Januari 5, 2011, ni siku aliyekuwa mchumba wa Dtk. Slaa alipokipigania CHADEMA kwa maumivu makali

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Mar 29, 2012
10,223
22,303
Januari 5, 2011
Arusha, Tanzania.

Hii ni siku ambayo wapenda amani wote hatutakaa tuisahau. Ni siku ambayo tuliondokewa na wapendwa wetu huku wengine wengi wakipata majeraha mabaya akiwemo aliyekuwa mchumba wa Dr Slaa. Hakika ilikuwa siku ya huzuni sana.

Nakumbuka mimi nilikuwa nimetoka Burka kwa mguu wakati nimepita kona ya Esso ndo nikaanza kugundua kuna tatizo mjini. Katikati ya mji hadi maeneo ya kaloleni ilikuwa kama eneo flani hivi la kivita. Mabomu ya machozi yalitapakaa. Ni tukio lililofanya Jo Makini kutunga wimbo mkali sana uitwao Bye Bye akimshirikisha G Nako Warawara. Nimekuwekea kwenye attachment usikilize.

Hadi nafika posta ya Meru nilikuwa bado sijapata jibu sahihi ya nini kinaendelea... lakini ghafla nikaona Hiace imekuja kwa kasi kama inatokea Kijenge ikasimama na jimama moja lililokuwa limefungasha makalio ya dunia nzima kwa bei elekezi likarukia ndani ya daladala na mimi nikajikuta tu niko kwenye daladala ileile aliyopanda jimama.

Nikiwa kwenye daladala nikawa na mixed feelings, upande mmoja nafikiria taharuki inayoendelea na upande mwingine jimama. Ila nikiwa mle ndani ya daladala ndo nikajua kuna vurugu zilizosababishwa na maandamano haramu ya CHADEMA.

Daladala ilisimama eneo la chini ya mti na mimi kuanza safari ya kuelekea Sanawari. Nilipofika maeneo ya nyuma ofisi ya PCCB Kaloleni kama unaelekea Meru Inn na Sarafina Bar ndo nikakuta manjagu wametanda hatari na watu wakikimbia ikawa taharuki tupu. Hayo maeneo walikuwepo viongozi kadhaa wa CHADEMA na ndo maeneo hayo mchumba wa Slaa alijeruhiwa kichwani na kuvuja sana damu.

Hakika Dr Slaa na mchumba wake waliibeba CHADEMA mabegani ila leo hii wanatukanwa hata na watoto ambao 2011 walikuwa wanaishi kwa wazazi wao. CHADEMA ya 2011 kwa Arusha ilikuwa ya moto mno, ilikuwa haishikiki. Laana ya aliyekuwa mchumba wa Dkt. Slaa haitawaacha salama CHADEMA. Alimwaga damu kwa ustawi wa CHADEMA. Chama kimtafute kimuombe radhi. Pia Dr Slaa asije akafanya kosa kurudi CHADEMA bila kuombwa msamaha na chama hadharani.

Mungu awalaze mahali pema wale wote waliopoteza maisha kwasababu ya kikundi cha watu wachache kutaka kujipatia sifa kisiasa.
 

Attachments

  • FB_IMG_1675179730187.jpg
    FB_IMG_1675179730187.jpg
    24 KB · Views: 7
  • afp_three_dead_in_tanzania_grenade_attack_on_political_rally.jpg
    afp_three_dead_in_tanzania_grenade_attack_on_political_rally.jpg
    21.6 KB · Views: 6
  • FB_IMG_1675179726663.jpg
    FB_IMG_1675179726663.jpg
    29.7 KB · Views: 7
  • FB_IMG_1675179712056.jpg
    FB_IMG_1675179712056.jpg
    18 KB · Views: 6
  • FB_IMG_1675179676912.jpg
    FB_IMG_1675179676912.jpg
    49 KB · Views: 7
  • Joh_Makini_ft_G_Nako_-_Bye_Bye.mp3
    3.9 MB
Back
Top Bottom