DR Slaa aeleza sababu ya CHADEMA kususa

DR Slaa aeleza sababu ya CHADEMA kususa

UFAFANUZI ZAIDI TOKA KWA DR SLAA
Nadhani message ya Wabunge na ya kwangu iko very clear isipokuwa kwa mtu anayetaka tu kuispin au kuibadilisha kwa sababu anayoitaka mwenyewe. Naomba kurejea mambo ya msingi kwa wale ambao kwa bahati mbaya yamewapita na wana nia ya kuelewa ili spinning hii isiwabughudhi.
Mara baada ya uchaguzi, tarehe 3 November, 2010 Dr. Slaa alifanya Press Conference Makao Makuu ya Chadema kama Mgombea Urais ambaye hakuridhika na mchakato wa uchaguzi na Matokeo yaliyokuwa yakitolewa kupita Vituo vya TV na Jaji Lewis Makame, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Katika Press Conference hiyo Dr. Slaa alitaja dosari nzito katika mchakato wa uchaguzi na hasa katika hatua ya kujumlisha na kutangaza Taifa ambapo matokeo yaliyokuwa yakitangazwa na NEC yalitofautiana kwa kiwango kikubwa sana na yale yaliyotangazwa na Wasimamizi wa Uchaguzi (W) pale ambapo zoezi hilo lilifanyika. Nikatoa Mfano wa Geita. Pili, nilieleza kuwa Katika majimbo takriban 25 zoezi la majumlisho halikufanyika kama inavyotakiwa na sheria na hivyo matokeo kutangazwa na wasimamizi kwa utaratibu kinyume na sheria na kanuni za uchaguzi. Tatu, nilieleza kuwa katika maeneo mengine kama Kinondoni masanduku yapatayo 25 ambayo tunayo namba zake tunazo yalipatikana katika ghala la Shule ya Sekondari ya Biafra Jijini Dar-Es-Salaam ambayo hayajahesabiwa na matokeo yamekwisha kutolewa.Nne, Siku ya tarehe 28 October, Tume ya Taifa ya uchaguzi ilialika Wataalam wa IT wa vyama, na kuwa mbele ya Wataalam hao mfumo wa computer uliokuwa unatumika uli "collapse" na Tume kuwajulisha Wataalam kuwa wataita LapTop zote kutoka nchi nzima zirejeshwe Dar kwa matengenezo ya program husika. Na kuwa wataitwa tena kujulishwa kama zimetengenezwa. Hawakuitwa tena. Hivyo mfumo wa Computer uliotumika kukusanya matokeo na upeleka Taarifa NEC unatia mashaka makubwa. Hata hivyo, baadaye tulipokea Barua kutoka NEC ya tarehe 28/10 ambayo ililetwa kwa Dispatch Makao Makuu Chadema tarehe 5 November, ikisema " Watalaam walikuwa na kukagua mfumo wa IT unaotumika na Tume na waliridhika" . Ni dhahiri barua hii inatia mashaka kwanini barua ya tarehe 8/10 iletwe kwa dispatch na ifike siku takriban 8 baadaye? Hali hii inatia mashaka kuwa barua hii imekuwa backdated kwa Tume kuficha ukweli wa Scandal kubwa iliyotokea katika mfumo ambao uligharimiwa kwa fedha nyingi na UNDP. Iwapo Tume inaweza kudanganya katika swala kama hili tutatukuwa na imani gani na Tume tena. Kutokana na dosari hizo kubwa (pamoja na mambo hayo yaliyojitokeza baadaye) Dr. Slaa, kama Mgombea aliitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi ifanye mambo yafuatayo:
i) Kusimamisha Zoezi la Kutangaza matokeo hadi uchunguzi kamili utakapokuwa umefanyika ili kuondoa hisia na tofauti zilizoanza kujitokeza. Ikumbukwe kuwa Tofauti hizi kimsingi ziligundulika na Wananchi wenyewe kutokana na Tarakimu alizosoma Jaji Makame kutofautiana na zile zilizotangazwa na Wasimamizi katika maeneo yao. Matokeo yake wananchi waliingia mitaani kupinga hali hiyo. Hayo yalitokea Geita, Shinyanga, Mbozi Mashariki na kadhaa. Matokeo yake wananchi hao waliokuwa wanadai haki zao walipigwa mabomu na polisi. Njia ya Busara ilikuwa kuitaka Tume kusitisha zoezi hili ili lisilete athari zaidi, japo hawakufanya hivyo. Chadema tulifanya jitihada za ziada kuwasihi wananchi wetu wasiingie mitaani kuepusha shari.
ii) Kuitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kufuta uchaguzi na kutangaza upya marudio ya uchaguzi kwa kuwa Tofauti zilizoko ni kubwa sana, na nikatoa mfano wa Tarakimu za Geita CCM 17,792 CDM 3,789 ( Iliyotangazwa na RO Geita CCM 30,960 CDM 22,031) Ni wazi kilichotokea hapa ni kuchakachua kwa lengo la kupunguza kabisa kura za Dr. Slaa, japo za JK nazo zimepunguzwa). Jimbo la Hai CCM 35,910 CDM 18,513 (Iliyotangazwa Hai na RO CCM 20,120 CDM 26,724) Uchakachuaji uliofanyika hapa ni wa kumwongezea JK kwa zaidi ya kura 15,000 na kupunguza za Dr. Slaa kwa zaidi ya 8,000). Nilitoa pia mfano wa Ubungo ambapo kwa mujibu wa CCM 68,727 CDM 65,450 (iliyotangazwa na RO CCM 70,472 CDM 72,252) hapa nako uchakachuaji ulioafanyika ni wa kupunguza kura za Dr. Slaa kwa Takriban 8,000 na kupunguza za CCM kwa kama 2000 hivi) Katika Jimbo la Bunda CCM 20,836 CDM 571 (Iliyotangazwa na RO CCM 20,836 CDM 18,445) Tarakimu za Bunda zimerekebishwa katika Taariffa ya mwisho ya NEC. Taarifa hii inaonyesha kuwa Dr. Slaa alipewa kura za Lipumba). Jimbo la Karatu ni kichekesho zaidi kwani kwa mujibu wa Taarifa ya awali ya NEC iliyonukuliwa na Mwananchi CCM 24,364 CDM 41 (iliyotolewa na RO CCM 24,364 CDM 43,137). Taarifa ya mwisho ya NEC imerekebishwa kufanana na ya RO Karatu. Tume ilikiri kuwa imekosea Taarifa ya Geita japo hadi leo haijarekebisha Taarifa hiyo.Hadi leo hii tarehe 19/11 Tume haijatangaza matokeo ya Geita, Tumbe, Tunduru Kaskazini, na Vunjo kwenye Website yake. ( Tume ilikiri siku ya kujumlisha matokeo Taifa kuwa Vunjo kulikuwa na Taarifa mbili na ikaamua kutumia ile ambayo haikusainiwa na mawakala na kutumia ambayo haina saini ya mawakala. Ni akili ya kawaida tu kujua kuwa kuna jambo hapo.
My take

Nimeona hapa jamvini tushirikiane ufafanuzi huo. Hiyo ni mifano dhahiri more will be revealed. Tuwaunge mkono wabunge wote wa chadema na wengine progressive kuwa kuna issue ya uchakachuaji ambayo wanaokataa wajue kuwa wananchi tunajua ipo na mchakato wa kutafutia ufumbuzi NI WA LAZIMA

Habari kamili Marafiki wa chadema - Friends of Chadema
 
Na bado tunaiita tume ya uchaguzi? hata kama si huru isingeweza kufanya ujinga wa namna hii (wa kushindwa 1+2=3) ni aibu kwa nchi na hata (in particular) kwa waliyemtangaza kuwa mshindi wa Urais katika mazingira haya?
 
Utingo, your signature tells the solution! "Being happy doesn't mean that everything is perfect, it mean's you've decided to look beyond the imperfections.."

progress.gif
 
Vilaza wa UDOM watuambie hiyo nayo wanaielewaje?? Wanatuambia wasomi wazima kuwa tuna Form IV failure. Natamani kuomba vipindi hapo ili niwatie adabu vilaza wanao-desa kupata degree.
 
Mimi nasema ili kuikomboa hii nchi ambayo ni tajiri na yenye neema tele watanzania wote tulilie mabadiko ya katiba. Tukiamua inawezekana kabisa mbona dalili zimeshaanza kuonekana kabisa!! Tuwape surport kubwa (MPs) wa CHADEMA ili tuikomboe nchi yetu. Mungu tuongoze katika yote.
 
Vilaza wa UDOM watuambie hiyo nayo wanaielewaje?? Wanatuambia wasomi wazima kuwa tuna Form IV failure. Natamani kuomba vipindi hapo ili niwatie adabu vilaza wanao-desa kupata degree.

Achana na wakurupukaji wale.
Hata kama NEC au mahakama haitotenda haki lakini angalau safari hii wananchi wanajionea uozo uliopo na ni jukumu lao kuamua nini wafanye kwa manufaa ya Taifa lao Tanzania.
 
Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi; those are the major issues now for this country; because kama nchi imeshakuwa na mfumo wa vyama vingi, kwanini katiba ibaki ilivyo? Maana hii katiba suits mfumo wa chama kimoja; wewe is justice? Hili lisipuuzwe maana ni crucial kwa wote wenye mapenzi mema na hii nchi.
 
  • Ina maana tume bado inahesabu kura za hayo majimbo kwani vipi?
  • Inabidi tumtafute makame atueleze hizo kura zilikuwaje?
  • Au ataongeza kama za Mrema Lyatonga?
  • Kama iko hivi basi vyombo vya habari havijafanya kazi kusaidia nchi hii
 
UFAFANUZI ZAIDI TOKA KWA DR SLAA
Nadhani message ya Wabunge na ya kwangu iko very clear isipokuwa kwa mtu anayetaka tu kuispin au kuibadilisha kwa sababu anayoitaka mwenyewe. Naomba kurejea mambo ya msingi kwa wale ambao kwa bahati mbaya yamewapita na wana nia ya kuelewa ili spinning hii isiwabughudhi.
Mara baada ya uchaguzi, tarehe 3 November, 2010 Dr. Slaa alifanya Press Conference Makao Makuu ya Chadema kama Mgombea Urais ambaye hakuridhika na mchakato wa uchaguzi na Matokeo yaliyokuwa yakitolewa kupita Vituo vya TV na Jaji Lewis Makame, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Katika Press Conference hiyo Dr. Slaa alitaja dosari nzito katika mchakato wa uchaguzi na hasa katika hatua ya kujumlisha na kutangaza Taifa ambapo matokeo yaliyokuwa yakitangazwa na NEC yalitofautiana kwa kiwango kikubwa sana na yale yaliyotangazwa na Wasimamizi wa Uchaguzi (W) pale ambapo zoezi hilo lilifanyika. Nikatoa Mfano wa Geita. Pili, nilieleza kuwa Katika majimbo takriban 25 zoezi la majumlisho halikufanyika kama inavyotakiwa na sheria na hivyo matokeo kutangazwa na wasimamizi kwa utaratibu kinyume na sheria na kanuni za uchaguzi. Tatu, nilieleza kuwa katika maeneo mengine kama Kinondoni masanduku yapatayo 25 ambayo tunayo namba zake tunazo yalipatikana katika ghala la Shule ya Sekondari ya Biafra Jijini Dar-Es-Salaam ambayo hayajahesabiwa na matokeo yamekwisha kutolewa.Nne, Siku ya tarehe 28 October, Tume ya Taifa ya uchaguzi ilialika Wataalam wa IT wa vyama, na kuwa mbele ya Wataalam hao mfumo wa computer uliokuwa unatumika uli "collapse" na Tume kuwajulisha Wataalam kuwa wataita LapTop zote kutoka nchi nzima zirejeshwe Dar kwa matengenezo ya program husika. Na kuwa wataitwa tena kujulishwa kama zimetengenezwa. Hawakuitwa tena. Hivyo mfumo wa Computer uliotumika kukusanya matokeo na upeleka Taarifa NEC unatia mashaka makubwa. Hata hivyo, baadaye tulipokea Barua kutoka NEC ya tarehe 28/10 ambayo ililetwa kwa Dispatch Makao Makuu Chadema tarehe 5 November, ikisema " Watalaam walikuwa na kukagua mfumo wa IT unaotumika na Tume na waliridhika" . Ni dhahiri barua hii inatia mashaka kwanini barua ya tarehe 8/10 iletwe kwa dispatch na ifike siku takriban 8 baadaye? Hali hii inatia mashaka kuwa barua hii imekuwa backdated kwa Tume kuficha ukweli wa Scandal kubwa iliyotokea katika mfumo ambao uligharimiwa kwa fedha nyingi na UNDP. Iwapo Tume inaweza kudanganya katika swala kama hili tutatukuwa na imani gani na Tume tena. Kutokana na dosari hizo kubwa (pamoja na mambo hayo yaliyojitokeza baadaye) Dr. Slaa, kama Mgombea aliitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi ifanye mambo yafuatayo:
i) Kusimamisha Zoezi la Kutangaza matokeo hadi uchunguzi kamili utakapokuwa umefanyika ili kuondoa hisia na tofauti zilizoanza kujitokeza. Ikumbukwe kuwa Tofauti hizi kimsingi ziligundulika na Wananchi wenyewe kutokana na Tarakimu alizosoma Jaji Makame kutofautiana na zile zilizotangazwa na Wasimamizi katika maeneo yao. Matokeo yake wananchi waliingia mitaani kupinga hali hiyo. Hayo yalitokea Geita, Shinyanga, Mbozi Mashariki na kadhaa. Matokeo yake wananchi hao waliokuwa wanadai haki zao walipigwa mabomu na polisi. Njia ya Busara ilikuwa kuitaka Tume kusitisha zoezi hili ili lisilete athari zaidi, japo hawakufanya hivyo. Chadema tulifanya jitihada za ziada kuwasihi wananchi wetu wasiingie mitaani kuepusha shari.
ii) Kuitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kufuta uchaguzi na kutangaza upya marudio ya uchaguzi kwa kuwa Tofauti zilizoko ni kubwa sana, na nikatoa mfano wa Tarakimu za Geita CCM 17,792 CDM 3,789 ( Iliyotangazwa na RO Geita CCM 30,960 CDM 22,031) Ni wazi kilichotokea hapa ni kuchakachua kwa lengo la kupunguza kabisa kura za Dr. Slaa, japo za JK nazo zimepunguzwa). Jimbo la Hai CCM 35,910 CDM 18,513 (Iliyotangazwa Hai na RO CCM 20,120 CDM 26,724) Uchakachuaji uliofanyika hapa ni wa kumwongezea JK kwa zaidi ya kura 15,000 na kupunguza za Dr. Slaa kwa zaidi ya 8,000). Nilitoa pia mfano wa Ubungo ambapo kwa mujibu wa CCM 68,727 CDM 65,450 (iliyotangazwa na RO CCM 70,472 CDM 72,252) hapa nako uchakachuaji ulioafanyika ni wa kupunguza kura za Dr. Slaa kwa Takriban 8,000 na kupunguza za CCM kwa kama 2000 hivi) Katika Jimbo la Bunda CCM 20,836 CDM 571 (Iliyotangazwa na RO CCM 20,836 CDM 18,445) Tarakimu za Bunda zimerekebishwa katika Taariffa ya mwisho ya NEC. Taarifa hii inaonyesha kuwa Dr. Slaa alipewa kura za Lipumba). Jimbo la Karatu ni kichekesho zaidi kwani kwa mujibu wa Taarifa ya awali ya NEC iliyonukuliwa na Mwananchi CCM 24,364 CDM 41 (iliyotolewa na RO CCM 24,364 CDM 43,137). Taarifa ya mwisho ya NEC imerekebishwa kufanana na ya RO Karatu. Tume ilikiri kuwa imekosea Taarifa ya Geita japo hadi leo haijarekebisha Taarifa hiyo.Hadi leo hii tarehe 19/11 Tume haijatangaza matokeo ya Geita, Tumbe, Tunduru Kaskazini, na Vunjo kwenye Website yake. ( Tume ilikiri siku ya kujumlisha matokeo Taifa kuwa Vunjo kulikuwa na Taarifa mbili na ikaamua kutumia ile ambayo haikusainiwa na mawakala na kutumia ambayo haina saini ya mawakala. Ni akili ya kawaida tu kujua kuwa kuna jambo hapo.
My take

Nimeona hapa jamvini tushirikiane ufafanuzi huo. Hiyo ni mifano dhahiri more will be revealed. Tuwaunge mkono wabunge wote wa chadema na wengine progressive kuwa kuna issue ya uchakachuaji ambayo wanaokataa wajue kuwa wananchi tunajua ipo na mchakato wa kutafutia ufumbuzi NI WA LAZIMA

Habari kamili Marafiki wa chadema - Friends of Chadema

Jamani nchi hii kuna mambo! Wanaojiita wasomi wakati wana hold vyeti vya kidato cha sita pekee (Wengi kama sio wote watakuwa undergraduate) hawajaliona hili?
 
Madai kama haya lazima tumeitoe ufafanuzi makini sana ndio chadema walisema kuwa kuna ulazima wa tume huru ya uchaguzi, Mungu saidia CHADEMA
 
Hii ni move nzuri sana hatuwezi kuendelea na mambo kama haya ya ajabu kama hivi
 
Chiligati ni sawa na Makamba, wanatumia vinywa vyao kufikiri badala ya akili.Wazo la kutaka kuwazuia wabunge wa Chadema kurudi bungeni ni wazo la kijinga kuliko yote niliyowahi kusikia msimu huu. Uhalifu uliofanywa na CCM kwa kushirikisha vyombo vyake viovu kama NEC,TISS,POLISI,JWTZ wa kuiba kura na kumtangaza mtu aliyekataliwa na watanzania kuwa ndiye mshindi wa kiti cha urais ulitosha kabisa kuilipua nchi hii na kuleta machafuko makubwa kama siyo busara za Dr Slaa kuwatuliza wafuasi na wale wote waliompigia kura. Kwa vile Katiba katika ibara ya 41-(7) inatoa kinga kwa uchakachuaji wa kura za rais, Chadema hawakuwa na njia nyingine ya kuelezea kilio chao zaidi ya njia za kisiasa kama walivyofanya bungeni. Njia waliyotumia Chadema ni ya kistaarabu mno ambayo haiwezi kusababisha uvunjifu wa amani kama wanavyotabiri kina Chiligati, lakini njia wanayotaka kutumia CCM ndiyo itakayoleta vurugu kwani watanzania uvumivu wetu umefika mwisho, tumepoteza muda wetu kushiriki zoezi la upigaji kura na kura zikachezewa na tukakubali kuwa wapole, sasa kiendo cha kuwaondoa wabunge wetu kwa hila za ubabe wa wingi wa wabunge wa CCM na mapandikizi yao hakikubaliki kwa viwango vyovyote vile . Na CCM eleweni kuwa wafuasi wa Chadema ni wengi kuliko wa CCM,CUF,NCCR,TLP&UDP, kama mnabisha jaribuni huo mpango wenu dhalimu muone, au mnafikiri hao polisi na jwtz mnaotegemea kuwatumia kutuua ni marobot hawana roho. Kwa yote yatakayotokea baada ya hapo lawama kwenu viongozi wa CCM.
 
Ni nzuri ila mkuu hii ilishaletwa hapa tango jana. Mods ziunganisheni hizi!

Kila mtu anataka kuanzisha thread yake hata kama tayari imeshaanzishwa hii inatokana na kutoelewa mambo.....
 
Ok,si mbaya kwani ndio mda wao huu,ila wajue kila jambo lina mwanzo na mwisho wake ipo siku tu hizi ajizi za kupeana madalaka zitakwisha

mapinduziii daimaaaaaa
 
Wabunge wa Chadema hatukuwatuma kwenda kufanya malumbano na Serikali bungeni.

Tuliwatuma kwenda kufanya kazi na Serikali ili kutuletea maendeleo majimboni mwetu.

Sisi wapiga kura hatuna muda wa kupoteza, tunashangaa wanapata wapi muda wa kuchezea badala ya kutimiza tuliyowatuma.

Usanii huu unaonyesha kuwa hawajakomaa kisiasa tofauti na tulivyowaona wakati wanatuomba kura.

Majibu ya mnayoyafanya mtayapata 2015.

Kumbe tulifanya makosa.
Kosa ulifanya wewe peke yako na ccm wenzako. Chadema endeleeni mbele kazi nzuri.
 
Habari ni nzuri sana. Na ni kama wengine wote watakavyokuwa wamehisi kukasirishwa na Prof. Wamba. Nimekosa la kusema ila siyo kwamba limekosekana bali litatoka neno baya tuu.... kwahiyo. Mungu ibariki Tanzania ni bora zidi!
 
Hivi hii nchi inamarais wangapi?

Swali tamu na fikirishi---ukitazama kwa nini EPA imeshindikana kushughulikiwa na kwa nini Richmond imepigwa danadana na kwa nini Sitta ameangushwa unaweza kupata njia ya kuelekea jibu.
 
Wabunge wetu wamechukua uamuzi mgumu sana, uamuzi ambao unataka ujasiri na uthubutu wa vitendo. Ni lazima tuelewe kuwa mgogoro uliopo siyo na Kikwete kama Kikwete, la hasha bali na mfumo uliomuingiza madarakani safari hii, mfumo ambao tunautuhumu kuwa haukuwa huru na wa haki. Uamuzi huu haukuwa wa chuki binafsi au kisirani dhidi ya Kikwete kama Kikwete, bali dhidi ya mfumo ulioundwa na kulelewa na CCM na ambao umetuonesha kuwa hauwezi na haupaswi kulelewa kwa muda mwingine wowote ujao.

Kuanzia wakati wa kutangaza matokeo tulitoa malalamiko yetu kwa Tume ya Uchaguzi ili waweze kuyafanyia kazi ili mshindi apatikane katika mazingira ya haki na uwazi. Tume haikusikiliza na ikaendelea na mfumo wake mbovu wa kutangaza matokeo bila kujali malalamiko yetu. Tukazungumza hadharani juu ya kutopatana kwa matokeo ya uchaguzi yanayotangazwa na tume na yale yaliyoko majimboni na kuomba tume wasitishe ili waangalie ushahidi tulio nao, tume haikusikiliza na matokeo yake wakamtangaza Kikwete kuwa Rais licha ya kwamba matokeo majimboni yalikuwa yanaashiria vinginevyo.

Ni muhimu kutambua kuwa ni rahisi kukubali matokeo ya Ubunge kwa sababu yanarasimishwa majimboni na yanaweza kupingwa mahakamani. Katika urais kimsingi ukiangalia Katiba utaona kuwa haijalishi nani kashinda kwenye kura, bali nani katangazwa mshindi. Tunachotuhumu sisi ni kuwa matokeo ya Uchaguzi yangetangazwa kama ilivyoahidiwa na Tume mwezi Machi yangeonesha wazi mshindi ni tofauti na yule aliyetangazwa. Lakini wao tume wakijua kuwa mara wakishatangaza hakuna mahakama inayoweza kuhoji wakafanya hila na haraka ya kutangaza matokeo ya Urais kwa kumtangaza Kikwete kuwa ni Rais.

Kama toka siku ya kwanza tulitoa malalamiko na zikapita siku tano bila kujibiwa wala kusikilizwa na baadaye tunatakiwa tukubali tu kwa vile "keshatangazwa" katika dhamira safi tunaweza vipi kufanya hivyo? Ugomvi wetu wa kisiasa (na siyo chuki wala uhasama binafsi) hauko zaidi na Kikwete bali natume iliyomtangaza. Na kwa vile yeye mwenyewe haoni matatizo katika tume au mfumo wetu wa uchaguzi tunaona kuwa aidha alitoa baraka zake au alikubali kunufaishwa na mfumo huo mbovu.

Hivyo, wabunge wetu kutoka nje ni kutuma ishara mbili: Kwanza, tunapinga mfumo wa kichakachuaji wa tume ya Uchaguzi uliomtangaza Kikwete kuwa Rais, na pili kwa vile Tume imeshindwa kutuonesha uwazi wa ushindi wa Kikwete tunashindwa kukubali kama ni mshindi halali. Ni mpaka pale uchunguzi huru wa kura utakapoonesha kuwa Kikwete kashinda kihalali ndipo tutakuwa tayari kumtambua ukiondoa uwezekano mwingine wa kuelewana.

Tukumbuke kuwa, kama uchaguzi huu ungeendeshwa katika hali ya uwazi, haki na ufanisi tusingefika hapa. CHADEMA siyo wa kulaumiwa katika hili wala wabunge wetu wasibebeshwe mzigo kwa hili; watu waliotufikisha hapa ni Serikali ya CCM na vyombo vyake ikiwemo Tume ya Uchaguzi. Wangeonesha weledi na kutokupendelea kwa wazi tusingefikia mahali pa kutulazimisha kuchukua hatua hizi ambazo kwa kila kipimo ni za wastani sana ukilinganisha na hatua ambazo tungeweza kuzichukua.

Nawasihi tuwaunge mkono wabunge wetu na uongozi wetu kwa kuwatia moyo kwani uamuzi waliouchukua ni uamuzi wa kijasiri lakini ulioweka historia katika Tanzania kuwa hatuwezi tena kusukumwa na kuburuzwa kwa kutumia nguvu ya taasisi au cheo cha mtu. Tuwatie shime na tusimame nao katika wakati huu wa kihistoria.

Pamoja tunaweza, mpaka kieleweke!

from: - Habari

Asante kwa maelezo hayo juu. Nionavyo mimi CHADEMA wangekuwa na press conference kuelezea namna kura zilivyochakachuliwa. So far, hakujawa na taarifa kamili juu ya nini kilichotokea baada ya uchaguzi. Hivyo wananchi wanashangaa mbona wabunge wanasusia kikao bila sababu? Wananchi wanahitaji kuelewa ni nini tume ilichokifanya mpaka CHADEMA wasusie. Nafikiri kama ni ushahidi utakuwa umeshakamilika. Tunaomba Dr.Slaa ajitokeze na kuelezea umma ili wananchi waelewe ni nini kilichotokea.
 
Back
Top Bottom