Dr. Slaa amuonya vikali Spika Anne Makinda

Dr. Slaa amuonya vikali Spika Anne Makinda

mkuu,ihi kitu inasikitisha sana mbunge wabunge wa ccm,badala ya kuisimamia serikali wao ndio kwanza wanaisemea sasa watu wanashangaa kazi ya bunge ni nini,

Mkuu kilicho baki nikutoa elimu ya uraia majumbani kwetu watu waelewe tofauti ya mbunge wa ccm na cdm.
 
tiba mimi nilifikili umekomaa kimawazo kumbe bado mchanga kiasi hicho unaeleaelea tu tulia au mpaka upepewe,unaweza kuongea ufisadi bila kumtaja slaa na mbowe? slaa aliiba pesa za kanisa mbona hujatuambia,mbowe anatumia pesa za ruzuku atakavyo na hakuna wa kuhoji akihoja unamfuata chacha wangwe unataka ufisadi gani,pesa za uswis ni nadharia tu zito muhuni anajijengea umaarufu wa uongo kwa kuwahadaa watu na hapo siagusia ufisadi wa wake za watu.

Wewe book 7 sidhani kama ni size yangu, siwezi kuendelea kubishana na wewe!!!!

Tiba
 
...Mbona hawakuahirisha bunge wakati Serukamba anachangia ili kamati ya maadili ikalipitie lile neno lake kabla hajaendelea kuchangia. au hapo kanunu za magamba zinaruhusu.

kanuni zinafanyakazi kwa chadema tu,
 
Kila siku anamuonya SPIKA wa bunge. HOW MANY TIMES?. Kwa nini sasa asichukue hatua. Inaonekana Kuonya kwa tafsiri ya Dr. Slaa ndiyo kuchukua hatua butu. Hizi ni kama kelele zisizokuwa na maana ambazo zinakosa hata mwelekeo maalum.

DO SOMETHING or just shuthole.
Kumbe mlevi wa gongo!!!! Najilaumu kupoteza muda wangu kusoma hii comment
 
Dr slaa hana uwezo wa kuingilia mambo yanayoendelea bungeni. anawaharibia bure wabunge wa chadema na sasa wamekuwa kama wamechanganyikiwa vile. ukiona sugu alivyowasilisha ile speech jana utakubaliana nami kuwa wabunge wa chadema sasa hawatumii hata chembe ya akili yao kufikiri. wanatekeleza tu maagizo ya mkubwa wao bila ya kujua athari zake
Mwigulu anatumia akili nyingi sana akisaidiwa na akina Wasira,Lukuvi,Makinda,Ndugai,hawa ni baadhi ya watu wenye akili nyingi kamamchwa!
MKUU UNAHANGAISHWA LA BUKU SABA TU ZA LUMUMBA.
Tatizo hamsikilizi hata watu mbali mbali wanavyo-comment nje ya mitandao humu,just kwenye kahawa kabisa,kwenye draft,na vijiwe vingine,ni watu wengi sana wanawa-support wabunge wa CDM,na kwa taarifa yako bila wabunge wa CDM hakuna bunge tena Tanzania,na wala hutokuta mtu anahangaika na kuangalia bunge kama sio wabunge wa CDM.hao ndio wanalifanya bunge lionekane bado lipo na ndio tegemeo la wanyonge kwamba siku moja ukombozi wa kweli utapatikana kutoka kwa wakoloni weusi chini ya Maccm.usijidanye kwamba watanzania bado wamelala kwa sehemu kubwa,no tena with capital letter NO!
 
Bunge siyo kijiwe ni muhimili wa dola huwezi kuokota maneno mitaani na kuyapeleka bungeni hilo aliwezekani. Bunge limejiwekea utaratibu wake kila mbunge ni wajibu wake kuufuata utaratibu.

Ungekuwa muungwana sana na mimi ningekuelewa vizuri iwapo tu ungeainisha kanuni ipi ilivunjwa na SUGU na Kambi nzima ya upinzani. Lakini mimi naomba nikusaidie wewe kwani ni wazi hukumwelewa vyema Dr WILBROAD SLAA ni kuwa aliyevunja kanuni ni Spika akisaidiwa na wabunge wenzake wa CCM. Si kuna kanuni inayozuia kusema uongo? Na iwapo kutatokea mbunge atasema jambo litakalotafsiriwa na baadhi kuwa ni la uongo si atatakiwa kuthibitisha hapohapo au kwa kupewa muda maalumu? Je, Spika kwa nini hakuzingatia kanuni hii na badala yake uchama au u-CCM ukafunika kabisa busara na ufahamu wake? Kwa nini Spika hakumpa nafasi Sugu kuthibitisha aliyoyadhania yeye na wenzake wa CCM ni uongo? Yeye Spika na wenzake wa CCM kwa kanuni zipi/ipi wanadiriki kuyabatiza maoni ya Sugu na kambi nzima ya upinzani bungeni kuwa ni uchochezi?????

Hili ndilo tatizo hasa la CCM na Serikikali!!.. Ni waoga tu wa kukabiliana na ukweli na hiki ni kikwazo cha maendeleo yetu ya kiuchumi na kisiasa......Hawa ndo maadui wetu!!....Lazima tuwapinge
 
Bunge siyo kijiwe ni muhimili wa dola huwezi kuokota maneno mitaani na kuyapeleka bungeni hilo aliwezekani. Bunge limejiwekea utaratibu wake kila mbunge ni wajibu wake kuufuata utaratibu.
Kaka mimi sidhani kama umeisoma hotuba ya Sugu,hakuna kilichookotwa mtaani!
 
Bunge siyo kijiwe ni muhimili wa dola huwezi kuokota maneno mitaani na kuyapeleka bungeni hilo aliwezekani. Bunge limejiwekea utaratibu wake kila mnge ni wajibu wake kuufuata utaratibu.
Kaka mimi sidhani kama umeisoma hotuba ya Sugu,hakuna kilichookotwa mtaani!
 
Bunge siyo kijiwe ni muhimili wa dola huwezi kuokota maneno mitaani na kuyapeleka bungeni hilo aliwezekani. Bunge limejiwekea utaratibu wake kila mbunge ni wajibu wake kuufuata utaratibu.

Kama maneno ya serukamba wenu na juma nkamia
 
mm nasubiri cku moja spika na naibu wake watwangwe ngumi, coz wana ubabe wakipumbavu
 
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa, amesema ikibidi Bunge livunjike au wabunge wa chama hicho wafukuzwe bungeni, lakini hawako tayari kuzibwa mdomo kuzungumzia masuala yanayohusu maisha ya Watanzania. Amesema chama hicho hakitakubali wabunge wake wapangiwe mambo ya kuzungumza kwa kutegemea busara za Spika au Naibu Spika, bali wataangalia na kufuata maelekezo ya kanuni za Bunge, akisema ndiyo msingi wa uendeshaji wa chombo hicho cha uwakilishi wa wananchi.

Akizungumza katika mikutano ya hadhara iliyohudhuriwa na maelfu ya watu jana katika maeneo ya Ngalangala, Basotu, wilayani Hanang na Haydom, wilayani Mbulu, kuhusiana na hotuba ya Sugu kuahirisha Bunge, Dk. Slaa alisema wabunge wa chama hicho daima wataendelea kuwasemea Watanzania wanyonge ndani na nje ya Bunge. “Moja ni tukio lililotokea leo (jana) bungeni. Kwa wale mliofuatilia mkutano wa Bunge mliona kilichotokea. Ninachotaka kumwambia Spika na wasaidizi wake bungeni ni kwamba Bunge linaongozwa kwa kanuni za bunge, si vinginevyo.

Uamuzi aliofanya wa kuagiza hotuba ya wabunge wetu ipelekwe kwenye Kamati ya Maadili ya Bunge ni kinyume na kanuni ambazo ndizo msingi wa utendaji kazi wa bunge. Hakuna sehemu yoyote katika kanuni inampatia mamlaka Spika ya kupeleka hotuba ile kwenye kamati hiyo, ili waelekeze nini kisemwe. Hakuna,” alisema Dk. Slaa huku akishangiliwa na umati mkubwa wa watu.

Alisema kuwa baada ya mawasiliano ya viongozi wa juu wa chama hicho na uongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, walikubaliana kuwa kwa sababu hotuba hiyo haikuvunja kanuni yoyote ile ya Bunge, hawatakubali kuondoa au kupunguza neno hata moja.

Source:Nipashe Jumanne.

hivyo ndivyo kiongozi anapashwa kuwa, mtu akienda hovyo unakemea mara moja sio kuchekacheka
 
Back
Top Bottom