Dr. Mpango na TRA, huu ni Uhujumu Uchumi!

Mwingereza

JF-Expert Member
Jan 21, 2014
1,110
2,736
Kinachoendelea sasa hivi kinaogopesha. Maafisa wa TRA wameanza kuvamia makampuni. Wanataka ripoti ya mapato yako yote, Bank Account, malipo ya VAT, Rekodi ya manunuzi ya miaka 5 chini ya masaa 72 etc…

Maafisa hawa wa TRA wanafanya mahesabu yao na kurudi kwako kwamba umekuwa ukikwepa kodi kwa maana hiyo wanafanya estimate ya kiwango unachodaiwa. Matajiri wanaulizwa chanzo cha utajiri wao, mwisho wa siku wanaomba watoe hela au account zao zizuiliwe.

Kampuni moja ndogo sana hapa Temeke wanadaiwa million 350 wakati hata kwa mwezi hawaingizi million 60.

Makampuni mengi sana na matajiri wanalalamika kwa uvamizi huu. Hali ni mbaya. Na hii ni uhujumu uchumi maana hawa watu wanaenda kufunga bila shaka.

Sasa, swali langu: Haya makamuni yakifungwa, serikali itapata wapi mapato, na waajiriwa wataenda wapi?
 
Mkuu ungetoa taarifa kwa wahusika. Kama kuna vitendo ama viashiria vya rushwa toa taarifa ama utaje hata kampuni zenyewe huenda wahusika wakaona na kuchukua hatua
 
Hao ndio TRA.

Kusema kweli kuna tatizo kubwa sana. Sijui kama mamlaka nyingine hazilioni.

TRA kuna baadhi ya wafanyakazi hawastahili kabisa kuwa huko. Wanapenda sana rushwa tena bila aibu na rushwa kubwa kweli kweli kwa vigezo vya kutimiza wajibu wao wa kazi.

Nchi hii ni yetu sote. Tuijenge kwa nidhamu na taratibu. Kuua hizi biashara itakuwa kwa faida ya nani?

Tusifumbie macho tatizo...umefika muda muafaka tuanze kufanyia kazi malalamiko haya
 
Mkuu Hawa jamaa Ni balaa. Juzi hapa majengo muuza kuku mmoja ivi alijipeleka kuomba kujisajili ila kabla ya kujisajili akaomba afanyiwe makadirio.

Kilichompata anakijua mwenyewe....alitoka ofisini hakurudi Tena.....

Tatizo jingine, watu wengi Sana Dodoma wanafunga biashara, ukipeleka barua tiaraei ili utolewe kwenye mfumo wa Kodi tiaraei hawakutoi. Siku ukirudi unakuta una Deni rumbesa.....hao ndio tiaraei tz.

Hawa jamaa ni waonevu Sana Sana

Kenya mazingira ya business Ni mazuri sana kulinganisha na hapa. Hapa tunalazimishwa Tena kwa kubambikiwa makodi lukuki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi Ushauri wangu mkulu wa Mwaloni aamke siku moja aaumuru hela zoote zililokuwemo kwenye akaunti zozote zile na kwenye Benki yoyote ile azihodhi na kuzihamishia kwake.

Kitakachofuatia ni aaitishe Kikao na Baraza lake la Mawaziri Achukue kitabu cha katiba anyofoe ukurasa mmoja asokotee Tumbaku halafu apige pafu zito akipumua awaaangaliee mawaziri halafu asikitike kwa furaha

Halafu awafukuze mawaziri wote na kutangaza Utawala wa KIFALME kabla Mawaziri hao hawaja react Ngoma za Asili zaKisukuma zilizokuwa zimeandaliwa kwa uSiri Mkubwa zianze kumbuiza.

Jenerali Mabeyo aje Kusujudu Mbele ya Mfalme na kuyaamuru majeshi yote yatii UFALME wetu mpya

Nyimbo za Kwaya za Kumsifu Malaika zifuatie Huku Nderemo vijijo na hoihoi zikiendelea kwa Siku saba
Wachawi Elfu sabini kutoka Usukumani wamzungumke mara Sabini Mfalme wetu mpya.
Waswezi Elfu tatu wapulize mapembe ya ya Tandala na kumpakaa Dawa Mfalme wetu
Wapiga Ngoma wa Kihutu Mia tatu wapige Ngoma kwa juhudi kubwa huku wakicheza kwa madaha.
Bundi Mia sita waachiwe hewani kama gesture ya Amani na Upendo.

THE KINGDOM EMAGUFUTINI itakuwa imezaliwa Rasmi.
 
Mimi Ushauri wangu mkulu wa Mwaloni aamke siku moja aamumuru hela zoote zililokuwemo kwenye akaunti yoyote ile na kwenue Benki yoyota ile aihodhi na kuihamishia kwake.

Kitakachofuatia ni aaitishe Kikao na Baraza lake la Mawaziri Achukue kitabu cha katiba anyofoe ukurasa mmoja asokotee Tumbaku

Halafu afukuze mawaziri wote na kutangaza Utawala wa KIFALME Ngoma za Kisukuma zilizokuwa zimeandaliwa kwa Siri zitumbuize

Jenerali Mabeyo aje Kusujudu Mbele ya Mfalme na kuyaamuru majeshi yote yatii UFALME wetu mpya

Nyimbo za Kwaya za Kumsifu Malaika zifuatie Huku Nderemo vijijo na hoihoi zikiendelea kwa Siku saba
Wachawi Elfu sabini kutoka Usukumani wamzungumke mara Sabini Mfalme wetu mpya.
Waswezi Elfu tatu wapulize mapembe ya ya Tandala na kumpakaa Dawa Mfalme wetu
Wapiga Ngoma wa Kihutu Mia tatu wapige Ngoma kwa juhudi kubwa huku wakicheza kwa madaha.
Bundi Mia sita waachiwe hewani kama gesture ya Amani na Upendo.

THE KINGDOM MAGUFUTINI itakuwa imezaliwa Rasmi.
Hivi sasa ni vitunguu swaumu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
27 Reactions
Reply
Back
Top Bottom