Hamis Mgeja adai kuna waliopandishwa vyeo kwa sababu ya ‘kumtukana Lowassa’

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,753
218,340
Ameyasema hayo alipozungumza na gazeti la Mwananchi kufuatia Msiba wa Rafiki yake Lowassa

Screenshot_2024-02-10-21-27-24-1.png

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Sinyanga na rafiki wa karibu wa Hayati Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, Hamisi Mgeja amesema kiongozi huyo alikuwa na uvumilivu wa hali ya juu kiasi cha kuwasamehe waliomtukana.

Akizungumza kwa simu na Mwananchi leo Februari 10, 2024, Mgeja amesema, “Lowassa alikuwa mvumilivu sana, alitukanwa na alibezwa na kuna watu walipandishwa vyeo kwa sababu ya kumtukana, lakini hakuwajibu, bali alisema wasameheni kwa kuwa hawajui watendalo."

Akifafanua kuhusu uvumilivu huo, Mgeja amekumbuka uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ambao Hayati Hohn Magufuli wa CCM alitangazwa mshindi kwa kupata zaidi ya asilimia 58 ya kura, Lowassa aliyepata zaidi ya asilimia 39 aliwazuia vijana waliopinga matokeo hayo.

“Baadhi ya vijana ambao hawakuridhishwa na matokeo yale, walikusanyika wakamwambia tunasubiri ruhusa yako tuingie barabarani.

“Lakini yeye kwa busara zake akawaambia wavumilie kwa matokeo yale na kwamba hayuko tayari kuingia Ikulu mikono ikiwa imejaa damu,” amesema Mgeja.
 
Huu msiba,yawezekana ushiriki wa baadhi ya watu waliomtukana na kumdhalilisha Lowasa enzi za uhai wake,wakafanyiwa fujo na baadhi ya wadau ambao hawakufurahishwa na aliyofanyiwa hasa kipindi cha uchaguzi.
Mi kwa maoni yangu,baadhi ya watu wasiende tu kwenye mazishi.
 
Back
Top Bottom