Dr. Slaa amkosoa Rais Kikwete kuhusu Rwanda

Dr. Slaa amkosoa Rais Kikwete kuhusu Rwanda

For your information katika hili suala la Kagame nimeanza kumpinga Kikwete hata kabla ya Slaa kusema aliyoyasema juzi. Mimi siyo kama wewe ambaye unamtetea Kikwete kama vuvuzela hata pale anapoboronga. Na katika hili nimefurahi Mzee Slaa ana maoni yanayoshabihiana na yangu.
lazima mushabihiane katika maoni because you belong together... wote ninyi ni MAADUI WA TAIFA LETU na akili zenu zimeshikiliwa na akina MUSHUMBU........
 
lazima mushabihiane katika maoni because you belong together... wote ninyi ni MAADUI WA TAIFA LETU na akili zenu zimeshikiliwa na akina MUSHUMBU........
Kwa hiyo nyie CCM wauza unga ndio marafiki wa taifa?
 
Kwa hiyo nyie CCM wauza unga ndio marafiki wa taifa?
Muulize FREEMAN na GODBLESS.
CHEZEA MANGI WEWE!!!! ni mwendo wa kukamuliwa ndimu mpaka mpofuke mioyo.. maana hapo mlipo akili,macho na ubongo ushapofushwa
 
Muulize FREEMAN na GODBLESS.
CHEZEA MANGI WEWE!!!! ni mwendo wa kukamuliwa ndimu mpaka mpofuke mioyo.. maana hapo mlipo akili,macho na ubongo ushapofushwa
Idd%20Azan2.jpg

Mbunge wa Kinondoni (Chadema), Godbless Lema lol!!, amesema yupo tayari kupigwa risasi au kunyongwa hadharani kama itathibitika anahusika na biashara ya madawa ya kulevya'.
 
Kila jambo linahitaji hekima. Mi naunga mkono dr Slaa kumkosoa kwani yakwake yamemshinda. Kwann asikubali kuunda tume huru ya kijaji ili awe mwanadiplomasia na mpenda demokrasia wa kweli? Huoni jinsi uchumi wa Rwanda unavyopaa?
 
For your information katika hili suala la Kagame nimeanza kumpinga Kikwete hata kabla ya Slaa kusema aliyoyasema juzi. Mimi siyo kama wewe ambaye unamtetea Kikwete kama vuvuzela hata pale anapoboronga. Na katika hili nimefurahi Mzee Slaa ana maoni yanayoshabihiana na yangu.

Kwa akili hizo mimi siwezi kuwa wewe hata siku moja labda ujifananishe na mtoto wangu 5th grade!
 
Jk yupo sahihi . Tuache ushabiki wa kisiasa penye ukweli tisipotoshe simply tuonekane tupo juu! wht is wrong wth JK?
sometimes tuache kuendekeza chuki za kijinga we'r mature!
 
usichukulie kwamba samaki mmoja akioza wote wameoza! u can simply say CCM ni wauza unga! are u mad?
mwakyembe, magufuli, filikunjombe, kina kangasheki ni wauza unga? acha uzembe wa kufikiri wewe!
basi hata silaa, Lisu, Kambe watakua hivyo kama ni kumtuhumu mtu kilahiso hivyo!
 
Kwa hili Babu umepotoka,naona unazeeka vibaya.JK alikuwa sahihi kabisa kusema hilo,Kagame hataki kupambana kwa sababu zake binafsi ni mkweli usiopingika hataki mupinzani nchini kwake ndo maana wapinzani wengi wamefungwa Rwanda na Jenerali Nyamwasa kutaka kuuwwawa na agent wa serikali yake kwa kuanza kumpinga akiwa kama balozi wa nchi ya Rwanda

Serikali ya Tanzania inwapa uhuru nyinyi akina Silaa Uhuru wa kupita kiasi ambao humom kwenu Chadema haupo,nani asiye jua kuwa Kafulila alifukuzwa CDM kwa suala la kuhoji demokrasia,na pia mlitaka kumfukuza ZITO kwa kuwa alitaka kugombea uenyekiti wa CDM

Nini chanzo cha kifo cha Chacha Wangwe ambaye alikuwa amejipanga kugombea uenyekiti wa CDM

Acha hizo,na kwa sasa Tanzania tunahitaji Rais mwenye muono wa mbali kiuchumi na sio mpiga kelele

....Nterahamwe!
 
Hoja ya Dr. Slaa ilikua kwamba Nchi haiwezi kuwa dragged vitani kwa sababu ya kauli ya Kikwete na vile vile akashsuri Kikwete aanze kwanza kukaa na wapinzani wake.

Aende kwanza yeye na familia yake wakiisha uawa ndo tumuulize kagame kama anataka kuendelea au anaona imetosha, akitaka kuendelea tutaingilia kati, akisema inatosha hatuna haja kugombelezea kiherehere cha mtu hata awe nani
 
Boss, kwani sisi tuna waasi? System tulizonazo inclusion iko automatic, tunga Bunge! Wapinzani na chama tawala wanajadiliana. Tuna taasisi ile ya vyama vienye wabunge bungeni inayoongozwa na Mh. Mbatia kote huko vyama vyote vinashiriki vinavyotaka.

Tuna majukwaa ya kisiasa ambapo kila mtu au chama viko huru kuongea lolote?


Tuko kwenye mchakato wa Katiba vyama vyote vinashiriki na CDM ifika mahali ikaenda ikulu...

Swali: Mnamtuhumu Kikwete kwamba haongei au hashirikishi wapinzani, niambieni mnatakiwa kufanyiwa nini?





Hapa ndio huwa nafika naona nchi hii ina wapumbavu kupitiliza, hivi mateso wanayopata watanzania huyaoni chini ya uongozi wa huyo baba yako;
Kwa taarifa nilimpigia kura mwaka 2005 kwa upendo mkubwa sana nikiwa si mwanachama wa chama chochote cha siasa, nilisafiri umbali mrefu kumpigia kura kwa gharama zangu mwenyewe nikitegemea makubwa sana toka kwake lakini akili yake na ile yako haina tofauti hivi huoni kwamba watanzania wanauwawa yuko kimya, watu wanatekwa kimya, watu wanamwagiwa tindi kali kimya, Mwigulu anachezea uvumilivu wa watanzania munao uita amani kimya, wabunge wake wanachezea maisha ya watanzania kwa kupiga kura ya ndiooooooooooooooooooooooo kimya(ulisha wahi kusikia wanapiga kura ya hapana nikupe zawadi? au serikali ni malaika haikosei) kimya, watu wanapigwa na mabomu kimya, unasema majukwaa ya siasa na bunge sehemu zilizojaa matusi na vijembe ndio unajivunia chinin ya uongozi wa baba yako pole sana!
Ndg yako asipo kaa kimya huwa anaonya sasa anashauri wenzie kukaa na waasi haoni matatizo ya hapa kwetu ya watu kufa na kupigwa na mabomu?
kuna tofauti gani ya mtu anaye uwawa Rwanda na bomu lililorushwa na waasi na anayekufa hapa kwetu kwenye mkutana wa hadhara kwa kurushiwa bomu na mtu asiyejulikana vyombo vyote vya usalama vipo nchini na vinatumia kodinzetu mbona hakukaa na watuhumiwa aongee nao(cdm, ccm,polisi,dini,n.k)
Acheni ushabiki usio kuwa na tija. Unatetea mtu ambaye tunaapa kumshitaki baada ya kustaafu kwa vifo na vilema alivyowaachia watanzania, kuuza mali za watanzania kwa watu weupe(wachina, wamarekani n.k) kila mwezi viongozi wastaafu wa marekani wako hapa nchini! watu wamepoteza maisha Mtwara kisa gesi!
Ngoja nikwambie ujue toka leo achana na maoni ya wana siasa, JK anatukosea sana mimi, wewe na vizazi vyetu amini usiamini tutakuja kuchekwa na vizazi vijavyo kuwa hatukuwa na uwezo wa kufikiri!
Mtu tuliyempa dhamana hata uteuzi wa mawaziri ana bahatisha kuwa huyu labuda anafaa mawaziri wake wakuu wote kichefu chefu mara mwingine mwizi alijiuzuru sasa anasaka uraisi kwa udi na uvumba anatumia fedha nyingi kujinadi kila mtu aone anakubalika anahonga watu kusambaza ujumbe kuwa anafaa kila kona iwe fb, jf hukosi sura yake kisa muone anapendeka watu tunaujua ukweli akiwa raisi ntaishi ukimbizini mpaka anasitaafu!, mwingine ni mtu wa piga tuuuuuuuuuuuu!
Sasa watanzania wanapigwa tuuuuuuuuuuu!!!!!!!!!! Ponda nasikia kapigwa tu! mawaziri ndo usiseme hicho kizazi mimi nasema wote uchaguzi ujao watanzania wangewapiga chini wote waliowahi kuwa mawaziri wa JK. maana hawana jipya wizi mtupu!
Mimi najua JK nafasi yake anapwaya na kwa kuwa mawaziri na wateule wake ni watu wa karibu naye sasa hawana tofauti maana watu wako wa karibu lazima mshabiane karibia asilimia 75, Tunasubiri waichezee nchi hasa kupitia katiba mpya mwisho wa siku tunawapeleka kizimbani!!!! kila kukicha mapya wameanzisha mchakato wa katiba sasa tena wanalazimisha mawazo yapite matakwa yao!
Hii nchi ni yetu sote tunasikitika kuona madawa ya kulevya yanatuchafua na Raisi anasema anawajua kwa nini sasa huchukui hatua? raisi anaonya i hadmajambazi kuwa nawapa wiki mbili mjisalimishe!!!!!!!!!! Raisi unaonya lini sasa unachukuwa hatua!
Kodi yetu ya kumpeleka Adis Ababa hatukumpeleka akatatue matatizo ya Rwanda au atugombanisha na nchi yeyote ile bali tulimpeleka ahakikishe watanzania tuko salama, masilahi yetu yanalindwa lakini pia tunanufaika kiuchumi, kisiasa,kitechnologia n.k siyo kutuingiza kwenye migogoro!!
Unauliza kama tuna waasi, kama watanzania wanafanyiwa matendo sawa na wanayo fanyiwa wananchi wa nchi zilizo na waasi unaulizaje swali la kijinga kama hilo?
Hujui wandishi wa habari wanatekwa na wengine kuawa?, hujui watu wanamwagiwa tindikali? hujui watu wanapigwa tu mabomu na risasi za moto? hujui watu wanatuhumiana kwa ugaidi hadi wanarumbana bungeni na Mwigulu anasema ana ushahidi na magaidi anawajua?
 
Hoja ya Dr. Slaa ilikua kwamba Nchi haiwezi kuwa dragged vitani kwa sababu ya kauli ya Kikwete na vile vile akashsuri Kikwete aanze kwanza kukaa na wapinzani wake.

Kwani ni Mara ngapi wakina mbowe wameenda kula kuku ikulu,acheni kuaminishwa hats vitu vilivyo wazi AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO
 
Dr Slaa alimwambia ukweli Kikwete kwamba aliboronga katika mkutano kule addis ababa kwa kumshauri Kagame, “akae na waasi m23 wazumgumze”
Kikwete alipaswa azungumze kwanza na mwenzake Kagame maongezi ya faragha kabla ya kumtaka afanye hivyo hadharani.
Hatimaye Kikwete ameamua kuzungumza na mwenzake Kagame baada ya kupondwa na Dr Slaa. Serikali iliamua kumuomba Museveni apatanishwe na Kagame, baada ya kuona maji yanazidi unga.
Kweli Dr Slaa ndiyo tumaini jipya la watanzania, Kikwete aliamua kulikoroga mwenyewe na hivyo ameamua kulinywa.

MY TAKE: FALSAFA YA HAYATI BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE ALISEMA “KWA UAMINIFU IKULU NI MZIGO MZITO ”
MCHUNGAJI PETER MSIGWA ALISEMA KWELI “AKILI NDOGO HAIWEZI KUONGOZA AKILI KUBWA”
 
Usiseme dr slaa sema raisi mtarajiwa. Namkubali sana dr slaa hakika huwa hakurupuki.
 
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, amemkosoa Rais Jakaya Kikwete, kuhusu kauli ya kumshauri Rais wa Rwanda, Paul Kagame, kuzungumza na waasi wa serikali yake.

Dk. Slaa amesema haoni busara kwa Rais Kikwete kuwaambia viongozi wa Rwanda, akiwamo Rais Kagame, kuzungumza na wafuasi wa chama cha FDRL walioko Congo kwa vile wanatambulika kama wauaji.

Alisema hayo wakati akizungumza katika kongamano la vijana wa Chadema (BAVICHA) la uchumi na ajira lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Alimshangaa kuwataka kuzungumza na watu ambao Kagame anawaita wauaji wenye asili ya kundi la jeshi la Nterahamwe, lililokuwa linaangamiza Watutsi.

“Rais Kikwete hapa nyumbani hawezi kuzungumza na wapinzani, hajachukua hatua dhidi wauaji wa mwandishi Daudi Mwangosi, alishauriwa amuwajibishe Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda, amempandisha cheo,” alisema.

Alisema Rais alitakiwa kuwaambia waje awapatanishe lakini si kuwaambia wazungumze na watu anaowatuhumu kuua Watutsi.

Kumezuka sitofahamu ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Rwanda, baada ya Rais Kikwete kutoa ushauri huo wakati wa mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia hivi karibuni.

Ushauri huo ulionekana kumchukiza Rais Kagame, anayedaiwa kuhutubia mikutano kadhaa nchini kwake na kutumia lugha ya matusi, kejeli na dhihaka dhidi ya Rais Kikwete na Tanzania.


CHANZO: NIPASHE

DR slaa aliapa kumkataa kikwete kwa lolote,
 
Back
Top Bottom