Dr. Slaa anastahili kuheshimiwa

Dr. Slaa anastahili kuheshimiwa

Wana Jf wasalaam!

Mmoja kati ya watu walio kuwa wanautaka Urais na walitegemea sana ndio wataongoza kijiti cha UKAWA ni Dr.W.Slaa ambaye kwa sasa amesusa kabisa baada ya kupatikana mbadala wake..!

WanaJf kama mtakumbuka siku ya mkutano wa CHADEMA pale mwanza Dr Slaa alipokelewa na wananchi kwenye gari la wazi huku akiwapungia mkono, kwakweli Dr alidhani kabisa ameshakuwa Rais na kwa kuonesha furaha alianza kuruka ruka kwa furaha,kama Mungu angemuonesha kuwa mbeleni atakatwa basi asingeliruka kabisa na angesusa kwenda kwenye mkutano kama alivyofanya sasa!

WanaJf tatizo la Dr Slaa sio Lowassa bali ni Urais, na laiti Lowassa asingegombea Urais wala Slaa asingesusa na kujifungia nyumbani kwake!

WanaJf, Slaa ana sifa zote za wanafiki waliotukuka maana asiye mnafiki husema wazi wala hakai kimya na kususa.Nilitegemea Slaa kama kweli anapinga suala la Lowassa ajitokeze hadharani na kusema sio kususa kama watoto

Watanzania hadi sasa hawajui msimamo wake na isitoshe wenzie wamesema na yeye alibariki Lowassa kushika kijiti cha UKAWA!

Kama kuna mwanaCHADEMA bado anafikiri Dr. Slaa bado ni mwana chadema basi mtu huyo atakuwa amechanganyikiwa!

Dr. Slaa sio mwana chadema tangu Lowassa alipokabidhiwa kijiti lakini kwa kuwa Slaa ni mnafiki sana basi hataki kuwambia ukweli anajifanya amesusa!

CHADEMA wanapoteza muda kumbembeleza Slaa lakini hawatofanikiwa kwa kuwa Slaa alishahamua kuachana na CHADEMA baada ya kukosa nafasi ya kugombea Urais..!

Sasa hivi anachofanya Dr. Slaa ni mbinu ya kuhakikisha kura za Lowassa hazitoshi kwa kuwagawa wana UKAWA na bila shaka atafanikiwa katika hili na hatoshiriki campaign za kumnadi fisadi!

Dr. Slaa aliizoea nafasi ya kuwa Rais kimvuli sasa anaona ndoto yake imepotea na hayuko tayari kuendelea na CHADEMA lakini kwa kuwa ni mnafiki basi hataki kuwambia ukweli CHADEMA!

Jambo ambalo wanaweza jaribu CHADEMA ili kumshawishi Slaa kumnadi Lowassa basi ni kumhaidi mshahara mnono kuanzia Million 20 kwa mwezi maana ili ndio tatizo lake na kamwe hawatofanikiwa kumshawishi kama hawatokwenda na wazo la Pesa!

Karibuni wanajamvi!



Ni upumbavu wa kiwango cha PHD kumponda na kumdis kwa namna yeyote Dr Slaa,nawachukia sana watu wa aina hyo
 
WanaJF na hasa wana CHADEMA wenzangu tuwe makini sana na maandishi yetu hapa jukwaani kuhusu huu ukimya wa DR SLAA, tafadhalini sana, DR ni kiongozi mkubwa sana anastahili kuheshimiwa, wale wenye uchungu na CHADEMA na tunaofahamu tulipotoka hatuwezi kumkashifu huyu mtu, kwa lipi hasa ?

Acheni kabisa jambo hilo, sikupenda kuandika jambo hili maana linaweza kuendeleza malumbano zaidi lakini nimelazimika kuliweka kama angalizo.



We love u Dr Slaa
 
Hivi huyu mzee hakujua kuwa mbowe ni fisadi namba moja hapa Tanzania

Hapo umetii angalizo la mtoa mada kwa Slaa lakini umekiuka angalizo hilo kwa Mbowe. Lakini sifa yake apewe hata kama itachukiza.
 
Kwa maoni yangu watanganyika wanamuhitaji sana slaa km kuna wenye access na dk aombwe arejee kwenye siasa tuwang,oe ccm kwa njia yoyote ile tubadili mfumo na kua serikali tatu yeye agombee urais wa tanganyika hapo tutajikwamua juu babalao pembeni (zanzibar) maalim pembeni kidogoa(tanganyika) slaa katikati uwaziri mkuu ( mbatia) mid filders km kina lipumba makaidi mbowe lisu na mareserve wanakuja oct25
 
hilo wazo lako ni la baadaye, kwa sasa tushikamane tuwangoe hawa wakoloni weusi by saa nne asubuhi tuwe tumeshamaliza kazi kama Mzee wetu alivyotuambia.
 
Nikweli fuso ndo maana natamani jembe lirudi tushambulie kwa pamoja
 
Kwa maoni yangu watanganyika wanamuhitaji sana slaa km kuna wenye access na dk aombwe arejee kwenye siasa tuwang,oe ccm kwa njia yoyote ile tubadili mfumo na kua serikali tatu yeye agombee urais wa tanganyika hapo tutajikwamua juu babalao pembeni (zanzibar) maalim pembeni kidogoa(tanganyika) slaa katikati uwaziri mkuu ( mbatia) mid filders km kina lipumba makaidi mbowe lisu na mareserve wanakuja oct25

Lowasa Rais wa Muungano, Slaa rais wa Tanganyika, Mbatia waziri mkuu, hivi nyie watu wa kaskazini mnadhani hii nchi ni ya babu yenu
 
Slaa hawezi kukaa meza moja na mafisadi hata kidogo anaheshimu misingi ya kanisa katoliki.
 
Lowasa Rais wa Muungano, Slaa rais wa Tanganyika, Mbatia waziri mkuu, hivi nyie watu wa kaskazini mnadhani hii nchi ni ya babu yenu
Unazungumza mambo ambayo hata kwenye katiba hayapo jielimishe kwanza.
 
Lowasa Rais wa Muungano, Slaa rais wa Tanganyika, Mbatia waziri mkuu, hivi nyie watu wa kaskazini mnadhani hii nchi ni ya babu yenu

mtu aliefilisika kisiasa ataleta hoja kama hizi. na ndio ccm wanazitumia kwa sasa kuzuia mafuriko
 
Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu kama sufu mkiwa ccm, zitakiwa nyeupe kama theluji ukiingia ukawa
 
Bora uwaeleze vilaza wa mbowe maana utadhani yamelogwa
 
Asante mkuu,kumpokea Lowassa then tukaruhusu kumpoteza Dr Slaa litakuwa kosa kubwa la kimkakati,Dr hajasema na siku akiongea atakuwa na haki zote,CDM bila Dr haiwezekani,chair nae apunguze kumpiga vijembe Dr inaboa na kutuboa

Hilo haikufaa kumtoka kinywani mtu anayeheshimiwa na wengi-tena dhidi ya mtu mzima na maadili yake.
Safari ya CDM imetoka mbali wale wote waliotoka mbali na safiri hii wanatakiwa kuwa na akiba ya kauli na fikra kisa tu safari ya magogoni ambayo bado kabisa hata gari halijaanza kuondoka.

 
Tangu ujio wa vyama vingi kumewahi tokea wapambanaji mahiri dhidi ya chama tawala ambao historia itawakumbuka. Hatahivyo ni ukweli usiopingika kuwa miongoni mwa wapambanaji hao, wapo waliojitokeza kuwa juu ya wenzao kwa upambanaji wao wa hali na mali. Tukianza na Mh. Dr. Wilbroad Slaa ambaye kwa ujio wake CHADEMA na hasa alipogombea urais alikipa nguvu kubwa chama hicho. Kwa ushirikiano wa karibu na Mwenyekiti Mh . Freeman Mbowe, pamoja na Zito Kabwe kwa hoja zao nzito zilisababisha CHADEMA kujipatia wabunge wengi na hata kuweza kuunda kambi rasmi ya upinzani bungeni.

CHADEMA daima imekuwa ni tumaini la wapenda mabadiliko, imekuwa ni mfariji kwa wanaoumizwa na mfumo wa chama tawala. Wabunge wake waliponyanyaswa bungeni, waliumia pamoja na wanachama. CHADEMA haikuwa na hulka ya ubaguzi wala unafiki licha ya kusemwa sana kwa ukabila. Mshikamano na uvumilivu wa Wana CHADEMA ulikifikisha chama hapo killipo. Tatizo limejitokeza hivi karibuni, kutimua viongozi wakuu wa CHADEMA.

Baada ya muungano wa vyama (UKAWA ) , kulikuwa na tumaini kuu kuwa mfumo unaenda kubadilika, lakini ghafla ndoto hiyo inapotezwa. Viongozi wakuu wa UKAWA wamejiudhuru. Uzuri ni kuwa hawakvihama vyama, wamejiudhuru uongozi kwa madai ya kutoridhishwa na baadhi ya mambo. Badala ya kuwa 'contain' kuna baadhi ya wanachama wanawabeza na kuwaita majina ya ajabu ajabu.

Ikiwa CCM ilimpoteza mh. Lowasa UKAWA wakamdaka kwa madai ana wanachama wengi, hamuoni kuondoka kwa vigogo wawili wa UKAWA kunaweza kupunguza wapambanaji wa kweli kutoka UKAWA? Je, ikiwa Sera imekuwa ni kuondoa CCM kivyovyote, ikiwa ni pamoja na kuchukua wanachama wake wengi hamuoni mnawaleta pamoja wanamfumo wa CCM kwa Jina tofauti ,yaani mfumo chotara (CCDM- Chama Cha Demokrasia na Mapinduzi), na hivyo watanzania wategemee yaleyale wanayoyakataa.

Leo viongozi wakuu wa UKAWA waliojiudhuru mnawaita majina mbaya, ikitokea UKAWA imeshindwa vibaya, wao Watakuwa ndio washindi, na historia itawahukumu ninyi kwa kukosa busara. UKAWA wakishinda, basi hawa viongozi wanaendelea kubeba majina mabaya mliyowapa mpaka pale matumaini ya watanzania yatakaposhindwa kufikiwa chini ya mfumo chotara wa mapinduzi.

Nashauri busara itumike kuwahandle viongozi hawa, siyo kwa kuwakejeli na kuwatukana. Upinzani uwe makini na wanachama wanaopokelewa, hasa kwenye kuwapa uongozi.
 
Ndugu zanguni

Katika wanasiasa ninaowaheshimu na kuwaona mashujaa na wanafaa kuigwa ni Dr Slaa

Ni vyema kama taifa likamuenzi na kumuweka kwenye orodha ya mashujaa wa nchi yetu alongside wanasiasa wengine.

Msimamo wake wa wazi juu ya yanayoendelea chadema leo ni wa kuigwa

Dr kakataa kuburuzwa na Mbowe na Lowassa na kawaachia chama waendelee

Inasikitisha kuona nyumbu wanafuata tu mkumbo wakati waliokijenga chama wamekataa kununuliwa
460%3E_3559850.jpg
 
  • Thanks
Reactions: mob
Back
Top Bottom