Dr. Slaa amkaanga Lowassa, adai hana hadhi ya kuomba Kura za Wananchi

MBONA LOWASA anapewa PROMO isiyomstahili sioni jipya lake na hata ukimsikiliza hana ushawishi mkubwa zaidi ya kupita kwenye nyumba za ibada tu!
Kuhusu point yake ya ajira kwa vijana leo waziri mhusika ana mkaba koo, so no more from him.
 
Anaenda kumkampenia mkwewe ili mbio za urais 2015 ziende vizuri
 
Nimeuliza swali.
Nijuavyo mimi hakuna swali la kijinga au swali tusi.

Watu wengine humu ni very senior member wa JF lakini wanashindwa kuongoza. Sasa hapa aliyejiunga Jan-March 2012 au anayetegemea kujiunga umemfundisha nn?? ni picha gani unafikiri unaipa JF??. Always Listen to yourself twice before you post anything!
 
KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa jana alimtolea uvivu Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa akisema hana hadhi ya kusimama mbele ya wananchi kuwaomba waipigie kura CCM kwani anakabiliwa na tuhuma ambazo hazijawahi kusafishwa.

Akizungumza katika mikutano ya hadhara kata za Songoro, Kikwe na Mbuguni, Dk Slaa alisema anamweka kiporo Lowassa akisubiri kwanza apande jukwaani kumnadi mkwewe Sioi Sumari.

Kauli ya Dk Slaa inafanana na ile iliyotolewa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe mwishoni mwa wiki iliyopita akisema kwamba chama chake hakimwogopi Lowassa kwa sababu ni kama makada wengine wa CCM akiwamo Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa.

Kauli ya Dk Slaa inakuja huku taarifa zikieleza kuwa Lowassa ametua rasmi katika jimbo la Arumeru Mashariki kwa ajili ya kumnadi mgombea wa CCM katika uchaguzi mdogo wa ubunge, Sioi Sumari.

Habari ambazo Mwananchi lilizipata jana na kuthibitishwa na watu wa karibu na Lowassa zilisema Mbunge huyo wa Monduli (CCM) aliwasili jana majira ya jioni akitokea Ifakara, wilayani Kilombero mkoa wa Morogoro.

Lowassa alikuwa Kilombero alikokwenda kushiriki sherehe za kumwingiza kazini Askofu wa Jimbo jipya Katoliki la Ifakara, Salutaris Libena pamoja na uzinduzi wa Jimbo hilo.

Hata hivyo haikuweza kufahamika mara moja ni lini kiongozi huyo anayetajwa kuwa na ushawishi mkubwa katika siasa za Arumeru atapanda jukwaani kwa ajili ya kumnadi Sioi ambaye anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mgombea wa Chadema, Joshua Nassari.

"Kweli mheshimiwa Lowassa yupo hapa, hilo nina uhakika nalo wala halina ubishi wowote, sasa ratiba nyingine siwezi kufahamu maana haijawekwa wazi kwa watu wote, lakini tusubiri maana kesho (leo) huenda ratiba ikapatikana," alisema mmoja wa viongozi wa CCM jana.

Habari zaidi zilisema upo uwezekano mkubwa wa Lowassa kuendesha mikutano ya ndani kwa lengo la kuwashawishi wazee kukipa ridhaa CCM katika uchaguzi huo mdogo utakaofanyika April 1 mwaka huu.

Kiongozi mwingine wa juu ndani ya CCM ambaye pia hakuwa tayari kutajwa alisema: "Sidhani kama Lowassa atapanda jukwaani sasa, anaweza kuamua kufanya mikutano ya ndani na ikiwa ataona mambo yana uelekeo mzuri ndipo atapanda jukwaani".

Hata hivyo wachambuzi wa mambo wanasema huenda kiongozi huyo akapata wakati mgumu kuwashawishi wazee ambao wana mtizamo kwamba msingi wa Lowassa kumpigia debe Sioi unatokana na kwamba ni mkewe anayemwoa mtoto wake, Pamela Lowassa.

Gazeti hili jana lilimtafuta Lowassa kupitia simu yake ya kiganjani lakini ilikuwa ikiita muda wote bila majibu.

source.
Dk Slaa: Mkataeni Lowassa akipanda jukwaani

Ukitaka kujua taarifa ya uongo angalia maandishi mekundu hayo na kwa wale ambao hawajui hili basi leo nawafungua akili zenu. Hata waandishi wa habari wa uongo utawajua, siku zote taarifa za haziko accuracy, consistency wala precise.
"Habari ambazo zilipatikana jana na kuthibitishwa na watu" watu gani? akina nani?
"Alisema mmoja wa Viongozi wa CCM jana" nani huyo ? mtaje tuthibitishe taarifa yako, una sababu gani ya kuogopa kumtaja? uongo huo.
Kiongozi mwingine wa juu wa CCM. Mwongo anarudia maneno yale yale.

"Hata hivyo wachambuzi wa mambo wanasema" teh teh teh , kweli inabidi nicheke kwa sababu hii ni kama comedy, hivi wewe ni mwandishi? mchambuzi? au umeamua kutengeneza taarifa yako, maandishi ya rangi si ndo kozi umetoka kusomea juzi juzi pale Buguruni Malapa kwa udhamini wa hao hao na ukafundishwa jinsi ya ku-format document?

Angalia sasa unavyojichanganya hapa " Gazeti hili" wapi umeandika jina la gazeti?
Unaharibu kabisa unaandika source:Dk Slaa: Mkataeni Lowassa akipanda jukwaani. sasa hapa tushike lipi ? source ya taarifa yako ni hiyo link au gazeti ambalo hata hujalitaja?
 
the person we thought was buried back in 2008 has risen from the dead and gaining popularity than the president himself!!!!now i believe this old gray haired man was playing president from the back door.
 
Lowassa ameanza kampeni kama kawaida yake. Watu wengi awamuelewi lowasa. Lowasa hatumii mara nyingi majukwaa kama wanasiasa wengine kutaka anachotaka. Ni mtaalamu sana wa kutengeneza mitandao na ikafanya kazi nzuri katika anachokihitaji. Kama itabidi kutoa hela ili kushinda hela itatolewa. Kama ni kumchamfua mtu kama walivyofanya kwa Salim watafanya hivyo. Na hata kama itabidi mtu/watu wapotezee maisha ili mtu wake ashinde kitafanyika. HUYU NDIO LOWASA.
Kama uamini kamuulize Kikwete na timu yake baada ya kuhama mtandao wa lowasa kama issue zao zinakwenda. Mgombea ubunge mwenyewe wa arumeru ni wa kambi ya lowasa pamoja na mwenyekiti wa chama kutokuwa uapnde wake ila walishindwa kumuengua.
 
21 MARCH 2012




  • Asema wanakimbilia makanisani kujisafisha

  • Ataka fedha zao zikataliwe zimejaa najisi
  • Asisitiza michango wanayotoa haina uhalali
  • NEC yatoa karipio kwa CCM, CHADEMA


Na Queen Lema, Arumeru

VIONGOZI wa makanisa nchini
wametakiwa kuwakimbia wanasiasa
ambao wanafanya ufisadi kwenye
miradi mbalimbali ya wananchi
na kisha kukimbilia makanisani
kujisafisha.

Kauli hiyo ilitolewa na Katibu wa
Mkuu wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA)
Dkt. Willibrod Slaa jana wakati
akihutubia mkutano wa kampeni
eneo la Migandini akimnadi
mgombea ubunge wa chama hicho,
Bw. Joshua Nassari.

Dkt. Slaa kwa nyakati tofauti
alisema kila fisadi wa Tanzania
a n a k i m b i l i a m a k a n i s a n i
kujisafisha. Alisema mafisadi hao
wanaokimbilia kwenye madhabahu
wanatia najisi makanisa kwa
kuwa fedha na michango ambayo
wanatoa haina uhalali, bali ni mali
ya Watanzania ambao wanateseka.

"Kila mara unasikia wanaenda
makanisani kutoa misaada ya
mamilioni ya fedha, lakini hizo
fedha si halali... sasa kama si
kutumia jina la Mungu kwa njia
chafu ni nini? Nawasihi ninyi
wachungaji kamwe msikubali
kupokea fedha za mafisadi ambao
wamegundua mbinu mpya ya
kujisafishia makanisani," alisema
Dkt. Slaa.

Aliongeza kuwa endapo
wachungaji wataendelea kuwapokea
mafisadi hao katika makanisa na
madhehebu yao ni wazi wananchi
wataendelea kupata shida kubwa,
huku nchi nayo ikikosa haki zake
za msingi.

Katika hatua nyingine meneja
kampeni wa mgombea wa chama
hicho, Bw. Izrael Natse, alisema
kuwa kwa sasa wapo baadhi ya
wanasiasa ambao wanatumia neno
la Mungu kufanya maasi.

Bw Izrael aliongeza kuwa
mchungaji ambaye ameitwa kwa
jina la bwana hapaswi kuhongwa
kwa kupewa rushwa ambayo
inalenga kukosesha jamii haki za
msingi, bali mchungaji ambaye
ni imara ni yule ambaye anapinga
ufisadi na wizi ndani ya jamii.

"Leo hapa tuna uchaguzi lakini
wapo wanasisasa ambao wanafanya
kampeni hadi kwenye nyumba
za ibada na kwa maana hiyo
wanawateka wachungaji, sasa
mimi nawaambia kuwa viongozi wa
dini hakikisheni kuwa mnasimamia
haki,"alisema Bw. Izrael.

Naye mgombea ubunge kupitia
chama hicho Bw. Nassari alisema
kuwa ifike mahali ambapo
wachungaji waseme ukweli kwa
kuwa nao wana nafasi kubwa ya
kuweza kusaidia jamii ya Jimbo la
Arumeru Mashariki.

Katika hatua nyingine vyama vya
CCM na CHADEMA vimepewa
onyo kali na Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (NEC) baada ya kubaini
kukiuka taratibu za kampeni na
uchaguzi.

Akizungumza na waandishi wa
habari Msimamizi wa Uchaguzi,
Bw. Trisias Kagenzi, alisema kuwa
amefikia hatua hiyo mara baada ya
kupokea malalamiko kutoka katika
vyama hivyo hivi karibuni ambavyo
vinashiriki uchaguzi mdogo wa
Jimbo la Arumeru.

Bw Kagenzi aliongeza kuwa
kwa sasa anatoa onyo kali dhidi ya
vyama hivyo viwili, lakini kama
havitasikia ataamua kufuata taratibu
za uchaguzi.

"Hadi sasa uchaguzi umefika
katikati ndani ya jimbo hili, lakini
kuna tofauti za malalamiko kwa
maana hiyo tumetoa onyo kali bila
kujali itikadi ya chama chochote,
na tunachokitaka hapa ni amani
tu ndani ya chama chochote kile"
alisema Bw. Kagenzi.


 
Wanamjua Lowassa, kwanini Makanisa Wanamkumbatia? kila kusimikwa kwa Askofu Serikali inatuma Mwakilishi na pia Lowassa yupo, ni kwanini?

Inashangaza kweli; Yeye ni nani?
 
Nasubiri kuona kama Lowassa atathubutu kumpigia kampeni mkwewe hadharani tofauti na sasa anavyofanya mambo chinichini.
Huu ni wakati mwingine wa kujua Lowassa ana mtaji gani kisiasa maana inaonekana dhahiri kuwa kiserikali bado ana ushawishi mkubwa na ndio maana hakuna yeyote ambaye anathubutu kusema lolote juu yake.
 
Mwaka huu MAFISADI hawana hamu tena na itikadi za 'Nguvu ya Umma' na kuwapelekesha mchaka mchaka ulimi nje wakati wote kwa kufichua yale ambayo hayakuweza kuzungumwa na mtu yeyote huko nyuma.

CHADEMA kanyaga twende, hakuna kulala mpaka haki za walalahoi zipatikane kwa manufaa ya taifa letu.


21 MARCH 2012


  • Asema wanakimbilia makanisani kujisafisha
  • Ataka fedha zao zikataliwe zimejaa najisi
  • Asisitiza michango wanayotoa haina uhalali
  • NEC yatoa karipio kwa CCM, CHADEMA

Na Queen Lema, Arumeru VIONGOZI wa makanisa nchini wametakiwa kuwakimbia wanasiasa ambao wanafanya ufisadi kwenye miradi mbalimbali ya wananchi na kisha kukimbilia makanisani kujisafisha.

Kauli hiyo ilitolewa na Katibu wa Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Willibrod Slaa jana wakati akihutubia mkutano wa kampeni eneo la Migandini akimnadi mgombea ubunge wa chama hicho, Bw. Joshua Nassari.

Dkt. Slaa kwa nyakati tofauti alisema kila fisadi wa Tanzania a n a k i m b i l i a m a k a n i s a n i kujisafisha. Alisema mafisadi hao wanaokimbilia kwenye madhabahu wanatia najisi makanisa kwa kuwa fedha na michango ambayo wanatoa haina uhalali, bali ni mali
ya Watanzania ambao wanateseka.

"Kila mara unasikia wanaenda makanisani kutoa misaada ya mamilioni ya fedha, lakini hizo fedha si halali... sasa kama si kutumia jina la Mungu kwa njia chafu ni nini? Nawasihi ninyi wachungaji kamwe msikubali kupokea fedha za mafisadi ambao wamegundua mbinu mpya ya
kujisafishia makanisani," alisema Dkt. Slaa.

Aliongeza kuwa endapo wachungaji wataendelea kuwapokea mafisadi hao katika makanisa na madhehebu yao ni wazi wananchi wataendelea kupata shida kubwa, huku nchi nayo ikikosa haki zake za msingi.

Katika hatua nyingine meneja kampeni wa mgombea wa chama hicho, Bw. Izrael Natse, alisema kuwa kwa sasa wapo baadhi ya wanasiasa ambao wanatumia neno la Mungu kufanya maasi.

Bw Izrael aliongeza kuwa mchungaji ambaye ameitwa kwa jina la bwana hapaswi kuhongwa kwa kupewa rushwa ambayo inalenga kukosesha jamii haki za msingi, bali mchungaji ambaye ni imara ni yule ambaye anapinga ufisadi na wizi ndani ya jamii.

"Leo hapa tuna uchaguzi lakini wapo wanasisasa ambao wanafanya kampeni hadi kwenye nyumba za ibada na kwa maana hiyo wanawateka wachungaji, sasa mimi nawaambia kuwa viongozi wa dini hakikisheni kuwa mnasimamia haki,"alisema Bw. Izrael.

Naye mgombea ubunge kupitia chama hicho Bw. Nassari alisema kuwa ifike mahali ambapo wachungaji waseme ukweli kwa kuwa nao wana nafasi kubwa ya kuweza kusaidia jamii ya Jimbo la Arumeru Mashariki.

Katika hatua nyingine vyama vya CCM na CHADEMA vimepewa onyo kali na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) baada ya kubaini kukiuka taratibu za kampeni na uchaguzi.

Akizungumza na waandishi wa habari Msimamizi wa Uchaguzi, Bw. Trisias Kagenzi, alisema kuwa amefikia hatua hiyo mara baada ya kupokea malalamiko kutoka katika vyama hivyo hivi karibuni ambavyo vinashiriki uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru.

Bw Kagenzi aliongeza kuwa kwa sasa anatoa onyo kali dhidi ya vyama hivyo viwili, lakini kama havitasikia ataamua kufuata taratibu za uchaguzi.

"Hadi sasa uchaguzi umefika katikati ndani ya jimbo hili, lakini kuna tofauti za malalamiko kwa maana hiyo tumetoa onyo kali bila kujali itikadi ya chama chochote, na tunachokitaka hapa ni amani tu ndani ya chama chochote kile" alisema Bw. Kagenzi.

 
Lawassa tumkatae mara ngapi Dk wa Kweli? Huyu hapa na mbio zake za sakafuni toka kanisa moja hadi ya kijiji cha pili, kwa ghafla tu katika maisha yake, wengi tu tunaendelea tu kumsanifu.

Jamani, mwacheni Lowassa aendelee kupiga mayowe kushoto na kulia na hizo fedha za ufisadi siku akikua kiroho na kisiasa ataacha.
 
Katika Zaburi 24:1 imeandikwa kwamba "Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana. Dunia na wote wakaao ndani yake." Hii ina
maana fedha na dhahabu ni za Bwana, tuwaache wazilete kanisani kuliko kuzihodhi wenyewe.

Duuh, mkuu,..hata shetani alitumia maandiko matakatifu kumjaribu Bwana Yesu akitumia phrase ya kuanzia.."imeandikwa..atakutumia malaika zake..na bla bla zingine"!..tafadhali kumbuka pia imeandikwa 'Ukileta sadaka yako ukiwa umekosana na nduguyo, rudi kwanza upatane na nduguyo na ndipo ulete sadaka yao"..maana yake, kukosana na nduguyo kwaweza kusababishwa na mengi,ikiwemo kumwibia (na kusababishia madhara-long term eg umasikini uliosababishwa na hawa waliopopoa mali zetu watanzania kwa kipindi kirefu).Hivyo, sadaka yako ni chafu mpaka pale utakapojipatanisha na nduguyo-so kama umemwibia 'go and do remedies-turudishie vyetu, si kwa unafiki wa kuleta sadaka chafu!
 
Lowassa ana strategic za ajabu kweli! Anaweza kufanya kampeni ya nguvu akiwa chumbani.

Tangu huyu mheshimiwa enzi akiwa waziri ktk office ya w/mkuu sijawahi mwona amesimama na kuhutubia/toa hoja zenye mashiko...media ndo inamsemea..hawezi panda jukwaa ataongea nini..
 
Back
Top Bottom