Elections 2010 Dr Slaa aitikisa Karatu

familia yake kumuunga mkono
mgombea mwenza wa cahdema
kampeni za dk slaa kanda ya pwani , tanga na Zanzibar
timu ya kampeni ya dk slaa
majibu ya maswala ya mahakama ya kadhi na oic kutoka kwa wananchi
hapa ndipo penye mgogoro

Mod, kile kitufe ulichosema kinaweza kuanza August huwezi ukakiwahisha kidogo? nina hamu ya kukitumia kwelikweli.
 
Wana JF kwa taarifa yenu Malaria Sugu ni mwandishi wa magazeti ya Habari corporations ya Mwananchi Mtanzania Rai vile vile huandikia gazeti la Majira. Habari zote za udini kwenye magazeti hayo hutungwa na Maralia Sugu wakishirikiana na anayejiita Tumain.
 
Malaria Sugu.....

Utaendelea kuona giza hadi utoke gizani........ Kwani nuru na giza havitangamani.

Halafu u malaria sugu, mbu kibao kwenye giza , mbona umejitambulisha vizuri, u malaria sugu, mbu wanaishi gizani , vichakani, na madimbwi machafu.. Kwa tafsiri zote na kauli zao , basi umejitambulisha vizuri na mfalme wa giza , ambaye ni baba wenu wa uongo...... Watoto wa giza , huyashabikia matendo ya giza... unaunga mkono UDINI, ufisadi.

Toka gizani, na Chadema imekuja kuleta NURU, NA NURU YANGA'A GIZANI NA KAMWE GIZA HALITAIWEZA NURU.

Una uhuru wa kutoka gizani au kuendelea kuwa mhanga wa giza na malaria sugu.

Huu ni mwaka wa CHADEMA mpende msipende.
 
Nahitaji msaada wa kujua yapi yaliyojiri huko karatu je wadau wameupokeje uamuzi wa Dk.Slaa? Nahitaji update anyone to help.
 
Dr. Slaa amepata mapokezi makubwa sana ya kumuanga, Kwa heri shujaaa wetu tutakumiss sana, na kutakia safari njema!
 
Wana JF kwa taarifa yenu Malaria Sugu ni mwandishi wa magazeti ya Habari corporations ya Mwananchi Mtanzania Rai vile vile huandikia gazeti la Majira. Habari zote za udini kwenye magazeti hayo hutungwa na Maralia Sugu wakishirikiana na anayejiita Tumain.
Quinine, nimeona post zako, nikatambua ugeni wako humu, hiyo inaitwa 'name calling' ni kosa na adhabu yake ni ban.
Mimi siamini kwenye adhabu lakini nayajua madhara ya name calling, hata ukimjua fulani ni nani, anafanyia wapi na itafuatia jina kamili, then unakuwa umemvua nguo huyo mhusika na kumuacha ...wa nyama, hali itakayopelekea kumpoteza kabisa kwani tumeshapoteza wengi, watu makini kama kina Kuhani au FMeS baada ya kuvuliwa nguo humu, wako wapi?, tusimvue nguo MS ili tusimpoteze.

Kwa upande wangu, huyu Malaria Sugu kama jina lake linavyoonyesha, imeishapanda kichwani, hivyo ni kama kichaa fulani, baadhi ya hoja zake ni changamoto na nyingine ni utumbo utumbo, ila pia anawashabiki wake humu kama wale wapendao kuvaa t-shirt na kofia za yanga kwenye medani za siasa, mwacheni msiingilie uhuru wake.
 
Ningependa kuona picha
slaa kurudisha fomu1.JPG
Photo credits:Gazeti la Mwananchi
 

Attachments

  • slaa kurudisha fomu.jpg
    slaa kurudisha fomu.jpg
    14.4 KB · Views: 78
Mkuu nafikiri ukisoma hii habari iliyoandikwa na Mwananchi unaweza kupata picha kidogo ya yaliotokea huko. Sidhani kama Chadema wana hisa na Mwananchi hivyo hakuna sababu ya kuhofia kuwa "story" ni "biased"

Dk Slaa: Nipeni urais ning'oe ufisadi
Mwananchi, Tuesday, 27 July 2010 10:26


Mussa Juma, Karatu

KATIBU mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa jana akichukua fomu ya kugombea nafasi ya urais kwa tiketi ya chama hicho na kuuambia umati uliofurika kumshuhudia akisema "nipeni urais ning'oe ufisadi".
Mamia ya wananchi hao walifurika kwenye Uwanja wa Bwawani mjini hapa kumshuhudia mbunge huyo wa Karatu akichukua fomu na hafla hiyo ilijaa shangwe, vigelegele na kelele zilizomtaja Dk Slaa kuwa ni rais.
Dk Slaa, ambaye amekuwa mbunge wa Karatu kwa takriban miaka 10 sasa, amebadili upepo kwenye mbio za urais kutokana na kukubali ushauri wa chama chake wa kumtaka agombee kiti hicho baada ya kung'ara ndani ya Bunge la Jamhuri ambako aliongoza vita dhidi ya ufisadi.
Akizungumza na wananchi katika mkutano huo, Dk Slaa aliwaambia wananchi hao kuwa amekubali maombi ya kamati kuu ya Chadema ya kumtaka agombee nafasi hiyo.
"Nilikuwa sina mpango wa kugombea nafasi ya urais ndiyo maana nikaamua kuchukua fomu ya kugombea nafasi ya ubunge," alisema Dk Slaa ambaye alikuwa mgombea pekee wa Chadema wa kiti cha ubunge wa Karatu.
"Sababu ya kutochukua fomu ya kugombea nafasi ya urais ni kwamba najua kuwa Ikulu si sehemu ya kukimbilia."
Dk Slaa alisema baada ya kuombwa kugombea nafasi hiyo, aliwaomba wananchi wa Karatu waseme kama wamekubali na wakamjibu kuwa wamekubali ndipo akarejesha fomu.
Huku akiwa anashangiliwa, Dk Slaa, ambaye aliongezeka umaarufu baada ya kutangaza orodha ya mafisadi iliyosababisha mabadiliko makubwa kwenye anga za kisiasa, ameahidi kupambana kwenye kampeni hadi ahakikishe anaibwaga serikali ya CCM ambayo imekuwa madarakani tangu uhuru.
Dk Slaa amewaomba Watanzania kumuunga mkono ili aendelee na vita dhidi ya ufisadi na kuwatetea masikini hapa nchini.
"Nawaomba Watanzania mniunge mkono ili niendeleze vita dhidi ya ufisadi pamoja na kuwatetea masikini hapa nchini," alisema Dk Slaa.
Naye mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema kuwa siku za Rais Jalaya Kikwete kukaa Ikulu zinahesabika kwani rekodi ya Dk Slaa haina doa na itamfikisha Ikulu.
Mbowe alitumia muda mrefu kuwaeleza wananchi wa Karatu sababu za kamati kuu kumuomba Dk Slaa agombee na aliwaahidi wananchi kuwa watapambana kwa kila hali ili jimbo la Karatu libaki mikononi mwa Chadema kwa sababu "tutaweka mgombea makini atakaye endeleza yale yote aliyoyafanya Dk Slaa".
Baada ya hotuba ya viongozi hao, mamia ya wananchi walijipanga foleni wakijaza majina kwa ajili ya kumdhamini Dk Slaa ikiwa zoezi hilo linaendelea hadi leo hii mjini hapo.
Dk Slaa aliingia mjini Arusha majira ya saa 7:00 na ndege ya Precision akiwa na baadhi ya wajumbe wa chama hicho.
Baada ya kupokelewa ulianza msafara wa mnagari 15 kwenda Karatu. Msafara huo ulihusisha wabunge Halima Mdee, Grace Kiwelu na Lucy Owenya na wafuasi mbalimbali wa Chadema toka Arusha na mkoani Kilimanjaro.
Ratiba ya chama hicho inaonyesha kuwa mara baada ya mkutano huo wa jana, leo itaanza ziara ya kutembelea tarafa zote za Karatu kwa helikopta kukusanya wadhamini na baadaye atakwenda Arusha mjini, Musoma, Mwanza, Singida, Bukoba, Dodoma ikiwa ni safari ya kusaka wadhamini.
 
MS anachangamsha jukwaa kila wakati...
Usitoe mapovu kubishana nae...
 
Quinine, nimeona post zako, nikatambua ugeni wako humu, hiyo inaitwa 'name calling' ni kosa na adhabu yake ni ban.
Mimi siamini kwenye adhabu lakini nayajua madhara ya name calling, hata ukimjua fulani ni nani, anafanyia wapi na itafuatia jina kamili, then unakuwa umemvua nguo huyo mhusika na kumuacha ...wa nyama, hali itakayopelekea kumpoteza kabisa kwani tumeshapoteza wengi, watu makini kama kina Kuhani au FMeS baada ya kuvuliwa nguo humu, wako wapi?, tusimvue nguo MS ili tusimpoteze.

Kwa upande wangu, huyu Malaria Sugu kama jina lake linavyoonyesha, imeishapanda kichwani, hivyo ni kama kichaa fulani, baadhi ya hoja zake ni changamoto na nyingine ni utumbo utumbo, ila pia anawashabiki wake humu kama wale wapendao kuvaa t-shirt na kofia za yanga kwenye medani za siasa, mwacheni msiingilie uhuru wake.
pasco usimtetee mdini asiingilie watu na imani zao
 
Dk Slaa afunika


PostDateIcon.png
Tuesday, 27 July 2010 06:33
*Wapigakura waafiki aache jimbo awanie urais
Na Tumaini Makene, Karatu
MSAFARA wa kumsindikiza mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Willibrod Slaa ulisimamisha shughuli za wananchi wa mikoa ya Arusha na Manyara kwa eneo la takribani kilometa 20.
Msafara huo uliokuwa ukimsindikiza Dkt. Slaa kwenda kuomba ridhaa ya wananchi wa Karatu ili agombee urais badala ya ubunge wa jimbo hilo, na kisha kuchukua fomu ya kugombea urais, ulijumuisha magari ya kila aina takribani 80 na pikipiki zaidi ya 100 kuanzia katika Uwanja wa Ndege wa Arusha hadi Karatu.

Kutoka Arusha msafara huo ulikuwa na magari ya kifahari kama vile VX, VGX, Benzi na mengine ya kawaida zaidi ya 15. Ulipofika eneo la Mto wa Umbo ambalo liko katika Wilaya ya Monduli- Arusha, ambao ni umbali wa takribani kilometa 20 kutoka Karatu, msafara ulipokelewa na magari mengine mengi na waendesha pikipiki.
Kutokea hapo msafara ulikwenda kwa 'mwendo wa pole' ambapo mbali ya magari na pikipiki, msafara huo kuanzia eneo hilo, ulinogeshwa na helkopta iliyokuwa ikiufuata kwa juu kwenda Karatu.
Huku Dkt. Slaa akiwa amesimama ndani ya gari na nusu ya mwili ukiwa nje akiwapungia mikono watu, wananchi katika maeneo hayo walisimama kando ya barabara kushuhudia msafara huo na kupunga mikono yao, na wengine wakiamua kukimbia riadha kwa hatua kadhaa kuufuata.
Pamoja na msafara huo kuunganisha magari katika eneo la Mto wa Mbu, magari na pikipiki yalizidi kuongezeka kujumuika kadri muda ulivyokuwa ukikaribia kufika Karatu.
Hali ya shangwe ilitawala miongoni mwa wafuasia wa CHADEMA, baada ya msafara wao kulakiwa na umati mkubwa wa watu Mjini Karatu, ambapo ilionekana wazi shughuli nyingi kusimama na wananchi kuukimbilia msafara huo kueleklea Uwanja wa Bwawani.
Ni hapo ndipo Dkt. Slaa, mmoja wa wanasiasa machachari na mahiri nchini, ambaye amekuwa bungeni kwa miaka 15, aliamua kuikabidhi fomu yake ya kugombea ubunge Jimbo la
Karatu na badala yake akachukua fomu ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kushawishiwa na watu wa kada mbalimbali nchini.
Alifikia uamuzi huo baada ya wananchi hao kuulizwa mara kadhaa na Mwenyekiti wa CHADEMA Bw. Freeman Mbowe na yeye mwenyewe Dkt. Slaa iwapo wanaridhia yeye kuacha ubunge na kwenda kugombea urais ili aweze kuwatumikia watu wengi zaidi na kupata mamlaka ya kutekeleza yale
ambayo amekuwa akiyapigania bungeni.
Akizungumza katika kadamnasi ya watu wa Karatu, Dkt. Slaa alikiri kuwa baada ya kushawishiwa na watu mbalimbali wakiwemo wasomi wa vyuo vikuu waliotuma maombi maalumu, wananchi wa kawaida na wanachama wa CHADEMA kugombea urais, alihuzunika kwa sababu
alijua atawaacha watu wake wa Karatu.
"Nina majonzi kuwaaga lakini ninayo furaha...ni baada ya kupata ridhaa yenu, sina budi kwenda kuwatumikia Watanzania walioniita wakinitaka niwe rais...sauti ya watu ni Sauti ya Sauti ya Mungu...Mwalimu Nyerere alisema Ikulu si mahali pa kukimbilia, lakini nimeombwa na watu...Mungu ndiye huweka viongozi tukimtegemea na kumnyenyekea yeye tutaingia ikulu.
"Ninazo sababu nyingi za kukubali kuchukua fomu ya urais, nchi hii sasa inahitaji kiongozi makini, baada ya Nyerere na Mwinyi mamlaka ya nchi yamepokwa na kikundi cha watu wachache...nchi haiwezi kuendelea, wala utawala bora na wa sheria hautakuwepo kama ufisadi
hautapigwa vita.
"Taifa limeparanganyika kwa kukosa uadilifu, sasa wananchi maskini wanabaguliwa katika kupata huduma kama vile elimu na afya, tunahitaji rais wa kurudisha hatima ya wananchi kuamua mstakabali wa raslimali na maendeleo mikononi mwao, rais atakayetutoa katika matumaini yaliyopotea kuturejesha kwenye matumaini mapya," alisema Dkt. Slaa katika mkutano huo ulioombewa na viongozi wa dini za kiislamu na kikristo.
Katika maombi yao viongozi hao kwa nyakati tofauti walisema suala la ukombozi wa nchi halina dini wala rangi ya mtu.
Mapema akimkaribisha Dkt. Slaa kuwaeleza wananchi wa Karatu sababu za kumwomba na kumruhusu Dkt. Slaa kuondoka bungeni na kugombea urais, Bw. Mbowe alisema kuwa CHADEMA kimejipanga kushinda urais na kupata majimbo mengi ya ubunge katika Uchaguzi Mkuu wa
Oktoba mwaka huu.
"Tumeweka mikakati maalumu ya kuwatumikia na kupigania maslahi ya Watanzania, Dkt. Slaa anakwenda kushinda urais tunaomba aungwe mkono...CCM wameshtuka kusikia anagombea urais. Zama zao na zama za Kikwete zimekwisha... ikitokea hajashinda na mkatupatia wabunge
wengi jueni kuwa Dkt. Slaa atakuwa ndiye spika wetu.
"Lakini pia msihofu kuwa Dkt. Slaa hatasikika, yeye ndiye Katibu Mkuu wa CHADEMA, ndiye mpishi wa mambo yote ya chama yanayoibuliwa na wabunge wa chama chenu bungeni, tumeamua kumtumia kuliokoa taifa, kama vile Mungu alivyomtoa mwanaye wa pekee, Yesu, kuwakomboa
wote wenye dhambi," alisema Bw. Mbowe.

SOURCE: Dk Slaa afunika
 
Back
Top Bottom