Dr. Mpango na TRA, huu ni Uhujumu Uchumi!

Pale unapoona umeonewa tafuta suluhu ya kisheria kudai haki yako kupitia vyombo vya haki nchini.
.
.
Badala ya kukimbilia huku kulalamika ambalo si jambo la msingi sana japo si baya pia tuwe na tabia ya kukimbilia mahakamani kwanza ili kuzuia hayo maovu ambayo tunaona hatutendewi sawa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
downloadfile-34.jpg
 
Kinachoendelea sasa hivi kinaogopesha. Maafisa wa TRA wameanza kuvamia makampuni. Wanataka ripoti ya mapato yako yote, Bank Account, malipo ya VAT, Rekodi ya manunuzi ya miaka 5 chini ya masaa 72 etc…

Maafisa hawa wa TRA wanafanya mahesabu yao na kurudi kwako kwamba umekuwa ukikwepa kodi kwa maana hiyo wanafanya estimate ya kiwango unachodaiwa. Matajiri wanaulizwa chanzo cha utajiri wao, mwisho wa siku wanaomba watoe hela au account zao zizuiliwe.

Kampuni moja ndogo sana hapa Temeke wanadaiwa million 350 wakati hata kwa mwezi hawaingizi million 60.

Makampuni mengi sana na matajiri wanalalamika kwa uvamizi huu. Hali ni mbaya. Na hii ni uhujumu uchumi maana hawa watu wanaenda kufunga bila shaka.

Sasa, swali langu: Haya makamuni yakifungwa, serikali itapata wapi mapato, na waajiriwa wataenda wapi?
Taja hayo makampuni umetumwa wewe kuichafua Serikali
 
Serikali haina pesa licha ya kujitapa kufanya miradi mikubwa kwa Steigler gorge, SGR na madege yasiyo na maana kwa walio wengi. Sasa wanataka kuwakamua zaidi wafanya biashara lakini kama hawana hiyo pesa hawatatoa na mtabakia kuwasweka ndani tu. Kwa hali ilivyo wana heri wale wasio na biashara yoyote au waliofunga hizo biashara. Huko Arusha nasikia biashara zaidi ya 600 'zitafungwa'.

Mmoja wa wafanya biashara, rafiki yangu nilikwenda kwa duka lake la nguo kwa majadiliano fulani. Kuanzi saa 3 asubuhi hadi saa 6 nikiwepo hakuna mteja aliyeingia. Nilipomuuliza inakuwaje ndugu yangu? Akasema "mbona tumesha zoea; namalizia tu hii stock halafu nijaribu namna nyingine"

Watu wamekata tamaa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tatizo ni namna ya matumizi ya mapato yatokanayo na kodi zetu, KIUHALISIA WENGI WETU kwa namna moja ama nyingine tunakwepa kodi sio kwa kutokuelewa umuhimu wa kodi bali kutokana namna zinavyotumika baada ya makusanyo.

Kwa nchi kama Norway, Switzerland, Sweeden etc wananchi wana uwezo wa kuhoji kukiwa na tatizo katika mfumo/mradi wowote uliojengwa kwa kutumia kodi za wananchi. KILA MWANANCHI HUWA ANALIPA KODI
 
Tutaminywa sana kwa sababu nchi inategemea chanzo cha ndani tu kupata fedha za kuendeshea nchi.Tujiandae kisaikolojia haswa muhula wa utawala unaokuja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao ndio TRA.

Kusema kweli kuna tatizo kubwa sana. Sijui kama mamlaka nyingine hazilioni.

TRA kuna baadhi ya wafanyakazi hawastahili kabisa kuwa huko. Wanapenda sana rushwa tena bila aibu na rushwa kubwa kweli kweli kwa vigezo vya kutimiza wajibu wao wa kazi.

Nchi hii ni yetu sote. Tuijenge kwa nidhamu na taratibu. Kuua hizi biashara itakuwa kwa faida ya nani?

Tusifumbie macho tatizo...umefika muda muafaka tuanze kufanyia kazi malalamiko haya
Hao hao TRA hawakuwa hivyo enzi za JK tusiwalaumu sana wanapewa shinikizo kutoka juu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilisema haya juzi kati kuna wati wakasema ni uzushi wakati nina ushahidi.

Sent using Jamii Forums mobile app


Mleta mada napenda nikushauri kuwa katika shauri hili zipo njia mbali mbali za kuweza kukusaidia.Nimesoma presentation moja wapo ambayo nilihudhuria ya hao jamaa mamlaka ya mapato aka TRA kuwa ukiona wamekuonea ipo bodi ya rufaa na mpaka mahakama ya rufaa.nadhani fanya hivo ili wakati mwingine wajue kuwa wananchi tupo makini tunazijua taratibu. Pia usikubali tu makadirio unayo haki kukata rufaa.Ila na sisi tuwe tunatunza kumbukumbu maana hapo ndipo tunawapa nafasi.
 
Wewe bhana acha kunvunja mbavu zangu, lakini unachosema ndicho kitatokea mark my words!
Mimi Ushauri wangu mkulu wa Mwaloni aamke siku moja aaumuru hela zoote zililokuwemo kwenye akaunti zozote zile na kwenye Benki yoyote ile azihodhi na kuzihamishia kwake.

Kitakachofuatia ni aaitishe Kikao na Baraza lake la Mawaziri Achukue kitabu cha katiba anyofoe ukurasa mmoja asokotee Tumbaku halafu apige pafu zito akipumua awaaangaliee mawaziri halafu asikitike kwa furaha

Halafu awafukuze mawaziri wote na kutangaza Utawala wa KIFALME kabla Mawaziri hao hawaja react Ngoma za Asili zaKisukuma zilizokuwa zimeandaliwa kwa uSiri Mkubwa zianze kumbuiza.

Jenerali Mabeyo aje Kusujudu Mbele ya Mfalme na kuyaamuru majeshi yote yatii UFALME wetu mpya

Nyimbo za Kwaya za Kumsifu Malaika zifuatie Huku Nderemo vijijo na hoihoi zikiendelea kwa Siku saba
Wachawi Elfu sabini kutoka Usukumani wamzungumke mara Sabini Mfalme wetu mpya.
Waswezi Elfu tatu wapulize mapembe ya ya Tandala na kumpakaa Dawa Mfalme wetu
Wapiga Ngoma wa Kihutu Mia tatu wapige Ngoma kwa juhudi kubwa huku wakicheza kwa madaha.
Bundi Mia sita waachiwe hewani kama gesture ya Amani na Upendo.

THE KINGDOM EMAGUFUTINI itakuwa imezaliwa Rasmi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usiongee vitu ambavyo haujui, ni wajibu wa makampuni kukadiria hesabu zao mwanzoni kabisa mwa mihula ya kibiashara ilogawanywa mara nne ndani ya miezi 12, ni wajibu wako pia mfanyabishara kuijulisha mamlaka ya mapato kila unapopitia ya kipato na mtiririko wa biashara yako kwa ujumla. Unapaswa kufahamu kuwa biashara inapaswa kurejesha mamlakani kiasi 30% ya faida ambayo umepata baada ya kufunga hesabu za mwisho za mwaka, na ikiwa umesajiri hasara hivyo mamlaka inawajibu wa kurejesha kodi ambayo uliilipa kama kadirio la mapato ya mwaka huo.
Wafanyabiashara unaowalalamikia hawatunzi kumbukumbu, hawafanya marejesho ya mapato wakati mwingine hata ongezeko la thamani mimi na wewe mlaji ndio walipaji wa hiyo kodi.
TRA wanawajibu wa kujiridhisha kuwa unalipa kodi stahiki lakini hii ni baada ya mfanyabiashara kufanya hesabu zake za mwisho za mwaka wa biashara.
Haujafanya return kwa miaka mitatu ni dhahiri kuwa kuna kitu unaficha, sasa mjinga mmoja anakuja tu hapa kuwa mamlaka inahujumu uchumi.
Kama haujui uliza au chukua muda wako kujifunza, kesho ukikamatwa kwa uchochezi serikali kandamizi.
Tumia akili
 
Siku hizi ukisikia jiwe kawaamrisha TRA kufanya kitu chenye mwelekeo positive kwa mlipa kodi WEWE CHUKULIA KINYUME CHAKE.
 
Back
Top Bottom