Dr. Slaa amechuja sana kisiasa

Dr. Slaa amechuja sana kisiasa

Status
Not open for further replies.
Sasa mkuu kuna hoja hapa kwenye mada hii? au kuchafua majina na umaaruf wa mtu. kuna hoja hapa? hebu tueleze hiyo hoja basi tuijadili.
Mtoa mada kashaeleza vizuri, heading inajieleza kwamba dr slaa amechuja kisiasa.Ingekuwa wale wa magazeti ya udaku wangeweza kuwa na heading kama'Mchumba wa josephine Mushumbuzi kafulia kisiasa' hapo usitumie jazba kujibu
 
Wewe unayetaka wasimsemee mbona unaungana na yule anayesema kachuja, ina maana anawasemea nani, kama kaona kwake kachuja si akae nalo moyoni, anamsemea nani? Mimi kwangu kwa moyo wangu nasema Rd Silaa ni silaha ya matatizo ya Watanganyika na tafadhali nyamaza sikusmei wewe
usiwasemee watanzania. jisemee wewe kuwa unamhitaji. maneno ambayo nadhani angepaswa kuyasema josephine
 
Sasa kama kachuja kinachokuliza hapa ni nini si unyamaze na kushangilia maana hayo makapi yenu yatashinda kwa urahisi? Kinachokufanya utangazie dunia yote nini? Mimi nijuavyo mtu anashangilia mabaya yanapomkuta adui wake, kinyume chake wewe unakuja na kulia lia hapa. Dr Silaa anawapa shida kweli nyie mafisadi
Hana tena mvuto, kasi ya kuchuja kwake inachagizwa zaidi na mpasuko uliokikumba chama chake CHADEMA mwaka jana ambao umekiacha chama na majeraha yasiyotibika kirahisi.

UKAWA ulimbeba kwa kiwango flani lakini nao wameanza kumshtukia kutaka kuwavuruga na kujijenga mwenyewe badala ya ukawa as a team ya wapinzani.

My take. Slaa apimzike tu abaki na majukumu ya familia.
 
Mtoa mada kashaeleza vizuri, heading inajieleza kwamba dr slaa amechuja kisiasa.Ingekuwa wale wa magazeti ya udaku wangeweza kuwa na heading kama'Mchumba wa josephine Mushumbuzi kafulia kisiasa' hapo usitumie jazba kujibu

Jaziba inasababioshwa na hoja za hovyo, za kizushi kwa watu makini, bora na wenyewafuasi wengi.

Huhitaji diploma kuelewa habari hiyo ya kutunga na uzushi, majibu ya uzushi na kupaka matope mtu wa kundi flani

tegemea matusi, na majibu ya hovyo-Maana msingi wa hoja ni fitina na uzushi tena kumchafua mtu bila vigezo vya

msingi na majibu yatakuwa hivyohivyo ya kizushi nk. usitegemee majibu ya maana kwenye hoja za uzushi na uwongo.
 
Kama humjui Dr.Slaa kaa kimya.Tanzania tunaitaji kiongozi makini,mbunifu,mzuia ufisadi wa mali ya umma na n.k. Usilete ujinga kwenye mambo ya msing. Tukiorodhesha mambo muhimu ktk jamii kati ya Jakaya na Dr Slaa ndio utapata jibu,tena mwingine yupo madarakani.Acha ujinga kuongea mambo ucyoyajua.
 
Jaziba inasababioshwa na hoja za hovyo, za kizushi kwa watu makini, bora na wenyewafuasi wengi.

Huhitaji diploma kuelewa habari hiyo ya kutunga na uzushi, majibu ya uzushi na kupaka matope mtu wa kundi flani

tegemea matusi, na majibu ya hovyo-Maana msingi wa hoja ni fitina na uzushi tena kumchafua mtu bila vigezo vya

msingi na majibu yatakuwa hivyohivyo ya kizushi nk. usitegemee majibu ya maana kwenye hoja za uzushi na uwongo.
Mimi sio shabiki wa vyama vya siasa, ni mshabiki wa watu makini wenye kujali maslahi ya taifa....kipindi kidogo cha nyuma cdm ilikuwa moto wa kuotea mbali sababu ya umakini uliokuwepo,, mikutano ilikuwa na hamasa kubwa na vilikuwa vinashushwa vitu vya maana ndani ya mikutano ya cdm....mfano tu hii escrow saga ati mpaka sasa hivi hatuwajui wanufaika kupitia bank ya stanbic, kipindi kile tayari tumeshayajua kupitia dr slaa.Kipindi hiko Zitto kashika kanda ya magharibi, Mbowe anapasua kaskazini wakati dr slaa shaaaa mwembe yanga ndani ya daresalama.Ilikuwa ni combination ya hataree tofauti na hawa vijana wa sasa hivi mara kaeni kwenye tv muone nitakachofanya bunge likianza, kubali ukatae speed imepungua.
 
barabara bora za lami nchi nzima. hospitali za rufaa kila mkoa. shule za sekondari kila kata. chezea mkweree weyee

Yaani wewe bure kabisa, wenzako na smart phones wewe unashangilia kisimu cha tochi... Dah kweli hii ndiyo Tanzania
 
Naona Maccm yanaweweseka tu,hakunaga bongo hii kama dr wa ukweli Slaa.Ndiye rais wetu atakayekomesha ufisadi,rushwa na kurejesha heshima ya taifa letu iliyopotezwa na hawa wachumia tumbo.
 
Hana tena mvuto, kasi ya kuchuja kwake inachagizwa zaidi na mpasuko uliokikumba chama chake CHADEMA mwaka jana ambao umekiacha chama na majeraha yasiyotibika kirahisi.

UKAWA ulimbeba kwa kiwango flani lakini nao wameanza kumshtukia kutaka kuwavuruga na kujijenga mwenyewe badala ya ukawa as a team ya wapinzani.

My take. Slaa apimzike tu abaki na majukumu ya familia.

Haya tuwekee orodha ya wasiochuja tuwaone kama wanauzika
 
ukweli ni kwamba slaa hana mvuto tena. anabebwa na historia. hana jipya
Duh huna hoja nyingine zaidi ya Slaa?

Muda uliotumia kuandika upuuzi huu ungejituma uweze hata kumlipia Masikini@Mkulima Deni analodaiwa kama ulivyoahidi kule Singida.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu, kuna muda huwa siwaelewi!

Hivi kuna nini cha kitoto hapo kuhusu Mzee Slaa?

Kama mtu hana mvuto tena kisiasa hamtaki isemwe?

Kumshauri mtu apumzike na kulea wajukuu ni utoto?

Kamuangukie VUTA NIKUVUTE akurudishie ile ID yako ya awali. Alishakuonya mara nyingi
 
Hana tena mvuto, kasi ya kuchuja kwake inachagizwa zaidi na mpasuko uliokikumba chama chake CHADEMA mwaka jana ambao umekiacha chama na majeraha yasiyotibika kirahisi.

UKAWA ulimbeba kwa kiwango flani lakini nao wameanza kumshtukia kutaka kuwavuruga na kujijenga mwenyewe badala ya ukawa as a team ya wapinzani.

My take. Slaa apimzike tu abaki na majukumu ya familia.

Ngoja niitunze hii thread tutaelewana tu mwezi Novemba, Mungu atujaalie uzima tutaona nani amechuja
 
Hi kwa nini Lumumba likitajwa jina la Dr Slaa mnatokwa na kinyesi hivyo. ni swali tu
 
Binkubwa binkubwa tu hata mukimpaka kalikiti,au munataka atembee na mkongoja IKULU,Dah! miaka 70 zilipendwa kama MAPALALA tu.
 
Mimi sio shabiki wa vyama vya siasa, ni mshabiki wa watu makini wenye kujali maslahi ya taifa....kipindi kidogo cha nyuma cdm ilikuwa moto wa kuotea mbali sababu ya umakini uliokuwepo,, mikutano ilikuwa na hamasa kubwa na vilikuwa vinashushwa vitu vya maana ndani ya mikutano ya cdm....mfano tu hii escrow saga ati mpaka sasa hivi hatuwajui wanufaika kupitia bank ya stanbic, kipindi kile tayari tumeshayajua kupitia dr slaa.Kipindi hiko Zitto kashika kanda ya magharibi, Mbowe anapasua kaskazini wakati dr slaa shaaaa mwembe yanga ndani ya daresalama.Ilikuwa ni combination ya hataree tofauti na hawa vijana wa sasa hivi mara kaeni kwenye tv muone nitakachofanya bunge likianza, kubali ukatae speed imepungua.

Inawezekana unazunguuka mbuyu

1. Unaweza kutueleza kwa data na ushahidi malumu kushuka kwa chadema? tumia dhana hii

a) Uchaguzi Serikali za mitaa imepanda imeshuka, imepata asilimia ngapi ukilinganisha na hapo awali au imepoteza ngapi

2. Nimikutano ipi ya chadema imekosa hamasa, unaweza itaja kwa majina ikibidi picha

3. Escrow, unataka nini zaid, kama jambo limeenda mpaka bungeni, rais kapewa maazimio na bunge nk unataka chadema ifanye nini? Iulize serikali kwanini haitaki wezi kupitia Stanbic waeleweke, inamechanism zote, cdm unailaum kwa lipi

4. Hoja hii kwa uzushi tu inamjadili Dr Slaa kwa uwongo na uchafuzi, Zitto unamtowa wapi? unataka kusema ZZK ndiyo chadema? huu nao niuzushi mwingine.

Elewa wazi tunaelekea uchaguzi mkuu 2015, kila chama kina

-Mikakati yake

-Agenda zake

-Mipangilio nk

Huwezi leta hoja hapa chadema imeshuka bila takwimu za

a) serikali za mitaa

b) kuongezeka au kupunguwa kwa wanachama

c) Kupoteza majimbo ya ubunge, udiwani nk

Hebu wewe mwenye hoja jadili sasa kwa hoja na takwimu tuone huo ukweli wa kuporomoka kwa chadema na Dr Slaa.

Tafadhali shusha takwim
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom