Dr. Slaa amkosoa Rais Kikwete kuhusu Rwanda

Dr. Slaa naye hapo amechanganya mambo, kwa mujibu wa gazeti la Nipashe anadai JK alitakiwa awaite Kagame na wapinzani wake ili awapatanishe; kwa madai kuwa Kagame hawezi kuongea na wauaji wa watusi. Ili mtu yeyote awe ktk nafasi ya kuwapatanisha maadui ni lazima kwanza watu hao wakubari kuongea na kupatanishwa, kwa hiyo hoja ya JK ya kumtaka Kagame aongee na waasi inaweza kubaki sahihi! Sijaona nguvu na mantiki ya hoja ya Slaa hapo.
 
ishu ya samaki wa mapanki jei kei(jah kaaya) aliwaka kweli na yeyote aliempinga alionekana mnafiki mwanzo kabisa enzi hizo ari mpya na nguvu mpya ilikuwa kwenye chati haya sasa si mliumbuka kwa ukweli au mshasahau hata hii ya kagame ni swala la muda tu baadae mtajua jah kaaya alichemka
 
Rock City,
Usiwadanganye Watanzania. Tishio la Tanzania halijadiliwi katika Mtandao. Ni muhimu Kama mtu huelewi jambo aka kimya. Kama kungelikuwa na Tishio la Watanzania kushikamana, kwa mujibu wa Katiba, Bunge japo Kamati ya Ulinzi ingelihusishwa. Pili Taifa kujulishwa juu ya Tishio Hilo. Hapo ungelizungumzia Uzalendo. Hapa tulipo tatizo ni kuwa Mambo yanajadiliwa kwa ushabiki, na kinachoonekana dhahiri nimkulinda " dhaifu" kwa udhsifu wake. Hamsaidii, mien mwenzenu ushauri mzuri. Narudia, nchi haitaenda vitamin tu kwa kauli ya marais wawili, ambao kimsingi wanajibizana wao. Simamia principle, mtu ukikosea na ulimi huteleza omba msamaha. Dhambi ni nini kuomba msamaha! Kwa hakika aliyejifanya mpatanishi kwa majirani wakati kwake kuna bomoka, safari hii kapatikana. Hakuna pa kujifichia. Nilikwisha sema, iwapo Kagame atashambulia Tanzania kwa ajili ya kiongozi mwenzake, watanzania kwa ujumla wetu tutanyanyuka na kuilinda nchi yetu. Naanza kupata hisia kuna zaidi ya Kauli? Kuna nini nyuma ya Pazia wakati JK anaelekea kwa kauli yake tayari amenyoosha mikono yake!

Wewe mtu usiyeshaurika leo ndio unazungumzia umuhimu wa kuomba msamaha?!!!

By the way, kwenye swala hili unajiabisha tu. Watanzania hawako radhi kulaghaika na porojo zako, wakati wamesikia maneno aliyoyatoa Kagame juu ya nchi yetu na Rais wake. Kama una deal na Kagame basi jua umeshapotea. Wewe na rafiki yako Kagame wote tutawadefeat...

Kagame ni muuaaji, hujui hilo?

Lini uliomba appointment na Rais kujadili swala la kitaifa ukakataliwa?
 
Slaa MNAFIKI sana, ndio maana hata goti lake hawezi kulikunja!!!

View attachment 105631
Na wewe ni MPU.MBA.VU. sana kama siyo mjinga! Au ukiwa magamba hata uwezo wa kufikri unakuwa sawa na akili ya maiti?

Matembezi ya kuchangisha pesa kwa ajili ya ujenzi wa Hospital ya CCBRT yana uhusiano gani na ushauri alioutoa mzee Slaa? Maana naona unatuwekea picha ya matembezi ya uchangishaji fedha au unafikiri sisi hatujui? Ukae ukijua kwenye hayo matembezi mzee Slaa hakuwa kama mpinzani bali kama mmoja wa board members wa CCBRT. Nyamb...ff!
 
Mzizimkavu,

This is too cheap. Kumbe kukosoa udhaifu ni kuunga mkono upande wa pili! Wenye kujua principles watanielewa. Ukifanya makosa lazima tutakuambia, ndio maana wakati wa EPA tuliwasema hadharani, bila kumumunya maneno. Wangapi wakati ule walituunga mkono! Tusingelikuwa majasiri tungekata tamaa. Tulishikilia, na hata sasa ninaamini kauli ya JK haina uhusiano na kuunga mkono upande wa pili! Hata wakati wa EPA tuliambiwa hatuna uzalendo, tunaaibisha Taifa, oh tutakosa misaada, oh! Oh! Oh, Taifa lisilo na watu wenye principle au misimamo linaenda kaburini.
 
Na wewe ni MPU.MBA.VU. sana kama siyo mjinga! Au ukiwa magamba hata uwezo wa kufikri unakuwa sawa na akili ya maiti?

Matembezi ya kuchangisha pesa kwa ajili ya ujenzi wa Hospital ya CCBRT yana uhusiano gani na ushauri alioutoa mzee Slaa? Maana naona unatuwekea picha ya matembezi ya uchangishaji fedha au unafikiri sisi hatujui? Ukae ukijua kwenye hayo matembezi mzee Slaa hakuwa kama mpinzani bali kama mmoja wa board members wa CCBRT. Nyamb...ff!

Lini Dr. Slaa au chadema waliomba appointment ya kuongea na Rais Ikulu wakakataliwa?

Hujui Mbowe alikuwa Ikulu juzijuzi kujadili mustakabali wa masuala mbalimbali?

Unajua wapinzani wa Kagame wanaishi katika mazingira gani?
 

Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, amemkosoa Rais Jakaya Kikwete, kuhusu kauli yake ya kumshauri Rais wa Rwanda, Paul Kagame, kuzungumza na waasi wa serikali yake ...


Dk. Slaa amesema haoni busara kwa Rais Kikwete kuwaambia viongozi wa Rwanda, akiwamo Rais Kagame, kuzungumza na wafuasi wa chama cha FDRL walioko Congo.

Slaa aliyasema hayo wakati akizungumza katika kongamano la vijana wa Chadema (BAVICHA) la uchumi na ajira lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.

“Rais Kikwete hapa nyumbani hawezi kuzungumza na wapinzani na hajachukua hatua dhidi ya wauaji wa mwandishi Daudi Mwangosi...


"Alishauriwa amuwajibishe Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda na badala yake amempandisha cheo,” alisema Slaa.


Kauli Dk Slaa imekuja siku moja baada ya Rais Jakaya Kikwete kueleza kuwa Tanzania haina mgogoro na nchi ya Rwanda, kutokana na kauli za kejeli na matusi zilizokuwa zikitolewa na viongozi wa nchi hiyo dhidi yake na Tanzania.



Kumezuka sitofahamu ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Rwanda, baada ya Rais Kikwete kuitaka Rwanza imalize ugomvi na waasi kwa njia ya mazungumzo ya amani...

Rais Kikwete aliutoa ushauri huo wakati wa mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia hivi karibuni.

Ushauri huo ulionekana kumchukiza Rais Kagame, anayedaiwa kuhutubia mikutano kadhaa nchini kwake na kutumia lugha ya matusi, kejeli na dhihaka dhidi ya Rais Kikwete na Tanzania.


Kitendo cha Dr Slaa kumkingia kifua Kagame kinatia shaka uzalendo wake na chama chake kwa taifa hili ...

Sote tumekuwa tukishuhudia matusi ya Kagame dhidi ya Tanzania.Iwaje Rais Kikwete aonekane mbaya kwa kumjibu Kagame, tena kwa lugha ya kizalendo??


Kagame amekuwa akituhumiwa na jumuiya mbalimbali za kimataifa kwa kutoa misaada ya kivita kwa waasi wa M23 ambao wamekuwa wakiua raia na kuwabaka wanawake....


Kauli ya Dr Slaa ina mambo mengi yaliyojificha na huenda yeye na chama chake ni wafuasi wa karibu wa M23 kama ilivyo kwa Kagame.

Kuwa mpinzani, haimaanishi ukosoe kila kitu.

chanzo.
WANYARWANDA WAANZA KUREJEA MAKWAO BAADA YA RAIS KIKWETE KUWAPA SIKU 14 ZA KUONDOKA

Ish we unamshangaa huyo mhaini?
 
Wewe ni mpuuzi na wakupuuzwa kama wahuni wenzio tu wanaoganga njaa hapa mtandaoni,

Umehama MMU sasa unadandia jukwa la siasa kijana?

Mods

Unganisheni ----- huu na uzi halisi wa "Dr Slaa ampinga jk",
 
Dr. Slaa sio kosa lake. Uwezo wake wa kufikiri umekuwa wa kiwango cha Josephine Mushumbusi.

Anasema Kikwete haongei na wapinzani wakati Slaa ameonekana mara kadhaa Ikulu akinywa juice. Sasa sijui walikuwa wanakunywa juice kimyakimya!!!

View attachment 105628

unajua wakati mwengne ukizeeka sana akili znapotea,huyu mzee ni mropokaji...kikwete rais makini.hakurupuki kama slaa
 
Sijaelewa alichojibu slaa hapa,kakanusha kuunga mkono au kakubalia anaunga mkono Rwanda? Hebu nifafanulieni haya mambo naona tunashindwa kutofautisha mambo ya kitaifa na kimataifa,
Kwa sababu mgogoro wa Rwanda tunachanganyiwa na habari za mwangosi hapa sielewi kabisa hawa wanasiasa wetu wana rangi gani.
 
Dr. Slaa Ameweka wazi kwamba, Kikwete ni Mnafiki. Asijifanye kutoa ushauri kwa Kagama wakati yeye mwenyewe hataki kuongea na wapinzani huku kazi yake ni kumtuma Ghaidi Mwigulu kuwalipua na Mabomu.......
 
Dr.W.Slaa,

Mimi nadhani kwenye hili sakata la malumbano ya kagame dhidi ya Kikwete usilifanye la kwao, kwani nimeona hoja yako inaonyesha wazi kuwa malumbano hayo ni baina ya Kikwete (umeuvua uhusika wake kama kiongozi wa nchi) na Kagame.

Hili suala halipaswi kufanywa ni jambo binafsi la Kikwete, Dr Slaa unapaswa uelewe kuwa kikwete akitoka nje ya mipaka ya Tanzania ana kuwakilisha mpaka wewe huko ughaibuni, hivyo anapotokea mtu yeyote na kumkashfu au kumtangazia uhasama Kikwete basi ujue mpaka wewe umejumuishwa.

Ningependa kuona kwenye hili suala tushikamane kama watanzania na tuwe kitu kimoja, si vyema kuingiza tofauti zetu za kisiasa na kiitikadi kwenye mambo yanayo gusa usalama na ulinzi wetu, hapa ikitokea vita sidhani kama kuna mtu atakumbuka u-CCM au u-CHADEMA, ila utasikia watu tukililia taifa letu Tanzania.

Jambo lingine, Dr Slaa una mdhihaki kikwete kuwa ana jipendekeza kufatilia mambo ya watu wengine ilhali ya kwake yamemshinda, sidhani kama ulikuwa makini wakati ukieleza haya, ila angalau ungejisumbua kidogo kuzijua nafasi za kikwete zaidi na urais tu, ni mwenyekiti wa mambo ya usalama (SADC) kwenye nchi za kusini mwa Afrika, hivyo kushauri Rwanda ni sehemu ya majukumu yake, na hata wewe sidhani kama umezuiliwa kwenda kufanya majadiliano na Kikwete, kama amewahi kufanya hivyo wenda unaweza ukawa na hoja ya msingi.
 
Last edited by a moderator:
Duuh.. kweli this's too low coming from u MziziMkavu.. Maana according to ur bandiko hapa Dr. Slaa amesema haoni busara kwa kauli ya JK kumuambia PK azungumze na magaidi wakati huku anashindwa kulifanya lile analolishauri kwa mwenzie.. Unaita huko ni kukosa uzalendo..? Hivi kweli kichwa cha habari kinaendana na maudhui..?
 
Last edited by a moderator:
Kwa kuwa slaa unauwezo wa kuropoka sana naomba uropoke na majina ya mtandao wa madawa ya kulevya nauhakika unawajua na kwa uzoefu ulionao ktka kuropoka naamini hili halitakushinda naamini kwa sifa nyingi utazolipatia taifa hili sidhani kama hatutajuwa ukweli ila kama unaona ni siri tutakuweka kundini natuamini upo kwenye mtandao huo ok tiririka slaa
 
Mzizi mkavu nafikiri nia ya kuandika hapa JF ni kutaka kuwaeleimisha watanzania. sasa mbona unataka kuwapotosha basi. Dr. anaeleweka kabisa. Kiongozi ambaye hayuko tayari kuwasikliza wapinzani ndani ya nchi yake pia na kuangalia wanavyo nyanyaswa na vyombo vya dola anapata wapi busra na umakini wa kutoa ushauri kwa kagame ili aongee na wapinzani!!!!!!!!!!!!!!!!!! Double standard hapa hakuna cha uzalendo ila wewe mleta maada hii u mnafiki tu!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom