Dr Slaa ajibu tuhuma dhidi yake

Dr Slaa ajibu tuhuma dhidi yake

Status
Not open for further replies.
mkuu tatizo lenu hamtuelewi sisi ccm hatuna tatizo na mkopo wa slaa, tatizo letu sisi ni slaa kugombea uraisi mwaka 2015! Tunataka kummaliza kabisa!na kuimaliza chadema.
sasa mkuu km tatizo ni urais 2015 si mumkolimbe tu yaishe???
 
Mwenye fomu ya maombi ya mkopo Chadema kupeana group aitundike jamvini sio mnakula peke yenu tu hata sisi tunahitaji mkopo watoto wamekwama kwenda shule.
 
WanaJF,
Nilidhani walioko humu ni great Thinkers. Nilisema hakuna hoja ya kujibiwa hivo sina muda wa kupoteza kujibu hoja za kufikkirika. Ni jukumu la mwenye kuleta hoja kutoa ushahidi si jukumu la mtuhumiwa. Ndio maana wakati wa EPA/B0T. Nilitoa account no, bank husika, majina ya wahusika, tarehe ya transaction na kadhalika. Kama ni kutamka anybody anaweza kutamka chochote hat a kichaa. Hivyo watanzania, nikikaa kimya maana yake nimepuuza kwa kuwa hakuna hoja ila wanaoleta wanadhamira tu ya kutuondoa kwenye hoja za msingi. Nagpenda kwa Mara ya mwisho niwahakikishie woe wenyewe mapenzi MEma Chadema iko makini, yote tunayofanya ni kwa mujibu wa taratibu zetu tulizojiwekea. Iwapo mwenye nia Njema anahitaji kufahamu jambo milango ya makao makuu yako wazi saa zote alimradi unafuata taratibu za kawaida za kiofisi.
rais wangu wala usiwajibu hawa, tuachie sisi tutapambana nao....
tatizo ni hofu yao juu yako kwa mwaka 2015,
 
Weka ushahidi kuonyesha kwamba sio 140 ni 20, na ushahidi kwamba zimelipwa zote...kwa hiyo yaya analipwa na chama?

Mkuu, ukisikia kuna akili za kuazima ndiyo hizo.
Mimi nilidhani wewe ndiwe unayetakiwa kututhibitishia kwamba Dr. ni muongo, kwamba alikopa mil. 140 na siyo mil. 20. Kisha unatuwekea na ushahidi usio na shaka yoyote humu JF. Hapa ndipo tutakapokuona unatumia akili zako mwenyewe.
Hivi tangu lini ulishawahi kuona mwizi akiambiwa athibitishe kwamba hajaiba?
 
Dr.W.Slaa,

Hakuna ambaye anataka kukutoa kwenye hoja ya msingi. Ili la kukopa ruzuku ya chama wewe unaona siyo hoja ya msingi.

Naomba kufahamu ndani ya Chadema mna utaratibu wa kukokopeshana pesa za ruzuku ya chama.

Unapokea milioni 7 kwa mwezi halafu unasema hakuna wa kukopesha ndiyo maana umeamua kujikopesha.

Juliana Shonza bila kuwambia wananchi tusingejua kama umekopa pesa ya chama kwa matumizi yako binafsi.
umeambiwa nenda makao makuu ya chama ukafuatilie upate ukweli, kwanini kubisha bisha kama chizi?
............yote tunayofanya ni kwa mujibu wa taratibu zetu tulizojiwekea.
 
Mwenye fomu ya maombi ya mkopo Chadema kupeana group aitundike jamvini sio mnakula peke yenu tu hata sisi tunahitaji mkopo watoto wamekwama kwenda shule.
Mkuu, mtaani kwenu hakuna msamiati wa 'SACCOS'?
 
TUNAJARIBU SIJUI ANALINDWA NA MUNGU GANI MKUU, tukifanikiwa hilo itakuwa ni bora zaidi, tunataka tumuue kwa sumu kumkolimba hapata kalika!
hapo kwenye sumu mnajidanganya, mumemshindwa mwaki... na mwando..wenye jeshi dogo mtamuweza Dr. mwenye jeshi hadi korido za Ikulu?
 
Options
Willibrod Slaa

Hoja ya kujikopesha kwa sura ya ufisadi ni "mfu" nimetamka nilikopa 20 kwa kuwa watumishi wa vyama hawawezi kukopa kwingine. Aidha siyo 140 Million. Zote 20 m zililipwa awamu ya mwisho June 2012. Hivyo hakuna deni la chama tena.
2. Josephine hajawahi kulipwa hata senti mmoja na chama kwa ziara za Mikoani, wala kwa shughuli yeyote ile isipokuwa wakati wa kesi Arusha alipokuwa na mtoto wa miezi 3 na tulihitaji yaya
....Siamini maneno haya kama yanatoka directly kwa Dr.Slaa (maana yeye huja humu jf na ID yake genuine)...na wala sitaki ku comment kumlaumu Dr.Slaa kwa tuhuma dhidi yake hata kidogo.....kwa kuwa najua yeye Slaa kama individual ni mtu safi sana na hayuko corrupt hata chembe.....historia yake kisiasa inathibitisha haya.....na hata ccm wanayajua haya. Nachotaka kusema hapa ni kuwa matatizo/lawama nyingi kwa Dr. Slaa toka kwa wabaya/wapinzani wake zinatokana na mahusiano yake na bi Mshumbushi.....yooote yanayohusishwa na Slaa leo yanatokana kwa asilimia 100% na mahusiano yake na Mshumbusi....kwasababu kabla ya hapo Dr hakuwahi kuwa na individual shutuma dhidi yake hata chembe...na ndio sababu aliweza hata kuyataja majina ya list of shame ya mafisadi(akiwemo JK na Mkapa)bila wasiwasi wowote na bila kupata upinzani wowote toka kwa wabaya wake wa leo.....

That said, nitoe tu angalizo kwa Dr.Slaa personally......Ni wakati sasa kwa yeye kujitahidi kumweka mbali na majukwaa ya siasa bi Mshumbusi.....maana kumekua sasa na shutuma kibao dhidi yake(pamoja na kwamba hazithibitishwi).....na ni wakati wa wote (Dr. Slaa na Bi Mshumbusi)kuwa makini sana na wanayofanya ndani ya chadema(haswa bi Mshumbusi).....maana imeshadhiirika sasa kuwa maadui wa chadema (mapandikizi ya ccm) wamo ndani ya chadema na wanayafuatilia kwa makini yooote yanayofanywa na Dr.Slaa na mchumba wake)......Umuhimu wa karibu uwe kwa yale yote afanyayo bi Mshumbusi.....kwa maana ya kumweka mbali na masuala ya majukwaa ya saisa....maana tayari anakuwa target ya maadui wa Slaa sasa.....Ni angalizo tu toka kwa ngosha.......
 
Dr.W.Slaa,

Wewe umesema CCM wameingiza mtambo wa kuiba kura wamenunua bilioni 2 bila kuweka ushahidi wowote. Watu kuhoji mkopo wako unasema walete ushahidi.
 
Slaa kajibu hii hoja kwa ufupi na ni very clear. Kakopa na kalipa. Hana cha kujibu zaidi kama mna swali waulizeni waliomkopesha. Ni ujinga kukomaa na issue hii.
Kuna viongozi wanatuhumiwa kuuza meno ya tembo hatujawasikia wakitoa majibu,wapo ambao viwanda vyao vimewapa maelfu ya WaTZ dawa feki za ARV wanajifia hawajajibu maana hawana majibu na wengine fedha za mradi wa gesi washakula percent ziko Uswiss hawajibu.
Hanuoni Slaa ni kiongozi wa mfano kwa kujitokeza kujibu pale penye mashaka hata kama ni mashaka ya kijinga?
 
Viongozi wa vyama vya siasa wangekuwa hawawezi kukopa Mbowe angekuwa hadaiwi na NSSF. Yaani na wewe unadanganyika haraka na kirahisi namna hiyo?! au ndio ile mtu akipenda chongo huita kengeza? Mikopo ipo kwa watu wote wanaokopesheka.Kama hakopesheki basi tatizo ni lingine lakini siyo kwa kuwa ni mwanasiasa. By the way, Slaa na mshahara wa milioni 7 alikuwa na ulazima gani wa kuchukua tena milioni 20 za chama?
Nadhani umekimbilia kuhukumu mapema bila kuangalia ukweli wa jambo jenyewe kama Jasusi alivyobainisha. Kwanza naomba nikuulize swali la msingi ,Una uhakika kwamba hayo maneneno ni Dr. Slaa ameyatoa hadharani kama utetezi?
 
Last edited by a moderator:
Weka ushahidi kuonyesha kwamba sio 140 ni 20, na ushahidi kwamba zimelipwa zote...kwa hiyo yaya analipwa na chama?

Komenti ya kipuuzi kabisa! Mstakakiwa alete ushahidi wa mashtaka anayoshtakiwa!? Kweli shule za kata ni janga!!!
 
umeambiwa nenda makao makuu ya chama ukafuatilie upate ukweli, kwanini kubisha bisha kama chizi?

Hakuna kubishana watu wanataka kujua. Kwa hiyo hata nyie mnalalamika humu JF serikali imejaa mafisadi ni machizi. Kwa nini msipeleke malalamiko yenu serikalini.
 
WanaJF,
Nilidhani walioko humu ni great Thinkers. Nilisema hakuna hoja ya kujibiwa hivo sina muda wa kupoteza kujibu hoja za kufikkirika. Ni jukumu la mwenye kuleta hoja kutoa ushahidi si jukumu la mtuhumiwa. Ndio maana wakati wa EPA/B0T. Nilitoa account no, bank husika, majina ya wahusika, tarehe ya transaction na kadhalika. Kama ni kutamka anybody anaweza kutamka chochote hat a kichaa. Hivyo watanzania, nikikaa kimya maana yake nimepuuza kwa kuwa hakuna hoja ila wanaoleta wanadhamira tu ya kutuondoa kwenye hoja za msingi. Nagpenda kwa Mara ya mwisho niwahakikishie woe wenyewe mapenzi MEma Chadema iko makini, yote tunayofanya ni kwa mujibu wa taratibu zetu tulizojiwekea. Iwapo mwenye nia Njema anahitaji kufahamu jambo milango ya makao makuu yako wazi saa zote alimradi unafuata taratibu za kawaida za kiofisi.
dr slaa wewe ni mwadilifu na uma wa watanzania tunalifahamu hilo,na tunakuombea munhu akupe uhai na akuepushe na hawa majangili wanaokuzunguka,magamba wenyewe walishakutafuta kila sehemu ili wakakuhusishe na kasha wakakuta kila sehemu upo safiii.hawa vibaraka wanatumia nguvu nyingi kukuchafua lakini kila doa linakosa ushahidi.achana nao hawa vimeo wewe piga kazi ili kuwakomboa wa tz,mchango wako umeoneka hata kwa watoto wachanga.kweli wewe ni mkombozi wa wanyonge.
 
Hakuna kubishana watu wanataka kujua. Kwa hiyo hata nyie mnalalamika humu JF serikali imejaa mafisadi ni machizi. Kwa nini msipeleke malalamiko yenu serikalini.
kahoji kwanza unakofanyakazi ya ukibaraka.pia wasauri kulikoni kijimilikisha mashule na majengo ya chama,waige mfano mzuri wa mtu mwadilifu dr slaa wakope kwenye chama maana mkopo huwa unalipwa,lakini kuiba ni kuboa kabisa.
 
Kama utetezi huu ni kweli ameundika Dr.Slaa(siamini), basi utetezi wake ni wakifisadi.

1. Kusema kuwa watumishi wa vyama hawaruhusiwi kukopa ni uwongo mtupu na uzushi.Hakuna sheria inayomzuia mtu kukopa. Kukopa na kukopeshwa ni makubaliano ya kimkataba kati ya mtu na mtu au mtu na taasisi kadiri wanavyoaminiana.
2. Je lengo msingi la fedha ya ruzuku ni kwaajili ya kukopeshana?
3. Yeye kama mtendaji mkuu wa chama, je haoni kujikopesha fedha za ruzuku kuna conflict of interests? Je haoni kwamba kitendo hiki kinajenga mashaka makubwa dhidi yake juu ya accountability, credibility,transparency?
4. Je haoni kuwa tendo hili la kujikopesha fedha za ruzuku ni tendo la kifisadi?
5. Je huku siyo kutumia vibaya madaraka?
6. Je haoni kuwa akiwa Ikulu kuna uwezekano mkubwa akajikopesha bajeti yote ya ikulu?

Tamko: Dr. Slaa hafai kuwa raisi.
Cha ajabu ni kwamba ishu hii ni ya Chadema, lakini wanaoonekana kujifanya kama wameumizwa zaidi ni MaCCM! Kweli Mchawi ndie hulia sana msibani kwa mtu aliyemuua.
 
Dr.W.Slaa,

Wewe umesema CCM wameingiza mtambo wa kuiba kura wamenunua bilioni 2 bila kuweka ushahidi wowote. Watu kuhoji mkopo wako unasema walete ushahidi.
dr slaa hakurupuki kama wewe,anaongea vitu vyenye ushaidi.kwani nimangapi mlidai hana ushahidi na akawapa nyaraka zote???
 
Options
Willibrod Slaa

Hoja ya kujikopesha kwa sura ya ufisadi ni "mfu" nimetamka nilikopa 20 kwa kuwa watumishi wa vyama hawawezi kukopa kwingine. Aidha siyo 140 Million. Zote 20 m zililipwa awamu ya mwisho June 2012. Hivyo hakuna deni la chama tena.
2. Josephine hajawahi kulipwa hata senti mmoja na chama kwa ziara za Mikoani, wala kwa shughuli yeyote ile isipokuwa wakati wa kesi Arusha alipokuwa na mtoto wa miezi 3 na tulihitaji yaya

Dr.Slaa huhutaji kupoteza muda kujibu kila tuhuma dhidi yako hasa tuhuma dhaifu kama hizi za kukopa, kwani kukopa ni kosa? nakushauri,badala yake tumia muda wako mwingi kujipanga utapambanaje kuhakikisha 2015 unaingia madarakani.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom