Dr. Slaa amuonya vikali Spika Anne Makinda

Dr. Slaa amuonya vikali Spika Anne Makinda

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, amesema ikibidi Bunge livunjike au wabunge wa chama hicho wafukuzwe bungeni, lakini hawako tayari kuzibwa mdomo kuzungumzia masuala yanayohusu maisha ya Watanzania. Amesema chama hicho hakitakubali wabunge wake wapangiwe mambo ya kuzungumza kwa kutegemea busara za Spika au Naibu Spika, bali wataangalia na kufuata maelekezo ya kanuni za Bunge, akisema ndiyo msingi wa uendeshaji wa chombo hicho cha uwakilishi wa wananchi.

Akizungumza katika mikutano ya hadhara iliyohudhuriwa na maelfu ya watu jana katika maeneo ya Ngalangala, Basotu, wilayani Hanang na Haydom, wilayani Mbulu, kuhusiana na hotuba ya Sugu kuahirisha Bunge, Dk. Slaa alisema wabunge wa chama hicho daima wataendelea kuwasemea Watanzania wanyonge ndani na nje ya Bunge. “Moja ni tukio lililotokea leo (jana) bungeni. Kwa wale mliofuatilia mkutano wa Bunge mliona kilichotokea. Ninachotaka kumwambia Spika na wasaidizi wake bungeni ni kwamba Bunge linaongozwa kwa kanuni za bunge, si vinginevyo.

Uamuzi aliofanya wa kuagiza hotuba ya wabunge wetu ipelekwe kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge ni kinyume na kanuni ambazo ndizo msingi wa utendaji kazi wa bunge. Hakuna sehemu yoyote katika kanuni inampatia mamlaka Spika ya kupeleka hotuba ile kwenye kamati hiyo, ili waelekeze nini kisemwe. Hakuna,” alisema Dk. Slaa huku akishangiliwa na umati mkubwa wa watu.

Alisema kuwa baada ya mawasiliano ya viongozi wa juu wa chama hicho na uongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, walikubaliana kuwa kwa sababu hotuba hiyo haikuvunja kanuni yoyote ile ya Bunge, hawatakubali kuondoa au kupunguza neno hata moja.

Source:Nipashe Jumanne.
 
Mimi nadhani uongozi wa bunge uvunjwe wanaendesha bunge kibabe sana. Hawa watu wanajua watatawala milele? Siju wakirudi huko mitaani watakuwa wageni wa nani? Hata wakipelekwa kwenye balozi za nje watazaraulika sana maana kila mtu analalamika kuhusu uongozi wa bunge.
 
Bunge siyo kijiwe ni muhimili wa dola huwezi kuokota maneno mitaani na kuyapeleka bungeni hilo aliwezekani. Bunge limejiwekea utaratibu wake kila mbunge ni wajibu wake kuufuata utaratibu.
 
Bunge,chombo kilichoheshimika sana sasa kimekuwa kichaka cha majangili na magaidi ccm
 
Ni wajibu wa bunge kuisimamia serekali sasa kama bunge haliwezi kuihoji serekali kwa vitu kama ambavyo jana ilihojiwa ni nani ataisimamia serekali?
 
slaa awaonye watembea na sumu hadi bar kwanza ndipo aweze kumuonya spika
 
Just 'cause Dr. Slaa got an opinion does that make him a politician? Jibu ni hapana.
 
bunge haliwezi kuvunjika kwa matakwa yake wala ya walalamikaji, litavunjwa kwa matakwa ya wananchi maskini na wavuja jasho
 
bungeni sio mkutano wa kampeni au mkutano wa hadhara wa chama flani kutafuta umaarufu kwa kupotosha mambo. ni ukumbi wa mikutano ya kutunga sheria za nchi, na kujadili mustakabali wa taifa
 
Bunge siyo kijiwe ni muhimili wa dola huwezi kuokota maneno mitaani na kuyapeleka bungeni hilo aliwezekani. Bunge limejiwekea utaratibu wake kila mbunge ni wajibu wake kuufuata utaratibu.

Ni kweli mkuu, kila mtanzania analifahamu hilo, Bunge ni mali ya Kikwete family & CO. ndo maana Kiti cha spika kinaendesha bunge kwa maelekezo kutoka magogoni. Je kama kuna kanunu na taratibu kwanini hazifatwi ?
 
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.
Willibrod Slaa, amesema ikibidi Bunge livunjike au wabunge wa chama
hicho wafukuzwe bungeni, lakini hawako tayari kuzibwa mdomo kuzungumzia
masuala yanayohusu maisha ya Watanzania. Amesema chama hicho
hakitakubali wabunge wake wapangiwe mambo ya kuzungumza kwa kutegemea
busara za Spika au Naibu Spika, bali wataangalia na kufuata maelekezo ya
kanuni za Bunge, akisema ndiyo msingi wa uendeshaji wa chombo hicho cha
uwakilishi wa wananchi.

Akizungumza katika mikutano ya hadhara jana katika maeneo ya Ngalangala,
Basotu, wilayani Hanang na Haydom, wilayani Mbulu, kuhusiana na hotuba
ya Sugu kuahirisha Bunge, Dk. Slaa alisema wabunge wa chama hicho daima
wataendelea kuwasemea Watanzania wanyonge ndani na nje ya Bunge. “Moja
ni tukio lililotokea leo (jana) bungeni. Kwa wale mliofuatilia mkutano
wa Bunge mliona kilichotokea. Ninachotaka kumwambia Spika na wasaidizi
wake bungeni ni kwamba Bunge linaongozwa kwa kanuni za bunge, si
vinginevyo.

Uamuzi aliofanya wa kuagiza hotuba ya wabunge wetu ipelekwe kwenye
Kamati ya Maadili ya Bunge ni kinyume na kanuni ambazo ndizo msingi wa
utendaji kazi wa bunge. Hakuna sehemu yoyote katika kanuni inampatia
mamlaka Spika ya kupeleka hotuba ile kwenye kamati hiyo, ili waelekeze
nini kisemwe. Hakuna,” alisema Dk. Slaa. Alisema kuwa baada ya
mawasiliano ya viongozi wa juu wa chama hicho na uongozi wa Kambi ya
Upinzani Bungeni, walikubaliana kuwa kwa sababu hotuba hiyo haikuvunja
kanuni yoyote ile ya Bunge, hawatakubali kuondoa au kupunguza neno hata
moja.

Source:Nipashe Jumanne.

Dr slaa yupo makini na huyu Kiongozi wa bunge awe makini na hili jambo.
 
Kila siku anamuonya SPIKA wa bunge. HOW MANY TIMES?. Kwa nini sasa asichukue hatua. Inaonekana Kuonya kwa tafsiri ya Dr. Slaa ndiyo kuchukua hatua butu. Hizi ni kama kelele zisizokuwa na maana ambazo zinakosa hata mwelekeo maalum.

DO SOMETHING or just shuthole.
 
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, amesema ikibidi Bunge livunjike au wabunge wa chama hicho wafukuzwe bungeni, lakini hawako tayari kuzibwa mdomo kuzungumzia masuala yanayohusu maisha ya Watanzania. Amesema chama hicho hakitakubali wabunge wake wapangiwe mambo ya kuzungumza kwa kutegemea busara za Spika au Naibu Spika, bali wataangalia na kufuata maelekezo ya kanuni za Bunge, akisema ndiyo msingi wa uendeshaji wa chombo hicho cha uwakilishi wa wananchi.

Akizungumza katika mikutano ya hadhara jana katika maeneo ya Ngalangala, Basotu, wilayani Hanang na Haydom, wilayani Mbulu, kuhusiana na hotuba ya Sugu kuahirisha Bunge, Dk. Slaa alisema wabunge wa chama hicho daima wataendelea kuwasemea Watanzania wanyonge ndani na nje ya Bunge. “Moja ni tukio lililotokea leo (jana) bungeni. Kwa wale mliofuatilia mkutano wa Bunge mliona kilichotokea. Ninachotaka kumwambia Spika na wasaidizi wake bungeni ni kwamba Bunge linaongozwa kwa kanuni za bunge, si vinginevyo.

Uamuzi aliofanya wa kuagiza hotuba ya wabunge wetu ipelekwe kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge ni kinyume na kanuni ambazo ndizo msingi wa utendaji kazi wa bunge. Hakuna sehemu yoyote katika kanuni inampatia mamlaka Spika ya kupeleka hotuba ile kwenye kamati hiyo, ili waelekeze nini kisemwe. Hakuna,” alisema Dk. Slaa. Alisema kuwa baada ya mawasiliano ya viongozi wa juu wa chama hicho na uongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, walikubaliana kuwa kwa sababu hotuba hiyo haikuvunja kanuni yoyote ile ya Bunge, hawatakubali kuondoa au kupunguza neno hata moja.

Source:Nipashe Jumanne.

Dr slaa hana uwezo wa kuingilia mambo yanayoendelea bungeni. anawaharibia bure wabunge wa chadema na sasa wamekuwa kama wamechanganyikiwa vile. ukiona sugu alivyowasilisha ile speech jana utakubaliana nami kuwa wabunge wa chadema sasa hawatumii hata chembe ya akili yao kufikiri. wanatekeleza tu maagizo ya mkubwa wao bila ya kujua athari zake
 
Slaa inaonekana anaishiwa hoja na nguvu ya kisiasa kwisha aangalie njia nyingine yakuweza kurudi kayika ulingo wa siasa tena.
 
Dr. Slaa anafurahisha sana, hawezi kukaa siku tatu bila ya kutafuta tukio la kutokea nalo kwenye jamii ya Watanzania na akikosa tukio analazimisha ili mradi tumsikie.

Viongozi wa CHADEMA hawana tofauti na RockStars.
 
Bunge siyo kijiwe ni muhimili wa dola huwezi kuokota maneno mitaani na kuyapeleka bungeni hilo aliwezekani. Bunge limejiwekea utaratibu wake kila mbunge ni wajibu wake kuufuata utaratibu.

Una shida gani wewe,unakula, unashiba na unalala......Unachokifanya kwa sasa ni kulinda maslahi tu.POLE VUVUZELA.
 
Wabunge wa CHADEMA wamekuwa kama wamechanganyikiwa. Hawajielewi. Wakaonane na Dr. Kigwangala wapatiwe tiba.
 
Hivi kinga ya bunge huwa ni kwa ajili ya nini?.

Na mbunge akisema uongo bungeni inafuata hatua gani?

Au baada ya kugundua kuwa yanayosemwa sio uongo na wakihitaji ushahidi wataumbuka, wanaona njia pekee ni kuzuia?.
 
Back
Top Bottom