Dr. Mpango na TRA, huu ni Uhujumu Uchumi!

Mkuu Hawa jamaa Ni balaa. Juzi hapa majengo muuza kuku mmoja ivi alijipeleka kuomba kujisajili ila kabla ya kujisajili akaomba afanyiwe makadirio.

Kilichompata anakijua mwenyewe....alitoka ofisini hakurudi Tena.....

Tatizo jingine, watu wengi Sana Dodoma wanafunga biashara, ukipeleka barua tiaraei ili utolewe kwenye mfumo wa Kodi tiaraei hawakutoi. Siku ukirudi unakuta una Deni rumbesa.....hao ndio tiaraei tz.

Hawa jamaa ni waonevu Sana Sana

Kenya mazingira ya business Ni mazuri sana kulinganisha na hapa. Hapa tunalazimishwa Tena kwa kubambikiwa makodi lukuki

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa Dodoma ni balaa ..hawataki kabisa ufunge biashara yako sijui wanangangania nini.barua ukipeleka wanakuzungusha weee kuipitisha hata siwaelewi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Endeleeni kufunguka wakuu , Mungu yuko pamoja nanyi .
Kuna tukio mojawapo nakamilisha kuanadaa baadi ya nyaraka ikiwamo makadirio bandia ya TRA, vikao walivyo kaa na wajumbe wake, utetezi waliokua wakitoa watuhumiwa na jinsi sakata lilivyoisha. Mambo yote yakiwa tayari nitamwaga mambo hapa watu wajionee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nina mtazamo tofauti. Ikumbukwe kuwa watumishi wa TRA ni watanzania wenye mitazamo tofauti ya kisiasa. Na inawezekana kabisa kuwa baada ya kuzibiwa mianya yao ya upigaji waliokuwa nayo mwanzo basi wameamua kufanya surbotage kwa kuwakadiria watu kodi zisizolipika ili wananchi wazidi kuichukia serikali yao na Rais wao. Maana ni jambo la kawaida sana kwa hao jamaa kukuandikia kodi huku wakikuambia hapa kazi tu. Kwa hali hiyo serikali Ina kazi nyingine ya kuchuja watumishi waadilifu wa TRA na wale wanaofanya kazi ili kuipaka matope serikali..
 
Mkuu ungetoa taarifa kwa wahusika. Kama kuna vitendo ama viashiria vya rushwa toa taarifa ama utaje hata kampuni zenyewe huenda wahusika wakaona na kuchukua hatua
ndugu, unaongelea wahusika gani?

watu washawahi kupeleka "takokuru" ushahidi wa rushwa kwa video na hakuna kilichofanyika.

we f..d ourselves in October 2015 and we'll remain f..d until and unless.....
 
Mimi Ushauri wangu mkulu wa Mwaloni aamke siku moja aaumuru hela zoote zililokuwemo kwenye akaunti yoyote ile na kwenye Benki yoyota ile aihodhi na kuihamishia kwake.

Kitakachofuatia ni aaitishe Kikao na Baraza lake la Mawaziri Achukue kitabu cha katiba anyofoe ukurasa mmoja asokotee Tumbaku halafu apige pafu zito akipumua awaaangaliee mawaziri halafu asikitike kwa furaha

Halafu awafukuze mawaziri wote na kutangaza Utawala wa KIFALME kabla Mawaziri hao hawaja react Ngoma za Asili zaKisukuma zilizokuwa zimeandaliwa kwa Siri Mkubwa zianze kumbuiza.

Jenerali Mabeyo aje Kusujudu Mbele ya Mfalme na kuyaamuru majeshi yote yatii UFALME wetu mpya

Nyimbo za Kwaya za Kumsifu Malaika zifuatie Huku Nderemo vijijo na hoihoi zikiendelea kwa Siku saba
Wachawi Elfu sabini kutoka Usukumani wamzungumke mara Sabini Mfalme wetu mpya.
Waswezi Elfu tatu wapulize mapembe ya ya Tandala na kumpakaa Dawa Mfalme wetu
Wapiga Ngoma wa Kihutu Mia tatu wapige Ngoma kwa juhudi kubwa huku wakicheza kwa madaha.
Bundi Mia sita waachiwe hewani kama gesture ya Amani na Upendo.

THE KINGDOM EMAGUFUTINI itakuwa imezaliwa Rasmi.
Hahahahahahahahahaa jinga kweli umenichekesha sana.
 
Kinachoendelea sasa hivi kinaogopesha. Maafisa wa TRA wameanza kuvamia makampuni. Wanataka ripoti ya mapato yako yote, Bank Account, malipo ya VAT, Rekodi ya manunuzi chini ya masaa 72 etc…

Maafisa hawa wa TRA wanafanya mahesabu yao na kurudi kwako kwamba umekuwa ukikwepa kodi kwa maana hiyo wanafanya estimate ya kiwango unachodaiwa. Matajiri wanaulizwa chanzo cha utajiri wao, mwisho wa siku wanaomba watoe hela au account zao zizuiliwe.

Kampuni moja ndogo sana hapa Temeke wanadaiwa million 350 wakati hata kwa mwezi hawaingizi million 60.

Makampuni mengi sana na matajiri wanalalamika kwa uvamizi huu. Hali ni mbaya. Na hii ni uhujumu uchumi maana hawa watu wanaenda kufunga bila shaka.

Sasa, swali langu: Haya makamuni yakifungwa, serikali itapata wapi mapato, na waajiriwa wataenda wapi?
Haya ndiyo matokeo ya kuongozwa na vichaa
 
Back
Top Bottom