Siasa za Ujenzi wa Viwanda: TRA na Wizara ya Viwanda ni watuhumiwa wa kwanza

Yusuf Kashaju

Member
Oct 20, 2019
57
89
Hongera CCM kwa kutimiza miaka 44.

Jana nimefuatilia kidogo mjadala wa CCM uliokuwa unaongozwa na Comred Polepole, wachangiaji wa mada walishindwa kueleza sababu hasa za nchi yetu kushindwa kutunga na kutekeleza na kusimamia sera za kujenga uchumi wa viwanda ili kutuondoa katika dimbwi la umasikini huku Mwenyezi Mungu alitujalia rasilimali nyingi.

Watuhumiwa wa kwanza ni TRA na Wizara ya Viwanda ndiyo wanatukwamisha na kukwamisha juhudi za serikali kujenga uchumi wa viwanda, na ninatoa sababu TRA.

Hawa TRA Serikali imetunga sheria ya kuhamasisha uletaji wa mashine nchini kwa ajili ya kuhamasisha uzalishaji wa bidhaa, ambapo sheria ya VAT inatoa msamaha wa VAT kwa mtu anayeingiza nchini mashine kwa ajili ya uzalishaji. TRA wakahujumu sera hii nzuri kwa kutunga kanuni za VAT na kuweka shariti gumu ambalo wanajua fika mtanzania wa kawaida na ambaye itakuwa mara yake ya kwanza kufanya jtihada za kuanzisha kiwanda litamshinda kulitimiza.

Sharti lililowekwa na TRA kupitia kanuni wanazotunga wao ni kuwa ili uweza kunufaika na msamaha wa VAT ni lazima mashine unayoingiza nchini kodi yake ya VAT iwe ni zaidi ya shilingi milioni 30. Kitendo hiki kilichofanywa na TRA kimewandoa watanzania na wajasiliamali wengi kukosa msamaha wq VAT na hivyo kuwawia vigumu kuanzisha viwanda vidogo. Sasa fikiri mashine nyingi za SMEs gharama yake ni dola 10,000 hadi dola 15,000!

Wizara ya Viwanda na Biashara
Hii Wizara kwa kujua au kutokujua imekuwa ni kikwazo hasa kutokana na kuikumbatia CTI na kuwa mratibu mkubwa wa kutekeleza sera zinazoshawishiwa na CTI, kila mtu aliyekuwa katika sekta binafsis na sekta ya umma Tanzania anajua lengo la CTI ni kulithibiti soko la Tanzania kama mali yao, hivyo muda wote CTI inafanya kila liwezekanalo kuzuia wazawa kuingia katika sekta ya viwanda na kwa wageni pia kuja kuwekeza nchini. Mfano halisi ni makampuni yanayotoka bara la Ulaya nchini kuanzisha nayo umoja wao nazani CTI waliona kuna kitu! Kwa takribani miaka 10 iliyopita CTI wamefanikiwa sana kuthibiti utungaji wa sera za kodi na viwanda nchini, uku Wizara ya Viwanda na Biashara ikiwa katika usingizi mzito. Nakumbuka walifikia hatua karibia wafute kodi zote kwenye maji na soda na juice.

CTI hana nia ya kukuza au kuona watanzania wengine wanaanzisha viwanda, chukua mfano wa ALAF baada ya kuthibiti soko la vifaa vya ujenzi sasa waviuza bei wanayotaka wananchi wanakamuliwa vifaa vya ujenzi viko juu gharama za ujenzi zimeongezeka sana lakini nani wa kuwauliza, wanafanya wanayotaka kwa kuwadanganya Wizara kuwa sasa Tanzania inajitoshereza kwa vifaa hivyo, lakini kwa gharama gani? Wizara haiwezi kujiuliza swali hili?

Halafu wameenda mbali kwa kuweka sera yao ya ndani ya kuzuia kuuza coils kwa mtu wa nje, hii maana yake ni kwanza hawataki kuwainua wazalishaji wadogo ambao wanazo mashine za corrugation of iron sheets, wanafanya hivyo wanajua hao wadogo hawana pa kukimbilia kwani tayari serikali imeshaweka ushuru mkubwa ktk coils ili kuilinda ALAF. CCM ni muhimu muyajue hayo akina COMRED POLEPOLE.

Nitaendelea wiki ijayo🎃🎃
 
Back
Top Bottom