Kauli za sasa za viongozi wa CHADEMA kwa Lowassa zinahitaji maswali na ufafanuzi?

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,621
46,265
CHADEMA huwa mna utaratibu wa wowote wa kujadiliana na kukubaliana katika kutengeneza nyaraka zenu na miongozo mbalimbali ya kichama kwa mambo ambayo yatakuwa na umuhimu sana "consequential"?

Nakumbuka Slaa aliwahi kusema "list of shame"/orodha ya aibu ambayo ilimtaja Lowassa kama mmojawapo wa mafisadi wakubwa aliiandika mwenyewe, ndio maana hata akaondoka CHADEMA mlipomkaribisha Lowassa kugombea.

Nimewahi kumsikia Kitila Mkumbo pia akisema kwamba yeye ndiye aliyewaandika ilani yenu ya uchaguzi ya mwaka 2015.

Hivi karibuni niliona Mnyika akiwasilisha mapendekezo kuhusu miswaada ya tume ya uchaguzi na sheria za uchaguzi na mojawapo ya kipengele kilichozua sana mjadala ni uwepo wa wabunge wawili kila jimbo wa jinsia tofauti, baadhi members wa jukwaani wanasema Mnyika ndiye aliyeandika mapendekezo hayo.

Kama chama kikuu cha upinzani mnahitaji kujipambanua kama watu mnaofanya mambo kwa weledi na umakini mkubwa sana mkijua matokeo ya baadaye yanaweza kuwaathiri kwa namna nyingi. Lakini pia mmekiwa walegevu kutoa ufafanuzi makini na thabiti kwa mambo ambayo ni controversial.
 
Nadhani kwenye suala la msiba tusiingize siasa. Sijaona kiongozi wa CHADEMA ambaye karopoka hadi sasa. Wote wameongea kistarabu sana kuhusu Hayati Lowassa. Hizi hoja zako hazina mashiko kwa sasa. Subiri wakati sahihi.
 
Yoda kwenye hii misiba, utambue tu sio kwamba marehemu wa kiafrika huwa hawana mabaya, wanayo, lakini tu kwa taratibu zetu huwa hatupendi kusema mabaya ya marehemu wakati huo.

Sio vizuri watu wamejumuika kwenye maombolezo kisha waanze kusikia mabaya ya marehemu, hiyo itawaweka pabaya zaidi kihisia wafiwa, hili jambo limekaa kisaikolojia na kiutu zaidi.

Wala sio unafiki kama wajinga wengine wanavyodhani, hawajui hata nao siku wakifariki watasitiriwa kwa namna hiyo hiyo ili kuwapa ndugu zao nguvu wakati wa maombolezo kwenye misiba yao, kwa sababu nao hawakuwa malaika hapa duniani, walikuwa na mabaya yao.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Subiri matusi
Washamtoa Lowassa list of shame .
Sasa ni mchapakazi mwenye nidham aliedhulumiwa Urais na Kikwete
Wewe chuki yako kwa Chadema imekutoa ufahamu kabisa yaani siyo The Boss yule mjenga hoja umekuwa kama Dulla Makabila tu muimba chakacha. So sad.
 
Back
Top Bottom