Dr. Slaa afunguliwa mashtaka mahakama kuu leo

Kiwi

JF-Expert Member
Sep 30, 2009
1,054
990
DR. SLAA AFUNGULIWA MASHTAKA MAHAKAMA KUU LEO


MGOMBEA urais kwa tiketi ya CHADEMA, Dk. Willbrod Slaa (pichani), amefunguliwa kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaami, akidaiwa fidia y ash. bilioni moja kwa madai ya kunyang'anya mke wa mtu.

Kesi hiyo namba 122 ya mwaka 2010, ilifunguliwa leo mahakamani hapo na Aminiel Mahimbo kwa kupitia ofisi ya mawakili ya Amicus.

Mahimbo anadai kuwa, Dk. Slaa kamnyang'anya mkewe wa ndoa Josephine Mushumbusi.

Kwa kupitia nakala ya hati ya madai, Mahimbo anadai fidia ya sh. milioni 200 kutokana na hasara alizozipata baada ya mdaiwa huyo, kumtangaza mkewe wa ndoa Josephine kuwa mchumba wake na sh. milioni 800 ikiwa ni hasara ya jumla aliyopata.

Mlalamikaji huyo, anadai Septemba 7, 2002 alifunga ndoa na mwanamke huyo katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ushirika wa Kijitonyama na kuishi maeneo mbalimbali ikiwemo Kimara, Baruti, Dar es Salaam.

Pia anadai katika maisha yao ya ndoa wamebahatika kuwa na watoto wawili ambao ni Upendo aliyezaliwa Mei Mosi, 2003 na Precious aliyezaliwa Machi 14, 2007.

Mahimbo alidai, ndoa kati yake na Josephine haijavunjwa na chombo chochote na kwamba, bado ni mke wake halali.

Kwa mujibu wa hati hiyo, Mahimbo alidai hivi karibuni, mkewe alikuwa na safari za mara kwa mara na aliamini ni za kikazi. Josephine ni mfanyabiashara ambaye anaendesha kampuni iitwayo Green World Clinic.

Alidai katika tarehe na mahali tofauti, Dk. Slaa alimtambulisha mwanamke huyo kuwa ni mkewe, suala ambalo si kweli.

Mlalamikaji huyo alidai, uhusiano uliopo kati ya watu hao wawili umemfanya adhalilike na kunyanyasika katika jamii na anaiomba mahakama kumzuia Dk. Slaa kuendelea kujihusisha kimahusiano na mkewe.

Anaiomba mahakama kumwamuru Dk. Slaa kumlipa bilioni moja na kulipa gharama za kuendeshea kesi.

Mahimbo amedai ameambatanisha na cheti cha ndoa na Josephine, picha za harusi, vyeti vya kuzaliwa vya watoto na nakala za vipande vya magazeti zilizopigwa wakati Dk. Slaa akimtambulisha mwanamke huyo kuwa ni mkewe.

Source: Michuzi

Hizi ni njama za ccm kumuwekea visiki Dr. Slaa asiendelee vizuri na kampeni za uraisi. Watanzania tufungue macho, tuone hila za CCM kung'ang'ania kutawala ili kuendeleza ufisadi na utawala mbovu. Watanzania wazalendo wote tuwe pamoja na Dr. Slaa wakati huu kumuunga mkono, na kulaani njama za CCM.

Kwa pamoja, hakika tutashinda kwa vile juhudi zetu ni za haki mbele ya Mwenyesi Mungu na wanadamu. Juhudi za CCM zimejaa uovu uliokithiri, na hakika watashindwa.

 
Umeanza na judgement wakati kesi iko mahakamani.

Tujifunze kuwa na political correctness.
 
This is a frivolous lawsuit that I am absolutely certain it will be tossed away. You watch.....
 
Hapo ndipo walipojifunga midomo kesi iko mahakamani Mahimbo hawezi tena kwenda kwenye media.
 
Jamani huyu dada alivyomzuri hakuna ambaye angempisha pembeni na kumuacha. Dr alikuwa right, Mahimbo ulikosea sana kumuacha mke mzuri hivi. Sasa hapo hiyo kesi ni rahisi umedanganywa na mke keshaondoka huyo.
 
By ABDUEL ELINAZA, 6th September 2010 @ 23:56 , Total hits: 34
MR Aminiel Chediel Mahimbo, who claims to be the husband of Ms Josephine Mushumbusi, the woman at the centre of a “marriage” dispute involving Chadema Union presidential candidate, Dr Wilbrod Slaa, is today expected to file a suit at the High Court demanding 1bn/- compensation from the presidential hopeful.
Advocate Abduel Kitururu of Amicus Attorneys, told a news conference in Dar es Salaam yesterday on behalf of his client that Mr Mahimbo has not divorced his wife, but Dr Slaa "snatched Josephine from him."

Mr Kitururu said Dr Slaa and Josephine would jointly be required to pay Mr Mahimbo 1bn/- being compensation for the marriage breakdown.

“We are having all relevant documents including marriage and children's birth certificates, as well as wedding photos to prove our case,” Mr Kitururu said.

There are also newspapers cuttings quoting Dr Slaa as saying that Josephine is his wife," the advocate said. He further said the court would determine the final amount of compensation. "It may increase or decrease what we are demanding from Dr Slaa and Josephine," he added.

Mr Kitururu dismissed as baseless claims that he was being used by some politicians including CCM officials to frustrate Dr Slaa in his presidential campaign. He said his client had long ago planned to go to court.

"This is just a coincidence," he noted. Dr Slaa, however, told the 'Daily News' that he was not losing his sleep on such baseless negative and mud-smearing campaigns against him.

He said the objective of the suit was to derail him from concentrating on the campaign trail and blamed the ruling CCM for what he claimed to be foul play. “Where do proceedings on matrimonial disputes start in accordance to the Law of Marriage Act of 1971.

Ask Mr Mahimbo, where was he when Josephine left him?" Dr Slaa queried. Mr Kitururu, however, said: “We are not talking about divorce. This is purely a matter of compensation because at this point there is a breach of contract."

The Chairman of Demokrasia Makini, Mr Jimmy Obedi Mshana, said it was high time for politicians to concentrate on serious national issues instead of matrimonial affairs.

“I think we have to change. Let us give more attention to development issues," Mr Mshana said. “A marriage is a contract and if one party breaches it, he or she must compensate the aggrieved party," Mr Kitururu insisted.

Mr Mahimbo and his wife were married at Kijitonyama’s Evangelical Lutheran Church of Tanzania in 2002. They have two daughters, according to Mr Kitururu
 
Wakili wa Mahimbo ni Abduel Kitururu mgombea udiwani Ubungo....kupitia CCM!
 
The puke of this type has been already been posted by a respectable member called KIWI!
Mods, hopefully take this to suicide!..huh!
 
very simple case

all wat Dr slaa needs to say is that,

FIRST , I DDNT KNW THAT SHE WAS A MARRIED WOMAN....and
SECOND, I HAVE NEVA HAD SEX WITH HER.....!


case closed!!!!!!!!!!

NO ONE CLD PROVE OTHERWISE..!
 
Acha upofu wewe au sababu nawe kazi yako ni dungua dungua hutaki kuoa!Chukulia wewe ndio ungevaa viatu vya mahimbo ungejisikiaje katika jamii inayokuzunguka wakati mkeo wa ndoa anatambulishwa hadharani kuwa ni mchumba wa Tandale one?
Kuwa na akili wakati wa kuchangia mada na si kutoa upuuzi kama huo,yaani mtu unampenda mwenzio hata kama kakosea hutaki kumshauri arekebishe makosa!Inaonyesha ni jinsi gani nyie wa chadema uwezo wenu wa kufikiri mnatumia yaliyomo katika pua na si yale ya kichwani mwenu ujinga!Kweli nimeamini wengi wenu mmepitia shule lakini itakuwa kazi ngumu kuelimika!Badilikeni na acheni ushabiki wa kishamba huo!

Na mpaka ifikie mke kutambulishwa hadharani huyo mume wa kweli alikuwa wapi? Muda wote ambao wametengana yeye tamaa zake za kimwili anamalizia wapi?
 
Jamani huyu dada alivyomzuri hakuna ambaye angempisha pembeni na kumuacha. Dr alikuwa right, Mahimbo ulikosea sana kumuacha mke mzuri hivi. Sasa hapo hiyo kesi ni rahisi umedanganywa na mke keshaondoka huyo.

On a serious note, tuache ushabiki wa kiasisa. Mahimbo na Josephine wana watoto 2, mmoja ana miaka saba nawa pili ana miaka mitatu tu. With a benefit of doubt as simjui huyu Josephine wala yaliyojiri kwenye ndoa yake, I feel for the kids jamani. How can one propose to a woman, without marital background.
 
Na mpaka ifikie mke kutambulishwa hadharani huyo mume wa kweli alikuwa wapi? Muda wote ambao wametengana yeye tamaa zake za kimwili anamalizia wapi?

Unahalalisha makosa ya Dr and Mrs Slaa to be. Ndoa it not all about kumaliza tamaa za mwili, it is about the family hasa pale unapokuwa na watoto wadogo. Nadhani Josephina ana makosa kuliko Slaa. Huyo mume alitakiwa amshtaki mkewe at the first place kwa kuvunja mkataba waliokubaliana kanisani, mbele ya mashahidi kuwa watakuwa pamoja kwa shida na raha hadi kifo kitakapowanganisha. Ni vyema kuona vithibitisho vya ndoa ya Josephine kuvunjwa, vinginevyo mama hana aibu ya kutambulishwa kama mpenzi huku akijua fika ana ndoa.
 
very simple case

all wat Dr slaa needs to say is that,

FIRST , I DDNT KNW THAT SHE WAS A MARRIED WOMAN....and
SECOND, I HAVE NEVA HAD SEX WITH HER.....!


case closed!!!!!!!!!!

You are very right, Dr Slaa alimtambulisha kama Mchumba wake na siyo mke wake
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom