Dr. Slaa amuonya vikali Spika Anne Makinda

Dr. Slaa amuonya vikali Spika Anne Makinda

nani anayeweza kusimama na kuwaeleza watu uadilifu wa viongozi wa chadema aje hapa na hoja na siyo kurukaruka tu binafsi huwa siuni hata chembe awali alikuwepo zito lakini sasa keshapotoka kitambo.
 
Just 'cause Dr. Slaa got an opinion does that make him a politician? Jibu ni hapana.

Sasa tukuite mzungu? au msomi!?au kilaza?hapa ueleweki kwanza dogo sikia uendeshwaji wa bunge unaendeshwa kwa kuilinda serikali Bunge halitakiwi kuilinda serikali kwa sababu ni muhimili wa dola nikama mahakama ikiuke vifungu vya sheria kwa sababu serikali imeshitakiwa wakati hakimu na mawakili wanatafsiri sheria!hivyo hata bunge wanatafsili kanuni hivyo spika hawezi kuvurunda kanuni,sheria kisa yeye ni spika! halafu eti watu wasimseme!!. niujinga kushabikia kwa itikadi wakati wakutetea maslahi ya taifa ujinga ndo unawafanya kuwa madraja ya mafisadi.
 
Kama katibu wa Chama Dr. Slaa anahaki zote za kikatiba ndani ya chama kumpigania Mbunge yeyote.
Kama Joseph Mbilinyi amezalilishwa kwa kukatishwa na Spika unategemea Katibu akae kimywa tu.

Spika asinyo na akili za kutosha kujua hata majina ya wabunge wake anamwita Joseph, wewe nani nanihii wewe Sijui "Sugu" hebu toka nenda kakae. Hii ni dharau ya hali ya juu kabisa kiongozi gani makini atavumulia mambo kama haya na mnataka Dr. Slaa akae kimywa tu, kwa lipi zuri.. Acheni bwana.. your days are numbered... Ipo siku. Hata Hitler hakujua kuwa siku moja mambo yatakwisha.. sasa yupo wapi.. ubabe wa nini?

Namlilia sana Anna wangu, Mama Makinga. Hakuwa hivi nilimfahamu sikunyingi sana... amebadilishwa maskini.. anatumika tu. pole mama.. bahati mbaya umefunikwa blanketi huoni.. Na mimi mdogowako hata nisemje huniskiii. Pole...
 
Wabunge wa CHADEMA wamekuwa kama wamechanganyikiwa. Hawajielewi. Wakaonane na Dr. Kigwangala wapatiwe tiba.
Yaani unavyo hangaika kama vile umekalia kitu cha ncha kali...bado kidogo utaanza kujijibu...
 
DR SLAA kweli ana lake jambo si bure!

Yani kiongozi mkubwa kama yeye anatoa maelezo ya uchochezi waziwazi hivyo?

Kwa hotuba ya jana ya kambi ya upinzani iliyosomwa na Sugu haina wasifu wa kusomwa bungeni, sana sana Sugu angeenda kuwasomea wavuta bangi na wabwia unga wenzie.

Taifa letu Tanzania aliwezi kukaa kusikiliza maneno ya kihuni kihuni aliyoyajaza Sugu na washirika wake kwenye hile hotuba.

DR SLAA muogope mungu, kujitangaza kwako kisiasa kusichafue viongozi wetu wa kitaifa. Kwanza vitabu vitakatifu vimeagiza tuziheshimu mamlaka zilizo wekwa na Mungu, wewe ni PADRE gani usie heshimu maelekezo haya ya Mungu?

Wewe ndo umuogope Mungu povu linakutoka!.tutakufa maskini kwa uwoga wa kimaandazi
 
Yale yale ya book 7. Hongera kwa kumchukia Dr. Slaa, lakini chuki zako si chochote si lolote, anasonga mbele mpaka kieleweke.

Tiba

Leo huduma za Mpesa naona zipo busy sana, MOLEMO kawapa watu ulaji humu ndani, wanajiuliza na kujijibu tiba naona inawaingia sasa. Achana nao madame hapa huwezi washinda kwenye majibizano huo ndo mwisho wa upeo wao wa kufikiri, hope unayakumbuka ya magonjwa ya Dr nani yule wa Uingereza aliyamwaga hapa JF,nikumbushe jina...
 
maisha ni magumu kwako tu wewe ambaye unaishi kwa hisani za dr slaa

Kwa hiyo wewe na mama yako maisha yenu ni mazuri na kama wewe na baba yako maisha yenu ni mazuri vipi majirani zanu nao maisha ni mazuri au unajitoa ufahamu....
 
Dr slaa hana uwezo wa kuingilia mambo yanayoendelea bungeni. anawaharibia bure wabunge wa chadema na sasa wamekuwa kama wamechanganyikiwa vile. ukiona sugu alivyowasilisha ile speech jana utakubaliana nami kuwa wabunge wa chadema sasa hawatumii hata chembe ya akili yao kufikiri. wanatekeleza tu maagizo ya mkubwa wao bila ya kujua athari zake

Lizaboni men,

You talkin' nonsense men!
Usifikiri ile Hotuba ya Kambi ya Upinzani ni ya kukurupuka. Kuna Mitanzania mijuha na mizezeta inataka kuwaaminisha Watanzania kuwa kila kinachosomwa au kusemwa na Kambi ya upinzania Bungeni ni Uchochezi, hii si kweli hata kidogo!!!

Hotuba ya KUB inakuwa imeendaliwa na kupitiwa kwa umakini kabla haijapelekwa kusomwa Bungeni. Yote aliyoyasema Waziri Kivuli-Habari,Vijana Utamaduni na Michezo Mhe. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugumen.

  1. Hivi ni Mtanzania gani asiyejua kuwa Daudi Mwangosi ALIUWA NA JESHI LA POLISI chini ya usimamizi wa RPC Kamuhanda mwaka jana???
  2. Ni Mtanzania gani asiyejua kuwa Absolom Kibanda alitekwa na watu wa State security(UWT)akang'olewa kucha,meno na kutobolewa Jicho??
  3. Ni Mtanzania gani asiyejua kuwa kiongozi wa Chama cha Madaktari Ulimboka Steven alitekwa na watu wa State security (UWT)?
  4. Ni Mtanzania gani asiyejua kuwa Mhariri wa gazeti la MwanaHalisi ndugu Saed Kubenea alivamiwa na watu akamwagiwa Tindikali pamoja na Mhariri mwenzake Dimara Tegambwage?
  5. Nani asiyejua kuwa Wahariri na vyombo vyao vya habari wanaoandika Habari za kuikosoa Serikali ya CCM wanawindwa usiku na Mchana ili wanyamazishwe????

Watanzania wanajua yote haya. Bunge linatumika kulinda na kuficha Udhaifu wa Serikali ya CCM chini ya Uongozi wa Rais dhaifu Bwana Jakaya Mrisho Kiwete!!!
 
Dr. Slaa anafurahisha sana, hawezi kukaa siku tatu bila ya kutafuta tukio la kutokea nalo kwenye jamii ya Watanzania na akikosa tukio analazimisha ili mradi tumsikie.

Viongozi wa CHADEMA hawana tofauti na RockStars.
Nafikiri sahihi hapa ni kuwa Serikali ya CCM ndo inamfanya Dk awe bize kutoa matamko kwa jinsi wanavyongoza nchi kwa remote control
 
Kila siku anamuonya SPIKA wa bunge. HOW MANY TIMES?. Kwa nini sasa asichukue hatua. Inaonekana Kuonya kwa tafsiri ya Dr. Slaa ndiyo kuchukua hatua butu. Hizi ni kama kelele zisizokuwa na maana ambazo zinakosa hata mwelekeo maalum.

DO SOMETHING or just shuthole.
wewe ulitaka akachukue bunduki akampige ama?
 
Leo huduma za Mpesa naona zipo busy sana, MOLEMO kawapa watu ulaji humu ndani, wanajiuliza na kujijibu tiba naona inawaingia sasa. Achana nao madame hapa huwezi washinda kwenye majibizano huo ndo mwisho wa upeo wao wa kufikiri, hope unayakumbuka ya magonjwa ya Dr nani yule wa Uingereza aliyamwaga hapa JF,nikumbushe jina...

masatu unajidhalilisha kwa hizo post zako
 
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, amesema ikibidi Bunge livunjike au wabunge wa chama hicho wafukuzwe bungeni, lakini hawako tayari kuzibwa mdomo kuzungumzia masuala yanayohusu maisha ya Watanzania. Amesema chama hicho hakitakubali wabunge wake wapangiwe mambo ya kuzungumza kwa kutegemea busara za Spika au Naibu Spika, bali wataangalia na kufuata maelekezo ya kanuni za Bunge, akisema ndiyo msingi wa uendeshaji wa chombo hicho cha uwakilishi wa wananchi.

Akizungumza katika mikutano ya hadhara iliyohudhuriwa na maelfu ya watu jana katika maeneo ya Ngalangala, Basotu, wilayani Hanang na Haydom, wilayani Mbulu, kuhusiana na hotuba ya Sugu kuahirisha Bunge, Dk. Slaa alisema wabunge wa chama hicho daima wataendelea kuwasemea Watanzania wanyonge ndani na nje ya Bunge. “Moja ni tukio lililotokea leo (jana) bungeni. Kwa wale mliofuatilia mkutano wa Bunge mliona kilichotokea. Ninachotaka kumwambia Spika na wasaidizi wake bungeni ni kwamba Bunge linaongozwa kwa kanuni za bunge, si vinginevyo.

Uamuzi aliofanya wa kuagiza hotuba ya wabunge wetu ipelekwe kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge ni kinyume na kanuni ambazo ndizo msingi wa utendaji kazi wa bunge. Hakuna sehemu yoyote katika kanuni inampatia mamlaka Spika ya kupeleka hotuba ile kwenye kamati hiyo, ili waelekeze nini kisemwe. Hakuna,” alisema Dk. Slaa huku akishangiliwa na umati mkubwa wa watu.

Alisema kuwa baada ya mawasiliano ya viongozi wa juu wa chama hicho na uongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, walikubaliana kuwa kwa sababu hotuba hiyo haikuvunja kanuni yoyote ile ya Bunge, hawatakubali kuondoa au kupunguza neno hata moja.

Source:Nipashe Jumanne.

Huyu mzee anazeeka vibaya yabidi Josephine awe ana mpeti peti na tukutuliza ari na munkari ya ubongo wake.
 
huyo SLAA anatapatapq, Chama hakina mamlaka yoyote ya kumuonya SPIKA.
 
Lizaboni men,

You talkin' nonsense men!
Usifikiri ile Hotuba ya Kambi ya Upinzani ni ya kukurupuka. Kuna Mitanzania mijuha na mizezeta inataka kuwaaminisha Watanzania kuwa kila kinachosomwa au kusemwa na Kambi ya upinzania Bungeni ni Uchochezi, hii si kweli hata kidogo!!!

Hotuba ya KUB inakuwa imeendaliwa na kupitiwa kwa umakini kabla haijapelekwa kusomwa Bungeni. Yote aliyoyasema Waziri Kivuli-Habari,Vijana Utamaduni na Michezo Mhe. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugumen.

  1. Hivi ni Mtanzania gani asiyejua kuwa Daudi Mwangosi ALIUWA NA JESHI LA POLISI chini ya usimamizi wa RPC Kamuhanda mwaka jana???
  2. Ni Mtanzania gani asiyejua kuwa Absolom Kibanda alitekwa na watu wa State security(UWT)akang'olewa kucha,meno na kutobolewa Jicho??
  3. Ni Mtanzania gani asiyejua kuwa kiongozi wa Chama cha Madaktari Ulimboka Steven alitekwa na watu wa State security (UWT)?
  4. Ni Mtanzania gani asiyejua kuwa Mhariri wa gazeti la MwanaHalisi ndugu Saed Kubenea alivamiwa na watu akamwagiwa Tindikali pamoja na Mhariri mwenzake Dimara Tegambwage?
  5. Nani asiyejua kuwa Wahariri na vyombo vyao vya habari wanaoandika Habari za kuikosoa Serikali ya CCM wanawindwa usiku na Mchana ili wanyamazishwe????

Watanzania wanajua yote haya. Bunge linatumika kulinda na kuficha Udhaifu wa Serikali ya CCM chini ya Uongozi wa Rais dhaifu Bwana Jakaya Mrisho Kiwete!!!

mie si miongoni mwa wanaoamini kuwa kila kinachowasilishwa na upinzani ni uchochezi. binafsi naamini sana michango ya mzee arfi na zito kabwe. wale jamaa wanashirikisha bongo zao ipasavyo. kuendelea kujadili mambo ambayo yamezuiwa na kanuni za bunge huko ni kukosa uelewa au wanafanya hivyo kwa makusudi ili kujitafutia umaarufu wa kisiasa
 
Nafikiri sahihi hapa ni kuwa Serikali ya CCM ndo inamfanya Dk awe bize kutoa matamko kwa jinsi wanavyongoza nchi kwa remote control
Na kinyume chake pia inaweza kuwa kweli, kwamba CDM wameishiwa hona za kuwashawishi watanzania kuwa wanaweza kuongoza nchi na badala yake wanatumia matamko kama njia ya kuonesha kuwa wanaweza kuongea. SLAA anatamani kurudi bungeni niini, akachukue form 2015
 
Bunge siyo kijiwe ni muhimili wa dola huwezi kuokota maneno mitaani na kuyapeleka bungeni hilo aliwezekani. Bunge limejiwekea utaratibu wake kila mbunge ni wajibu wake kuufuata utaratibu.
Tatizo CCM mmegeuza bunge kama NGO yenu, na mnataka muwapangie watu waseme nini na wafanye nini? Hapa cha msingi ni kwamba bunge linaendeshwa kwa kanuni. Sasa ni vema mueleze ni kanuni gani za bunge ambazo hotuba ya upinzani ilizivunja? Kwanini hamkuacha hiyo hotuba isomwe halafu muombe ushahidi juu ya yale yaliyosemwa? Si kuna kanuni zinazohusiana na kusema uwongo bungeni? Kwanini hamkufuate hizo? Hili bunge la sasa ni la kihuni na linaongozwa kihuni.
 
Back
Top Bottom