DR Slaa aeleza sababu ya CHADEMA kususa

Vumbi

Senior Member
Nov 7, 2010
191
27
Wabunge wetu wamechukua uamuzi mgumu sana, uamuzi ambao unataka ujasiri na uthubutu wa vitendo. Ni lazima tuelewe kuwa mgogoro uliopo siyo na Kikwete kama Kikwete, la hasha bali na mfumo uliomuingiza madarakani safari hii, mfumo ambao tunautuhumu kuwa haukuwa huru na wa haki. Uamuzi huu haukuwa wa chuki binafsi au kisirani dhidi ya Kikwete kama Kikwete, bali dhidi ya mfumo ulioundwa na kulelewa na CCM na ambao umetuonesha kuwa hauwezi na haupaswi kulelewa kwa muda mwingine wowote ujao.

Kuanzia wakati wa kutangaza matokeo tulitoa malalamiko yetu kwa Tume ya Uchaguzi ili waweze kuyafanyia kazi ili mshindi apatikane katika mazingira ya haki na uwazi. Tume haikusikiliza na ikaendelea na mfumo wake mbovu wa kutangaza matokeo bila kujali malalamiko yetu. Tukazungumza hadharani juu ya kutopatana kwa matokeo ya uchaguzi yanayotangazwa na tume na yale yaliyoko majimboni na kuomba tume wasitishe ili waangalie ushahidi tulio nao, tume haikusikiliza na matokeo yake wakamtangaza Kikwete kuwa Rais licha ya kwamba matokeo majimboni yalikuwa yanaashiria vinginevyo.

Ni muhimu kutambua kuwa ni rahisi kukubali matokeo ya Ubunge kwa sababu yanarasimishwa majimboni na yanaweza kupingwa mahakamani. Katika urais kimsingi ukiangalia Katiba utaona kuwa haijalishi nani kashinda kwenye kura, bali nani katangazwa mshindi. Tunachotuhumu sisi ni kuwa matokeo ya Uchaguzi yangetangazwa kama ilivyoahidiwa na Tume mwezi Machi yangeonesha wazi mshindi ni tofauti na yule aliyetangazwa. Lakini wao tume wakijua kuwa mara wakishatangaza hakuna mahakama inayoweza kuhoji wakafanya hila na haraka ya kutangaza matokeo ya Urais kwa kumtangaza Kikwete kuwa ni Rais.

Kama toka siku ya kwanza tulitoa malalamiko na zikapita siku tano bila kujibiwa wala kusikilizwa na baadaye tunatakiwa tukubali tu kwa vile "keshatangazwa" katika dhamira safi tunaweza vipi kufanya hivyo? Ugomvi wetu wa kisiasa (na siyo chuki wala uhasama binafsi) hauko zaidi na Kikwete bali natume iliyomtangaza. Na kwa vile yeye mwenyewe haoni matatizo katika tume au mfumo wetu wa uchaguzi tunaona kuwa aidha alitoa baraka zake au alikubali kunufaishwa na mfumo huo mbovu.

Hivyo, wabunge wetu kutoka nje ni kutuma ishara mbili: Kwanza, tunapinga mfumo wa kichakachuaji wa tume ya Uchaguzi uliomtangaza Kikwete kuwa Rais, na pili kwa vile Tume imeshindwa kutuonesha uwazi wa ushindi wa Kikwete tunashindwa kukubali kama ni mshindi halali. Ni mpaka pale uchunguzi huru wa kura utakapoonesha kuwa Kikwete kashinda kihalali ndipo tutakuwa tayari kumtambua ukiondoa uwezekano mwingine wa kuelewana.

Tukumbuke kuwa, kama uchaguzi huu ungeendeshwa katika hali ya uwazi, haki na ufanisi tusingefika hapa. CHADEMA siyo wa kulaumiwa katika hili wala wabunge wetu wasibebeshwe mzigo kwa hili; watu waliotufikisha hapa ni Serikali ya CCM na vyombo vyake ikiwemo Tume ya Uchaguzi. Wangeonesha weledi na kutokupendelea kwa wazi tusingefikia mahali pa kutulazimisha kuchukua hatua hizi ambazo kwa kila kipimo ni za wastani sana ukilinganisha na hatua ambazo tungeweza kuzichukua.

Nawasihi tuwaunge mkono wabunge wetu na uongozi wetu kwa kuwatia moyo kwani uamuzi waliouchukua ni uamuzi wa kijasiri lakini ulioweka historia katika Tanzania kuwa hatuwezi tena kusukumwa na kuburuzwa kwa kutumia nguvu ya taasisi au cheo cha mtu. Tuwatie shime na tusimame nao katika wakati huu wa kihistoria.

Pamoja tunaweza, mpaka kieleweke!

from: - Habari
 
Wabunge wetu wamechukua uamuzi mgumu sana, uamuzi ambao unataka ujasiri na uthubutu wa vitendo. Ni lazima tuelewe kuwa mgogoro uliopo siyo na Kikwete kama Kikwete, la hasha bali na mfumo uliomuingiza madarakani safari hii, mfumo ambao tunautuhumu kuwa haukuwa huru na wa haki. ?Uamuzi huu haukuwa wa chuki binafsi au kisirani dhidi ya Kikwete kama Kikwete, bali dhidi ya mfumo ulioundwa na kulelewa na CCM na ambao umetuonesha kuwa hauwezi na haupaswi kulelewa kwa muda mwingine wowote ujao.

Kuanzia wakati wa kutangaza matokeo tulitoa malalamiko yetu kwa Tume ya Uchaguzi ili waweze kuyafanyia kazi ili mshindi apatikane katika mazingira ya haki na uwazi. Tume haikusikiliza na ikaendelea na mfumo wake mbovu wa kutangaza matokeo bila kujali malalamiko yetu. Tukazungumza hadharani juu ya kutopatana kwa matokeo ya uchaguzi yanayotangazwa na tume na yale yaliyoko majimboni na kuomba tume wasitishe ili waangalie ushahidi tulio nao, tume haikusikiliza na matokeo yake wakamtangaza Kikwete kuwa Rais licha ya kwamba matokeo majimboni yalikuwa yanaashiria vinginevyo.

Ni muhimu kutambua kuwa ni rahisi kukubali matokeo ya Ubunge kwa sababu yanarasimishwa majimboni na yanaweza kupingwa mahakamani. Katika urais kimsingi ukiangalia Katiba utaona kuwa haijalishi nani kashinda kwenye kura, bali nani katangazwa mshindi. Tunachotuhumu sisi ni kuwa matokeo ya Uchaguzi yangetangazwa kama ilivyoahidiwa na Tume mwezi Machi yangeonesha wazi mshindi ni tofauti na yule aliyetangazwa. Lakini wao tume wakijua kuwa mara wakishatangaza hakuna mahakama inayoweza kuhoji wakafanya hila na haraka ya kutangaza matokeo ya Urais kwa kumtangaza Kikwete kuwa ni Rais.

Kama toka siku ya kwanza tulitoa malalamiko na zikapita siku tano bila kujibiwa wala kusikilizwa na baadaye tunatakiwa tukubali tu kwa vile "keshatangazwa" katika dhamira safi tunaweza vipi kufanya hivyo? Ugomvi wetu wa kisiasa (na siyo chuki wala uhasama binafsi) hauko zaidi na Kikwete bali natume iliyomtangaza. Na kwa vile yeye mwenyewe haoni matatizo katika tume au mfumo wetu wa uchaguzi tunaona kuwa aidha alitoa baraka zake au alikubali kunufaishwa na mfumo huo mbovu.

Hivyo, wabunge wetu kutoka nje ni kutuma ishara mbili: Kwanza, tunapinga mfumo wa kichakachuaji wa tume ya Uchaguzi uliomtangaza Kikwete kuwa Rais, na pili kwa vile Tume imeshindwa kutuonesha uwazi wa ushindi wa Kikwete tunashindwa kukubali kama ni mshindi halali. Ni mpaka pale uchunguzi huru wa kura utakapoonesha kuwa Kikwete kashinda kihalali ndipo tutakuwa tayari kumtambua ukiondoa uwezekano mwingine wa kuelewana.

Tukumbuke kuwa, kama uchaguzi huu ungeendeshwa katika hali ya uwazi, haki na ufanisi tusingefika hapa. CHADEMA siyo wa kulaumiwa katika hili wala wabunge wetu wasibebeshwe mzigo kwa hili; watu waliotufikisha hapa ni Serikali ya CCM na vyombo vyake ikiwemo Tume ya Uchaguzi. Wangeonesha weledi na kutokupendelea kwa wazi tusingefikia mahali pa kutulazimisha kuchukua hatua hizi ambazo kwa kila kipimo ni za wastani sana ukilinganisha na hatua ambazo tungeweza kuzichukua.

Nawasihi tuwaunge mkono wabunge wetu na uongozi wetu kwa kuwatia moyo kwani uamuzi waliouchukua ni uamuzi wa kijasiri lakini ulioweka historia katika Tanzania kuwa hatuwezi tena kusukumwa na kuburuzwa kwa kutumia nguvu ya taasisi au cheo cha mtu. Tuwatie shime na tusimame nao katika wakati huu wa kihistoria.

Pamoja tunaweza, mpaka kieleweke!

from: - Habari

Upuuzi mtupu!
 
That's a plus for any smart Party, its quite clear that they wanted this message out there their voice to be heard in a prime time of full coverage and free. Some could have done demonstration which always got a long process and permission or they could have done through media/TV'S stations but also means money with a very short coverage with power cut risk.
By comparison this was the only window to send the message of Free election committee and New constitution
 
Upuuzi mtupu!

Nakubaliana na wewe ni upuuzi mtupu kumtakasa Kikwete wakati hatakasiki, amehusika moja kwa moja katika kuiagiza NEC ambayo iliwapora wananchi kura zao. NEC aliyoituma Kikwete ikapiga kura badala ya wananchi. Sijui kwa nini upuuzi kama huu unaletwa hapa
 
Mwanzo nzuri. Haki haipatikani kirahisi lazima kupambana. Mi nashukuru njia iliyotumika ni nzuri kuliko mngeingia mtaani na kuwashawishi watu kuandamana na kupigana. Pambaneni hata uhuru na haki za nchi nyingi zilipatikana kwa shida sana. Kweli katiba ya nchi inahitaji mabadiliko na hilo liko wazi lakini kwa vile hoja ni ya wapinzani basi hilo siyo muhimu kwa serikali.

"Resources in Tanzania is not a problem but institutions which are in place need to be amended for development" Some of us ask why are we poor while we have blessed with plenty of resources from GOD?

Tanzania inahitaji mabadiliko (siyo lazima kubadili chama) ila mifumo na taratibu zilizopo.
 
Chukua Chako Mapema!, Chama Cha Majambazi!, Chama Cha Majangili!, Chama Cha Majizi!,.........
EU: Kwa nini TZ masikini????????????????????
Kiwete: Hata mimi sijui kwa nini TZ Masikini!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Upuuzi Mtupu!
 
eti upuuzi mtupu..mkwere jasho la pua lilimtoka jana....hatakaa asahau aibu aliyoipata jana kukataliwa live mbele ya wageni waalikwa na mabalozi..hahaaaaa shame on you JK..na bado
 
kimsingi mkwere hana mandate aor moral authority ya kuwa address watanzania kwa kuwa baada ya uchakachuaji kaingia madarakani kutokana na chini ya 50% ya waliopaswa kupiga kura kujitokeza vituoni kupiga kura (42.8%); na kati ya hao ni 27% ya watanzania waliopaswa kupiga kura waliomuingiza madarakani kinyume kabisa na historia ya kidemokrasia ya nchi hii. Tujiulize ni kwanini hawa watanzania wenzetu 51.2% walisusia zoezi la upigaji kura?

Historia ya nchi hii kuwa idadi ya watu wanaojitokeza kupiga kura haijawahi kupungua 70%; kwa mantiki hiyo chadema inawawakilisha hawa wote ambao walisusia zoezi la uchaguzi feki wa tanzania.
 
Chukua Chako Mapema!, Chama Cha Majambazi!, Chama Cha Majangili!, Chama Cha Majizi!,.........
EU: Kwa nini TZ masikini????????????????????
Kiwete: Hata mimi sijui kwa nini TZ Masikini!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Upuuzi Mtupu!

Yet you count yourself a GREAT THINKER!!!! Shame on you!
 
On this one CHADEMA is completely wrong take it or leave it.In the process they discredit themselves from the public eyes, whoever doesn't believe me wait till 2015. The sits won on parliament was a good success for CHADEMA but now with this move any wise man will tell you that is a wrong move!!
 
Bwana Vumbi mbona kichwa cha habari yako"DR Slaa aeleza sababu ya CHADEMA kususa" hakiendani na maelezo uliyoyatoa?????. Acha kuwatimulia VUMBI wa JF
 
Ebo kwanini Wabunge wanaweza kupingwa mahakamani na raisi asiweze kupingwa mahakamani,hayo ndio mapungufu,kuna hatari tume kuja kutangaza FISADI kuwa raisi na wananchi tukaishia kutawaliwa na FISADI
 
On this one CHADEMA is completely wrong take it or leave it.In the process they discredit themselves from the public eyes, whoever doesn't believe me wait till 2015. The sits won on parliament was a good success for CHADEMA but now with this move any wise man will tell you that is a wrong move!!

Kwa kigezo gani?????
 
Walipogoma CUF zenji mlisema hivyo hivyo subirini 2000 kama watapata seats,wakaendelea kuvipata mpaka mkaamua kuyagawa majimbo,na bado ngoma iko vivi!.2010 wakachukua mkachakachua ili mradi chechemea ibaki madarakani bara na visiwani.
hapo unanyesha jinsi ulivyo mvivu wa kuchambua mambo.
endelea kuamini hivyo kwani ndo mwisho wa upeo wako!
 
On this one CHADEMA is completely wrong take it or leave it.In the process they discredit themselves from the public eyes, whoever doesn't believe me wait till 2015. The sits won on parliament was a good success for CHADEMA but now with this move any wise man will tell you that is a wrong move!!

you'll be right in your prediction ONLY IF WISDOM HAS LOST the meaning!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom