
Huku akikosoa takwimu za Nape, Komu alisema
Dk. Slaa analipwa Sh 7,174,000 kama kwa mwezi,
na si Sh. 7,500,000.
Alisema vilivyochukuliwa vipengele vichache sana
katika marupurupu ya mbunge, hivyo si sahihi
kusema kuwa Dk. Slaa alipwa sawa na mbunge.
Mkurugenzi huo yalisema vipengele hivyo ni
mshahara wake Sh. 1,725,000, wakati mbunge
analipwa Sh. 2,305,000 kabla ya kukatwa kodi.
Komu alisema kiongozi huyo analipwa mafuta ya
kwenda ofisini na kurudi nyumbani kwake lita 30
kwa siku, sawa na lita 900 kwa mwezi; kwa bei
ya kila lita moja Sh. 2000.
Wakati mbunge analipwa lita 1,000 kwa mwezi
kwa bei ya kila lita moja Sh. 2,500, bei ambayo
haipo, lakini Bunge limeridhia kulipa.
Alisema sekretarieti ya Kamati Kuu ilipeleka
pendekezo hilo katika vikao vya Kamati Kuu na
Baraza Kuu kupitishwa kwa njia ya uwazi na
likaingizwa katika mpango kazi wa chama.
"Wakati wote wa kujadili pendekezo hilo, Dk. Slaa
aliachia nafasi yake na kikao kiliendeshwa na
katibu wa Wanawake, Dk. Naomi Kaihula, ambaye
ni mbunge wa Viti Maalum kutoka Mbeya,"
ilisema.
Alisema mbunge akikaa katika kikao cha Kamati
ya Bunge au akihudhuria mkutano wa Bunge
analipwa Sh. 70,000 kama posho ya kikao, Sh.
30,000 posho ya mafuta na Sh. 80,000 posho ya
kujikumu akiwa Dodoma.
Na akiwa Dar es Salaam, mbunge analipwa Sh.
50,000 kama posho ya mafuta, Sh. 70,000 posho
ya kikao na Sh. 80,000 kama posho ya kujikimu
huku fedha hizo zikilipwa bila kujali kama mbunge
huyu amekuja na gari lake Dar es Salaam na
amekwenda nalo Dodoma.
Akahoji: "Mbona hakuna mtu alishawahi kuuliza
wakati hizo zote ni fedha za umma?"
Alihitimisha kwamba Dk. Slaa anastahili kulipwa
kiasi hicho kwa kuwa aliombwa na chama
kugombea urais, naye kukubali, zaidi kukubaliwa
na umma pamoja na wanachama kutokana na
ukweli wake katika kazi ya siasa.
"Baada ya kukubaliwa na umma, alionyesha
umakini, umahiri na uwezo wa hali ya juu katika
kujenga hoja zenye tija kwa taifa, na kwamba Dk.
Slaa alithibitisha na bado anaendelea kuthibitisha
kuwa yeye ni kiongozi bora na shupavu
anayestahili kulipwa mshahara mzuri," alisema
Komu.
Alisema matokeo ya uchaguzi mkuu uliopita,
ambapo Dk. Slaa alikuwa mgombea wao wa urais
yanathibitisha kuwa hata bila kuzingatia
uchakachuaji wa kura, ameanzisha ukurasa mpya
wa mwisho wa mwanzo wa zama za mwisho wa
CCM.
 
Wana Ukumbi,

Katibu mkuu wa CHADEMA, Dr Slaa, ametoa madai mapya ya kuongezewa mshahara na stahiki zake kufuatia mafanikio aliyoyapata ya kuongezewa mshahara katika madai yake yaliyopita ambayo yalikuwa ni ongezeko la asilimia 40 tu ya kile kiwango alichokitaka!

Mchanganuo sahihi wa mshahara wa katibu mkuu wa CHADEMA na stahiki zake:

Mshahara anaolipwa Dr Slaa kwa sasa ni Tshs. 9,300,000 kwa mwezi wakati kabla ya madai yake ya mara ya mwisho alikuwa akilipwa Tshs. 6,600,000. Ambalo ni ongezeko la 40%.

Stahiki za Dr Slaa kama Katibu Mkuu:

Dr Slaa anawekewa kiasi cha lita 1000 za mafuta ya Petrol kila mwezi ambayo kwa wastani ni Tshs milioni 2,000,000 katika gari lake alilokabidhiwa na chama ambalo pia ulitumia kwa shughuli zake binafsi na za chama. Ifahamike, hii ni nje ya mshahara!

Haijaishia hapo, Dr Slaa pia anapewa pesa kiasi cha Tshs 2,500,000 kama fedha ya matumizi ya ofisi ya katibu mkuu wa chama kila mwezi. Hii pia ipo nje ya mshahara wake na matumizi yake hayaeleweki.

Kama hiyo haitoshi, Dr Slaa kila afanyapo vikao vya chama vya ngazi mbalimbali uinuka na wastani wa Tshs. 1,500,000 kwa kikao kimoja.

Madai Mapya:

Mshahara: Dr Slaa kwa sasa ameitaarifu CHADEMA kuwa wakati wa kukamilisha asilimia 60 zilizobaki za madai yake ya awali ya mshahara wake umewadia. "Hii ni kutokana na ongezeko la gharama za maisha na pia kuongezwa mkataba wa kutumikia chama kwa nafasi ya ukatibu mkuu" alieleza Dr Slaa.

Hivyo basi, kama CHADEMA itaridhia madai hayo mapya na kumuongeza Dr Slaa kiasi cha asilimia 60 kilichobaki, Dr Slaa ndiye atakuwa katibu mkuu wa chama cha siasa anayelipwa pesa nyingi kuliko wote katika nchi za ukanda wa Afrika mashariki! Kiasi hicho kitafikia Tshs. 13,200,000 kwa mwezi huku kikienda sambamba na kuongezeka kwa posho na stahiki zingine.

Pamoja na uzumbukuku wako, fikra finyu na kutokujua ukweli wa chama kisichokuhusu...! Majangili wanaoiba bila kudai kwa njia halali unawasemeaje?? je unaweza utumegee kidogo 'Jangili mkuu'...aka 'Elephant Chief Dentist' kama Katibu mkuu wa Genge linalokufadhili yeye analipwa kiasi gani, mbali na kutokomeza 'nyara za taifa' zenye thamani ya mabilioni...ambayo wewe huna fikra hata chembe ya kuyazungumzia! Kama ingekuwa unao ukweli kuhusu Malipo ya Dr Slaa na madai yake..., ungetumia fikra kidogo kuya-linganisha na angalau 1 ya 100 ya fedha ambazo wanaokutuma wameliibia taifa, na Ma-containers ya pembe za ndovu zilizokamatwa Hong Kong, ingekuwa mshahara wa Makatibu wangapi kama Dr Slaa?? kwa upunguani wako huzioni hizo..unahangaikia chama usichokuwa na chembe ya gharama, fikra, itikadi au jasho?? Hoja nyingine ni kama samadi...useless mind!
 
Dude hamy D

Dont be narrow minded. Scope ya Uzalishaji haipo narrowed kwenye defn yako hiyo.

Uzalishaji could be kueneza chama; kuongeza wanachama, kuimarisha utendaji wa chama.

Mkuu,

Wewe unaongelea social benefits ambazo chama imapata kwa jitihada za viongozi waandamizi na mimi katika ile post ambayo umeijibu nilikuwa naongelea profit itokanayo na production kwenye makampuni.

Mabenki biashara yao kuuza pesa na upata profit kupitia riba. Mishahara yao inakuwa determined na faida wanayoipata.

Vivyo hivyo kwa makampuni mengine yawe natoa huduma au yanazalisha bidhaa. Huko hata wakilipana milioni mia moja who cares? Hizo ni pesa zao na the bigger the salary the larger tax contribution, actually I encourage walipwe zaidi ili wazidi kulipa kodi kupitia PAYE.


Kwa upande wa vyama, hao uzalishaji wao sio huo ambao nimeuzungumzia hapo. Uzalishaji wao unakuwa kisocial zaidi na sio katika mfumo wa manetary form. Hivyo, vyama vya siasa vipo upande wa kutumia mapato ya serikali badala ya kuingiza mapato serikalini.

Katika hali hiyo, ni vyema tunapotoa michango yetu hapa tuelewe kuwa pesa inayotumika kumlipa Dr Slaa, ndiyo hiyo hiyo itumikayo kuwalipa wabunge, mawaziri na hata rais. Hivyo kama tunachukizwa na jinsi pesa za walipa kodi zinavyofujwa na serikali kwa njia za hanasa, basi tuchukizwe vilevile na huo utaratibu wa CHADEMA kujilimbikizia maslahi makubwa halafu mbaya zaidi hata hiyo income tax hawalipi huko CHADEMA.
 
Last edited by a moderator:
Ili ujue ugonjwa walionao ccm,hawajawahi kuweka wazi Katibu Mkuu na Nape wanalipwa shilingi ngapi,kama chama hakiwezi kuweka wazi malipo ya vigogo wake,kinawezaje kuwaamrisha mawaziri na serikali nzima kuweka peupe mikataba ya serikali?
 
ooghs...(mwayo), huu uchaguz si ufike tu maana hzi siasa znachosha sasa!
 
Wala huwa halipwi salary....

CHADEMA National Party Chairman Freeman Mbowe, has admitted that the party's Secretary General, Dr Wilbroad Slaa, pockets 7m/- tax-free each month in 'allowances.'

This follows reports by some section of the media on Sunday quoting officials from the Tanzania Revenue Authority (TRA) , saying that Dr Slaa has been avoiding taxes.

Mr Mbowe told journalists on the sidelines of the ongoing parliamentary committee meetings in Dar es Salaam on Tuesday that all of Chadema leaders are volunteers who are hardly paid anything.

''Save for members of the Secretariat who are given some allowances otherwise all party leaders are not paid anything,'' remarked Mr Mbowe, who is also the Leader of the Opposition in the National Assembly.

Dr Slaa was among a handful of candidates who contested for presidency during last year's General Elections and lost to President Jakaya Kikwete.

According to Mr Mbowe, since Dr Slaa is the Chief Executive of the party, it was decided by the party National Executive Committee (NEC) that some package should be allocated for him to be able to build the party.

''We decided that since he will not be doing any other job some amount of money be allocated for him to cover his expenses such as transport, medication, housing among others,'' he said.

The Hai legislator maintained that since the amount is 'just an allowance,' it needs not to be taxed.

''It is not true that Dr Slaa is paid a lot of money as claimed by some people. What he earns is just some money for his upkeep and not his own income per se,'' explained the opposition politician cum businessman.

He said statements by TRA officials that Dr Slaa has been avoiding taxes is a retribution towards the former Roman Catholic Church priest turned politician, for 'revealing TRA's misdeeds' during his time as an MP.

Efforts to get comment from the Registrar of Political Parties, Mr John Tendwa and TRA Commissioner General, Mr Harry Kitilya, were not successful on Tuesday.


SOURCE: Daily News
Duh, hapo mkuu wangu mshikaji kakosea sana maana sio swala la chama kuamua nani alipe tax nani asilipe. Na kibaya zaidi itakapo fanyika Auditing nyngine, Mbowe atakuwa amejikanyaga kutoa ushahidi kuwa baadhi ya fedha ambazo zilitakiwa kuwa mshahara zimewekwa kwenye matumizi ya Posho ili Katibu alisipe kodi.

Msidhanie kwamba ukisha file tax na zikakubalika ndio mwisho wa hoja. Kodi zinaweza itishwa upya na kupitiwa wakati wowote na wanaweza rudi nyuma miaka mitano..Sielewi sheria za kodi za Tanzania lakini hakuna posho ya Tsh millioni 7 kwa mwezi, ila Posho hutokana na malipo ya dharura iwe safari au vikao na sii kiwango sawa kila mwezi ili kujikimu na maisha.
 
---- japo hatujui kama habari ni ya kweli, katibu wa ccm analipwa sh ngapi? na mwenezi sh? nk! malipo ni malipo tu zote hela! mbaya zaidi ni zetu walipa kodi na wapiga kura! toeni evidence zote! tuone nyoka wa makengeza na wasio na makengeza--
 
Mtoa mada unaleta polojo na uzushi dhidi ya Chadema ili ulipwe nini? Mods kama wanatenda haki unatakiwa upigwe ban.

Unatumiwa na ibilisi kuvuruga amani na muda wa watu. Unasababisha JF kuwa kijiwe cha wahuni. Ukiendelea hivi kuandika mambo makubwa kama haya bila vielelezo unatakiwa upigwe ban ya milele.
 
wakuu kwa dokta kupewa lita 1000 kwa mwezi nadhani ni sahihi kwa sababu mi nakaa kimara nafanya kazi zangu kariakoo natumia toyota gx ya cc 2000 na kwa mwezi natumia lita 300.
 
Katibu mkuu wa CHADEMA, Dr Slaa, ametoa madai mapya ya kuongezewa mshahara na stahiki zake kufuatia mafanikio aliyoyapata ya kuongezewa mshahara katika madai yake yaliyopita ambayo yalikuwa ni ongezeko la asilimia 40 tu ya kile kiwango alichokitaka!

Mchanganuo sahihi wa mshahara wa katibu mkuu wa CHADEMA na stahiki zake:

Mshahara anaolipwa Dr Slaa kwa sasa ni Tshs. 9,300,000 kwa mwezi wakati kabla ya madai yake ya mara ya mwisho alikuwa akilipwa Tshs. 6,600,000. Ambalo ni ongezeko la 40%.

Stahiki za Dr Slaa kama Katibu Mkuu:

Dr Slaa anawekewa kiasi cha lita 1000 za mafuta ya Petrol kila mwezi ambayo kwa wastani ni Tshs milioni 2,000,000 katika gari lake alilokabidhiwa na chama ambalo pia ulitumia kwa shughuli zake binafsi na za chama. Ifahamike, hii ni nje ya mshahara!

Haijaishia hapo, Dr Slaa pia anapewa pesa kiasi cha Tshs 2,500,000 kama fedha ya matumizi ya ofisi ya katibu mkuu wa chama kila mwezi. Hii pia ipo nje ya mshahara wake na matumizi yake hayaeleweki.

Kama hiyo haitoshi, Dr Slaa kila afanyapo vikao vya chama vya ngazi mbalimbali uinuka na wastani wa Tshs. 1,500,000 kwa kikao kimoja.

Madai Mapya:

Mshahara: Dr Slaa kwa sasa ameitaarifu CHADEMA kuwa wakati wa kukamilisha asilimia 60 zilizobaki za madai yake ya awali ya mshahara wake umewadia. "Hii ni kutokana na ongezeko la gharama za maisha na pia kuongezwa mkataba wa kutumikia chama kwa nafasi ya ukatibu mkuu" alieleza Dr Slaa.

Hivyo basi, kama CHADEMA itaridhia madai hayo mapya na kumuongeza Dr Slaa kiasi cha asilimia 60 kilichobaki, Dr Slaa ndiye atakuwa katibu mkuu wa chama cha siasa anayelipwa pesa nyingi kuliko wote katika nchi za ukanda wa Afrika mashariki! Kiasi hicho kitafikia Tshs. 13,200,000 kwa mwezi huku kikienda sambamba na kuongezeka kwa posho na stahiki zingine.

Source: dar24.blogspot.com
 
Kwa kazi anayoifanya bado kiasi hicho cha hela ni kidogo sana anatakiwa alipwe angalau 30,000,000/= kwa mwezi. Wewe ulitaka alingane na wewe unaelipwa buku 7?
 
Sio tatizo lako. Tatizo shule. Mbona mshahara wa Kinana na Ayatollah ZZK hamtaji?. Hata km analipwa huo mshahara na Cdm wameridhia tatizo liko wapi?. Acheni Majungu Act/CCM.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom