Dr. Mwakyembe na Dr. Slaa watishiwa kuuawa

Dr. Mwakyembe na Dr. Slaa watishiwa kuuawa

Dk. Mwakyembe amesema kwenye barua hiyo, “Pamoja na kwamba taarifa hii ni mpya yenye matukio ya takriban mwezi moja tu, naamini kwa dhati kuwa msingi wake (kwa maana ya wahusika na maudhui) hautofautiani na ule wa matukio mengine ya awali ambayo baadhi yake yalisharipotiwa Polisi na vyombo vingine vya usalama kwa lengo la kuchunguzwa.

Maelezo ya Barua ya Mwakiembe

“Bado nina imani kubwa na Jeshi letu la Polisi kwamba litaifanyia kazi taarifa hii bila kujali nguvu ya ukwasi na ya kisiasa ya watuhumiwa na kwa kuzingatia misingi ya haki na ukweli.
“Msingi wa mimi kushtuka na kuamua kulivalia njuga suala hili kwa kuwataarifu watu mbalimbali wenye uelewa na kuvitaarifu vyombo vya dola, ni taarifa nilizozipata kutoka Songea tarehe 22/01/2011 kuhusu kundi la watu saba lililoingia mjini humo usiku wa tarehe 21/01/2011 kwa gari iliyodaiwa kuwa ya Wizara yangu (Ujenzi) aina ya Land Cruiser yenye usajili nambari STK 686… (ambayo kipindi fulani katika safari hiyo ilibadilishwa namba yake kuwa STK 6869). Gari hiyo iliwateremsha “abiria” hao saba sehemu iitwayo Madaba na baadaye kuchukuliwa na gari nyingine (Hardtop Land Cruiser yenye namba za usajili T76…BDU) hadi Top Inn ya mjini Songea.
“Majina ya baadhi ya watu hao saba ni: Wasomali wawili Hafidh na Faraj; kijana wa Kichagga kwa jina Mustafa a.k.a “Master”, Mkusa, jamaa ambaye wenzake wanaamini kuwa yuko Usalama wa Taifa; na (jina tunalo) kutoka Tanga anayedaiwa kuwa na utaalamu mkubwa wa kukaba watu.
“Mwenyeji aliyewapokea Songea watu hao saba ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya … akiongozana na mtu aitwaye Manya. Kilichowafanya baadhi ya watu waanze kulidadisi kundi hili, ni dhamira ya safari yao. Tetesi zilisema walikuwa wanaelekea Mbunde, kwa mganga maarufu wa kienyeji kwa jina Majungu. Hivyo, udadisi ukaongezeka kujua nani anakwenda “kulogwa” safari hii. Tetesi zikarejea na jina langu na msululu wa majina mengine: Dk. Slaa (Wilbrod), Anne Kilango- Malecela, Reginald Mengi, Profesa Mwandosya na Benard Membe.

Akana kuamini ushirikina huku akiuhofia

“Pamoja na kwamba sina imani na ushirikina au nguvu za giza, kutajwa kwa jina langu na fursa ya pekee niliyokuwa nayo ya kujua kilichokuwa kinafanyka, kukanipa ari, nguvu na shauku ya aina yake kutaka kulielewa zaidi suala hili ili ikibidi, niwataarifu wenzangu nao waelewe.
“Usiku wa Jumamosi tarehe 22/01/11 kundi hilo lilielekea Mbunde, wilayani Namtumbo (kwa gari aina ya Defender STK 265…, likiendeshwa na (jina tunalo) kukutana na ‘mganga’ Majungu …ambaye anaishi ndani ya Selous Game Reserve with impunity. Defender hiyo iligeuza kurejea Songea siku mbili baadaye na kuwaacha ‘wageni’ hao kwa mganga ambako walikaa siku saba ‘wakitengenezwa’. Walirejea Songea tarehe 29/01/11 na kesho yake tarehe 30/01/11 wakaanza safari ya kurejea Dar es Salaam.

“Kutoka Songea hadi Mafinga walitumia ile Hard Top iliyowatoa Madaba hadi Top Inn ya Songea (T76… BDU). Walifika Mafinga milango ya saa mbili usiku na kukuta gari mbili zikiwasubiri: Hilux Mayai ya (kampuni moja) na Defender iliyowaongoza hadi Morogoro. Walipokewa Morogoro na askari (jina tunalo). Hapo kundi likagawanyika: watu wanne wakiwemo wale Wasomali wawili wakaingia kwenye Nissan Patrol (T84… ADH) mali ya (kampuni jina tunalo) na wengine wakabaki Morogoro.

“Kufuatana na ‘mganga’ Majungu mwenyewe, ambaye wapelelezi wako wanaweza kuongea naye kama walivyofanya walionipa taarifa hizi, aliwapa masharti ya kutotumia silaha za moto ila njia nyingine kumuua kwanza Mwakyembe, baadaye Slaa, n.k., n.k, n.k. kwa zamu; alitengeneza dawa ya kuwapooza wale wengine (wanaosubiri) kwenye orodha ya kuuawa (Dk. Slaa, Anne Kilango, Mengi, Mwandosya na Membe) wasitaharuki na kupiga kelele za nguvu hata kuamsha hasira za wananchi mauaji yakitokea; aliwazindika vilivyo wasiweze kudhuriwa na tendo la kuua na alitengeneza dawa ya kuwapumbaza “waliohukumiwa kifo” (wawe mfano wa mbwa mbele ya chatu).

“Jijini Dar es Salaam ‘wahitimu’ hao wa Profesa Majungu walifikia Kiwalani karibu na kiwanda cha Mohamed Enterprises. Jirani na kiwanda hicho kuna jengo la ghorofa: chini ni msikiti wa Waarabu unaoitwa Malkaz na juu ni sehemu ya kuishi. Tarehe 05/02/11, wageni wawili zaidi waliwasili kwa ndege kutoka Uganda; mwanaume mmoja (aliyechanganya rangi) na mwanamke mmoja (mweusi vilivyo). Walipokewa na gari mbili; moja ya Polisi (PT 028…) na ya pili yenye namba za kibalozi (aina ya RAV 4).

Aelezea ushiriki wa Al Shabaab

“Jioni wakawa na mazungumzo ya kina na Wasomali wawili niliowaelezea awali ambao inadaiwa ni wapiganaji wa Harakat al-Shabaab al-Mujahideen (kwa kifupi Al-Shabaab).

Aelezea
“Niliweza kupata picha pana zaidi kwa nini wapiganaji wa kikundi hicho (kinachopambana na wanaodhaniwa kuwa maadui wa Uislamu) wameingizwa nchini. Nimeweza kukusanya taarifa zinazodai kuwa awali walifikiriwa kuletwa wapiganaji kutoka Rwanda, lakini wazo hili lilikataliwa na wafadhili wa mpango huu ambao walitaka ‘wanaharakati’ wa aina hiyo watoke Somalia. Ndipo kikundi hicho kikashawishiwa kwamba Tanzania kuna tatizo la udini, la Uislamu kutishiwa. Mimi na wenzangu hao watano tumejengewa hoja kuwa maadui wa Uislamu tunaotumiwa na makanisa, hivyo hatuna budi kukatishwa maisha yetu.

“Niliweza vile vile kupata picha kuwa wafadhili wa kundi hili, wana mahusiano ya karibu na Sheikh …(jina tunalo) ambaye baadhi ya utabiri wake unatokana na agenda za wafadhili hao. Inadaiwa kuwa utabiri wa sheikh … mwaka jana ulimlenga Dk. Slaa ambaye alidaiwa kubebwa na makanisa. “Utabiri” huo haukutimia kwa kuogopa kuiingiza nchi kwenye machafuko makubwa ya kisiasa/kidini ambayo yangewaweka pabaya hata wafadhili wa mpango huo.
“Inadaiwa kuwa Sheikh … ameombwa tena kutoa utabiri wa mwanasiasa na kiongozi mmoja kupoteza maisha mwezi huu (Fabruari). Inadaiwa kuwa mwanasiasa huyo anayetembea na kifo ni mimi na tayari maandalizi ya ‘hukumu yangu’ yamefanywa:

“(a) Kijana mmoja kwa jina la Hassan alitumwa kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma siku ya Jumamosi tarehe 05/02/11 kwa “maandalizi” hayo (mahali pa kufikia kikosi hicho cha mauaji, utambuzi wa nyumba ya kuishi niliyopangiwa na kumtafuta mhudumu mmoja wa Bunge ili ile portion ya Mganga Majungu ya kunipumbaza kabla ya hukumu, iweze kunyunyizwa kwenye kiti changu Bungeni);
“(b) Kesho yake (Jumapili) tarehe 6 Februari, mnamo saa nne usiku, kikosi hicho cha mauaji kikiwa na watu watano kiliondoka Dar es Salaam kwenda Dodoma kwa gari aina ya Land Cruiser nyeupe ya mkongo (T36… AKU) na kimejichimbia Dodoma mpaka leo (Februari 9).
“Waliomo kwenye kikosi hicho ni: Wasomali wale wawili, mgeni moja (wa kiume) kutoka Uganda, Mustafa a.k.a “Master” na kijana mmoja ambaye tarehe 19/01/11 aliwabeba Wasomali hao kutoka Morogoro hadi Ununio kupitia Kibaha na Baobab kwa gari aina ya VX Land Cruiser (T65…APF). Kijana huyo ana shepu ya Kitutsi na anaongea Kifaransa.
“Utabiri atakaoufanya Sheikh … (pengine aamue kuachana nao sasa baada ya kubaini kuwa tunaujua) utakuwa na lengo la kuwapumbaza wananchi waelekeze macho na masikio yao zaidi kwenye utabiri wake kuliko kwenye njama za kundi hilo za muda mrefu za mauaji.
“Kila siku ya Mungu napata taarifa za ziada kutoka kwa raia wema kuhusu suala hili. Naziingiza kwenye taarifa hii ili ziwasaidie katika upelelezi:

“Inadaiwa kuwa Wasomali hao waliingia nchini kutokea Kenya na wakaja kwa barabara hadi Dodoma. Walitumia gari aina ya RAV4 (new model – T81… AQS) tarehe 08/01/11 na kusafirishwa hadi Morogoro ambako walipokewa na askari niliyemtaja awali… wa Polisi Morogoro.
“Mjini Morogoro, walikaa hoteli mbili tofauti: Hilux Hotel Morogoro na Top Life. Aliyewafanyia Wasomali hao booking hapo Top Life ni mmiliki wa hoteli (jina la hoteli na mmiliki tunalo).
“Magari waliyotumia wakiwa Morogoro ni RAV4 T81… AQS, VX Land Cruiser STK 128…, Mercedes Benz (Station Wagon) T87… BDT, Toyota Mark II GX100 nyeupe T21… BKR na wakiwa Dar es Salaam wametumia magari VX Land Cruiser T65… APF, Nissan Patrol T84… ADH.”

Dk. Mwakyembe anaongeza, “Naomba nihitimishe maelezo haya kuwa nimekuwa muwazi kwa asimilia 100 na hata sources zangu ni miongoni mwa watu hao niliowataja katika taarifa hii ambao naamini utachukua hatua ya kuwahoji kulipatia ufumbuzi suala hili.
“Suala la msingi hapa, si uhai wangu, kwani ipo siku lazima nitakufa kama ambavyo hao mafisadi wanaodhani wanaweza kufadhili vifo vya wenzao watakavyokufa hata wao hatimaye, watake sasitake, It is simply a question of time. Suala la msingi hapa ni mustakabali wa Taifa letu, Taifa aliloliasisi Mwalimu Nyerere na kulilea kwa misingi ya usawa, haki, umoja, amani na utulivu.
“Nimejieleza awali kuwa nina imani kubwa na Jeshi letu la Polisi kwamba litaifanyiakazi taarifa hii bila kujali nguvu ya ukwasi na ya kisiasa ya watuhumiwa na kwa kuzingatia misingi ya haki na ukweli.

“Hata hivyo nalazimika kusema nitasikitika sana ikiwa taswira ya ‘ukorofi’ niliyopewa kwenye kesi moja ya awali (2009) itapewa nafasi kwenye suala hili, hivyo kuninyima fursa ya kusikilizwa vizuri na ulinzi ninaostahili kama raia kikatiba na kisheria. Niko tayari wakati wowote na mahali popote kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi litakaponihitaji.”
.


Maelezo haya sio ya mtu aliyekurupuka, kuna kitu kinachoendelea hapa!!
 
hapana, tusijadili hili kwa juu juu!! Serikali-maana yake-ni SIRIKALI!! Ndo maana upo uvumi na waweza kuwa kweli kuwa ile ajali ya Mhe.hayati Sokoine iikuwa ya kupangwa. Waswahili husema kuwa "lisemwalo lipo na kama halipo laja". Hivyo, si swala la mtu kupuuza maelezo ya mtu mzima na akili zake kupoteza muda kukusanya ushahidi mrefu mlolongo huo wa ki mazingira. Hii inamanisha kuna kitu fulani kipo, tena kinaihusisha serikali yenyewe hii ya jk. Hata kama plot haikuwa kumuua mwakeyembe au dr. slaa, mengi n.k; bali kunakitu kinachopangwa kisicho cha kawaida!!! Hivyo, inabidi uchunguzi wa kina kufanywa tena kwa uwazi kubaini ni nini hasa, na polisi kutoa maelezo hadhalani. Hatutaki watu "kukolimbiwa tena tz"!!!
 
nyie chukulieni mzaa wakati tu ....huu mpango upo sana..........
 
PJ

Mtanzania wame pre empty hii story kwa sababu ni tuhuma ambazo ziko mikononi mwa polisi. Lengo ni kuzifanya ziwe mchuzi mwepesi baada ya kuona kuwa wamestukiwa.

Mkuu umepiga ndipo: Mtanzania a.k.a Dowans/Richmond/Rostam/Lowassa, wanajaribu kuififisha taarifa ya hatari iliyofikishwa mikononi mwa vyombo vya dola. Ukiisoma story yenyewe ni ya kijinga kweli kweli. Inasema: "wasomi, wanasiasa wamshangaa Mwakyembe". Ukiwatafuta wasomi na wanasiasa hao huwaoni kwenye story nzima, unakuta para moja tu ikiwaongelea kiporojo porojo tu! Kinachoonekana hapa ni kuwa IGP Mwema aliandikiwa barua ya tuhuma nzito mwezi uliopita ili azipeleleze. Badala ya kumpatia mlalamikaji na wananchi matokeo ya upelelezi huo, barua yake inaishia mikononi mwa fisadi nambari moja nchini, Rostam, ambaye bila kujali miiko ya nyaraka za siri za Serikali anaianika gazetini mwake na kutufanya Watanzania wajinga kwa kuchakachua ukweli na kuingiza maoni yao ya kijinga. IGP ana wajibu kutueleza amefikia wapi na upelelezi huu na kwa nini barua yake imeishia mikononi mwa fisadi Rostam. Pengine IGP na wamiliki wa Mtanzania/Dowans/Richmond hawajui: wakichafua hali ya amani ya nchi hii, watafute mahali pengine pa kuishi na familia zao.
 
Nimeisoma kwa makini habari inayo muhusu Mwakyembe na malalamiko ya kuuwawa kwake na watu wengine. Ukiangalia ile habari inachangamoto kubwa kisheria hata kama amesingiziwa kwa yaliyoandikwa itamuwia vigumu kukanusha au kushtaki.

Ukiisoma vizuri hasa katika nukuu zao zenye utata, ile habari binafsi nahisi kama imelenga katika kumchafua Mwakyembe. Fuatlia kila wanapojifanya wamemnukuu Mwakyembe huwa hawaindiki jina lake harisi, majina wanayotumia ni Mwakiembe na Mwaky-embe. Kwa mtazamo wangu nahisi wametumia hayo majina ili Mwakyembe asiwe na nguvu za kisheria kuwaburuza mahakamani maana kisheria hawajasema kama wamemnukuu yeye. Sehemu zisizo na utata wametumia jina lake harisi.


Lisome vizuri MTANZANIA ukurasa wa pili utakutana na yafuatayo.....

Sub heading: "Maelezo ya Barua ya Mwakiembe"

Na ukiendelea zaidi utakutana na vitu kibao vimeandikwa katika style ya kidaku zaidi, kwa mfano huwezi ukamnukuu mtualiyetaja namba ya gari fulani anayoituhumu alafu unashindwa kuiandika namba nzima, kwanini uogope kama nukuu zako hazina uzushi. Nasikitika hiligazeti limenipotezea Tshs500 zangu na mda wa kulisoma.
 
Source: Gazeti la Mtanzania katika Mapitio ya magazeti Magic FM (Huwa sinunui magazeti ya RA)

Kumbe tuko wengi. Hata mimi sinunui gazeti la Mtanzania na RAI (Rostam Aziz Info). Yameanzishwa kutukuza ufisadi wa kila aina na kumfagilia Richard Monduli awe Rais baada ya Kikwete. Patachimbika.
 
mwaka jana au juzi mwakiembe si alishasema alitaka kuchomwa kisu kesi imeishia wapi. tanzania tuna wanasihasa vituko. kila wakiona wanachuja wanakuja na kituko kipya.
 
kama akitumia busara basi hiyo sio habari ya kujibu, MwakIEmbe na Mwak-yembe ndio wajibu.
kama Dr Slaa alivyosema, ukitaka mtu amwage data , mchokoze .......
 
Jamani huu ni ukweli, kumbukeni kuwa
  • Mwakyembe ni mtu mzima, hana sababu ya kuongopea umma wa wa Tz
  • Mwakyembe ni mtu msomi, ana PhD ya sheria, hawezi kutoa taarifa bila kuwa na impeccable evidence juu ya madai yake
  • Mwakyembe ni Waziri wa nchi, ana uhusiano wa karibu na dola na vyombo vyake. Hivyo ni rahisi kwake kupata habari nyeti dhidi ya nchi au yake.
Jamani, kwa hali ya nchi na uongozi wa rais anayeanza kuingiza udini katika siasa, aliyeingia madarakani kwa mikakati ya kundi la mafisadi, aliyerudi madarakani kwa mbinu za mkato (yaani si za kidemokrasia), habari hii inaweza kuwa ya uongo kwa probability 0. Kila mtu mwenye akili zake anaweza kufahamu kuwa, Mwakyembe ametumia mbinu rahisi sana ya kujilinda...ni kwa kuitoa siri yote nje, na hivyo kukwamisha mkakati wote.

Sasa vyombo vya dola hata vikishindwa kuifanyia kazi lakini kundi la wauaji haliwezi tena kutekeleza mkakati wao wa kishetani = alshabab nk = ufisadi = umafia wa kuua wazalendo wa nchi yetu.
 
Nimeisoma kwa makini habari inayo muhusu Mwakyembe na malalamiko ya kuuwawa kwake na watu wengine. Ukiangalia ile habari inachangamoto kubwa kisheria hata kama amesingiziwa kwa yaliyoandikwa itamuwia vigumu kukanusha au kushtaki.

Ukiisoma vizuri hasa katika nukuu zao zenye utata, ile habari binafsi nahisi kama imelenga katika kumchafua Mwakyembe. Fuatlia kila wanapojifanya wamemnukuu Mwakyembe huwa hawaindiki jina lake harisi, majina wanayotumia ni Mwakiembe na Mwaky-embe. Kwa mtazamo wangu nahisi wametumia hayo majina ili Mwakyembe asiwe na nguvu za kisheria kuwaburuza mahakamani maana kisheria hawajasema kama wamemnukuu yeye. Sehemu zisizo na utata wametumia jina lake harisi.


Lisome vizuri MTANZANIA ukurasa wa pili utakutana na yafuatayo.....

Sub heading: "Maelezo ya Barua ya Mwakiembe"

Na ukiendelea zaidi utakutana na vitu kibao vimeandikwa katika style ya kidaku zaidi, kwa mfano huwezi ukamnukuu mtualiyetaja namba ya gari fulani anayoituhumu alafu unashindwa kuiandika namba nzima, kwanini uogope kama nukuu zako hazina uzushi. Nasikitika hiligazeti limenipotezea Tshs500 zangu na mda wa kulisoma.

Ngoja nikachukue Mtanzania, kama ni kweli basi hata mimi wamenichanganya kidogo na habari yao.
 
mwaka jana au juzi mwakiembe si alishasema alitaka kuchomwa kisu kesi imeishia wapi. tanzania tuna wanasihasa vituko. kila wakiona wanachuja wanakuja na kituko kipya.

sijui kama uko sawa , na siku akifa usichangie chochote humu jf, Maana wanafiki wengi humu. Tunajua kutokana na kazi yake ile ya tume baada ya hapo mambo mengi tumeyajua kuwa nchi inatafunwaje!!! na aligusa maslahi ya watu hadi watu kuachia vyeo vyao, alivuruga dira na mipango ya wakubwa, kwa hiyo suala la kumuondoa lipo hata ukibisha. Wewe unasema wanachuja wanakuja na vituko vipya. Wewe unadhani namba zote za magari zilizotajwa na vyumba walipolala ni uongo . AGGHHHHHHH unataka kuniudhi wakati leo wanawake wote wako kileleni mwa siku yao( Siku ya Wanawake) akifa mzee wa watu usichangie lolote wala kuonesha masikitiko hapa. Kaa kimya, Jenifa jina la mwanangu alafu unarop......................... aghhhhh unataka kuniaribia siku. Jaribu kuwa analytical
 
New Habari wanajifunza kutoka kwa mmiliki wao maana kwenye nyaraka tata anajiita Rustam, Rostamu, Rastam n.k Hakya nani humfikishi mahakama yoyote wala huwezi kutaifisha mali zake maana Rostam hamiliki kitu lakini ndio "Rais"
 
Anawatuhumu jeshi la polisi, usalama wa taifa, na waganga wa kienyeji

Source: Gazeti la Mtanzania katika Mapitio ya magazeti Magic FM (Huwa sinunui magazeti ya RA)

ongeza hoja mkuu,,,,,kama zimeniconfuse kiaina!!!
 
hivi jamani kuuliza sio ujinga.
hivi siku hizi toilet paper huwa zina maandishi?
kweli tz tumeendelea.
rost tamu+ufisadi=mtanzania?
hilo hesabu hata mtoto mdogo anapatia.
 
Wanaobeza tuhuma za mwakyembe hawaoni mbali hata kidogo. Jamani mwakyembe ni mtu pekee aliyediriki kumtaja rostam azizi kuhusika na dowans/richmond ktk vikao rasmi vya chama (wabunge wa CCM). Mimi naamini hata ile 'ajali' ya mwakyembe ilipikwa. Hivi rais kawapa uwaziri mwakyembe na sitta kwa sababu anajua ni wachapa kazi au aliona wanapiga sana kelele?

Halafu huyu sheikh anaesemwa ktk taarifa hii yupo karibu sana na UwT toka muda mrefu-rejea story ya Ludovick Mwijage (The dark Side of Nyerere Legacy). Hebu angalia utabiri wake wa karibuni-eti siri nyingi za serikali zataanikwa! Huu sio utabiri, ni common sense tu-kama maovu yanatendeka na hakuna anaechukua hatua then siri zitatoka tu! A bitter truth is that govts all over the world does some dirty works! Hili tulikubali, serikali zinafanya mambo ambayo yanapokuja kujulikana inakuwa aibu kubwa sana.Tofauti ni kwamba nchi zilizoendelea, mara nyingi zinafanya kwa ajili ya ustawi wa watu wao. Sisi tunafanya kwa ajili ya ustwai wa kikundi cha watu. Ya profesa Jwani Mwaikusa nayo ni laana ya kujadiliwa siku nyingine....
 
mwaka jana au juzi mwakiembe si alishasema alitaka kuchomwa kisu kesi imeishia wapi. tanzania tuna wanasihasa vituko. kila wakiona wanachuja wanakuja na kituko kipya.


Kweli kuna watu wanamatatizo hapa duniani,yaani mtu anaandaliwa kifo wee unasema kituko,duhuuu kazi ipoooo,kitu kingine tueleze mwakyembe kachuja wapi na lini?....acha mambo ya kukurupuka dada,au na wewe upo kwenye huo mpango nini?
 
mwaka jana au juzi mwakiembe si alishasema alitaka kuchomwa kisu kesi imeishia wapi. tanzania tuna wanasihasa vituko. kila wakiona wanachuja wanakuja na kituko kipya.

Jenifa Wanasema Siasa ni Sayansi....Teh teh..... ngoma imeanza
 
these are serious allegations which should not be left unquestionable.
 
Back
Top Bottom