Dr. Slaa afunguliwa mashtaka mahakama kuu leo

DR. SLAA AFUNGULIWA MASHTAKA MAHAKAMA KUU LEO

MGOMBEA urais kwa tiketi ya CHADEMA, Dk. Willbrod Slaa (pichani), amefunguliwa kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaami, akidaiwa fidia y ash. bilioni moja kwa madai ya kunyang’anya mke wa mtu.

Kesi hiyo namba 122 ya mwaka 2010, ilifunguliwa leo mahakamani hapo na Aminiel Mahimbo kwa kupitia ofisi ya mawakili ya Amicus.

Mahimbo anadai kuwa, Dk. Slaa kamnyang’anya mkewe wa ndoa Josephine Mushumbusi.

Kwa kupitia nakala ya hati ya madai, Mahimbo anadai fidia ya sh. milioni 200 kutokana na hasara alizozipata baada ya mdaiwa huyo, kumtangaza mkewe wa ndoa Josephine kuwa mchumba wake na sh. milioni 800 ikiwa ni hasara ya jumla aliyopata.

Mlalamikaji huyo, anadai Septemba 7, 2002 alifunga ndoa na mwanamke huyo katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ushirika wa Kijitonyama na kuishi maeneo mbalimbali ikiwemo Kimara, Baruti, Dar es Salaam.

Pia anadai katika maisha yao ya ndoa wamebahatika kuwa na watoto wawili ambao ni Upendo aliyezaliwa Mei Mosi, 2003 na Precious aliyezaliwa Machi 14, 2007.

Mahimbo alidai, ndoa kati yake na Josephine haijavunjwa na chombo chochote na kwamba, bado ni mke wake halali.

Kwa mujibu wa hati hiyo, Mahimbo alidai hivi karibuni, mkewe alikuwa na safari za mara kwa mara na aliamini ni za kikazi. Josephine ni mfanyabiashara ambaye anaendesha kampuni iitwayo Green World Clinic.

Alidai katika tarehe na mahali tofauti, Dk. Slaa alimtambulisha mwanamke huyo kuwa ni mkewe, suala ambalo si kweli.

Mlalamikaji huyo alidai, uhusiano uliopo kati ya watu hao wawili umemfanya adhalilike na kunyanyasika katika jamii na anaiomba mahakama kumzuia Dk. Slaa kuendelea kujihusisha kimahusiano na mkewe.

Anaiomba mahakama kumwamuru Dk. Slaa kumlipa bilioni moja na kulipa gharama za kuendeshea kesi.

Mahimbo amedai ameambatanisha na cheti cha ndoa na Josephine, picha za harusi, vyeti vya kuzaliwa vya watoto na nakala za vipande vya magazeti zilizopigwa wakati Dk. Slaa akimtambulisha mwanamke huyo kuwa ni mkewe.

Source: Michuzi

Hizi ni njama za ccm kumuwekea visiki Dr. Slaa asiendelee vizuri na kampeni za uraisi. Watanzania tufungue macho, tuone hila za CCM kung'ang'ania kutawala ili kuendeleza ufisadi na utawala mbovu. Watanzania wazalendo wote tuwe pamoja na Dr. Slaa wakati huu kumuunga mkono, na kulaani njama za CCM.

Kwa pamoja, hakika tutashinda kwa vile juhudi zetu ni za haki mbele ya Mwenyesi Mungu na wanadamu. Juhudi za CCM zimejaa uovu uliokithiri, na hakika watashindwa.

******* tu!!!
 
Hii sasa itakata mzizi wa fitina. Manake magazeti yamefungwa midomo sasa, hakuna kusema sema tena, na wakati huo huo, Dr. Slaa hajawekewa pingamizi juu ya ugombea wake wa Urais, kwa hiyo ataweka tu advocates waendelee kuichora hiyo kesi wakati yeye akiendelea na kampeni. Hapa tena CCM imechemka strategy. Na kuna kila sababu ya kuhoji, ni kwa vipi kesi hii imefunguliwa mahakama kuu na si mahakama ya mwanzo kama zilivyo nyingine. Advocates wa Dr Slaa, take that into account, hii kesi inaweza kushindwa kabla ya kusikilizwa. Just keep your eyes and ears wide open.
 
Hiyo ni binu chafu! Kesi ya namna hii iko natokea kila siku!
Hiyo mabo ya chama tawala ambaye inasubuka kusima moto ya Dr Slaa
 
Marriage is a contract..and a contract can b valid,void or voidable...contract inakua valid when there is clear consent btwn parties to contract...kwa case hii tuna two parties namely mahimbo and josephine...kwa hiyo kama kuna breach ya condations and warranties then the affected party without a reasonal doubt has a right to sue the other party b4 the court...kwa hiyo mahimbo ana haki ya kufungua kesi na kulingana na ushahidi wa vielelezo na wa kimazingira its 100 per cent Mr.Mahimbo atakua billionaire veri soon...the bottom line ni kua kama Slaa ameweza kudiriki kupora mke pamoja na watoto wa mahimbo just imagine akiwa raisi si atawapora wake wa akina Zitto,Prof Baregu,Mbowe na Mnyika(kama ameoa)....mwisho natabiri Dr.Slaa kuenguliwa katika mbio raisi...let us wait and see
 
Umeanza na judgement wakati kesi iko mahakamani.

Tujifunze kuwa na political correctness.

Mahimbo alipoenda kwenye media kulalamika, na kutoa vielelezo vyote anavyokusudia kutumia kujitetea, tayari ameingilia uhuru wa mahakama kutoa uamuzi ulio huru na haki. Mahakama ikitoa uamuzi kinyume na matarajio ya watu, basi, inaonekana kwamba imependelea upande mmoja.

Hii ndio sababu ya kuzuia kuzungumziwa kwa kesi yoyote ambayo iko mahakamani au inayokusudiwa kupelekwa mahakamani, isipokuwa kutoa taarifa zake kwamba kesi hiyo imepelekwa mahakamani.

Waandishi wanaotangaza habari za kesi hiyo kwa undani wake WANAHARIBU matokeo ya kesi hii. Kisheria, kesi hii tayari ni 'nolle prosequi' kwa kuwa imeshakuwa 'frustrated'. Wanasheria najua mtanikosoa, lakini huu ndio mtazamo wangu... labda nimekosea.

-> Mwana wa Haki
 
CCM wajanja wanatapatapa tu. Hizo mbinu na propaganda zao sidhani kama zitamsumbua ndugu yetu mkombozi Dr Slaa. Wanataka tu wamchanganye ili ashindwe kuzingatia uchaguzi. Na huyo anayedai ni mme original wa Josephine sijui amehongwa kiasi gani na CCM. Nadhani hizo pesa alizohongwa ndio zile walizoiba kwenye EPA na ma-ufisadi mengine, ambazo kama zisingeibiwa zingetumika kufanyia mambo ya maana kama kujenga mazahanati n.k. Lakini hii inaonyesha jinsi CCM wanavyotapatapa! Mbaya zaidi nadhani CCM hawana washauri wazuri. Wamekosea kweli kumshtaki Dr Slaa, kwani nimjuavyo ni mtu makini na asingekurupuka kufanya maamuzi ya kuingia kwenye ndoa kabla hajafanya utafiti wa first lady wake to be kama ni mtu wa namna gani na ana background gani!
 
usituvunge hapa, huyu hana nia moja safi, sasa kusema kuwa kaishi na miaka mingi na kuzaa nae kisha kaamua kumuoa huyu huo usafi uko wapi ?

hivi si ukristo unasema katika amri ya sita, usizini ? au kuzini kuna tafsiri gani hadi slaa asiwe mzinifu aliishi maisha yake kwa uzinzi hadi akapata watoto wawili

na kuhusu huyu wa sasa anatembea nae na kulala nae hivi ukristo ndio unavyotufundisha mtu ukitaka kumuoa mufanye hivi kwenye majukwaa ya siasa na kutembea nae?

watu wa maadili mko wapi?

mm nampinga slaa kwanza kuutukanisha ukristo na biblia ambayo mm na wenzangu tunaiheshimu sana

pili kuidhalilisha familia ya huyo muhuni wake wa kwanza kwa kukaa na mtoto wa watu hadi kuzaa nae bila kumuoa

tatu kuiba mke wa mtu na kumtangaza hadharani
nne kuwakosea heshima wazee na wanandugu wa huyu muhuni mwenziwe mpya

tano kuwakosea heshima watanzania ambao waliamini kuwa dr Slaa(padri aaliestaafu baada ya kujigundua kuwa anapenda uzinzi) ni mfano mwema wa kuigwa ni mwenye uchungu na nchi na kutaka watu wa heshimu nchi na kuheshimiana kumbe sivyo

sita kuwakosea wanachadema kwa kuamini kuwa wamesimamisha mgombea anaeweza kuuzika baada yule wa WAPUKI(kundi la wavuta bangi la sehemu fulani walipokuwa vijana) lkn matokeo yake ni kiongozi hata bure hanunuliki

kwa kweli huyu ni muhuni tu

Slaa KAFELI Upadri , KAFELI ndoa mnategemea ataweza nini? mtu ufeli basic mathematics mnategemea intergral ktk space ataiweza??
 
Niseme nashindwa kuelewa kitu kimoja:

Mwaka 1995, alitumika Angelina Mrema over Augustine Mrema (kama mnakumbuka), ikatumika kumdhoofisha Mrema kwa kila namna iliyowezekana, baada ya uchaguzi hata haikueleweka aliishia wapi huyu!

Mwaka 2005, akatumika Mahita over CUF, tukaaminishwa kuwa CUF ni chama cha kigaidi, wakadai wameleta lori la visu na majambia n.k na watanzania wakaiogopa CUF kabisa! Baada ya uchaguzi hata hatujui hizo silaha ziliishia wapi!

Mwaka huohuo 2005 wakamdhalilisha VIBAYA mwanasiasa ninayemkubali ndani ya CCM, Salim Ahmed Salim na kumwita "Mwarabu" na tena "Muuaji", ikamshushia heshima na akajikuta anaamua kukubali yaishe, baada ya uchaguzi hatukusikia lolote, akabembelezwa kuwa 'makundi yaishe'.

Sasa naona 2010 ni maalum kwa Slaa, maanake nini hii? Ni siasa gani hizi? Nani huwa nyuma ya mikakati hii?
USALAMA wa TAIFA period!
 
usituvunge hapa, huyu hana nia moja safi, sasa kusema kuwa kaishi na miaka mingi na kuzaa nae kisha kaamua kumuoa huyu huo usafi uko wapi ?

hivi si ukristo unasema katika amri ya sita, usizini ? au kuzini kuna tafsiri gani hadi slaa asiwe mzinifu aliishi maisha yake kwa uzinzi hadi akapata watoto wawili

na kuhusu huyu wa sasa anatembea nae na kulala nae hivi ukristo ndio unavyotufundisha mtu ukitaka kumuoa mufanye hivi kwenye majukwaa ya siasa na kutembea nae?

watu wa maadili mko wapi?

mm nampinga slaa kwanza kuutukanisha ukristo na biblia ambayo mm na wenzangu tunaiheshimu sana

pili kuidhalilisha familia ya huyo muhuni wake wa kwanza kwa kukaa na mtoto wa watu hadi kuzaa nae bila kumuoa

tatu kuiba mke wa mtu na kumtangaza hadharani
nne kuwakosea heshima wazee na wanandugu wa huyu muhuni mwenziwe mpya

tano kuwakosea heshima watanzania ambao waliamini kuwa dr Slaa(padri aaliestaafu baada ya kujigundua kuwa anapenda uzinzi) ni mfano mwema wa kuigwa ni mwenye uchungu na nchi na kutaka watu wa heshimu nchi na kuheshimiana kumbe sivyo

sita kuwakosea wanachadema kwa kuamini kuwa wamesimamisha mgombea anaeweza kuuzika baada yule wa WAPUKI(kundi la wavuta bangi la sehemu fulani walipokuwa vijana) lkn matokeo yake ni kiongozi hata bure hanunuliki

kwa kweli huyu ni muhuni tu

Mh! Pesa ya mafisadi at work!
 
Marriage is a contract..and a contract can b valid,void or voidable...contract inakua valid when there is clear consent btwn parties to contract...kwa case hii tuna two parties namely mahimbo and josephine...kwa hiyo kama kuna breach ya condations and warranties then the affected party without a reasonal doubt has a right to sue the other party b4 the court...kwa hiyo mahimbo ana haki ya kufungua kesi na kulingana na ushahidi wa vielelezo na wa kimazingira its 100 per cent Mr.Mahimbo atakua billionaire veri soon...the bottom line ni kua kama Slaa ameweza kudiriki kupora mke pamoja na watoto wa mahimbo just imagine akiwa raisi si atawapora wake wa akina Zitto,Prof Baregu,Mbowe na Mnyika(kama ameoa)....mwisho natabiri Dr.Slaa kuenguliwa katika mbio raisi...let us wait and see

Huyu naye ni great thinker!
 
Niseme nashindwa kuelewa kitu kimoja:

Mwaka 1995, alitumika Angelina Mrema over Augustine Mrema (kama mnakumbuka), ikatumika kumdhoofisha Mrema kwa kila namna iliyowezekana, baada ya uchaguzi hata haikueleweka aliishia wapi huyu!

Mwaka 2005, akatumika Mahita over CUF, tukaaminishwa kuwa CUF ni chama cha kigaidi, wakadai wameleta lori la visu na majambia n.k na watanzania wakaiogopa CUF kabisa! Baada ya uchaguzi hata hatujui hizo silaha ziliishia wapi!

Mwaka huohuo 2005 wakamdhalilisha VIBAYA mwanasiasa ninayemkubali ndani ya CCM, Salim Ahmed Salim na kumwita "Mwarabu" na tena "Muuaji", ikamshushia heshima na akajikuta anaamua kukubali yaishe, baada ya uchaguzi hatukusikia lolote, akabembelezwa kuwa 'makundi yaishe'.

Sasa naona 2010 ni maalum kwa Slaa, maanake nini hii? Ni siasa gani hizi? Nani huwa nyuma ya mikakati hii?
invisible, its a million dollar question... but if you trace carefully na kusoma vi\zuri habari za akina kambona na mzee wetu bhoke munanka, utajua ni propaganda iliyoanzia kwenye ujamaa na nyerere pia alimwagilia vizuri sana maji bustani hii ya propaganda

sasa basi, the only way to stop this is a radical change in our mindset na utajua hata sasa, wapinzani pia hutumia mbinu hizohizo mfano cuf, chadema na TLP ni mbinu hizohizo...

in short aliye nyuma yake ni itikadi tuliyorithi na unfortunately tumebadili mfumo wa democracy but we havent change our mindset
 
Acha upofu wewe au sababu nawe kazi yako ni dungua dungua hutaki kuoa!Chukulia wewe ndio ungevaa viatu vya mahimbo ungejisikiaje katika jamii inayokuzunguka wakati mkeo wa ndoa anatambulishwa hadharani kuwa ni mchumba wa Tandale one?

Kuwa na akili wakati wa kuchangia mada na si kutoa upuuzi kama huo,yaani mtu unampenda mwenzio hata kama kakosea hutaki kumshauri arekebishe makosa!

Inaonyesha ni jinsi gani nyie wa chadema uwezo wenu wa kufikiri mnatumia yaliyomo katika pua na si yale ya kichwani mwenu ujinga!Kweli nimeamini wengi wenu mmepitia shule lakini itakuwa kazi ngumu kuelimika!

Badilikeni na acheni ushabiki wa kishamba huo!

Woooooooooooooooooo nimefurahi sana,kama mimi vile natamani ni inunue,maana huyu jamaa namjua vizuri sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa,kachemka kwelikweli,mtaona sisiemu itakavyo mtosa atakapoanza kushindwa.ushahidi mmoja tu ninao, alimuaga nakumwambia baki na kibaanda chako naenda kwanye nyumba yangu sasa hapo patamu sijui hakumbuki hilo mpaka aseme ameporwa?/
 
Kama watoto wako na Mama na Baba hajui wanakula nini na wanavaa nini nani kashindwa kazi ya malezi hapa. Josephine alitakiwa awe ameshampeleka huyo mwanaume ustawi wa jamii kwa kushindwa kuhudumia watoto

jamani acheni utata,nimewaambia huyu mtu namjua nendeni mkawaulize jirani zake pale baruti,yote mnayodai yamefanyika,hamuoni kuwa Dk yuko fit?na mashaka huyu baba hajui kwa sababu hakutoa ushirikiano.yaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaani ccm hapo ndipo mtakapo ona maharage ni dawa ya usingizi.
 
Back
Top Bottom