Elections 2010 Dr Slaa aitikisa Karatu

Maudhi mengine Bwana, Siasa ni uchafu, inanuka kero tupu. Sasa sijui Mbowe kshikishwa na CCM? Kama una akili timamu huwezi kumuachia Dr.Slaa agombee Uraisi huku ukijua hatashinda matokeo yake Bunge litasinzia, litabaki halina msisimko.

Sleep away my friend!!! Hivi unafikiri wale jamaa Uyole waliomrushia mawe JK wameshamsamehe??? Safari hii ngoma kwisha kwa SISIEM unless waalete yale mazingaombwe yao ya ZNZ.
 
We will take our chance.

Ni heri kukosa Mbunge Slaa kuliko kuwa na Watanzania Makondoo wanaotaka watafuniwe kila kitu na hata hivyo kumeza bado watasema hawawezi. Sijui kuwaingizia mirija kwenye makoromeo yao na kuwapitishia Wakurya wakiitacho "NYUKA?" (uji).

Tumewachokeni wote mnaosema JIMBO LA KARATU. Muanze kufahamu kuwa TGV limeshaondoka kuelekea Magogoni. Au mnapanda na sisi kuelekea huko au mkae kimya. Mstari umeshachorwa.............

UKO NA SLAA AU UKO NA MAFISADI.

Hapo chini kwenye BOLD, hata Yesu na Nyerere walisema "Sintakuwa nanyi milele........" Kwa nini msitafute wabunge wengine walete msisimko? Kwa nini mnaendelea kuwachagua haohao CCM mkifahamu kuwa wanaleta usingizi?
Mmekuwa mkilalamika kuwa KIKWETE anaogopa kufanya MAAMUZI MAGUMU, haya basi. Mmepata mtu anayefanya maamuzi magumu na mnaanza kuleta story nyingine nyingiiiii..... Kama wewe ni mwanamume basi naanza kuamini wimbo wa Lady JD kuwa "Wanaume kama Mabinti". Kama wewe na wanaolilia jimbo la Karatu ni Wanawake basi sintashangaa maana ni HULKA (nafahamu kuwa siyo wote, akina mama msiniuwe).

Mzee Sikonge, Watanzania ni wasahaulifu sana. Kama kweli uko Sikonge nafikiri itakuwa vizuri ujaribu kushirikiana na jamaa (CHADEMA) kuwaandikia hotuba ili waseme kile wananchi watapenda na kitawagusa akisikia. Nafikiri Dr. Silaa na timu yake kama kweli wako makini kama tunavyofikiria itabidi atafute na nguvu kadhaa kutoka humu JF ili wampe mawazo. Obama alikuwa na watu wa kawaida sana kwenye timu yake ya ushindi. CCM kule habari choka, wao wanapanga tu jinsi ya kufanya mazingaombwe kama wanavyofanyaga ZNZ.
 
Mabadiliko ya kweli yamewadia.

Tanzania inatarajia kupata Mwanga mpya na kuhitimisha harakati zenye upofu,Ovu,na Ubakaji wa hali ya juu wa rasilimali za nchi kwa maslahi ya matajiri wachacheambao eti wamejimilikisha uchumi wa nchi wanaodhulumu haki za waliowengi na wavuja jacho wakubwa wa Taifa hili.

Chondechonde watanzania tusipoteze bahati hii tuliyopewa kwa kumchagua mpiganaji kamanda mkuu wa vita dhidi ya ufisadi Daktari Peter Wilbrod Slaa.Ambaye anahitaji Nguvu yetu katika kuhitimisha wizi na ufisadi wa hali ya juu nakutuingiza watazania katika harakazi ya kumliki rasilimali zetu wenyewe.Ninani ambaye hatafurahi akiona anafaidika mojakwa moja na faida itokanayo na madini,utalii na rasilimali nyngi tulizo neemeshwa na mungu?

Hivi ni nani mwananchi wa kawaida leo hii anaweza kujivunia kufaidika na rasilimali za nchi hii?Watanzania tufunguke macho tufanye mabadiliko makumbwa katika sanduku la kura kwa kuipa kura CHADEMA ilikuhitimisha harakazi za kifisadi na ubakaji wa haki zetu unaoendelea hivi sasa ni nani kipofu asiyeona?

Eti tumevuka lengo tumezalisha ajira Mil1.3 hahhahhahha kule ATCL VIPI TRL JE ? WAMEZALISHA AJIRA MIL1.3 WAMEUA AJIRA 5MIL TUWAPIGE CHINI JAMANI.
 
Nimeona kwenye ITV slaa akiwa huko karatu.jamani ule umati unatisha.swala ni je hawa watu wamejiandikisha kupinga kura?na je siku hiyo kama wamejiandikisha watakwenda.Kunahitajika elimu ya kutosha kabla ya tarehe ya uchaguzi ule umati unahamasisha sana.
 
Nimeona kwenye ITV slaa akiwa huko karatu.jamani ule umati unatisha.swala ni je hawa watu wamejiandikisha kupinga kura?na je siku hiyo kama wamejiandikisha watakwenda.Kunahitajika elimu ya kutosha kabla ya tarehe ya uchaguzi ule umati unahamasisha sana.

Nyie wana-Chadema mnaishi kwa matumaini mno hapa JF! Mnavyowekeza mawazo yenu mnataka kufanya kama vile kila mtu yuko CHADEMA hapa. Hali halisi hamuioni kabisa. Alikuja Mrema hapa, 1995, hakuna makundi makubwa kama yale yaliyowahi tokea; Wapi? Alikuja Mbowe na Helikopter yake,,, hata mimi nilienda kushangaa helicopter, watu kibao; wapi. Angalau hata kwa percentage tu, tuone nchi imeshtuka! Nasema hivi, huko Ground, ziliko roots, watu hawajui hata kama kuna kitu kinaitwa Chadema duniani. Mageuzi muhimu sana kama ni ya lazima, ila TZ still have another 20 years to make real change. Come october, we will see.
 
Naona hapa Sultan CCM ameafanikiwa kumteka au kumnunua SLAA ili kuugawa upinzani na pia kuhatarisha jimbo kutekwa na CCM ,jamani Slaa na uraisi wapi kwa wapi ? Ninawasiwasi Chadema wanatuika kuzigawa kura za WaTZ
 
Naona hapa Sultan CCM ameafanikiwa kumteka au kumnunua SLAA ili kuugawa upinzani na pia kuhatarisha jimbo kutekwa na CCM ,jamani Slaa na uraisi wapi kwa wapi ? Ninawasiwasi Chadema wanatuika kuzigawa kura za WaTZ

Ohoooo, we karagabaho!! Slaa huyooooooo Magogoni BRAVO AND GOD BLESS
 
GS, over excitement si jambo jema sana! Mikakati ndiyo muhimu!

Bibi Ntilie,

Ndiyo unatakiwa kuwapenyezea akina GS mikakati ili wakikutana kwenye vikao vyao pale Kinondoni Manyanya, Makao Makuu ya chama, waweze kujadili michango ya mikakati ya ushindi. Kila mtu mwenye mapenzi mema na anayeitakia mema nchi yetu ni wakati muafaka kutoa michango ya mikakati ya ushindi.
 
Watanzania wanajua Dr. Slaa ana nia ya kupigana na mafisadi. Sasa anawaomba wampe nguvu ya kufanya hivyo. Akipata nguvu ya Urais itamtosha.

Tuna uhakika 100% kwamba tukimchagua JK aendelee kwa miaka 5 tena hali ya Watanzania itaendelea kuwa mbaya. Yeye na CCM na TANU wametutawala tangu tupate Uhuru bila kuweza kutuongoza kwenye maisha bora.

Mazoea ni mabaya. Kuna waliozoea kutawaliwa na CCM kiasi kwamba wanadhani haiwezekani kuleta mabadiliko. Inawezekana, timiza wajibu wako. Mbona imewezekana Kenya na Zambia?

I am not easily given to emotion, but my eyes misted when I saw the picture of Slaa standing infront of a massive crowd in Karatu. It made me feel that perhaps the Lord Himself is on our side. Slaa is loved in our country. You will see it.

CCM inajua haiwezi kumshinda Slaa kwa hoja. Watatafuta mbinu nyingine. Watatumia mbinu chafu kama ikibidi. They are good at that. See what some of their kind are doing in their campaign for nomination in Moshi. CCM lives and thrives on evil. CHADEMA must guard Slaa very vigilantly.

Naamini huu ndio mwanzo wa mwisho wa ukiritimba wa madaraka kwa CCM. Mwaka ujao utakuwa kweli mwaka mpya kwa Watanzania. It will be the end of the false start that they made nearly 50 years ago.

Allow me to paraphrase Jesse Jackson and say: "If not now then when? If not Slaa then who?" Go Slaa Go!
 
Naona hapa Sultan CCM ameafanikiwa kumteka au kumnunua SLAA ili kuugawa upinzani na pia kuhatarisha jimbo kutekwa na CCM ,jamani Slaa na uraisi wapi kwa wapi ? Ninawasiwasi Chadema wanatuika kuzigawa kura za WaTZ

Mwiba hii sio CUF na siasa za Zanzibar za kufanywa mabwege na CCM, cha muhimu ni kuwashauri hao jamaa zako wa CUF wamsupport SLaa, ili angalau Lipumba apate japo uwaziri wa Fedha ama Mambo ya nje
 
Ni muhimu wote tumuunge mkono japo mafisadi wataiba kura ila fundisho watalipata.PEOPLE POWER WILL BE THERE SOON.:A S angry:
 
Mashinda Mtei, GS tunashukru sana kwa picha wakuu, tunaomba hotuba ya Karatu pia mutuwekeee! Go Dr. Slaa Goooooooooooooo!
 
Back
Top Bottom