PPM
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 838
- 230
Upuuzi mtupu!
Kwa Nchi zinazojua haki zao, watu kama wewe Dar es Salaam ni wakunyongela mbali, haufai kwenye jamii ya Demokrasia
Upuuzi mtupu!
Katiba mpya hailetwi kwa CHADEMA kutoka Bungeni , na hilo lililofanyika la kumkataa RAIS wataalamu wote wa mambo ya siasa wanasema halina athari yoyote kwani Rais na Serikali yake wataendelea na wajibu wao kama kawaida. Nyie Mkisusa wenzenu wala na mwisho wa yote mtarudi kwa huyo huyo JK ili mambo yenu yatengemae.
chaka chua matokeo=ccmchukua chako mapema!, chama cha majambazi!, chama cha majangili!, chama cha majizi!,.........
Eu: Kwa nini tz masikini????????????????????
Kiwete: Hata mimi sijui kwa nini tz masikini!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
upuuzi mtupu!
Huu siyo upuuzi tu bali pia ni UJINGA mtupu. Wako baadhi ya watu ndani ya CHADEMA ambao wana mwelekeo wa uhaini. Wabunge wa CHADEMA kususia hotuba ya JK ni kielelezo cha upungufu na ufinyu wa mawazo na fikra na pia kukosa heshima kwa RAIS na jamii nzima. Wanachojaribu kufanya CHADEMA ni kuchochea uasi dhidi ya RAIS na mamlaka. Wanataka ionekane kuwa Tanzania haitawaliki. CHADEMA wamekosea mno. It is a political blunder. It is the beggining of CHADEMA's demise. Definetly watanzania walio wengi hawawezi kukubaliana na upuuzi wa CHADEMA. Come 2015 CHADEMA will never get more than five seats in the parliament. Unasusia hotuba wakati unatembelea gari la serikali ya JK, unapata posho inayotolewa na serikali ya JK; unapiga kura kwa jina la Waziri Mkuu lililoteuliwa na JK. ama huu siyo upuuzi na ujinga ni nini basi?
eti upuuzi mtupu..mkwere jasho la pua lilimtoka jana....hatakaa asahau aibu aliyoipata jana kukataliwa live mbele ya wageni waalikwa na mabalozi..hahaaaaa shame on you JK..na bado
Acha uwongo kwani hiyo Posho na hayo magari JK anatoa mfukoni kwake?? si ni kodi za watanzania ambao wengine ndio hao walioamua kutoka nje na kuwakilisha mawazo ya wale wale waliowachagua
On this one CHADEMA is completely wrong take it or leave it.In the process they discredit themselves from the public eyes, whoever doesn't believe me wait till 2015. The sits won on parliament was a good success for CHADEMA but now with this move any wise man will tell you that is a wrong move!!
Katiba mpya hailetwi kwa CHADEMA kutoka Bungeni , na hilo lililofanyika la kumkataa RAIS wataalamu wote wa mambo ya siasa wanasema halina athari yoyote kwani Rais na Serikali yake wataendelea na wajibu wao kama kawaida. Nyie Mkisusa wenzenu wala na mwisho wa yote mtarudi kwa huyo huyo JK ili mambo yenu yatengemae.
King Kingo achana na huyo 1954 hana maana angalia post zake zote, ina harufu ya utumwa wa fikra, ufupi wa mawazo na ukosefu wa busara:whoo:
Safi sana,ni mwanzo mzuri tuendelee kufichua wizi wote hata wafadhili wajue wasiendelee kuwapa wezi misaada.Wabunge wetu wamechukua uamuzi mgumu sana, uamuzi ambao unataka ujasiri na uthubutu wa vitendo. Ni lazima tuelewe kuwa mgogoro uliopo siyo na Kikwete kama Kikwete, la hasha bali na mfumo uliomuingiza madarakani safari hii, mfumo ambao tunautuhumu kuwa haukuwa huru na wa haki. Uamuzi huu haukuwa wa chuki binafsi au kisirani dhidi ya Kikwete kama Kikwete, bali dhidi ya mfumo ulioundwa na kulelewa na CCM na ambao umetuonesha kuwa hauwezi na haupaswi kulelewa kwa muda mwingine wowote ujao.
Kuanzia wakati wa kutangaza matokeo tulitoa malalamiko yetu kwa Tume ya Uchaguzi ili waweze kuyafanyia kazi ili mshindi apatikane katika mazingira ya haki na uwazi. Tume haikusikiliza na ikaendelea na mfumo wake mbovu wa kutangaza matokeo bila kujali malalamiko yetu. Tukazungumza hadharani juu ya kutopatana kwa matokeo ya uchaguzi yanayotangazwa na tume na yale yaliyoko majimboni na kuomba tume wasitishe ili waangalie ushahidi tulio nao, tume haikusikiliza na matokeo yake wakamtangaza Kikwete kuwa Rais licha ya kwamba matokeo majimboni yalikuwa yanaashiria vinginevyo.
Ni muhimu kutambua kuwa ni rahisi kukubali matokeo ya Ubunge kwa sababu yanarasimishwa majimboni na yanaweza kupingwa mahakamani. Katika urais kimsingi ukiangalia Katiba utaona kuwa haijalishi nani kashinda kwenye kura, bali nani katangazwa mshindi. Tunachotuhumu sisi ni kuwa matokeo ya Uchaguzi yangetangazwa kama ilivyoahidiwa na Tume mwezi Machi yangeonesha wazi mshindi ni tofauti na yule aliyetangazwa. Lakini wao tume wakijua kuwa mara wakishatangaza hakuna mahakama inayoweza kuhoji wakafanya hila na haraka ya kutangaza matokeo ya Urais kwa kumtangaza Kikwete kuwa ni Rais.
Kama toka siku ya kwanza tulitoa malalamiko na zikapita siku tano bila kujibiwa wala kusikilizwa na baadaye tunatakiwa tukubali tu kwa vile "keshatangazwa" katika dhamira safi tunaweza vipi kufanya hivyo? Ugomvi wetu wa kisiasa (na siyo chuki wala uhasama binafsi) hauko zaidi na Kikwete bali natume iliyomtangaza. Na kwa vile yeye mwenyewe haoni matatizo katika tume au mfumo wetu wa uchaguzi tunaona kuwa aidha alitoa baraka zake au alikubali kunufaishwa na mfumo huo mbovu.
Hivyo, wabunge wetu kutoka nje ni kutuma ishara mbili: Kwanza, tunapinga mfumo wa kichakachuaji wa tume ya Uchaguzi uliomtangaza Kikwete kuwa Rais, na pili kwa vile Tume imeshindwa kutuonesha uwazi wa ushindi wa Kikwete tunashindwa kukubali kama ni mshindi halali. Ni mpaka pale uchunguzi huru wa kura utakapoonesha kuwa Kikwete kashinda kihalali ndipo tutakuwa tayari kumtambua ukiondoa uwezekano mwingine wa kuelewana.
Tukumbuke kuwa, kama uchaguzi huu ungeendeshwa katika hali ya uwazi, haki na ufanisi tusingefika hapa. CHADEMA siyo wa kulaumiwa katika hili wala wabunge wetu wasibebeshwe mzigo kwa hili; watu waliotufikisha hapa ni Serikali ya CCM na vyombo vyake ikiwemo Tume ya Uchaguzi. Wangeonesha weledi na kutokupendelea kwa wazi tusingefikia mahali pa kutulazimisha kuchukua hatua hizi ambazo kwa kila kipimo ni za wastani sana ukilinganisha na hatua ambazo tungeweza kuzichukua.
Nawasihi tuwaunge mkono wabunge wetu na uongozi wetu kwa kuwatia moyo kwani uamuzi waliouchukua ni uamuzi wa kijasiri lakini ulioweka historia katika Tanzania kuwa hatuwezi tena kusukumwa na kuburuzwa kwa kutumia nguvu ya taasisi au cheo cha mtu. Tuwatie shime na tusimame nao katika wakati huu wa kihistoria.
Pamoja tunaweza, mpaka kieleweke!
from: - Habari
Harufu ya utumwa!!!!!!!! Kuna wakuja maeneo ya mkoa wa Tabora wana nguvu hadi leo kuwaweka Waafrika utumwani!!! -- kwa mlo wa siku moja tu! Sisemi zaidi.
Asiyejua kusoma ataishia kuzungumza na simu tu....! Kamwe hasomi wala kutuma message, na akituma basi huenda akatuma a wrong message, au to the wrong destination kama wewe....! CCM wana mtandao wao, kwanini usipeleke huko? Na, message iliyotumwa na CHADEMA kwa umma wataisoma waelwa tu, wenye akili, busara. Lakinia vipofu kama wewe kamwe hawatapata ujumbe huo na maana yake....! Ingeweza kutafsiriwa kama ulivyo wewe katika karne ya 18, lakini sio sasa....! Hii inaonesha ni jinsi gani ulivyofungwa vifungo vya ubongo wa kuchambua mbichi na mbivu....! Aidha, sikulaumu, maana katika kila jamii watu kama wewe lazima watakuwepo, hata hivyo, ndio maana wazungu walisema; "many people are alive only because it is illegal to shoot them".On this one CHADEMA is completely wrong take it or leave it.In the process they discredit themselves from the public eyes, whoever doesn't believe me wait till 2015. The sits won on parliament was a good success for CHADEMA but now with this move any wise man will tell you that is a wrong move!!
Nakuunga nkono kabisa Mama Salma!!Upuuzi mtupu!
inawezekana we do wale ambao ilimladi pamkucha(mbumbu wa kufikari) au ni miongoni wale wanaofaidika na hao majizi. tusikubali watu jama hawa ndani jfUpuuzi mtupu!