Dr. Slaa amkaanga Lowassa, adai hana hadhi ya kuomba Kura za Wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr. Slaa amkaanga Lowassa, adai hana hadhi ya kuomba Kura za Wananchi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MziziMkavu, Mar 21, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa jana alimtolea uvivu Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa akisema hana hadhi ya kusimama mbele ya wananchi kuwaomba waipigie kura CCM kwani anakabiliwa na tuhuma ambazo hazijawahi kusafishwa.

  Akizungumza katika mikutano ya hadhara kata za Songoro, Kikwe na Mbuguni, Dk Slaa alisema anamweka kiporo Lowassa akisubiri kwanza apande jukwaani kumnadi mkwewe Sioi Sumari.

  Kauli ya Dk Slaa inafanana na ile iliyotolewa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe mwishoni mwa wiki iliyopita akisema kwamba chama chake hakimwogopi Lowassa kwa sababu ni kama makada wengine wa CCM akiwamo Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa.

  Kauli ya Dk Slaa inakuja huku taarifa zikieleza kuwa Lowassa ametua rasmi katika jimbo la Arumeru Mashariki kwa ajili ya kumnadi mgombea wa CCM katika uchaguzi mdogo wa ubunge, Sioi Sumari.

  Habari ambazo Mwananchi lilizipata jana na kuthibitishwa na watu wa karibu na Lowassa zilisema Mbunge huyo wa Monduli (CCM) aliwasili jana majira ya jioni akitokea Ifakara, wilayani Kilombero mkoa wa Morogoro.

  Lowassa alikuwa Kilombero alikokwenda kushiriki sherehe za kumwingiza kazini Askofu wa Jimbo jipya Katoliki la Ifakara, Salutaris Libena pamoja na uzinduzi wa Jimbo hilo.

  Hata hivyo haikuweza kufahamika mara moja ni lini kiongozi huyo anayetajwa kuwa na ushawishi mkubwa katika siasa za Arumeru atapanda jukwaani kwa ajili ya kumnadi Sioi ambaye anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mgombea wa Chadema, Joshua Nassari.

  "Kweli mheshimiwa Lowassa yupo hapa, hilo nina uhakika nalo wala halina ubishi wowote, sasa ratiba nyingine siwezi kufahamu maana haijawekwa wazi kwa watu wote, lakini tusubiri maana kesho (leo) huenda ratiba ikapatikana," alisema mmoja wa viongozi wa CCM jana.

  Habari zaidi zilisema upo uwezekano mkubwa wa Lowassa kuendesha mikutano ya ndani kwa lengo la kuwashawishi wazee kukipa ridhaa CCM katika uchaguzi huo mdogo utakaofanyika April 1 mwaka huu.

  Kiongozi mwingine wa juu ndani ya CCM ambaye pia hakuwa tayari kutajwa alisema: "Sidhani kama Lowassa atapanda jukwaani sasa, anaweza kuamua kufanya mikutano ya ndani na ikiwa ataona mambo yana uelekeo mzuri ndipo atapanda jukwaani".

  Hata hivyo wachambuzi wa mambo wanasema huenda kiongozi huyo akapata wakati mgumu kuwashawishi wazee ambao wana mtizamo kwamba msingi wa Lowassa kumpigia debe Sioi unatokana na kwamba ni mkewe anayemwoa mtoto wake, Pamela Lowassa.

  Gazeti hili jana lilimtafuta Lowassa kupitia simu yake ya kiganjani lakini ilikuwa ikiita muda wote bila majibu.

  source.
  Dk Slaa: Mkataeni Lowassa akipanda jukwaani

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Kwa nia njema kabisa CCM, haijalishi Lowasa anamvuto mtamu na upi kwa wana Arumeru kamwe wasimpe Jukwaa kwa kuwa walipofikishana na CDM kwa sasa CDM wameshika mpini na CCM kupitia makada wake aina ya Lowasa wameshika makali ya kisu na kisu chenyewe kimetoka kunolewa jana tu kupitia Mzee Mkapa na watu aina ya Mzee Wasira, Job Lusinde na Ole Sendeka.

  Ni vyema CCM,wakajituma kutumia watu wenye CV njema mbele ya Umma na sio wenye mafairi ambayo CDM wakiyachambua jamii inafunguka kupata maswali ambayo mbaya zaidi yanasambaa Nchi nzima kwa kuwa masikio ya Watanzania kwa sasa yako Arumeru.

  Ikibidi wamnyofoe Lowasa toka huko, ngoma hiyo inayoendelea Arumeru ni bomu lake,kwa kuwa kifamilia linamuhusu na kwa uhalisia ngoma hiyo ni yake, hivyo awaachie wengine waandae hiyo shughuri ili kwa nafasi hii ndogo iliyobaki japo wanameru wadanganywe na sera kiasi zinazoweza kufikilika kutekelezeka japo kidogo, kulikoni akiwepo Lowasa kwa kuwa uwepo wake yeye hakika ndio kabisa wana arumeru hawata pata hoja za faida kwao zaidi ya kusikia siri za familia yake na mkwe wake zikianikwa hadharani na CCM kukosa ubunge na aibu ya kashfa ya uongozi wa familia na si uongozi wa chama kutumikia wana arumeru kwa kuwa baadhi ya makada wamesema SIOI apewe Ubunge kupozwa ili atunze familia na si kuwatumikia wana arumeru na Taifa kwa ujumla.
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Now this is what I was talking about... you fire warning shots.. swali ni je EL yuko tayari kuanzisha safari yake ya Urais kwa mpambano wa Arumeru Mashariki? Akisimama jukwaani manake yuko tayari.. patanoga sana.
   
 4. s

  sanjo JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Kwa sababu ya kukosa uwajibikaji na uadilifu sitashangaa EL akisimama na kuanza kudanganya bila aibu yoyotea.Subirini muone maajabu ya Musa.
   
 5. Jay One

  Jay One JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 11,077
  Likes Received: 4,661
  Trophy Points: 280

  EL he knows 4 real he won't be able to reply or attack Dr. Slaa verbally, kwani AKIKOSEA NA Dr. Slaa akaanza ukomando wake wa kuwa na evidences za mtu like EL ndoto za EL za kuwania Urais zitachafuka sana, so EL inabidi awe very very careful kwa kufanya haya ili asijichafulie njia zaidi 2015,
  1: awe kimya hasa akirushiwa tuhuma na mtu kama Dr. Slaa maana EL he knows Dr. Slaa ni brainy sio saizi yake, hahongeki, haogopi
  na ana ushahidi wa kila kitu asemacho
  2: au aache kwenda kumnadi mkewe aokoe njia yake
  ya urais isichafuke zaidi thru upinzani
  1
   
 6. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #6
  Mar 21, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Mmmm, hivi, huyu Lowasa hana uwezo wa kuwa na kampuni binafsi na kuwa tycoon kama Bakhresa au Mengj, akaheshimika!!!! Ci ameiba mali nyingi xana!!! Lowasa Trading Corporation inamiliki mabasi, viwanda..... Fikiria mtu kama Bloomberg pale Wasngton  Nasema wasomi wanasiasa wa Bongo ni vilaza, wanataka kuiba tuuuu, hawawez kujitafutiaaaa
   
 7. MBUTAIYO

  MBUTAIYO JF-Expert Member

  #7
  Mar 21, 2012
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 532
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Dk. Slaa amewasihi viongozi wa dini kuwa makini na watu wanaotoa michango kwa wingi makanisani na misikitini, kwani fedha hizo ni chafu na zingine zimetokana na ufisadi!
   
 8. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #8
  Mar 21, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  kuwa makini ni muhimu ili msitekwe akili lakini pesa walete tu zitatakaswa zikalee yatima na kujenga mashule na zahanati ndogondogo
   
 9. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #9
  Mar 21, 2012
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Katika Zaburi 24:1 imeandikwa kwamba "Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana. Dunia na wote wakaao ndani yake." Hii ina
  maana fedha na dhahabu ni za Bwana, tuwaache wazilete kanisani kuliko kuzihodhi wenyewe.
   
 10. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #10
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa jana alimtolea uvivu Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa akisema hana hadhi ya kusimama mbele ya wananchi kuwaomba waipigie kura CCM kwani anakabiliwa na tuhuma ambazo hazijawahi kusafishwa.

  Akizungumza katika mikutano ya hadhara kata za Songoro, Kikwe na Mbuguni, Dk Slaa alisema anamweka kiporo Lowassa akisubiri kwanza apande jukwaani kumnadi mkwewe Sioi Sumari.

  Kauli ya Dk Slaa inafanana na ile iliyotolewa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe mwishoni mwa wiki iliyopita akisema kwamba chama chake hakimwogopi Lowassa kwa sababu ni kama makada wengine wa CCM akiwamo Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa.

  Kauli ya Dk Slaa inakuja huku taarifa zikieleza kuwa Lowassa ametua rasmi katika jimbo la Arumeru Mashariki kwa ajili ya kumnadi mgombea wa CCM katika uchaguzi mdogo wa ubunge, Sioi Sumari.

  Habari ambazo Mwananchi lilizipata jana na kuthibitishwa na watu wa karibu na Lowassa zilisema Mbunge huyo wa Monduli (CCM) aliwasili jana majira ya jioni akitokea Ifakara, wilayani Kilombero mkoa wa Morogoro.

  Lowassa alikuwa Kilombero alikokwenda kushiriki sherehe za kumwingiza kazini Askofu wa Jimbo jipya Katoliki la Ifakara, Salutaris Libena pamoja na uzinduzi wa Jimbo hilo.

  Hata hivyo haikuweza kufahamika mara moja ni lini kiongozi huyo anayetajwa kuwa na ushawishi mkubwa katika siasa za Arumeru atapanda jukwaani kwa ajili ya kumnadi Sioi ambaye anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mgombea wa Chadema, Joshua Nassari.

  “Kweli mheshimiwa Lowassa yupo hapa, hilo nina uhakika nalo wala halina ubishi wowote, sasa ratiba nyingine siwezi kufahamu maana haijawekwa wazi kwa watu wote, lakini tusubiri maana kesho (leo) huenda ratiba ikapatikana,” alisema mmoja wa viongozi wa CCM jana.

  Habari zaidi zilisema upo uwezekano mkubwa wa Lowassa kuendesha mikutano ya ndani kwa lengo la kuwashawishi wazee kukipa ridhaa CCM katika uchaguzi huo mdogo utakaofanyika April 1 mwaka huu.

  Kiongozi mwingine wa juu ndani ya CCM ambaye pia hakuwa tayari kutajwa alisema: “Sidhani kama Lowassa atapanda jukwaani sasa, anaweza kuamua kufanya mikutano ya ndani na ikiwa ataona mambo yana uelekeo mzuri ndipo atapanda jukwaani”.

  Hata hivyo wachambuzi wa mambo wanasema huenda kiongozi huyo akapata wakati mgumu kuwashawishi wazee ambao wana mtizamo kwamba msingi wa Lowassa kumpigia debe Sioi unatokana na kwamba ni mkewe anayemwoa mtoto wake, Pamela Lowassa.

  Gazeti hili jana lilimtafuta Lowassa kupitia simu yake ya kiganjani lakini ilikuwa ikiita muda wote bila majibu

  Mwananchi
   
 11. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #11
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  tumesikia kampeni zake ni chini kwa chini,hataki kuharibiwa mipango yake ya urais 2015
   
 12. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #12
  Mar 21, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Subiri ataibukia kanisani jumapili
   
 13. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #13
  Mar 21, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Lowassa ana strategic za ajabu kweli! Anaweza kufanya kampeni ya nguvu akiwa chumbani.
   
 14. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #14
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Chumbani?
  Anafanya kampeni kwa kutumia ukuni?

   
 15. Said Bagaile

  Said Bagaile JF-Expert Member

  #15
  Mar 21, 2012
  Joined: Jun 23, 2011
  Messages: 686
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ukuni!
   
 16. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #16
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145

  Hakuna siasa saizi Arumeru imebaki kupakana matope.
   
 17. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #17
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Re: Lowassa atua Arumeru mashariki..........Hivi Lowassa ana mabawa siku hizi ? Kawa Malaika au?
   
 18. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #18
  Mar 21, 2012
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Watu wengine humu ni very senior member wa JF lakini wanashindwa kuongoza. Sasa hapa aliyejiunga Jan-March 2012 au anayetegemea kujiunga umemfundisha nn?? ni picha gani unafikiri unaipa JF??. Always Listen to yourself twice before you post anything!
   
 19. odinyo

  odinyo JF-Expert Member

  #19
  Mar 21, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 428
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  mkuu,
  ni kweli kabisa, tujitambue kabla ya kutuma msg zetu. kuna maada zingine za utani na zingine ni serious. act accordingly.
   
 20. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #20
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  naunga mkono hoja,halafu kuna member wamejiunga siku nyingi humu lakini kila SIKU NI KULaumu member wapya
   
Loading...