Dr. Slaa na CHADEMA ni lazima wamtambue Kikwete. Kama wana manumg'uniko yoyte,hayo manung'uniko yataweza kutanzuliwa kwa urahisi zaidi kama wakimtambua Kikwete. Kikwete amefanya ustaarabu sana. Hakuonyesha hasira wale watu walipotoka nje. Pia akasema labda anaweza kuwapa uwaziri katika Cabinet. Dr. Kikwete ameonyesha subira ambayo ndiyo hallmark ya CCM.
Sasa wanatokea watu wengine katika CCM ambao wanasema wanataka CHADEMA wafukuzwe kutoka kwenye Bunge. Kwa hiyo matatizo ya Uchaguzi badala ya kuisha,sasa ndiyo wanataka yaanze.
Babaji alisema kwamba ukweli ni lile jambo ulilolifikria kwanza kablaya kubadili mawazo yako. The truth is that which you thought first,before you changed your mind. Kwa sababu watu wengi,wakikaa na mtu siku chache tu,wanaanza kusema kwamba wamegundua kwamba huyo mtu ni mnafiki,mzandiki,siyo kama vile walivyofokiri kwanza.
Kama Ndugu Rais amesema kwamba labda atawapa CHADEMA cabinet post,that is the truth,hilo neno lililosemwa kwanza.
Wapo wabunge wengi katika CHADEMA ambao nadhani wanaweza kuchaguliwa kuwa waziri,kama vile Prof. Kulikoyera Kahigi,na wengine .
Kwa hiyo ni bora Ndugu Rais afanye kama alivyosema anaweza kufanya,na Chadema wakubali kutumikia katika Cabinet,kama bado malalamiko ya Uchaguzi,yatatazamwa baadaye.
Haiwezekani CHADEMA waseme kwamba hawamtambui Rais. Kwa sababu,siyo katika Bunge tu,Rais anaongea na wananchi sehemu nyingi sana,na wabunge watatakiwa kuwepo. Wakisusia kila mara Rais anapoongea na wananchi,watakosa sympathy ya wananchi.
Mimi naongea kama mwanachama wa CCM. Kadi yangu ya CCM ni na. AC 23552218 ya Kata ya Msasani,Bonde la Mpunga,na kadi hii haiondoki mfukoni. CCM peke yake ndiyo inayoweza kuwaongoza watu na kuwafanya wawe na moyo thabiti na kuleta maendeleo.