Dr Slaa aitikisa Karatu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dr Slaa aitikisa Karatu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Regia Mtema, Jul 25, 2010.

 1. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #1
  Jul 25, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Mgombea Urais kipitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kesho ataunguruma Nyumbani kwake Karatu. Dr Slaa anakwenda kukutana na wanakaratu aliowatumikia kwa kipindi cha miaka kumi tano(15) akiwa Mbunge. Kabla Dr Slaa hajaenda tayari kuna timu moja toka Makao Makuu imeshakwenda jana kwaajili ya kufanya maandalizi kwa kushirikiana na Watu wa Karatu.

  Timu nyingine ikiongozwa na Kamanda Freeman Mbowe inaondoka leo kuelekea huko.Viongozi wa ngazi ya juu wa chama pamoja na Prof Baregu ndio timu inayomsindikiza Dr Slaa. Baada ya kuzungumza na Wanakaratu Dr Slaa atacchukua fomu na kuzunguka nchi nzima kwaajili ya kupata wadhamani. Safari ya kuzunguka nchi nzima Dr Slaa atasindikizwa na Kamanda mwenzake Freeman Mbowe.

  Wengine tumebaki Makao Makuu tukiendeleza mapambano.Leo tutakuwa na wawakilishi/mashujaa wa wanazuoni walisaini kutaka Dr Slaa agombee Urais kwaajili ya kupanga mikakati ya namna ya kumuunga mkono Dr Slaa kwa staili mpya kabisa. Mkutano huo unatarajiwa kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 7 mchana Makao Makuu Kinondoni Manyanya Mtaa wa Ufipa.Mnakaribishwa sana kwa wale mnaopenda kushiriki harakati hizi muhimu.

  Find attachment hotuba ya Ufunguzi ya Mwenyekiti wa Kamati ya BAVICHA-Bw John Mnyika.

  Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke.

  Angalia picha chini:

  [​IMG]
  Dr. Slaa akikabidhi fomu kwa Mwenyekiti Mbowe

  [​IMG]

  Karatu wakiridhia Dr. Slaa awe mgombea Urais.
   

  Attached Files:

 2. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Akienda huko karatu asisahau kum-endorse na kuwatambulisha wana karatu mgombea mpya wao wa ubunge kwa tiketi ya chadema..


  nawatakia kila la kheri wana chadema wote.
   
 3. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  CCM yajulikana kwa fitina na mizengwe ndani na nje ya chama! Kikubwa chenye matamanio yangu ni kwamba - Dr. Slaa anapewa ulinzi madhubuti na afya yake inatiliwa maanani na kulindwa. Pilikapilika ni nyingi, na katika vikumbo vya hapa na pale katika hizi kampeni, ulinzi na afya vyaweza kuwa overlooked. Usalama kwanza! Haitopendeza kuanza kusikia story kama za akina Yushchenko wa Ukraine...

  Nawatakia kampeni njema.
   
 4. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mafisadi wajinyonge
   
 5. P

  Paul S.S Verified User

  #5
  Jul 25, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Namuamini sana Dr lakini kwahili naona kama anaenda kuliweka jimbo la karatu rehani
   
 6. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  acha woga!!! jimbo litabaki na mengine yataongezeka. ukombozi wa Tanzania ni sasa!! tuna imani sana na Dr. Slaa
   
 7. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Heri aiweke karatu rehani ila aiokoe Tanzania kuliko sasa hivi nchi iko rehani hewani kabisa
   
 8. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Kama kweli Lipumba ni mpenda mabadiliko, angemuunga Mkono Dr. Slaa. Ingekuwa vizuri kama viongozi wa CUF na CHADEMA wakawa kwenye maongezi katika ngazi ya juu kabisa. Bila muungano wa namna moja au nyingine hatuwezi kuwashinda mafisadi.
   
 9. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #9
  Jul 26, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Kwa vyombo vya habari vinavyoelezea rushwa za CCM katika kura za maoni sasa hivi, kweli njia ni nyeupe kwa CHADEMA!...Tuko nyuma yenu GS.
   
 10. R

  Ramos JF-Expert Member

  #10
  Jul 26, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Binafisi niko tayari kwa HALI na MALI katika kuunga mkono harakati hizi za ukombozi. Naamini huku Morogoro tutakuwa na kazi kubwa ya kufanya katika kusaidia haya mambo...
   
 11. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #11
  Jul 26, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,656
  Likes Received: 21,868
  Trophy Points: 280
  Kila lakheri Dr Slaa, kila lakheri waTanzania. Mapambazuko yamewadia na tusipoteze fursa hii adimu ya kubadilisha mwelekeo wa nchi.
   
 12. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #12
  Jul 26, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Tumejipanga vya kutosha.Hatuwapi nafasi maadui ng'o..Tupo kamili gado.
   
 13. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #13
  Jul 26, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Saa tano kamili atapokelewa na maelfu uwanja wa ndege wa Arusha na kusindikizwa mpaka Karatu ambapo leo atawasha moto huko.

  Stay tuned..
   
 14. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #14
  Jul 26, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kila la kheri Dr. tupo nyuma yako tunakuunga mkono.
   
 15. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #15
  Jul 26, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  GS tuhabarishe kila kinachojiri
   
 16. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #16
  Jul 26, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Habari nitazileta.Atapokelewa saa tano mchana uwanja wa ndege wa Arusha na mamia ya wakazi wa Arusha na Moshi na kusindikizwa na magari mpaka Karatu.
   
 17. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #17
  Jul 26, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  tupo pamoja Dr Slaa
   
 18. Uncle Rukus

  Uncle Rukus JF-Expert Member

  #18
  Jul 26, 2010
  Joined: Jun 16, 2010
  Messages: 2,430
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Na msikitikia sana dokta Maslaa, Ndio mwisho wake huu ametolewa kafara na Chadema!
   
 19. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #19
  Jul 26, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,646
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280

  umekata tamaa ki hivyo?
   
 20. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #20
  Jul 26, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,646
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280

  all the best GS...usisahau kutupatia nakala ya yatakajojiri leo kwenye mkutano!
   
Loading...