Mfiaukweli
JF-Expert Member
- Aug 30, 2018
- 5,636
- 8,774
Usiongee vitu ambavyo haujui, ni wajibu wa makampuni kukadiria hesabu zao mwanzoni kabisa mwa mihula ya kibiashara ilogawanywa mara nne ndani ya miezi 12, ni wajibu wako pia mfanyabishara kuijulisha mamlaka ya mapato kila unapopitia ya kipato na mtiririko wa biashara yako kwa ujumla. Unapaswa kufahamu kuwa biashara inapaswa kurejesha mamlakani kiasi 30% ya faida ambayo umepata baada ya kufunga hesabu za mwisho za mwaka, na ikiwa umesajiri hasara hivyo mamlaka inawajibu wa kurejesha kodi ambayo uliilipa kama kadirio la mapato ya mwaka huo.
Wafanyabiashara unaowalalamikia hawatunzi kumbukumbu, hawafanya marejesho ya mapato wakati mwingine hata ongezeko la thamani mimi na wewe mlaji ndio walipaji wa hiyo kodi.
TRA wanawajibu wa kujiridhisha kuwa unalipa kodi stahiki lakini hii ni baada ya mfanyabiashara kufanya hesabu zake za mwisho za mwaka wa biashara.
Haujafanya return kwa miaka mitatu ni dhahiri kuwa kuna kitu unaficha, sasa mjinga mmoja anakuja tu hapa kuwa mamlaka inahujumu uchumi.
Kama haujui uliza au chukua muda wako kujifunza, kesho ukikamatwa kwa uchochezi serikali kandamizi.
Tumia akili
TRA hukataa makadirio yaliyofanywa na mlipa kodi mwenyewe na kubandika watakayo wao.